Biz TV

Biz TV Tunawaletea habari za biashara kutoka Tanzania | Bringing you business news from Tanzania

Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amezindua Bodi   ya Wakurugenzi wa TIC  na kuwataka kutumia sheria mpya ya Uwekezaji iliiyobores...
28/05/2023

Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na kuwataka kutumia sheria mpya ya Uwekezaji iliiyoboreshwa kuhakikikisha wanapata wawekezaji wengi zaidi.

“Dhamira yetu ni njema kuendelea kujenga uwezo ili tutakapoingia na bidhaa hii tuwe na uwezo mkubwa wa kupeleka katika e...
22/05/2023

“Dhamira yetu ni njema kuendelea kujenga uwezo ili tutakapoingia na bidhaa hii tuwe na uwezo mkubwa wa kupeleka katika eneo kubwa la Afrika” Dkt Ashatu Kijaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa. Bw. Amo...
15/05/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam.

Women Take Charge of Your Financial Future with Amana Bank's Annisaa Account.ANNISAA ACCOUNTThis is customized saving ac...
20/04/2023

Women Take Charge of Your Financial Future with Amana Bank's Annisaa Account.

ANNISAA ACCOUNT
This is customized saving account that suits women of all walks of life who choose to save for a long period of time to satisfy their financial needs. This account has been specially designed in recognition of the outstanding contribution made by women in family and society. They are unsung heroines of our nation.

FEATURES
- Minimum Opening Balance of TZS 20,000/- or USD, EUR, GBP 100, AED 150
- Minimum Account Maintenance Balance of 100,000 USD ,EUR ,GBP 200, AED 300
- Available in TZS and USD ,EUR ,GBP , AED
- Access to Internet Banking, Amana Bank App and Amana Bank Sim Banking with Instant Transaction Alerts (SMS Alerts)
- Low Monthly Maintenance Fee and other Bank charges are applied as per Bank Tariff

BENEFITS
- Easy to Open and Operate
- Private and Comfortable Banking Services including Customized Teller Services at all our Branches
- Personalized ATM Debit Card
- 24hrs access through Mastercard network and Withdrawal Services Through Nationwide Mastercard ATMs
- Free Cash Transfers Within the Bank
- Free Over the Counter Balance Inquiry Service
- ATM mini Statement

REQUIREMENTS
Private Individual/employees
- One passport size photograph
- Copy of national identity card / passport / voter card / new driver license
- Introduction letter from local government or utility bill water, (electricity or telephone) having the applicant’s name
- Residence / work permit for non-residents.
The Annisaa Account is an ideal savings plan for women who aspire to achieve their financial goals. Amana Bank is committed to empowering women by providing them with financial support and innovative banking solutions. Amana Bank Ltd


https://biztv.co.tz/news/i/women-take-charge-of-your-financial-future-with-amana-bank-s-annisaa-account-1448

KAMPUNI YA JUBILEE HOLDING YAPONGEZWA KWA HUDUMA ZA BIMA NCHINI
05/01/2023

KAMPUNI YA JUBILEE HOLDING YAPONGEZWA KWA HUDUMA ZA BIMA NCHINI

Ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa taifa darasa la nne umeshuka kwa asilimia 3.35 kutoka 86.30 mwaka 2021 hadi asilim...
04/01/2023

Ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa taifa darasa la nne umeshuka kwa asilimia 3.35 kutoka 86.30 mwaka 2021 hadi asilimia 82.95.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa leo Jumatano, Januari 4, 2023, Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), jumla ya wanafunzi 1,320,700 kati ya 1,592,235 wenye matokeo sawa na asilimia 82.95 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B, C na D.

https://youtu.be/Xgnapv6zMM8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia tukio la kuanza...
22/12/2022

https://youtu.be/Xgnapv6zMM8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia tukio la kuanza kujaza maji Kwenye Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji, Mkoani Pwani leo tarehe 22 Desemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia tukio la kuanza kujaza maji Kwenye Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere lilil...

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza kufunga mauzo ya hati fungani yake iliyofahamika k**a NBC Twiga Bond kwa maf...
15/12/2022

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza kufunga mauzo ya hati fungani yake iliyofahamika k**a NBC Twiga Bond kwa mafanikio makubwa ambapo benki hiyo imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh Bil 38.9 ikilinganishwa na sh bil 30 zilizotarajiwa kukusanywa hapo awali. Mafanikio hayo ni asilimia 130 ya malengo yaliyotarajiwa..

Akizungumza kwenye hafla fupi ya utangazaji wa matokeo ya mauzo ya hati fungani hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta fedha nchini wakiwemo wawakilishi kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru alisema dhamana hiyo ya mwezi mmoja ilifungwa rasmi Disemba 7 mwaka huu kwa mafanikio makubwa ikilinganishwa na matarajio ya benki hiyo.

“Awali lengo letu lilikuwa ni kukusanya takribani kiasi cha bilioni 30 na tumefunga hati fungani hii tukiwa tumefanikiwa kukusanya kiasi cha sh Bil 38.9 ambayo ni sawa na asilimia 130 ya malengo yetu ya awali. Kiasi kilichopatakana kimetoka kwa wawekezaji takribani 661 kutoka sekta mbalimba ikiwemo wawezekazi binafsi wakubwa kwa Watoto chini ya usimamizi wa wazazi ,taasisi na mashirika mbalimbali kutoka kila kona ya nchi,’’ alibainisha Bw Ndunguru.

Kwa mujibu wa Bw Ndunguru, hiyo ni mara ya kwanza kwa Benki kutoa hati fungani kwa ajili ya umma na ikiwalenga Wajasiriamali, wakulima na wafanyabiashara wadogo ambao ndio sehemu kubwa ya ajira za vijana nchini Tanzania.

“Wawekezaji katika Hati fungani ya NBC Twiga Bond watapata riba kubwa ya 10% kwa mwaka, inayolipwa nusu mwaka katika kipindi chote cha miaka mitano hadi Novemba 2027. Kiwango cha riba kinacholipwa hakina punguzo la kodi.’’ Alisema.

NMB Bank Plc Imezindua suluhisho la kisasa ‘NMB Pesa Akaunti’ ambayo ni akaunti Ya kidijitali inayomwezesha mteja kufung...
14/12/2022

NMB Bank Plc Imezindua suluhisho la kisasa ‘NMB Pesa Akaunti’ ambayo ni akaunti Ya kidijitali inayomwezesha mteja kufungua na kuanza kuitumia ndani ya dakika mbili tu, imezinduliwa leo stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Magufuli Bus Terminal.

Hatua hiyo kubwa inaongeza msukumo mpya katika jitihada za taifa za ujumuishwaji wa kifedha na upatikanaji wa huduma za fedha kidijitali kiurahisi.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw Filbert Mponzi, sifa kubwa ya suluhisho la NMB Pesa Akaunti ni kuwa na mchakato mfupi wa kufungua akaunti mpya.

“Hii ni suluhisho yakusaidia kutatua changamoto za kifedha ambayo si tu ni akaunti inafunguliwa hapo hapo mteja alipo lakini pia utaweza kupata mikopo isiyo na dhamana, kutoa, kuweka au kutuma fedha, kulipia bili mbalimbali na kubwa zaidi haina gharama za ada za mwezi,” Bw Mponzi alisema.

Benki ya NMB Imezindua suluhisho la kisasa ‘NMB Pesa Akaunti’ ambayo ni akaunti Ya kidijitali inayomwezesha mteja kufungua na kuanza kuitumia ndani ya dakika...

'KIPINDI MAALUM NA MKURUGENZI MKUU EPZA' MATOKEO YA UTENGAJI MAENEO YA UWEKEZAJIhttps://youtu.be/0s20Fcb_O_4 Tanzania Ex...
13/12/2022

'KIPINDI MAALUM NA MKURUGENZI MKUU EPZA' MATOKEO YA UTENGAJI MAENEO YA UWEKEZAJI
https://youtu.be/0s20Fcb_O_4 Tanzania Export Processing Zone Authority - EPZA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutenga kiasi...
09/12/2022

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutenga kiasi cha dola za Marekani bilioni 1 zitakazotolewa kwa njia ya mkopo nafuu kwa Tanzania kupitia Mfuko wa Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF), kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi miaka mitano

“Septemba mwaka 2022, Tanzania na Korea tulisaini makubaliano yatakayoiwezesha Tanzania kupata mkopo wenye riba nafuu wenye thamani ya dola za Marekani bilioni moja ambapo Tanzania itakopa mkopo huo kwa riba ya asilimia 0.01 kwa mwaka na kuulipa kwa kipindi miaka 40 ambacho kimeambatana na kipindi cha neema cha miaka 15.” alisema Dkt. Nchemba

Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang aliahidi kuwa mradi wa kuboresha usambazaji maji na mazingira wa Iringa uamuzi wake wa kuutekeleza utafanyika mwishoni mwa mwaka huu na utekelezaji utaanza mara moja ilihali mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar, taratibu za kitaalam zitakamilishwa ndani ya miezi sita ili utekelezwe.

Tufuatilie kupitia
#
#



  kila la kheri katika siku hii ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru tangu kuupata uhuru 9 Disemba 1961.
09/12/2022

kila la kheri katika siku hii ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru tangu kuupata uhuru 9 Disemba 1961.

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imeweka mkakati wa kuchochea wafanyabiashara kulipa kodi, ili kuongeza mapato ya serikal...
06/12/2022

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imeweka mkakati wa kuchochea wafanyabiashara kulipa kodi, ili kuongeza mapato ya serikali kwa kuweka mabango kwenye maeneo mbalimbali ya wazi yenye kuonesha ujumbe mbalimbali wa kodi, ikiwemo kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki za kutoa risiti (EFD).

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu wakati wa uzinduzi wa mabango hayo yanayoelekeza kutoa na kudai risiti za EFD, katika eneo la kibiashara la Kariakoo.

Amesema mkakati wa pili wa TRA ni kuwasajili wamachinga wote waliopo katika eneo la biashara Kariakoo, ikiwa ni pamoja na kununua mashine za kielektroniki za kutoa risiti.

Aidha amesema mkakati huo ni kwa ajili ya kuboresha usimamizi wa kodi katika eneo hilo, ambalo ndio kitovu kikuu cha biashara nchini.

Amesema kazi ya kusajili wamachinga hao inaendelea nampaka sasa wemeshasajiliwa wafanyabiashara wadogo wapatao 5, 273 ndani ya Mkoa wa Kariakoo.

Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya kibenki ya kidijitali inayoitwa “Funga Mwaka Kibabe na NBC Bank" ikiwa ni ka...
06/12/2022

Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya kibenki ya kidijitali inayoitwa “Funga Mwaka Kibabe na NBC Bank" ikiwa ni katika juhudi za kukuza miamala na malipo ya bila kutumia fedha taslimu nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias, amesema kampeni hiyo mpya inalenga kuhakikisha wateja wanaweza kupata pesa zao kwa usalama na kufanya miamala kwa urahisi, kuongeza urahisi zaidi wa huduma na kuboresha uzoefu kwa wateja.

“Tunataka kuwapa wateja wetu muda wa kutosha kwa ajili ya familia na wapendwa wetu katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwahakikishia kwamba wanaweza kufanya miamala yote ya benki wakiwa katika hali ya starehe wakiwa majumbani mwao.

“Tunaelewa kuwa wengi watakuwa likizoni na pengine kujiingiza katika matembezi mengi ya matumizi katika wakati huu. Benki ya NBC imehakikisha kuwa unaweza kufanya miamala kwa urahisi na kwa ufanisi ukiwa nyumbani huku ukipata nafasi ya kujishindia zawadi,” ameongeza Ulrik.

EPZA'S CONTRIBUTION TO THE GROWTH OF BUSINESS SECTOR.
02/12/2022

EPZA'S CONTRIBUTION TO THE GROWTH OF BUSINESS SECTOR.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa kwanza wa uandaaji wa hesabu kwa mwaka 2021 katika kundi la Taasisi...
01/12/2022

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa kwanza wa uandaaji wa hesabu kwa mwaka 2021 katika kundi la Taasisi za Umma.

Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) jijini Dar es Salaam.

Serikali imetaka NBAA kurahisisha utoaji huduma kwa njia ya kidijitali.
30/11/2022

Serikali imetaka NBAA kurahisisha utoaji huduma kwa njia ya kidijitali.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Biz TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Category


Other TV Channels in Dar es Salaam

Show All