23/04/2020
*CANDY DANIELA 03*
Mtunzi:Suleymani Ally
Insta@golden_de_lacorte
Page:Story za suley
Group:Uwanja wa simulizi za suley
Whatsapp:0652479233
..................................
"Candy Daniela binti mrembo asiepnda majivuno wala kujikweza kwa mtu,jina lake limekua maarufu sana kwenye vinywa vya watu kila kukicha hakuna siku iyendayo kwa Mungu basi asizungumziwe binti huyu....kitendo ambacho kimekuwa kero kwa wanandoa wengi hususani wanawake wenzie,hivyo chuki na vinyongo vilizidi juu yake lakini ukija upande wa wanaume kila mtu alihitaji kua nae kimahusiano..lakini walipo jaribu kutupa karata zao mara zote waliambulia patupu kwani ni binti mwenye msimamo mkali mno..hakuwa na tamaa ya fedha k**a walivyokua wanawake wengine waliokosa akili kichwani mwao na kutumia miili yao k**a chanzo cha kipato na fimbo kwa wanyonge...mara zote yeye wasichana wenzie wa namna ile alikua akiwaona ni mataira kwani wameweka mbele tamaa kuliko utu wao..viongozi wa dini wazee kwa vijana matajiri kwa masikini wote walikua wakilitamani penzi la Candy mwana wa Daniela.
Rangi yake ya maji ya kunde,uso wake ulikua mpana kidogo ulikua hauna hata chembe ya kipele wala chunusi,urembo wake ulikua wa asili,shepu yake ya umbo namba nane vijana wengi wa mjini hupenda kusema uzuri wa nyumba choo,basi kwa Candy sio choo cha nje ni self-contained,k**a TV basi ni Hitachi ya chogo wala sio flat screen,pua yake ilichongoka kidogo mithiri ya mshumaa..macho yake yalikua makubwa ya mviringo,akikutizama utaweza sema anakurembulia kumbe ndio yalivyo..nyusi zake zilikua nyingi na kumkaa vizuri machoni na kuzidi kuupendezesha uso wake zaidi...(LAKINI JE NANI ATAFANIKIWA KUMPATA BINTI HUYU SONGA MBELE NAMI MTUNZI WAKO SULEYMANI ALLY) ..................................
Jonathan alichukua pesa yake na kupingia mkono gari aina ya kosta ya abiria waendao mjini,kisha akalipia nauli yake na kuzidi kusonga mbele na safari yake..huku baadhi ya abiria wenzie aliokua nayo kwenye gari ya kwanza wao walirudi hawakutaka kuendelea na safari kwani nyoyo zao zilijawa na hofu,lakini si kwa Jonathan kijana mdogo aliejawa na ujasiri na maneno ya hekima ndani yake,mtu ambae asiekubali kukata tamaa kiurahisi..hakuna kazi inayomjia mbele yake yeye akachagua bali huifanya ilimradi mkono wake uweze kwenda kinywani.
Wakati yupo njiani alikua na mawazo tele kumuhusu Mama yake kule alipomuacha,huku moyo wake ukijawa na shauku ya kutaka kufika mjini haraka alitama angepewa angalau mabawa awe na uwezo wa kurandaranda angani angalau apaone huko mjini palivyo..
Haikuchukua muda mrefu sana walianza kukutana na vibao vya kuwakaribisha mjini,Jonathan alifurahi sana alitoa simu yake na kumtumia ujumbe rafiki yake ambae atakuja kumpokea wakaishi wote,Alfredy aliupata ujumbe ule wa Jonathan alimjibu poa nakuja...alibadilisha nguo na kuelekea kituo cha mabasi ili kumsubiri aweze kufika.
*usikose no.4*