“Watawala wanatumia vitisho ili kuendelea kupata Madaraka,wanategemea sana vyombo vya usalama”.
Sheikh Ponda Issa Ponda katika mahojiano na Haki Tv kuhusu kukamatwa na kuteswa kwa viongozi wa CHADEMA. @chadema_in_blood @chadematzofficial
Cc @humanrightstz
“Jeshi la Polisi lisikubali kutumiwa na chama kimoja cha siasa, maana tatizo hapa linakuja Watawala wanalitumia Jeshi la Polisi wao wanatoa maagizo, sasa yale maagizo ya wanasiasa hayawi maagizo ya kisheria wala sio maagizo ya kitalaam wale wanaagiza tu hawa wafanyeni hivi, wafanyeni hivi.
Sasa inatakiwa jeshi lisitumiwe na wasiasa maana likitumiwa na wanasiasa inaleta matatizo maana wao wanalinda maslahi yao”.
Sheikh Ponda Issa Ponda katika Mahojiano na Haki Tv kuhusu kukamatwa na kuteswa kwa Viongozi wa CHADEMA @chadema_in_blood @chadematzofficial .
Cc @humanrightstz
“Matukio mengi ya Utekwaji yametokea na hakuna kauli ya kiongozi wa juu ametoka kusema hii ni mbaya sana”.
Sheikh Ponda Issa Ponda katika mahojiano na Haki TV kuhusu Utekaji wa viongozi na wafuasi wa CHADEMA tunapoelekea Uchaguzi 2024-2025.
“Haturidhishwi na kasi ya ufutiliaji wa matukio ya kutekwa, kupotea na kuuwawa kwa watoto yanayoendelea katika nchi yetu. Uchunguzi wa matukio haya upews kipaumbele na umma upewe taarifa sahihi na kwa wakati”.
Mdau akisoma tamko la kulaani mauaji ya watoto nchini Tanzania.
Getrude Dyabene Afisa Mwandamizi Dawati la jinsia LHRC na Wadau wengine wa haki za watoto katika tamko la kulaani vitendo vya ukatili na mauaji ya watoto vinavyoendelea nchini Tanzania.
“Bajeti bado haijapitishwa na toka jumapili walikuwa wanachukua maoni ya wadau na sisi tulitoa maoni jumatatu, sasa kama walikuwa wanachukua maoni kwa ajili ya kuboresha tunashukuru, lakini kama walikuwa wanachukua kwa ajili ya kutimiza wajibu wa kuchukua maoni ya wadau tutakuwa tumesikitika sana, lakini jukumu letu pia kuiambia serikali kwamba tunaona kinachofanyika na tuna maoni yetu”.
Wakili Fulgence Massawe-Kaimu Mkurugenzi LHRC akiongea na Waandishi wa habaro hii leo akitoa maoni ya LHRC kuhusu Bajeti ya Serikali 2024/2025.
“Sisi rai yetu kwa serikali ni kupunguza ukubwa wa matumizi yasiyokuwa yalazima, matumizi ya kawaida sasa kwenye matumizi ya kawaida kuna matumizi ya stahiki za watumishi kwa mfano mshahara na mambo mengine, lakini kuna yale matumizi ambayo ni ya anasa mfano, tunaweza kurudi nyuma kipindi cha Waziri Mkuu Pinda, walipitisha azimio bungeni kwamba ni aina gari yha magari yatatumika na serikali, wakakubaliana yatatumika magari madogo nay ha bei rahisi,
lakini magari yote yanatumika sasa hivi ni ya kifahari na ya bei kubwa na kuyaduhumia ni gharama, mfano ingekuwa rahisi sana kwa serikali kama mtumishi anastahili kupewa gari akopeshwe gari ambalo anaweza kulipa kwa mshahara wake, ina maana hilo gari atalitumia kwenye utumishi na atawekewa mafuta na serikali, akimaliza muda wake ataondoka na gari yake, matokeo ya kununua haya magari ya kifahari ni mzigo kwa serikali”.
Fulgence Massawe Mkurugenzi Mtendaji LHRC
“Deni la Taifa limekuwa ni changamoto sio kwa Tanzania tu hata kwa nchi jirani na kinachopelekea migomo huko Kenya ni deni la Taifa limechangia kwa kiasi kikubwa, na nikwambie deni linalolalamikiwa bado litaendelea kukopwa tu, ukiangalia kwenye tamko letu tumejaribu kuonyesha namna gani limekuwa likiongezeka toka mwaka mmoja Kwenda mwaka mwingine sio kiashria kizuri kumbukeni deni linapoongezeka bado litaendelea kulipwa… ina maana tunalipa kidogo tunakopa zaidi kwahiyo kila deni linapokuwa limefikia umri wake linalipwa lakini kwa bahati mbaya tunakopa zaidi”
Fulgence Massawe Kaimu Mkurugenzi Mtendaji LHRC akitoa maoni ya LHRC kuhusu makadirio ya mapendekezo ya Bajeti ya Serikali, 2024/2025.
Katibu Mtejdaji wa Tume ya Haki za Binadamu ma Utawala Bora (CHRAGG) akieleza jukumu la Tume hiyo katika kutekeleza uandaaji wa mpango kazi wa haki za binadamu na biashara nchini Tanzania.
Wakili Getrude Dyabene akitoa Elimu kuhusu Ukatili wa kijinsia
Maoni ya Wadau wa Haki za Binadamu na Biashara kuhusu maandalizi ya mpango kazi wa Haki za Binadamu na Biashara nchini Tanzania.
Joyce Komanya Afisa Programu Mwandamizi Uwajibikaji wa Makampuni-LHRC @humanrightstz akiongelea utekelezaji wa Mpango kazi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania.
Rais Samia asikitishwa na mauaji ya kikatili kwa mtoto mwenye Ualbino aitwaye 'Asimwe'
Salamu za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) katika siku ya mtoto wa Afrika 2024.
Kaulimbiu “Elimu jumuishi kwa watoto: Izingatie Maarifa na Stadi za kazi”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Anna Henga ameonana na aliyekuwa Ngariba wa ukeketaji Wilaya kutoka kijiji cha Masanga kata ya Nyamwale Wilaya ya Tarime Bhoke Ryoba (66) aliyetekeleza ukeketaji kwa mabinti zaidi ya 2,000 kwa miaka kumi aliyofanya kazi hiyo mapaka alipostaafu mwaka
Katika mahojiano na Dkt. Anna Henga Bhoke alisema jamii ya Wakurya wanaheshimu na kuenzi ukeketaji na endapo angeachana na shughuli hiyo mapema angeweza kupoteza maisha.
Amesema alikuwa anafanya hivyo ili kuwasaidia mabinti waweze kuolewa bila shida na kujipatia fedha ambazo zimemsaidia kujenga nyumba mbili na kusomesha watoto.
“Gharama ya kulipia zoezi la ukeketaji ni Sh 10,000 na hiyo ni kwa miaka ya 2008 na kwa wakati huu gharama inafika mpaka Sh 20,000 kwa msimu wa ukeketaji huwa tunakeketa zaidi ya mabinti 200 na wazazi wao lazima walipie fedha na zinagawanywa kwa wazaee wa Mila na Mangariba.
“Nilikuwa sijui kama kukeketa ni kosa kisheria jamii ya huku wanaamini binti asipokeketwa anakuwa hajatimia ndio maana hii mila badoa inaendelea huku kwa kifupi huu ni mradi wa mangariba kujipatia fedha” alisema Bhoke akiwa nyumbani kwake alipohojiwa na Dkt. Anna kuhusiana na harakati hizo.
Wanajamii Tarime wakubaliana ukeketaji uishe
Kufuatia Maadhimisho ya siku ya watu wenye Ualbino Juni 13 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt. Anna Henga amekemea matukio ya ukatili kwa watu wenye ualibino yanayoendelea kujitokeza nchini Tanzania ambayo mengi yanachochewa na imani za kishirikina.
Dkt. Henga @annahenga ameiasa jamii kutafuta mali kwa njia za kihalali na sio kujikita katika kufanya mauaji kwa watu wa kundi hilo ikiwa ni njia mojawapo ya kujipatia utajiri.
“Watu hawa wamekuwa wakipata changamoto kubwa sana za kuuwawa na kukatwa viungo vyao kwa imani za kishirikina lakini mimi naziita imani za kichawi, kwa sababu huwezi kuwa katika dunia ya sayansi na teknolojia alafu unaamini katika ushirikina, tulinganishe nchi zilizoendelea zimeendelea kwa ajili ya kukata viungo? “.
Dkt. Anna Henga Mkurugenzi Mtendaji LHRC.
Leo 13 Juni 2023, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) @humanrightstz kimepinga hoja za Umoja wa Vijana CCM #UVCCM @uvccm_tz za kuufungia mtandao wa X, uliokuwa unaitwa Twitter zamani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt. Anna Henga @annahenga amesema hoja hizo zinarudisha nyuma harakati za kutetea na kupata haki ya taarifa, uhuru wa kujieleza na haki za kidigitali huku akishangazwa na tamko hilo kutolewa na vijana ambao walitakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha haki za kidigitali badala ya kuzipinga.
“Kwanza ningetegemea vijana ndo wawe mstari wa mbele kutetea haki za kidigitali,ila tamko la vijana kusema kwamba mitandao izimwe ni la kushangaza sana”. Dkt. Anna Henga Mkurugenzi Mtendaji LHRC.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) @humanrightstz imemuonya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa kauli zake za udhalilishai kwa Mtumishi wa Longido.
Haki TV imefanya Mahojiano na Wakili Mariam Mageta wa Dawati la familia juu ya ‘Taratibu za malezi na matunzo ya watoto kwa wazazi waliotengana /Wazazi ambao hawako pamoja’.
Tembelea YouTube chaneli ya Haki TV kwa undani wa Mahojiano hayo