Babirousa heroique

Babirousa heroique Kituo cha télévision , na radio ,kwa lengo ya kutoa abari za Dunia, michezo Na burudani .

Scoutisme
22/03/2024

Scoutisme

Pour les scout Salut......
22/03/2024

Pour les scout Salut......

Manchester City ilipokea kipigo cha kwanza cha Ligi ya Premia kutoka kwa Arsenal katika kipindi cha miaka minane siku ya...
09/10/2023

Manchester City ilipokea kipigo cha kwanza cha Ligi ya Premia kutoka kwa Arsenal katika kipindi cha miaka minane siku ya Jumapili na kushuka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo, lakini kiungo Bernardo Silva alisema kupoteza “sio mwisho wa dunia”.
Baada ya mechi iliyopiganwa kwa karibu huko Emirates, mchezaji wa akiba Gabriel Martinelli alifunga bao la dakika za mwisho na kupata ushindi wa 1-0 Arsenal wakisonga mbele kwa pointi 20 na vinara wa ligi Tottenham Hotspur. Champion City ina pointi 18.
City, ambayo imepoteza mechi zake mbili za mwisho za Ligi ya Premia, ilihusika katika mbio kali ya kuwania taji la pande mbili na Arsenal msimu uliopita, ambapo City ilikuwa ikiburuza mkia kabla ya Arsenal kuzembea katika mchujo.
“Tunahitaji kupumzika kiakili na kimwili ili kuwa tayari kwa mechi zinazofuata kwa sababu zitakuwa ngumu, na kuimarika katika maeneo ambayo tunaweza kuimarika k**a msimu uliopita,” Silva alisema katika mahojiano kwenye tovuti ya City.
“Tutajaribu kurejea kwa nguvu kutoka kwa mapumziko ya kimataifa. Sio mwisho wa dunia. Tumekuwa katika nafasi mbaya zaidi.
“Tunahitaji kujaribu kurejea kutoka kwa vipigo hivi viwili mfululizo kwenye Ligi ya Premia na kurejea kileleni ambapo nadhani tunastahili.”
City itarudi uwanjani mnamo Oktoba 21, itakapomenyana na Brighton & Hove Albion,kisha itamenyana na mpinzani wake Manchester United mnamo Oktoba 29.
Meneja Pep Guardiola alitoa wito kwa upande wake kurejea kutokana na kupoteza kwao, akiwaambia waandishi wa habari: “Tuko nyuma, lakini ni Oktoba. Sio mara ya kwanza. Msimu uliopita ilitokea, tulikuwa nyuma zaidi, lakini msimu ni mrefu.

# Uncle A simba Geniu's.
# Uncle A TV online new.

Whozu Akiri Kupewa Hifadhi na Wema SepetuMsanii ambaye pia ni muigizaji Whozu kutoka Tanzania amekiri wazi wazi kwamba a...
09/10/2023

Whozu Akiri Kupewa Hifadhi na Wema Sepetu

Msanii ambaye pia ni muigizaji Whozu kutoka Tanzania amekiri wazi wazi kwamba anakaa kwa mpenzi wake ambaye pia ni muigizaji Wema Sepetu.

Whozu alifuchua haya akiwa jukwaani Iringa wakati wa tamasha linaloendelea la Wasafi.

Akiwa jukwaani, mashabiki walianza tambo za kumuimbia nyimbo wakitaja Wema Sepetu jambo lililomchochea pia kuimba naoi li kupandisha mzuka.

Whozu alimuimbia Wema Sepetu na kusema kwamba yeye ndiye amemuweka nyumbani kwake na wala haoni aibu kusema hivyo.

“Wema huyo, Weeema Wema nakaa kwake eeh, Wema Wema huyo Wema,” Whozu aliimba.

Penzi la Wema na Whozu limeduku kwa Zaidi ya mwaka mmoja huku katikati kukiwa na ukakasi kwamba huenda halitodumu.

Whozu amefichua haya siku chache tu baada ya video ikimuonesha mamake Wema akitimba katika hafla moja kwa fujo na kuonekana kumtuhumu binti yake kwa kuwa na mpenzi – Whozu- bila ya kumtambulisha kwake rasmi k**a mpenzi wake.

Siku ya Alhamisi, wiki jana, Bi Mariam alipokuwa akitoa hotuba yake wakati wa karamu ya bintiye alimkosoa kuhusu uhusiano wake na mwimbaji Whozu akitaja kuwa haukubarikiwa.

Chapisho la Wema Sepetu la Alhamisi jioni linadokeza kuwa tukio la wiki iliyopita lilimuumiza sana muigizaji huyo na kumuacha na majeraha moyoni.

Wema katika mkutano na waandishi wa habari Jumapili jioni, aliahidi kwamba ifikapo Jumatatu saa nne usiku, ataweka wazi kila kitu katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio, kile alichokisema kwamba ni ukakasi wote atakaoutoa.

# Uncle A simba Geniu's
# Uncle A TV online new

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Leo Oktoba 09, 2023 akiwa kwenye ziara yake nchini India ame...
09/10/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Leo Oktoba 09, 2023 akiwa kwenye ziara yake nchini India amezuru kaburi la Hayati Mahatma Gandhi lililopo kwenye Makumbusho ya Mahatma Gandhi Rajghat New Delhi nchini India.
Mahatma Gandhi ambaye ni baba wa Taifa hilo alikuwa mwanasheria, mwanafalsafa, mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa siasa nchini India ,Anajulikana hasa k**a kiongozi wa harakati za uhuru wa India aliyepinga na kushinda Ukoloni kwa njia ya amani bila ya matumizi wa mabavu au silaha, Mahatma Gandhi ambaye alifariki January 30, 1948 akiwa na miaka 79.
Mapema leo Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake nchini humo alimgusia Mahatma Gandhi kuwa wakati wa safari yake ya kwenda nchini Afrika kusini alilala hotel kubwa Zanzibar iiitwayo Tembo House Hotel.

# Uncle A simba Geniu's.
# Uncle A TV online new

Ukanda wa Gaza ni eneo la urefu wa kilomita 41- (maili 25) na upana wa kilomita 10 kati ya Israeli, Misri na Bahari ya M...
08/10/2023

Ukanda wa Gaza ni eneo la urefu wa kilomita 41- (maili 25) na upana wa kilomita 10 kati ya Israeli, Misri na Bahari ya Mediterania.

Ni nyumbani kwa wakazi wapatao milioni 2.3 na lina mojawapo ya msongamano mkubwa zaidi wa watu duniani.

Israel inadhibiti anga juu ya Gaza na ufuo wake wa bahari na imeweka vikwazo vya ni nani na bidhaa gani zinazoruhusiwa kuingia na kutoka kupitia vivuko vya mpaka wake.

Vile vile, Misri inadhibiti wanaopita na kutoka katika mpaka wake na Gaza.

Takriban 80% ya wakazi wa Gaza wanategemea misaada ya kimataifa, kulingana na Umoja wa Mataifa, na takriban watu milioni moja wanategemea chakula cha kila siku.

Kwa nini Israel na Hamas wanapigana?

Kuna mvutano wa mara kwa mara kati ya Israel na Hamas, lakini mashambulizi ya wanamgambo hao siku ya Jumamosi yaliwashangaza wengi

Hamas ilirusha maelfu ya roketi dhidi ya Israel huku makumi ya wapiganaji wakivuka mpaka na kuvamia jamii za Israel, na kuua makumi ya raia huku wengine wakichukuliwa mateka.

Israel ilianzisha mashambulizi ya angani mara moja, ikisema kuwa inalenga maeneo ya wanamgambo huko Gaza.

Je, shambulio hili halina kifani?

K**a Mhariri wetu wa Kimataifa Jeremy Bowen anavyoandika, hii ndiyo operesheni kabambe zaidi ambayo Hamas imewahi kuzindua kutoka Gaza na shambulio baya zaidi la kuvuka mpaka ambalo Israel imekabiliana nalo katika zaidi ya kizazi kimoja.

Wanamgambo walivuka waya unaotenganisha Gaza na Israel katika maeneo mengi.

Shambulio hilo ambalo halijawahi kutokea limekuja siku moja baada ya kumbukumbu ya miaka 50 ya shambulio la kushtukiza la Misri na Syria mnamo 1973 ambalo lilianzisha vita vikuu vya Mashariki ya Kati.

Umuhimu wa tarehe hiyo hautasahaulika kwa uongozi wa Hamas.

Je, Ujasusi wa Israel ulizembea?

Ndiyo, anasema mwandishi wetu wa usalama Frank Gardner.

Kwa juhudi za pamoja za Shin Bet, ujasusi wa ndani wa Israeli, Mossad, wakala wake wa kijasusi wa nje na mali zote za Jeshi la Ulinzi la Israeli, anasema inashangaza ukweli kwamba ha

Orodha ya nyota wa Afrika wanaolipwa hela ndefu kwa wiki☆☆☆☆☆☆👇👇👇👇👇👇👇1. Sadio Mane 🇸🇳 - £661,0002. Riyad Mahrez 🇩🇿 - £48...
06/08/2023

Orodha ya nyota wa Afrika wanaolipwa hela ndefu kwa wiki☆☆☆☆☆☆👇👇👇👇👇👇👇

1. Sadio Mane 🇸🇳 - £661,000

2. Riyad Mahrez 🇩🇿 - £481,000

3. Kalidou Koulibaly 🇸🇳 - £412,000

4. Mohamed Salah 🇪🇬 - £350,000

5. Edouard Mendy 🇸🇳 - £227,000

6. Thomas Partey 🇬🇭 - £200,000

7. Achraf Hakimi 🇲🇦 - £176,000

8. Nicolas Pepe 🇨🇮 - £140,000

9. Andre Onana 🇨🇲 - £115,000

By: Uncle A simba Geniu's.

MWANA MZIKI WA BONGO FLEVA MAUWA SAMA KAJA NA NDOGO KWA ZUCHU ☆👇👇👇👇👇👇👇.Japo hajamtaja jina lakini kwa asilimia kubwa ina...
06/08/2023

MWANA MZIKI WA BONGO FLEVA MAUWA SAMA KAJA NA NDOGO KWA ZUCHU ☆👇👇👇👇👇👇👇.

Japo hajamtaja jina lakini kwa asilimia kubwa inaonesha wazi, msanii wa Bongo Fleva Maua Sama ametupia kijembe mrembo kutoka WCB, Zuhura Othman 'Zuchu'.
Hiyo inajidhihirisha kufuatia kauli yake aliyoiposti kenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika hivi:

"Maisha haya! Maroboti yameanza kuoneana Wivu."

Mwishoni alimalizia kwa kuweka viemoji vya kucheka. Kwa nini inaonesha amemlenga Zuchu? Jana kwenye ukurasa wake wa Instagram kipengele cha Insta Story, Zuchu aliweka stori kuwa anawashangaa wasanii wanaonunua views.
Bila shaka alimlenga Zuchu maana ndiye aliyeonesha kuwashangaa wasanii wanaonunua views kupitia maroboti ya YouTube.

by: Uncle A simba Geniu's

MWINJAKU ANA MJIA JUU  RAYVANNY ☆👇👇👇👇👇👇👇👇.Baada ya Show alioifanya Staa wa Muziki  huko Albania, Hichi ndicho alichokian...
06/08/2023

MWINJAKU ANA MJIA JUU RAYVANNY ☆👇👇👇👇👇👇👇👇.

Baada ya Show alioifanya Staa wa Muziki huko Albania, Hichi ndicho alichokiandika Dc wa Instagram ...

" wewe ni mkubwa sasa achana na kujikomba komba kwa MWAMBINO (Diamond) HAKUWEZI wala hato kusaidia kitu.

Hizi level hajawahi kufika , kwenye nchi za watu umeisimamisha NEMBO na BENDERA ya TANZANIA . Umemuacha mbali MBALI SAAAANA.
Tangaza kambi ya UPINZANIA RASMIII UIOKOE BONGO FLEVA k**a anavo fanya MFALME kwa sasa."

By: Uncle A simba Geniu's

KIONGOZI WA UPIZANI KENYA☆☆☆☆☆👇👇👇👇👇👇.Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametoa uamuzi wake kwa serikali, Jum...
06/08/2023

KIONGOZI WA UPIZANI KENYA☆☆☆☆☆👇👇👇👇👇👇.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametoa uamuzi wake kwa serikali, Jumamosi, juu ya mazungumzo ya kumaliza mgogoro unaokumba Kenya kuhusiana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Bwana Odinga alisisitiza umuhimu wa kufanya mazungumzo hayo bila masharati lakini pia akatoa onyo juu ya kushindwa kufanyika kwa mazungumzo hayo.

‘’Kushindwa kufikia makubaliano hadi Agosti 31, kutamaanisha kufanyika kwa maandamano zaidi’’, Raila alisema.

Bwana Odinga aliongeza kuwa wao k**a wana Azimio wako tayari kuzungumza na wamewapa wenzao wa muungano wa Kenya Kwanza siku 30 kufanikisha mazungumzo hayo na ikiwa hayatakuwa yamefanyika kufikia wakati huo, atatoa amri nyingine.

Bwana Odinga alikubali mazungumza ya pande mbili yenye kujumuisha watu 5 kutoka kila upande huku upinzani ukiongozwa na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na serikali ikiongozwa na kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wah katika kikao ambacho kitaongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo.

Jumanne, 25 Julai, Rais William Ruto alisema yuko tayari kukutana ana kwa ana kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ‘’wakati wowote’’.

By: Uncle A simba Geniu's

UFARANSA YATOWA AHADI KWA NIGER☆☆☆👇👇👇👇👇👇👇.Ufaransa ilisema Jumamosi itaunga mkono juhudi za kurejesha uongozi wa kiraia ...
06/08/2023

UFARANSA YATOWA AHADI KWA NIGER☆☆☆👇👇👇👇👇👇👇.

Ufaransa ilisema Jumamosi itaunga mkono juhudi za kurejesha uongozi wa kiraia nchini Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi, siku moja baada ya jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kusema kuwa una mpango wa kuingilia kijeshi.

Mapinduzi ya kijeshi ya Niger, ambayo ni ya saba katika Afrika Magharibi na Kati katika kipindi cha miaka mitatu, yametikisa eneo la Sahel magharibi, Niger ikiwa mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani yenye umuhimu wa kimkakati kwa mataifa yenye nguvu duniani.

Wakuu wa Ulinzi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wananuia kuchukua hatua za kijeshi ikiwa viongozi wa mapinduzi hawatamrejesha madarakani Rais aliyechaguliwa Mohamed Bazoum ifikapo Jumapili, na hivyo kuzua hali ya mzozo zaidi katika eneo ambalo tayari linapigana na uasi wa wapiganaji wa Kiislamu.

Kiongozi wa mapinduzi mwenye umri wa miaka 59, Jenerali Abdourahamane Tiani, ambaye alipata baadhi ya mafunzo yake ya kijeshi nchini Ufaransa, alisema jeshi halitarudi nyuma.

"Ufaransa inaunga mkono kwa uthabiti na azma juhudi za ECOWAS kushinda jaribio hili la mapinduzi," wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema katika taarifa yake baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Catherine Colonna kukutana na Waziri Mkuu wa Niger Ouhoumoudou Mahamadou mjini Paris.

By: Uncle A simba Geniu's

Bomu la angani lililoongozwa na Urusi limeshambulia kituo cha damu kaskazini-mashariki mwa Ukraine, na kuua na kujeruhi ...
06/08/2023

Bomu la angani lililoongozwa na Urusi limeshambulia kituo cha damu kaskazini-mashariki mwa Ukraine, na kuua na kujeruhi raia, rais wa Ukraine amesema.

Volodymyr Zelensky amesema waokoaji sasa wanajaribu kukabiliana na moto baada ya shambulio hilo lililotokea eneo la Kupiansk katika mkoa wa Kharkiv Jumamosi usiku.

Urusi hadi sasa haijatoa maoni yoyote hadharani kuhusu shambulio hilo lililoripotiwa.

"Kushinda magaidi ni jambo la heshima kwa kila mtu anayethamini maisha," aliongeza.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, Bw Zelensky aliwataja wahalifu hao k**a "wanyama" ambao walikuwa wakitafuta "kuharibu kila kitu kinachoruhusu uhai".

"Uhalifu huu wa kivita pekee unasema kila kitu kuhusu uvamizi wa Urusi," alisema.

Hakusema ni watu wangapi wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Hata hivyo, BBC haijaweza kuthibitisha ripoti hiyo mara moja.

Hapo awali Urusi ilikanusha madai yote ya uhalifu wa kivita au kuwalenga raia.

Mji wa Kupiansk na makazi ya karibu yalitekwa na wanajeshi wa Urusi katika siku chache za kwanza za uvamizi wake nchini Ukraine, uliozinduliwa mnamo Februari 2022.

Eneo hilo lilikombolewa wakati wa shambulio la kushtukiza la Ukraine lililofanyika Septemba iliyopita.

Rais Zelensky pia alisema kuwa siku ya Jumamosi Urusi ilifanya shambulio jingine la kombora, ikilenga kampuni ya masuala ya angani inayoendeshwa na kundi la Motor Sich katika mkoa wa Khmelnytskyi magharibi.

Mashambulizi ya Urusi yanafanyika baada ya Moscow kuishutumu Ukraine kwa kuishambulia meli ya mafuta ya Urusi iliyokuwa na wafanyakazi 11 katika Bahari Nyeusi - shambulio la pili la ndege zisizo na rubani ndani ya siku nyingi.

Maafisa wa baharini wa Urusi walisema chumba cha injini ya meli ya mafuta ya Sig kiliharibiwa katika shambulio hilo kwenye Mlango Bahari wa Kerch na hakuna aliyejeruiwa.

By: Uncle A simba Geniu's

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema Ijumaa kuwa imelazimika kufunga ofisi yake nchini Uganda na kwamba...
06/08/2023

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema Ijumaa kuwa imelazimika kufunga ofisi yake nchini Uganda na kwamba itasitisha rasmi shughuli zake nchini humo Jumamosi.

Katika taarifa yake ya kutangaza kufungwa, Volker Turk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu alisema, "Ninasikitika kwamba ofisi yetu nchini Uganda ililazimika kufungwa baada ya miaka 18, ambapo tuliweza kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya kiraia, na watu wa tabaka mbalimbali nchini Uganda, pamoja na kushirikiana na taasisi za serikali kwa ajili ya kukuza na kulinda haki za binadamu za Waganda wote.”

Msemaji wa kamishna mkuu, Ravina Sham-dasani, aliiambia VOA kwamba serikali iliifahamisha Turk mwezi Februari kwamba haitasaini upya mkataba wa nchi mwenyeji, ambao unaruhusu ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kufanya kazi nchini humo.

"Kwa maoni yao, Uganda ilikuwa na uwezo wake wa kusimamia hali ya haki za binadamu ambapo ofisi ya haki za binadamu haikuhitajika tena," alisema.

"Sisi, bila shaka, tunajutia sana uamuzi huu. Tumekuwa nchini Uganda kwa miaka 18…na tumejaribu kutumika k**a daraja kati ya serikali na mashirika ya kiraia.”

Sauti ya Amerika ilijaribu kuwasiliana na ujumbe wa Uganda mjini Geneva, Uswizi, lakini haikupata maoni yoyote kuhusu kwa nini serikali iliamua kuliondoa shirika la Umoja wa Mataifa nchini humo.

By: Uncle A simba Geniu's

Ngolo Kante ni mchezaji ambaye Hupendwa sana karibia na kila mwanasoka  au shabiki wa mpira wa miguu Duniani. Leo nitaon...
21/07/2023

Ngolo Kante ni mchezaji ambaye Hupendwa sana karibia na kila mwanasoka au shabiki wa mpira wa miguu Duniani.

Leo nitaongelea maisha ya Kante kabla hajajiunga na soka la kulipwa Duniani ✍🏻✍🏻✍🏻
KANTE!KANTE!KANTE!
Naamu file lake hili hapa naomba twende kwa pamoja kujua maisha ya start huyu Ngolo Kante yalianzaje✍🏻✍🏻✍🏻
👉Wazazi wa Kante walihamia nchi ya Ufaransa wakitokea nchi ya Mali. Walikuwa ni watu wa familia duni sana.
👉Wazazi wa Kante walikuwa ni ombaomba kwenye jiji lao na Kante alikuwa ni mwanao wa kwanza. Kitu ambacho hakikumoendeza Kante akaamua kuanza biasha ya kuokota mokopo kwenye jiji lao akizunguka zaidi ya kilometa 20 kwa siku ili ajipatie makopo yakwenda kuuza. Japo biashara hiyo haikuwa na msaada sana kwa familia yao kutokana na fedha kidogo alizopata.
👉Akiwa na umri wa miaka saba alipelekwa shule na shukeni alipenda kucheza mchezo wa Rugby.
👉Mwaka 1998 kombe la dunia lilichezwa nchini Ufaransa ambapo Kante hakuweza kushuhudia mchezo hata mmoja. Ila alikuwa akisikia majina ya wachezaji wakubwa wakitajwa kwenye mashindano hayo ambapo aligundua kuwa majina mengi makubwa yalikuwa ya wachezaji kutoka Afrika k**a yeye. Hii ilimpa faraja sana na akawwmbia wenzake wanookota naye makopo kuwa anandoto siku moja aje kuwa k**a hao japo wenzake walimcheka nakumwona kichaa.
👉 Kipindi hicho cha kombe la dunia biashara yake ilipamba moto sana kutokana na nje ya viwanja aliweza kujiokotea makopo mengi. Japo fedha aliyopata haikuwasaidia sana kimaisha na yeye aliweza pia kujilipia ada ya shule.
👉Kombe la dunia lilipoisha hali ikaanza kuwa ngumu tena akashindwa kujilipia ada ya shule akaamua kuacha shule.
👉 Akiwa na miaka 8 Kante alijiunga na club ndogo ya mpira iliyokuwa mtaani kwake iliyokuwa inaitwa JS Suresness Akiwa anacheza na wachezaji wenzake walimdharau kwa kuwa kimo chake kilikuwa ni kidogo.
👉Ilimlazimu kocha wa club hiyo kumpa dk 10 za mwishoni alikuwa anacheza k**a kichaa ndani ya dk zile kumi na mwalimu wake alihofia ataumia ila kante a

ZARI THE BOSS LADY ☆☆☆👇👇👇👇👇👇.Mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Uganda  amewatolea uvivu watu wanaosema anatoka kimape...
26/06/2023

ZARI THE BOSS LADY ☆☆☆👇👇👇👇👇👇.

Mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Uganda amewatolea uvivu watu wanaosema anatoka kimapenzi na mwanaume mwenye umri sawa na mtoto wake,ni baada ya passport zao kuvujishwa na promoter siku ya jana.

Passport hizo zinaonyesha Zari amezaliwa 1978 huku mumewe akizaliwa 1992, amedai kuwa yeye kazaliwa 1980 na sio 1978 k**a passport inavyosema huku akisema kwenye passport watu wanaweka miaka tu kwa sababu fulani.

Zari Hassan amedai passport yake na mumewe zimevujishwa na promoter ambae aliandaa party ya all Zari white party London baada ya kushindwa kuelewana.

By: Uncle A simba Geniu's

SUDAN ☆👇👇👇👇👇👇.Operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji inaendelea katikati mwa Atlantiki baada ya manowari ya watalii ku...
20/06/2023

SUDAN ☆👇👇👇👇👇👇.

Operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji inaendelea katikati mwa Atlantiki baada ya manowari ya watalii kutoweka wakati wa kupiga mbizi kwenye eneo la ajali ya Titanic siku ya Jumapili.

Mawasiliana na manowari hiyo ndogo yalipotea k**a saa moja na dakika 45 baada ya kupiga mbizi, walinzi wa Pwani wa Marekani walisema. Kampuni ya watalii ya OceanGate ilisema njia zote zilikuwa zikichunguzwa ili kuwaokoa watu watano waliokuwemo ndani.

Tikiti zinagharimu dola 250,000 (£195,000) kwa safari ya siku nane ikijumuisha kupiga mbizi kwenye eneo la ajali ya meli ya Titanic yenye kina cha 3,800m (12,500ft).

mabadiliko ya serikali, wanamaji wa Marekani na Canada na biashara ya kibiashara ya kina kirefu ya bahari yanasaidia shughuli ya uokoaji, mamlaka walisema.

Ajali ya Titanic iko umbali wa maili 435 (700km) kusini mwa St John's, Newfoundland, ingawa kazi ya uokoaji inaendeshwa kutoka Boston, Massachusetts.

Meli iliyotoweka inaaminika kuwa ya OceanGate ya chini ya maji ya Titan, ndogo kwa ukubwa wa lori ambayo huchukua watu watano na kawaida hupiga mbizi na dharura kwa siku nne ikiwa na oksijeni.

Siku ya Jumatatu alasiri, afisa wa kijeshi John Mauger wa Walinzi Pwani ya Marekani aliambia mkutano mkuu wa habari: "Tunatarajia kuna mahali kati ya saa 70 na 96 zinazopatikana kwa wakati huu."

Hamish Harding, mfanyabiashara bilionea wa Uingereza na mlelezi mwenye umri wa miaka 58, ni miongoni mwa wale waliokuwa kwenye manowari iliyotoweka, familia yake ilisema. Katika mtandao wa maisha maisha mwa juma,

Bw Harding alisema "anajivunia kutangaza" kwamba atakuwa ndani ya eneo la ajali ya Titanic - lakini akaongeza kuwa kwa sababu ya "baridi mbaya zaidi huko Newfoundland katika miaka 40, siku hii inaweza kuwa ujumbe wa kwanza na wa pekee kwa Titanic mnamo 2023" .

By: Uncle A simba Geniu's

Serikali ya Somalia imesema kwamba wanamgambo 43 wa al-Shabab, wakiwemo mak**anda wawili waandamizi, waliuawa na vikosi ...
20/06/2023

Serikali ya Somalia imesema kwamba wanamgambo 43 wa al-Shabab, wakiwemo mak**anda wawili waandamizi, waliuawa na vikosi vya Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA) wakati wa shambulio la anga la mwishoni mwa wiki, takriban kilomita 14 kutoka Wilaya ya Jamame katika eneo la Lower Jubba.

Serikali ya Somalia imesema kwamba wanamgambo 43 wa al-Shabab, wakiwemo mak**anda wawili waandamizi, waliuawa na vikosi vya Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA) wakati wa shambulio la anga la mwishoni mwa wiki, takriban kilomita 14 kutoka Wilaya ya Jamame katika eneo la Lower Jubba.

"Shambulio hilo la anga lilifanikiwa kuwaangamiza viongozi wakuu wa al-Shabab Aden Abdirahman Aden na Idris Abdirahim Nur, ambaye alikuwa na asili ya Kenya, na jumla ya wapiganaji 43 wa Al-Shabab," Shirika la Habari la Kitaifa la Somalia (SONNA) liliripoti Jumatatu.

SONNA ilisema shambulio hilo, lililofanywa na "washirika wa kimataifa wa Somalia," lilifanyika Ijumaa wiki jana wakati wanamgambo na mak**anda wao walikusanyika kupanga mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali katika kambi ya kijeshi ya Barsanguni, ambayo ni nyumbani kwa Jeshi la Taifa la Somalia na vikosi vya ndani. Taarifa hiyo haikutaja mshirika wa kigeni aliyefanya shambulizi hilo la anga, lakini mara nyingi ndege zisizo na rubani za K**andi ya Marekani barani Afrika, hufanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji nchini Somalia.

"Kutatizwa kwa mafanikio yashambulio hilo lililopangwa, kunaonyesha ufanisi wa juhudi zinazoendelea za kupambana na al-Shabaab na kuwalinda watu wa Somalia," taarifa hiyo iliongeza.

Hayo yanajiri wakati ambapo nalo Baraza la Mawaziri la Somalia limemteua Brigedia Jenerali Ibrahim Sheikh Muhyadin Addow k**a k**anda mpya wa Jeshi la Kitaifa la Somalia.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Somalia alisema uteuzi huo unafuatia pendekezo la kumuondoa Jenerali Odawa Yusuf, ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu Machi 2019.

By: Uncle A simba Geniu's

Subira huvuta kheri, ndio pengine methali ambayo wengi wanahisi inamfaa msanii wa muda mrefu ndani ya lebo ya Wasafi WCB...
20/06/2023

Subira huvuta kheri, ndio pengine methali ambayo wengi wanahisi inamfaa msanii wa muda mrefu ndani ya lebo ya Wasafi WCB, Lavalava.

Msanii huyo katika miaka ya hivi karibuni ametoweka machoni pa mashabiki wa muziki, licha ya kujisatiti na kujitahidi kuachia miziki kila mara, lakini miziki yake imekuwa ikiishia kwenye paa za studio za Wasafi tu!

Wengi walimsahau k**a alikuwepo, kiasi kwamba hata bosi wake Diamond Platnumz kuonekana kumsahau k**a alikuwa msanii mwenye mkataba chini ya lebo yake.

Diamond aliwekeza nguvu zake nyingi katika promo za wasanii Zuchu na Mbosso ambao kwa sasa wanafanay vizuri, lakini kwa muda hakuwahi kuonekana akifanya udhubutu wa kusukuma kazi za Sanaa za Lavalava, k**a ambavyo imekuwa kawaida yake tangu enzi za msanii wake wa kwanza – Harmonize.

Lakini baada ya Lavalava kuachia kibao chake kipya hivi majuzi kinachokwenda kwa jina ‘Tajiri’, bosi wake aliguswa na mapenzi tena, na kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kumpiga promo hatari Lavalava kwa kupakia kionjo cha kibao hicho.

Diamond aliandika kwamba alikipenda kibao hicho na katika masikio yake kilikuwa kinaimba kwa kujiradidi k**a kibwagizo kwenye shairi.

“Kwenye kujirudia rudia na Lavalava,” Diamond aliandika.

Itakumbukwa wiki chache zilizopita baada ya Lavalava kushirikishwa na msanii wa muda mrefu kutoka Kenya, Jaguar kwenye kibao cha ‘Unthinkable’, Jaguar alionekana kukisukuma kibao hicho mwenyewe na kwa kurasa za Lavalava wala halikuonekana tangazo hata moja ya promo.

Jaguar alipoulizwa kwa nini, alisema kuwa bosi wa Lavalava – Diamond Platnumz hakuwa ametoa ruhusa kwa kibao hicho kutolewa na Jaguar alichokifanya ni ukaidi tu, jambo ambalo lilimfungia nje Lavalava kutosukuma kibao chao, kwani kipengele cha mkataba wake hakimruhusu kufanya baadhi ya mambo hayo.

By: Uncle A simba Geniu's

Benki Kuu ya Tanzania imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekez...
20/06/2023

Benki Kuu ya Tanzania imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusia kutumika nchini, hivyo hakuna Mtu au Kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa kwa malipo yoyote halali na kwamba kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya Tanzania ni kuvunja Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.
“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuukumbusha umma kwamba Serikali ilishatoa tamko kuhusu katazo la matumizi ya fedha za kigeni kwa Wakaazi wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma nchini, tamko la kwanza lilitolewa mwezi Agosti 2007 na la pili mwezi Desemba 2017”
“Hata hivyo, katika siku za karibuni imebainika kuwepo kwa ukiukwaji wa tamko hilo, hivyo Benki Kuu inapenda kuukumbusha umma kwamba maagizo yaliyotolewa hapo awali kuhusu matumizi ya fedha za kigeni yanapaswa kuendelea kuzingatiwa kuwa bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania, bei hizi zinajumuisha kodi za kupangisha ardhi, nyumba na ofisi, gharama za elimu, huduma za afya, vifaa tiba na vitendanishi, gharama za usafiri, lojistiki za bandari, vifaa vya kielektroniki na huduma za mitandao ya mawasiliano”
“Bei ambazo walengwa wake Wakuu ni Watalii au Wateja wasio Wakaazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni, bei hizi zinajumuisha gharama za hoteli, usafiri, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa Wageni, usafirishaji kwenda Nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za mizigo bandarini”

By: Uncle A simba Geniu's

Kanya Boya ni bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Burundi. Bondia huyu Felix Kanyaboya kati ya Miaka ya 1986 / 1987 alikuj...
20/06/2023

Kanya Boya ni bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Burundi. Bondia huyu Felix Kanyaboya kati ya Miaka ya 1986 / 1987 alikuja kucheza Tanzania , Alikuwa anafikia Hotel za
Kariakoo.

Bondia huyu alikuwa na Mikwara mingi saana na siku ya Mechi anatoka Hotelini Kariakoo anatembea kwa Miguu akiwa kavalia kabisa Gloves , ring bout, Gum shield, anapiga shadow box njia nzima na watu wanamshangilia mpaka Railways Club Gerezani. Akipanda Ulingoni Round zake 2 tu kapigwa KO mbaya na akina Habibu Kinyogoli, na Omary Yazidu. Ndipo Jina lake likavuma k**a *KANYABOYA* NI KUMBUKUMBU TU Kutoka Maktaba.

By: Uncle A simba Geniu's

Soka ya New Zealand (NZF) ilisema itawasiliana na Fifa kuhusu kuwalinda wachezaji dhidi ya ubaguzi wa rangi baada ya tim...
20/06/2023

Soka ya New Zealand (NZF) ilisema itawasiliana na Fifa kuhusu kuwalinda wachezaji dhidi ya ubaguzi wa rangi baada ya timu ya taifa ya wanaume kuachana na mechi ya kirafiki dhidi ya Qatar wakati wa mapumziko wakipinga shutuma zinazodaiwa kuwa za ubaguzi wa rangi dhidi ya mmoja wa wachezaji wao.
New Zealand ilisema mpinzani wa Qatar alielekeza “matusi makubwa ya ubaguzi wa rangi” kwa Michael Boxall, ambaye ana asili ya wa Kisamoa, timu hiyo ilisema iliripoti tukio hilo na kwa pamoja waliamua kutoingia uwanjani baada ya mapumziko kwa sababu hakuna hatua rasmi zilizochukuliwa.
Ilikuwa moja ya mechi mbili zilizoachwa nchini Austria siku ya Jumatatu baada ya madai ya ubaguzi wa rangi. Chama cha soka cha Ireland kilisema timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 21 imeachana na mchezo wao dhidi ya timu ya Olimpiki ya Kuwait baada ya mchezaji wa Kuwait kutumia lugha ya kibaguzi dhidi ya mchezaji wa akiba wa Ireland.
Mtendaji Mkuu wa NZF, Andrew Pragnell, alisema: “Hakika tunataka kuwasiliana na Fifa juu ya hili. Unajua hivi karibuni wameanzisha kikosi kazi kuhusu ubaguzi wa rangi; zaidi inapaswa kufanywa ili kuwalinda wachezaji dhidi ya mashambulizi ya rangi uwanjani. Kuna imekuwa mageuzi; hatufikirii yanasonga haraka vya kutosha kwa hivyo tunataka kuchangia hilo.”
Kocha wa Qatar, Carlos Queiroz, alisema kikosi chake kilisimama karibu na mwenzao wakati wa tukio hilo na ni suala la viongozi wa soka. “Inaonekana wachezaji wawili walirushiana maneno, na hatujui nani alikuwa wa kwanza, nani alikuwa wa pili; ni kati yao tu,” aliambia Chaneli za Michezo za Alkass. “Wachezaji wa New Zealand waliamua kumuunga mkono mwenzao na pia tuliamua kumuunga mkono mchezaji wetu.”
Video ya mchezo huo wa kirafiki wa New Zealand ilionyesha wachezaji wengi wa All Whites wakigombana na mchezaji wa Qatar muda mfupi baada ya mpira wa adhabu kutolewa.
Baada ya mazungumzo marefu na nahodha wa New Zealand, Joe Bell, mwamuzi, Manuel Schüttengruber, alipiga hadi mapumziko New Zealand wakiwa mbele kwa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, 78, alitangaza Jumatatu kwamba ameanza tena kazi yake ya kawaida, baada ya kuashiria map...
20/06/2023

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, 78, alitangaza Jumatatu kwamba ameanza tena kazi yake ya kawaida, baada ya kuashiria mapema Juni kwamba alipimwa na kuambukizwa Covid-19.
“Nikiwa na afya njema iliyothibitishwa, sasa ninaweza kuanza tena mikutano ya mwili, kuanzia na serikali mchana huu,” alitangaza kwenye Twitter.
Mkuu huyo wa nchi, ambaye ameitawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1986, alikuwa ametangaza tarehe 8 Juni kwamba amepimwa na kukutwa na Covid-19, akitaja “dalili ndogo”. “Nimekabidhi kazi yangu ya leo na kesho kwa Waziri Mkuu Robinah Nabbanja,” alisema.
—-With a confirmed clean bill of health, I am now able to get back to physical meetings, starting with cabinet this afternoon at State House Entebbe Entebbe
Wiki iliyopita, Rais wa Uganda hakushiriki katika ujumbe wa wakuu kadhaa wa nchi za Afrika ambao walisafiri kwenda Ukraine na Urusi kujaribu kumaliza mzozo huo.
Mara baada ya kusifiwa kuwa mwanamageuzi, Yoweri Museveni alichukua hatamu ya Uganda mwaka 1986, na kusaidia kukomesha tawala za kimabavu za Idi Amin Dada na Milton Obote.
Lakini kiongozi huyo wa zamani wa waasi tangu wakati huo amekabiliana na upinzani na kubadilisha katiba ili kujiweka madarakani.
Kulingana na Wizara ya Afya, Uganda imerekodi rasmi kesi 170,775 za maambukizo ya coronavirus na vifo 3,632 tangu kuanza kwa janga hilo mnamo 2020.

By: Uncle A simba Geniu's

Kila mwaka ifikapo Juni 20, dunia huadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, siku ya kimataifa ya kuwaenzi watu ambao wamela...
20/06/2023

Kila mwaka ifikapo Juni 20, dunia huadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, siku ya kimataifa ya kuwaenzi watu ambao wamelazimika kukimbia.
Kwa pamoja, tunaweza kutetea haki yao ya kutafuta usalama, kujenga usaidizi wa ushirikishwaji wao wa kiuchumi na kijamii, na kutetea suluhu za masaibu yao.
Ulimwengu unashuhudia viwango vya juu zaidi vya uhamIaji kwenye rekodi.
Watu milioni 70.8 wasio na kifani duniani kote wamelazimika kutoka nyumbani kutokana na migogoro na mateso mwishoni mwa 2018 Miongoni mwao ni karibu wakimbizi milioni 30, zaidi ya nusu yao wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.
Pia kuna mamilioni ya watu wasio na utaifa, ambao wamenyimwa utaifa na kupata haki za msingi k**a vile elimu, huduma za afya, ajira na uhuru wa kutembea.
Kufikia mwisho wa 2022, idadi ya wakimbizi duniani ilifikia milioni 35.3, ongezeko la zaidi ya milioni nane kutoka mwaka uliopita, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).
Zaidi ya nusu (asilimia 52) ya wakimbizi wote walitoka nchi tatu tu: Syria (milioni 6.5), Ukrainia (milioni 5.7) na Afghanistan (milioni 5.7).
Chini ya sheria za kimataifa, wakimbizi ni watu wanaolazimika kukimbia nchi zao ili kuepuka mateso au tishio kubwa kwa maisha yao, uadilifu wa kimwili au uhuru.
Ili kuongeza ufahamu kuhusu hali ya wakimbizi duniani kote, Umoja wa Mataifa uliteua Juni 20 kila mwaka kuwa Siku ya Wakimbizi Duniani.
Uturuki kwa sasa inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani huku takriban watu milioni 3.6 wakitafuta hifadhi huko. Iran inashikilia nafasi ya pili kwa idadi ya wakimbizi milioni 3.4, ikifuatiwa na Jordan yenye milioni tatu.
Kati ya idadi ya wakimbizi na watu wanaohitaji ulinzi wa kimataifa, asilimia 76 wanachukuliwa na mataifa ya kipato cha chini na cha kati na asilimia 70 wanahifadhiwa na nchi jirani.

“Maneno yaliyoenea bado ni kwamba wakimbizi wote wanakwenda katika nchi tajiri. Hili si sahihi. Ni kinyume kabisa,” Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi Filippo Grandi alisema

Chelsea ilimsajili fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku kutoka RB Leipzig kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 53 Ju...
20/06/2023

Chelsea ilimsajili fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku kutoka RB Leipzig kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 53 Jumanne.
Nkunku alikuwa tayari amekubali mkataba wa awali na klabu hiyo ya Premier League mwezi Disemba na sasa ameweka muhuri wa kuhamia Stamford Bridge.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameweka bayana kuhusu kandarasi ya miaka sita yenye faida kubwa na The Blues, ambao wanaanza ukarabati wa msimu wa karibu huku wakitarajia kurejea kutoka kwa kampeni mbaya.
“Chelsea ina furaha kutangaza Christopher Nkunku atajiunga na klabu hiyo kutoka RB Leipzig kabla ya msimu wa 2023/24,” taarifa kwenye tovuti ya Blues ilisema.
Nkunku ni mmoja wa nyota wanaochipukia katika soka la Ulaya na alifunga mabao 23 katika michezo 36 aliyoichezea Leipzig msimu uliopita ni mchezaji wa kwanza mkubwa kusajiliwa tangu Mauricio Pochettino kuthibitishwa kuwa meneja mpya wa Chelsea mwishoni mwa Mei.
“Nina furaha sana kujiunga na Chelsea. Juhudi kubwa ilifanywa kunileta katika klabu,” Nkunku alisema. “Natarajia kukutana na kocha wangu mpya na wachezaji wenzangu na kuwaonyesha wafuasi wa Chelsea kile ninachoweza kufanya uwanjani.”
Nkunku, ni mhitimu wa academy ya soka ya kitaifa ya Ufaransa huko Clairefontaine, alikaa miaka minne Paris Saint Germain kabla ya kuhamia Leipzig mnamo 2019.
Nkunku alicheza mechi yake ya kwanza Ufaransa mwaka jana na amecheza mara 10 na aliondolewa kwenye Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar kutokana na jeraha la mguu.

By: Uncle A simba Geniu's

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Babirousa heroique posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Category


Other TV Channels in Dar es Salaam

Show All