The Chanzo

The Chanzo Uchambuzi, maoni, uchunguzi na habari zenye kugusa jamii
(5)

06/09/2024

'Tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja' Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud

05/09/2024

Mbeya: Washinikiza barabara ipanuliwe kupunguza ajali

CCM Distances Itself From Former Longido DC’s Election-Rigging Remarks
05/09/2024

CCM Distances Itself From Former Longido DC’s Election-Rigging Remarks

Speaking on Wednesday, September 4, 2024, to CCM and government leaders in Arusha, the party’s Secretary for Ideology, Publicity, and Training, Amos Makalla, emphasised that CCM cannot be propped up in elections.

Tanzania, China, and Zambia Agree on the Improvement of the TAZARA Railway
05/09/2024

Tanzania, China, and Zambia Agree on the Improvement of the TAZARA Railway

A press release from the Tanzanian State House explained that President Samia highlighted the importance of this agreement for regional development after the signing.

04/09/2024

Yanayomliwaza, kumliza Babu Duni akitafakari maisha yake ndani, nje ya ACT-Wazalendo.

04/09/2024

"Asanteni": Babu Duni ashindwa kuzuia hisia zake ACT-Wazalendo wakimuenzi

04/09/2024

Mbeya: Mradi wa njia nne mashakani kukamilika kwa wakati

03/09/2024

Usitupe chupa ovyo, zinachakatwa kuwa bidhaa.

03/09/2024

'Tutaboresha WHO ili iwe imara' Faustine Ndugulile

Ado Shaibu: Ninavyomfahamu Richard Mabala, Mwalimu Hodari, Mwanaharakati MachachariLeo nimemkumbuka ndugu yangu, Richard...
03/09/2024

Ado Shaibu: Ninavyomfahamu Richard Mabala, Mwalimu Hodari, Mwanaharakati Machachari

Leo nimemkumbuka ndugu yangu, Richard Mabala, Mtanzania aliyeacha alama kwenye sekta ya elimu, hasa kupitia kazi zake za ualimu, uandishi na harakati. Miaka kadhaa nyuma nimewahi kuandika makala kuhusu yeye niliyoiita Masuala 10 Usiyoyajua Kuhusu Richard Mabala. Kwenye thread hii nitayachapisha tena kwa muhtasari.

Jambo moja ambalo baadhi ya wasomaji wa vitabu na makala zake wanaweza wasijue kuhusu yeye, hasa kutokana na anavyokimudu Kiswahili kwa uweledi wa hali ya juu, ni kwamba Richard Mabala ni Mzungu.

Richard Mabala alikuja nchini mwaka 1973 akiwa miongoni mwa wafanyakazi wa kujitolea chini ya mpango wa wafanyakazi wa kujitolea, au Voluntary Service Oversea (VSO). Yeye alikuwa miongoni mwa Waingereza walioendelea kufanya kazi nchini hata pale Tanzania ilipovunja mahusiano yake ya kidiplomasia na Uingereza.

Soma https://thechanzo.com/2024/09/03/ado-shaibu-ninavyomfahamu-richard-mabala-mwalimu-hodari-mwanaharakati-machachari/

Juma Duni Haji: Tafsiri ya Mwanasiasa MnyenyekevuNa Zitto KabweSikutaka kuandika makala haya. Hukupaswa kuisoma kabisa. ...
03/09/2024

Juma Duni Haji: Tafsiri ya Mwanasiasa Mnyenyekevu

Na Zitto Kabwe

Sikutaka kuandika makala haya. Hukupaswa kuisoma kabisa. Unaisoma kwa sababu ya maneno ambayo nimeambiwa jijini Mbeya na mmoja wa wanasiasa waandamizi katika siasa za upinzani mkoani humo, na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla.

Niliomba kupata naye kifungua kinywa asubuhi ya siku nimeandika makala haya. Katikati ya mazungumzo yetu marefu ambayo yalikuwa yanapitia hali ya siasa ya mkoa wa Mbeya na mapito yake, mwanasiasa huyu akatamka maneno yaliyoniingia kichwani na moyoni.

Soma https://thechanzo.com/2024/09/03/juma-duni-haji-tafsiri-ya-mwanasiasa-mnyenyekevu/

03/09/2024

Jengo lazinduliwa Z'bar kuwapiga jeki wenye vipaji.

03/09/2024

Mbeya: Mashirika yasiyo ya Kiserikali yalia kukosa wafadhili

Ubashiri Hatma ya Samatta Stars Haukutakiwa KuwepoNa Angetile OsiahKumeibuka ubashiri tofauti baada ya mshambuliaji wa k...
02/09/2024

Ubashiri Hatma ya Samatta Stars Haukutakiwa Kuwepo

Na Angetile Osiah

Kumeibuka ubashiri tofauti baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, kutotangazwa katika orodha ya wachezaji wa timu ya taifa walioingia kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Ethiopia kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.

Baadhi walimtaka kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco, kutomuacha mchezaji huyo, wakisema bado ni muhimu kwa taifa, wengine wakidhani kuwa ameachwa pengine kwa sababu kiwango chake kinashuka kutokana na umri.

Na baadhi walisema kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa ya England alikataa kujumuishwa kwenye kikosi hicho kitakachoicheza mechi mbili. Ni haki yao mashabiki kuwa na hisia tofauti kuhusu mshambuliaji huyo ambaye aliandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya England.

Soma https://thechanzo.com/2024/09/02/ubashiri-hatma-ya-samatta-stars-haukutakiwa-kuwepo/

02/09/2024

"Tumekuwa nchi ya waongo" Jenerali Ulimwengu

Dr Salim Ahmed Salim Archive: A Digital Memoir About AfricaBy Jasper SabuniAfrica may have been blessed and enriched wit...
02/09/2024

Dr Salim Ahmed Salim Archive: A Digital Memoir About Africa

By Jasper Sabuni

Africa may have been blessed and enriched with many things, but I would presume that one of the continent’s proudest and most valuable blessings is the pure, genuine and remarkable soul and gem, in the name of Dr Salim Ahmed Salim – an indeed proud son of Africa!

As a teen, I was often encouraged to learn and follow in Dr Salim’s footsteps. Upon growing up and gaining consciousness, I would wonder how and what would make one imagine that I had anything within me to walk along the path and steps of this incredible treasure born in the islands of Zanzibar.

Read https://thechanzo.com/2024/09/02/dr-salim-ahmed-salim-archive-a-digital-memoir-about-africa/

Hatma ya Muswada wa Sheria ya Kupambana na Rushwa Wenye Kipengele Tata Kujulikana LeoNa Ibrahim MgazaDar es Salaam. Leo,...
02/09/2024

Hatma ya Muswada wa Sheria ya Kupambana na Rushwa Wenye Kipengele Tata Kujulikana Leo

Na Ibrahim Mgaza

Dar es Salaam. Leo, Septemba 2, 2024, Bunge linatarajia kupitisha au kutupilia mbali marekebisho yanayopendekezwa kwenye Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2024, hususan kifungu 10(b) kinachoeleza kwamba mtu ambaye atabainika kudai au kushwawishi kutoa rushwa ya ngono basi naye atashtakiwa.

Kipengele hicho kimeenda mbali zaidi na kueleza kuwa endapo mtu huyo atakutwa na hatia basi atahukumiwa kulipa faini au kufungwa jela na pengine kukumbana na adhabu zote kwa pamoja.

Wakitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari Agosti 31, 2024, Mtandao wa Kupinga Rushwa ya Ngono Nchini ulieleza kwamba endapo mapendekezo hayo yatapitishwa basi sheria hiyo itakwenda kuhalalisha na kuendeleza matumizi mabaya ya mamlaka kwa njia kumhukumu muathirika wa rushwa ya ngono k**a mbinu ya kumnyamazisha na kuzima moto wa mapambano dhidi ya rushwa ya ngono.

Mtandao huo ukaendelea kueleza kwamba kifungu cha 25 kilichopo kwenye Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 kinajitosheleza na wala hakihitaji marekeisho yoyote kwani hakina mapungufu kwenye falsafa ya sheria kwa sababu kinamlinda muathirika wa rushwa ya ngono.

Kifungu hicho cha 25 cha Sheria ya Rushwa ya Ngono ya Mwaka 2007 kinamlinda muathirika wa rushwa ya ngono kwa kuwadhibiti maofisa wakuu wanaotumia nyazifa zao na madaraka vibaya kuomba kupokea na kuomba rushwa.

31/08/2024

Mtazamo Kwamba Tunaweza Kutumia Ngono Kuwaadhibu Watu Waliotukosea ni Jini Tuliloliumba Wenyewe na Ambalo Limeendelea Kututafuna

Na Otuck William

Hivi karibuni, vichwa vya habari vilitawaliwa na habari ya ‘Binti wa Yombo’ anayedaiwa kufanyiwa ukatili wa kingono na vijana wa nne, kwa kile kinachoaminika kuwa ni kisasi cha kuibwa kwa mume kilichofanywa na “afande” aliyewatuma vijana hao kutekeleza uhalifu huo.

Tukio hili limegusa hisia za watu wengi sana kwenye jamii, kila mmoja akitaka hatua stahiki zichukuliwe ili kuhakikisha haki ya binti inapatikana, na wahusika wote wanafikishwa mbele ya sheria, ikiwemo wale vijana, afande aliyewatuma, na wengine kwenda mbali zaidi kutaka mume anaedaiwa kuchepuka naye kuwajibishwa.

Ingia https://thechanzo.com/2024/08/31/mtazamo-kwamba-tunaweza-kutumia-ngono-kuwaadhibu-watu-waliotukosea-ni-jini-tuliloliumba-wenyewe-na-ambalo-limeendelea-kututafuna/

30/08/2024

Nani aliyewateka,kuwapoteza Watanzania hawa?

Fuatilia Makala nzima hapa Youtube The Chanzo

29/08/2024

Malalamiko takribani 800 yaifikia Tume ya Haki za Binadamu tangu Julai 1, 2024.

29/08/2024

Mahak**a Kuu Yatupilia Mbali Shauri Kupinga Uhalali wa Mawakili wa Nyundo na Wenzake

Dodoma: Mahak**a Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma imetupilia mbali maombi ya marejeo yaliyowasilishwa na Wakili Leonrad Mashabala ya kuangalia uhalali wa mawakili wanaowatetea watuhumiwa wanne wa kesi ya ubakaji wa kundi na ulawiti kwa binti mkazi wa Yombo Jijini Dar es salaam.

Jaji Suleiman Hassan ametupilia mbali maombi hayo leo yaliyofunguliwa na Mashabala kwa kuwa amewaunganisha na wajibu maombi ambao hawapo kwenye kesi ya msingi.

Shauri hilo linatoa nafasi ya kuendelea kwa kesi ya msingi namba 23476 ya mwaka 2024, inayowakabili watuhumiwa wanne ambao ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), MT 140105 Clinton Damas almaarufu k**a Nyundo, Askari Magereza C1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson maarufu Machuche na Amin Lema maarufu k**a Kindamba.

29/08/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amemtunuku nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ), Mkuu wa Majeshi, Jacob Mkunda.

Sambamba na Mkuu wa Majeshi Rais Samia anawatunuku nishani maofisa na askari wa JWTZ kumi na tano kwa niaba ya wenzao waliopo katika utumishi hadi hapo Septemba Mosi, 2024.

Kabla ya kutunukiwa nishani hiyo na Rais, ulisomwa wasifu wa mkuu wa majeshi, Jenerali Mkunda.

Jumapili, Septemba Mosi, JWTZ itatimiza miaka 60 tangu kuasisiwa kwake Septemba Mosi, 1964.

Address

Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Chanzo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to The Chanzo:

Videos

Share


Other Media/News Companies in Dar es Salaam

Show All

You may also like