Watafiti wa China wamezindua matofali maalum kwa kusudi kwamba siku za zijazo huenda yakatumika kujenga kwenye ardhi ya mwezi. Kwa mujibu wa wanasayansi hao wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Huazhong , matofali hayo ambayo yametengenezwa kwa kutumia viungo vinavyoiga udongo unaopatikana mwezini yana nguvu mara nne zaidi ya matofali ya kawaida au yale yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji.
Tabasamu nzuri ni dhihirisho la furaha ya ndani ya roho. Jiunge nasi kufurahia mdundo wa umoja tukitumbuizwa na huu muziki huku tukisherehekea ushirikiano kati ya China na Afrika. #FOCAC2024 #africa #China
MDUNDO WA UMOJA, USHIRIKIANO WA CHINA-AFRIKA: Tabasamu nzuri ni dhihirisho la furaha ya ndani ya roho. Jiunge nasi kufurahia mdundo wa umoja tukitumbuizwa na huu muziki huku tukisherehekea ushirikiano kati ya China na Afrika. #FOCAC2024 #africa #China
Rais wa China Xi Jinping mapema leo alihudhuria hafla ya mapokezi alipowasili nchini Hungeria kwa ziara rasmi. Hafla hiyo iliandaliwa na kuhudhuriwa na mwenyeji wa Xi, rais wa Hungeria Tamas Sulyok pamoja na waziri mkuu wa nchi hiyo Viktor Orban katika mji wa Budapest #GLOBALink
Majenerali wawili wa jeshi la Marekani waliokuwa kwenye msitari wa mbele kutekeleza mpango wa Rais Joe Biden kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan leo walitoa ushahidi wao mbele ya bunge, huku viongozi wa chama cha Republican wakimtaka Biden kuwajibikia mauti yaliyotokea wakati wa kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan baada ya uvamizi wa miaka 20.
Majenerali hao ambao tayari wamestaafu walilaumu Wizara ya Mambo ya Kigeni kwa kuchelewa kutekeleza amri ya uhamishaji, zaidi ya mwezi moja baada ya Wizara ya Ulinzi kuanza kuondoa vikosi vya Marekani kutoka Afghanistan.
Watu 2 walifariki mapema leo na wengine 3 wangali hawajabainika waliko baada ya meli ya mizigo kugonga nguzo za daraja na kuliporomosha katika mji wa bandari wa Guanzhou, nchini China. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usalama wa Bahari katika mji wa Guangzhou, kishindo cha ajali hiyo kilisababisha magari matano, likiwemo basi la abiria na pikipiki moja iliyokuwa kwenye daraja hilo kutumbukia baharini ama juu ya meli nyingine iliyokuwa imetia nanga pembeni.
Video hii ya kustaajabisha ambayo ilirekodiwa kwa kutumia ndege isiyo na rubani inaonyesha mbwa mwitu wakichimba mahandaki ndani ya theluji katika mkoa huru wa Xinjiang, kaskazini magharibi ya Uchina.
Polisi wa Kuwait waonyesha ujuzi wao kwenye hafla ya mahafali katika mji wa Kuwait mnamo Februari 19, 2024.
Patrick Yoram Sudae ni fundi wa viatu kutoka Dar es Salaam, Tanzania ambaye amebobea katika ufundi wa kutumia tairi kuukuu kutengeneza makubazi.
Idadi ya mifugo ambao wamefariki kutokana na hali ya baridi kali nchini Mongolia imefikia 667,840 msimu huu wa baridi, mamlaka ya Udhibiti wa Majanga nchini humo imesema.
Dzud, kama inavyofahamika nchini Mongolia, ni hali ya baridi kali inayopelekea mifugo kufa njaa baada ya ardhi na nyasi kuganda hadi kuwa barafu. Baadhi ya mikoa ambayo ya Mongolia mbao imeathiriwa na hali hii ni pamoja na Sukhbaatar, Khentii, Dornod ,Dornogovi na Arkhangai.
Ajuza wa miaka 97 afurahia kuunganishwa na kitukuu chake kwenye hafla ya Mwaka Mpya wa Kichina iliyoleta pamoja jamaa kutoka vizazi vinne vya familia yake.
Hasara ya Vita vya Gaza
Mohammed al-Yazji; mtoto wa kiume wa miaka 13 amebaki yatima na mlezi wa ndugu zake 12, akiwemo dadake mchanga wa miezi 6, baada ya wazazi wao kuuawa kwenye mapigano kati ya Israel na Hamas. #Gaza #khanyounis #palestine #israel #Rafah