Wasiwasi wa utekaji nyara
Shirika la kutetea haki Afrika laelezea wasiwasi
Inaarifiwa kuwa 26 waliotekwa hawajulikani waliko
Wanaharakati wasema visa 83 vya utekaji nyara vimeripotiwa
Serikali imetakiwa kuchukua hatua za haraka kufanya uchunguzi
#SemaNaCitizen
Vyama vya ushirika
Seneti yaraiwa kuidhinisha mswada wa vyama vya ushirika
Mswada huo kusaidia kudhibiti vyama vya ushirika
Mswada huo kuzuia kusambaratika kwa vyama vya ushirika
#SemaNaCitizen
Afueni kwa wafanyibiashara Machakos
Zaidi ya wafanyibiashara 4,000 wanufaika Machakos
Kaunti yaweka majokofu ya kuhifadhi mboga na matunda
Hatua hiyo kuzuia hasara ya mazao kuharibika sokoni
#SemaNaCitizen
Wafanyibiashara wa miraa wateta
Wafanyibiashara wa miraa Pumwani walalamika
Wanadai kuna njama ya kuwaondoa eneo hilo
Wafanyibiashara wanasema kaunti iliwatengea sehemu hiyo
Wanamtaka Gavana Sakaja kuingilia kati swala hilo
#SemaNaCitizen
Kizaazaa cha uhamisho Luanda
Wazazi watishia kuvuruga masomo shuleni Kimabole
Hii ni baada ya walimu kuhamishwa kila mara
Mwalimu mkuu mpya amehamishwa ghafla
#SemaNaCitizen
Matibabu yarejelewa Kisii
Wauguzi Kisii wamesitisha mgomo wao
Mgomo huo uliathiri zaidi ya hospitali 160 Kisii
KNUN imetia sahihi mkataba wa kurejea kazini
#SemaNaCitizen
Msaada kwa wakazi Gatanga
Wakaazi wa Kijiji cha Mbugiti Gatanga wapata msaada
Kampuni ya Hego imewapa chakula na bidhaa zinginezo
Kampuni moja ya ujenzi wa barabara imeajiri wakazi 200
Barabara hiyo ina urefu wa Kilomita 27
#SemaNaCitizen
Hazina ya karo Kijijini Mfangano:
Wakaazi wa Kijiji cha Soklo waanzisha hazina
Hatua hiyo inalenga kuimarisha masomo kisiwani Mfangano
Wameazimia kuhakikisha wanafunzi wote wamerejea shuleni
#SemaNaCitizen
Utunzaji wa msitu wa Kaya
Wazee wa Kaya Kwale wataka misitu ya Kaya kulindwa
Wazee hao wataka serikali kuwaondoa wakazi msituni
Mpango huo utasaidia kuhifadhi misitu ya Kaya
#SemaNaCitizen
Tamu chungu za pacha
Mwanamke mmoja Nakuru ajifungua watoto wanne
Susan Chepkemei kutoka Nakuru sasa ana watoto kumi
Mwanamke huyo wa miaka 31 asema alitarajia watoto watatu
#SemaNaCitizen
Walimu wadai uhamisho Butula
Walimu wa shule ya Bumula wataka kuhamishwa
Waliandamana hadi ofisi za TSC wakitaka kuhamishwa
Walimu hao wanadai kuhofia usalama wao shuleni
Wazazi na wanafunzi wa shule hiyo waliandamana
#SemaNaCitizen