17/06/2020
SUNGURA NI HALALI KUFUGA NA KULA.
Je, kufuga na kula Sungura ni halali kwetu? Naomba majibu ya-support aya za Quran au hadithi kuwa, imepokelewa wapi, na K**a ni swahihi au dhaifu pamoja na milango ya hadithi hizo.
Shukran.
JIBU
Wa Alaykumus-Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh!
BISMILLAH!
Sungura ni halali kumla. Si Qur’ani wala Si Sunna imekataza kumla. Na chochote kile ambacho hakijakatazwa navyo basi ni halali.
Bali Sunna imethibitisha kujuzu kumla, kwa kauli na vitendo.
Imepokewa kutoka kwa Mtume ﷺ k**a ifuatavyo, katika Bukhari na Muslim.
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه أنه صاد أرنباً ، وأتي بها أبا طلحة (فَذَبَحَهَا فَبَعَثَ بِوَرِكِهَا وَفَخِذَيْهَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَأَتَيْتُ بِهَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَبِلَهُ) البخاري (5535) ومسلم (1953)
1953. Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik رضى الله عنه akisema: Tulisafiri kupitia upenyu wa Dhahraan [ujia wa baina ya majabali, karibu na Makka], tukamuona sungura kwenye ujia huo. Wakamkimbiza mpaka wakamchosha. Basi nikamkimbilia na kumk**ata. Nikampelekea Abu Twalha, akamchinja na kumtayarisha. Nikampelekea Mtume ﷺ kiuno chake na mapja yake mawili, kwa pamoja. Mtume ﷺ akapokea!” Ameipokea Muslilm, Hadithi Nam. 1953. Bukhari Hadithi Nam.5535 Muttafaq Alayhi.
وعن محمد بن صفوان (أو صفوان بن محمد) أنه قال : (صدت أرنبين فذبحتهما بمروة , فسألت رسول الله صلى الله عليه وسلم فأمرني بأكلهما)
Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Safwan (kwa jina jengnne Swafwaan bin Muhammad) رضى الله عنه akisema:”Niliwinda sungura wawili, nikawachinja Marwa. Nikamuuliza Mtume ﷺ . Akaniamrisha niwale.”
Hivyo, Mtume ﷺ ameruhusu kuliwa na amekula. Na Maswahaba kadhaa wamekula, miongoni mwao Sa’d bin Abi Waqqas, Abu Sa’id al-Khudriyy, Ibn Musayyib, ‘Ata’ bin Rabah, al-Lyth bin Sa’d, Ibn al-Mundhir, Abu Thawr, Shafi, Malik, Abu Hanifa.
Zaidi, Sungura haingiii katika vigezo vya wanayama waliokatazwa, si kwa majina wala kwa vigezo vya Kuwinda kwa Nabu, Makucha na kadhalika.
Hivyo, kilicho halali kukila ni halali kukifuga, na kilicho halali kukifuga ni halali kukununua au kukiuza.
Ila unapofuga mnyama, basi uchunge taratibu za kufuga kiumbe cha Mwenyezi Mungu; kwani ameingizwa motoni mwanamke kwa sababu ya paka tu; kamfungia bila ya chakula wala kumuachilia akajitafutie riziki yake nje.
والله أعلم
وبالله التوفيق
السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
NI RUHUSA KUNUKUU, k**a ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye WhatsApp na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.
[email protected]