18/07/2024
WILAYA YA MAGHARIB A
Wanawake nchi wametakiwa kutokata tamaa katika harakati zao za kila siku za kujitafutia maisha badala yake kupambana Hadi kufikia malengo walio kusudia.
Ameyasema hayo Bi Mariya ambae ni Mwenyekiti wa kikundi Cha kamba ndefu wakati akizungumza na Nuru yetu amesema wanawake wanaweza endapo atasimama imara bila ya kujali kuyumbishwa na maneno ya watu yanayoweza kumkatia tamaa .
Amesema endapo mwanamke atasimama imara na kufanya juhudi katika kuhakikisha anashika nafasi mbambali za kuongoza ataepuka na kudhalilishwa na kuwa tegemezi katika jamii.
Aidha Bi Maria amesema mpaka kufikia kuwa kiongozi amepitia changamoto mbalimbali ikiwemo kukatishwa tamaa lakini alipambana mpaka kufikia kumiliki kikundi chake ambacho kumesaidia kutoa ajira Kwa wengine.