Manara tv

Manara tv Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Manara tv, Digital creator, Chunya, Mbeya.

Hivi Karibuni Kuna Video Imesambaa sana Mitandaoni inaonesha Kiongozi wa Dini, Dalai Lama wa 14 akimbusu Mtoto wa Kiume....
11/04/2023

Hivi Karibuni Kuna Video Imesambaa sana Mitandaoni inaonesha Kiongozi wa Dini, Dalai Lama wa 14 akimbusu Mtoto wa Kiume.

Baada ya video hiyo kusambaa, Ofisi ya Dalai Lama wa 14 kwa niaba yake Imeomba Msamaha kwa Mtoto huyo, Familia Yake pamoja na Wale wote waliokerwa na Maudhui ya Video hiyo.

Inasemekana video hii ilirekodiwa Tarehe 28 February Jijini Dharamshala, India.

Watu wa Tibet-China wanamfahamu Dalai Lama wa 14 k**a "Gyalwa Rinpoche", Ni Kiongozi wa Juu wa Dini (Buddhism) eneo la Tibet-China tangu Mwaka 1940, Jina lake halisi anaitwa "Lhamo Thondup".

Dalai Lama wa 14 amezaliwa Mwaka 1935 kijiji cha Taktser, China, Ni Miongoni mwa Viongozi wa Dini Duniani wenye Ushawishi mkubwa sana, Amefanikiwa kubeba tuzo mbalimbali, Mfano; Nobel Peace Prize, German Media Prize, Lantos Human Rights Prize, Templeton Prize, Nakadhalika.

NB. "Dalai Lama" ni Jina analopewa kiongozi wa Dini ya Wabudha Eneo la Tibet-China, Huyu wa Sasa ni wa 14.


Rihanna () ndiye Malkia mpya wa Twitter hivi sasa baada ya kufikisha zaidi ya wafuasi Milioni 108.2  na kumfanya kuwa mw...
11/04/2023

Rihanna () ndiye Malkia mpya wa Twitter hivi sasa baada ya kufikisha zaidi ya wafuasi Milioni 108.2 na kumfanya kuwa mwanamke mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao huo wa Elon Musk.

Badgal Riri ni wa nne duniani akiwa nyuma ya Elon Musk ambaye ni mmiliki wa mtandao huo na kinara akiwa na wafuasi Milioni 134+, Barrack Obama Milioni 132M+ na Justin Bieber mwenye Milioni 113+


Je unaupa alama ngap kwa muonekano mpya wa Morrison?
05/04/2023

Je unaupa alama ngap kwa muonekano mpya wa Morrison?


GSM Fc imezinduwa  rasmi jezi zao  kwaajili ya michuano ya Silent Ocean Ramadhani Cup 2023Michuano ambayo inafanyika mae...
29/03/2023

GSM Fc imezinduwa rasmi jezi zao kwaajili ya michuano ya Silent Ocean Ramadhani Cup 2023

Michuano ambayo inafanyika maeneo ya Gerezani Kariakoo, Kidonge Chekundu katika Uwanja wa JMK Park.

Ambapo GSM Fc watashuka dimbani majira ya Saa nne usiku hii leo kuwakabili Usangu Fc.



📸


Majeruhi wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea Februari 22, 2023, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya...
29/03/2023

Majeruhi wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea Februari 22, 2023, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya yake kuimarika.

Taarifa ya kuruhusiwa kwa Osam, imetolewa leo, Machi 28, 2023 na Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), Patrick Mvungi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Milanzi alipokelewa MOI Februari 22, 2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A.

"Ndugu Milanzi alipokelewa MOI akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia.

"Ndugu Milanzi ataendelea na huduma k**a mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili.

"Aidha, Tunatoa shukran za dhati kwa Watanzania wote, vyombo vya habari ambao kwa pamoja wameshirikiana nasi katika kumuombea na kumtangaza ndugu Osam Milanzi," imeeleza taarifa hiyo.


Taarifa kuhusu Kikosi cha Simba kilichoanza safari jana kwenda nchini Morocco. Kikosi cha  kimeshindwa  kuendelea na saf...
29/03/2023

Taarifa kuhusu Kikosi cha Simba kilichoanza safari jana kwenda nchini Morocco.

Kikosi cha kimeshindwa kuendelea na safari ya Morocco kupitia Qatar baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata itilafu za kiufundi.

Kikosi kilianza safari saa tisa na robo jijini Dar_es_salaam na kupitia Uwanja wa kilimanjaro (kia)
Nakupewa taarifa kuwa Ndege hiyo imeshindikana kuendelea na safari hivyo watalala Mkoani Arusha Mapema Jumatano wataendelea na safari ya kuelekea Morocco.



updates

Huyu jamaa anajulikana k**a PRINCE RANDIAN,alizaliwa mnamo mwaka 1871 na alikufa mnamo mwaka1935 akiwa na umri wa miaka ...
27/03/2023

Huyu jamaa anajulikana k**a PRINCE RANDIAN,alizaliwa mnamo mwaka 1871 na alikufa mnamo mwaka1935
akiwa na umri wa miaka 64 ni moja kati ya watu walioacha historia ya kutukuka na ya kuigwa duniani na yakipekee zaidi kutokana na kipaji chake/uwezo wake wa kuchora picha mbalimbali kwa kutumia mdomo wake.
Pia alikua na uwezo wa kusokota misokoto ya tumbaku,kuiwasha na kuvuta yote hayo aliyafanya kwa kutumia mdomo wake pekee kwani alizaliwa bila mikono wala miguu.


Benchi la Ufundi la Yanga, limepanga kumuandaa kimbinu na kisaikolojia kipa wao Metacha Mnata ili akae golini wakati tim...
26/03/2023

Benchi la Ufundi la Yanga, limepanga kumuandaa kimbinu na kisaikolojia kipa wao Metacha Mnata ili akae golini wakati timu hiyo, itakaporudiana dhidi ya TP Mazembe.

Kipa namba moja raia wa Mali, Djigui Diarra ataukosa mchezo huo kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Metacha akiwa anaichezea Yanga, msimu wa 2021 aliwahi kuokoa mchomo wa penalti dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana katika mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Aprili 2, mwaka huu huko DR Congo, mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar na Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 3-1.

Mataifa mbalimbali yanarudi katika mashindano ya kutafuta nafasi ya kushiriki Michuano ya EURO 2024.                    ...
23/03/2023

Mataifa mbalimbali yanarudi katika mashindano ya kutafuta nafasi ya kushiriki Michuano ya EURO 2024.

Mshambuliaji kinda wa klabu ya Yanga, Clement Mzize amebadili Dini na kuwa Muislamu mbele ya Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa w...
23/03/2023

Mshambuliaji kinda wa klabu ya Yanga, Clement Mzize amebadili Dini na kuwa Muislamu mbele ya Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Omari ofisini kwake.

Akizungumza na Manara TV Mzize alithibitisha kuwa amebadili dini na sasa atatambulika kwa jina la Walid Mzize.

Nyota huyo amebadili dini katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.


*AWESO AMWAKILISHA RAIS SAMIA UMOJA WA MATAIFA*Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso anamwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia...
23/03/2023

*AWESO AMWAKILISHA RAIS SAMIA UMOJA WA MATAIFA*

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso anamwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji unaofanyika Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 22-24 Machi 2023.

Waziri Aweso amehutubia Mkutano huo jana jioni ambapo Katika hotuba yake amebainisha umuhimu wa dunia kukaa pamoja na kusimamia agenda ya maji; thamani ya maji katika maisha na uchumi; kuongeza uwekezaji katika eneo la maji; ushirikiano wa kimataifa katika maji; pamoja na utafutaji wa fedha kwa ajili ya maji.

Aidha, Katika mkutano, Tanzania imebeba agenda mbili ambazo ni utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Tatu (Water Sector Development Programe III) ambayo inahitaji Dola za Marekani Bilioni 6.47 katika kipindi cha 2022-2025.

Vilevile, Tanzania imejipambanua kwa agenda ya uwekezaji katika Sekta ya Maji ili kufikia Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Tanzania Water Investment Programme 2023-2030). Programme ambayo bado inaandaliwa na ipo hatua za mwisho ku*induliwa inakadiriwa kuwa na bajeti ya zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 25 na itazinduliwa Mei 2023.

Kuna Video inasambaa mitandaoni tangu jana,inayo onesha  Rapper "Tekashi 6ix9ine" akishambuliwa na kundi la watu."Lance ...
22/03/2023

Kuna Video inasambaa mitandaoni tangu jana,inayo onesha Rapper "Tekashi 6ix9ine" akishambuliwa na kundi la watu.

"Lance Lazzaro"-Mwanasheria wa rapper huyo amesema kwamba Jana Tekashi 6ix9ine alikuwa GYM, Florida kusini kisha kushambuliwa gafla na kundi la watu, Tekashi 6ix9ine alijaribu kupamba lakini kutokana na wingi wa washambuliaji hao aliishia kupigwa.

Mwanasheria huyo amefunguka kwamba Tekashi 6ix9ine hakuwa na Walinzi wakati anashambuliwa.

Baada ya shambulio hilo Wafanyakazi wa GYM waliwasiliana na Meneja kisha Wakatoa Taarifa Polisi.

Polisi walifanikiwa kufika haraka na ambulance na "Tekashi 6ix9ine" kuwahishwa hospitali.

Mwanasheria wa Tekashi 6ix9ine ameeleza kwamba Mpaka sasa Upelelezi dhidi ya shambulio hilo linaendelea.

SERIKALI KUTENGA FEDHA KULINDA HADHI YA URITHI WA MJI MKONGWE ZANZIBAR-RAIS DK.MWINYIRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa B...
22/03/2023

SERIKALI KUTENGA FEDHA KULINDA HADHI YA URITHI WA MJI MKONGWE ZANZIBAR-RAIS DK.MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindu*i Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka Wananchi waelewe dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Mji Mkongwe unabaki k**a ulivyokuwa miaka mia mbili iliyopita na si kuubadilisha .Aliyasema hayo katika hafla fupi ya ufungu*i wa Jengo jipya la Hoteli ya Tembo, iliyofanyika Ukumbi wa Tembo House Hoteli ,Shangani leo tarehe 22 Machi 2023 Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk.Mwinyi amesema wapo wanaojaribu kupotosha kuwa Serikali ina lengo la kuubadilisha Mji Mkongwe kwa kuugawa na kubinafsisha na akaeleza lengo ni kuwapa watu wenye uwezo kuyajenga majengo hayo , kuyatunza ili yaweze kudumu miaka mia mbili ijayo akitolea mfano Jengo la sasa la Tembo Hoteli lilikuwa Ubalozi wa Marekani mwaka 1831 na Jengo lililozinduliwa leo kwa marekebisho ilikuwa ni Skuli mwaka 1944.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewakaribisha wawekezaji waje kushirikiana na Serikali kurudisha hadhi ya Mji Mkongwe na kuujenga huku akitoa miezi mitatu kwa waliopewa Majengo mbalimbali kwa ajili ya kuyarekebisha na kuyaendeleza wakishindwa Serikali itayachukua .Pia ameeleza Serikali imeamua kutenga fedha kuhakikisha inaleta mfumo bora wa maji, mfumo wa kisasa wa umeme , huduma ya Internet, ujenzi wa barabara katika Mji Mkongwe ili kuwa kivutio kwa utalii .

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Mfalme wa Oman Sultan Haitham Bin Tariq M Said na Serikali yake kwa msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 21 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Beit-al-Ajaib na kulirudisha katika hadhi yake na mkandarasi ameshapatikana na ujenzi utaanza hivi karibuni.

📅 22 Machi, 2023

📍Ukumbi wa Tembo House, Shangani, Mkoa wa Mjini Magharibi.


Waamu*i wa Ligi Kuu England (EPL) wameruhusiwa kusimamisha michezo ya ligi hiyo itakapofika muda wa kufungulia swaumu, i...
21/03/2023

Waamu*i wa Ligi Kuu England (EPL) wameruhusiwa kusimamisha michezo ya ligi hiyo itakapofika muda wa kufungulia swaumu, ili kutoa nafasi kwa wachezaji na waumini wa dini ya Kiislamu kufungua funga yao kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Arsenal na Manchester City, Emmanuel Adebayor ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa m...
21/03/2023

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Arsenal na Manchester City, Emmanuel Adebayor ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 39.

Raia huyo wa Togo amewahi pia ku*ichezea Monaco, Real Madrid, Tottenham na Crystal Palace katika miaka 21 ya maisha yake ya soka yaliyoanzia katika klabu ya Metz.

“Shukrani kwa mashabiki wangu ambao wamekuwa nami siku zote. Ninajihisi mwenye furaha sana kwa ajili ya kila kitu, na nina matamanio kwenye kinachofuata,” amesema kupitia video kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Katika maisha yake ya soka ametunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa Togo mara tano mfululizo kati ya mwaka 2005 na 2009.

Katika muongo mmoja aliocheza Ligi Kuu ya England akivaa u*i wa Spurs, Arsenal na Man City alifunga magoli 79.

Adebayor, moja ya majina makubwa ya Soka Afrika amestaafu akichezea klabu ya AC Semassi ya Togo.


Serikali kupitia Wizara ya Afya imethibitisha uwepo wa Virus vya Marburg ambavyo husababisha Ugonjwa ujulikanao k**a (Ma...
21/03/2023

Serikali kupitia Wizara ya Afya imethibitisha uwepo wa Virus vya Marburg ambavyo husababisha Ugonjwa ujulikanao k**a (Marburg Viral Disease) ambapo kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO.

Ugonjwa huo kwa Mara ya Kwanza Uligundulika Nchini Ujerumani mwaka 1967 katika Mji wa Maburg. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akithibitisha Juu ya Uwepo wa Ugonjwa huo Leo Jijini Dar es Salaam, amesema kwa hapa nchini Ugonjwa huo Umegundulika Katika Kata za Maruku na Kanyangereko Halmashauri ya Bukoba Vijijini.

Waziri Ummy amesema Uchungu*i uliofanywa katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii imethibitisha uwepo wa Virusi hivyo hapa nchini baada ya baadhi ya Wananchi katika Kata hizo kuonesha Dalili za Ugonjwa huo, ambazo ni homa, Kutokwa na Damu sehemu mbalimbali za Mwili, Kutapika na Figo Kushindwa kufanya kazi.

"Ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa Binadamu Mmona kwenda kwa Mwingini kupitia majimaji, ama wakati mwingine Huambukizwa kutoka kwa Wanyama kwenda kwa Binadamu, mpaka sasa Ugonjwa huu hauna tiba mahususi isipokuwa hutibiwa kulingana na Dalili" amesema Waziri Ummy.


Wachezaji wa Timu ya Taifa ya DR Congo,Henock Inonga na Fiston Mayele Tayari wamejiunga na Kambi ya Timu ya Taifa ya DR ...
21/03/2023

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya DR Congo,Henock Inonga na Fiston Mayele Tayari wamejiunga na Kambi ya Timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na Michezo Miwili ya kufuzu AFCON 2024 dhidi ya Mauritania.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kesho Jumatano March 22,2023 katika maeneo...
21/03/2023

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kesho Jumatano March 22,2023 katika maeneo mengi ya Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya Makazi kujaa maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi “Tafadhali zingatia na ujiandae”

Mchezaji Klyian Mbappe achukua mikoba ya unahodha ya Ufaransa 🇨🇵 baada ya aliyewahi kuwa nahodha wa timu hiyo Hugo Llori...
21/03/2023

Mchezaji Klyian Mbappe achukua mikoba ya unahodha ya Ufaransa 🇨🇵 baada ya aliyewahi kuwa nahodha wa timu hiyo Hugo Lloris kustaafu timu ya Taifa.

Rais William Ruto amesema kwamba hatakubali "kutoijali nchi" baada ya maandamano ya ghasia kukumba mji mkuu, Nairobi na ...
21/03/2023

Rais William Ruto amesema kwamba hatakubali "kutoijali nchi" baada ya maandamano ya ghasia kukumba mji mkuu, Nairobi na mji wa magharibi wa Kisumu.

Maandamano hayo yaliandaliwa na mwanasiasa wa upinzani Raila Odinga ambaye analaumu sera za serikali kwa ku*idisha kupanda kwa gharama ya maisha.

Pia amedai bila ushahidi kwamba alishinda uchagu*i wa urais wa mwaka jana.

"Nitahakikisha k**a rais kwamba nchi hii inaongozwa na sheria, na hakuna chochote zaidi ya sheria na katiba kitakachokuwa sehemu ya kile tunachofanya," Bw Ruto alisema.

Rais amemshutumu Bw Odinga kwa kujaribu kuanzisha mgogoro kwa mara ya pili, akisema alifanya vivyo hivyo baada ya uchagu*i wa 2017 na kumlazimisha Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta kufikia makubaliano ambayo yalimpa mapendeleo ya serikali.

Hata hivyo, Bw Odinga amekanusha madai hayo.

Source: BBC


Maofisa Polisi nchini Kenya, wamewak**ata wafuasi wa upinzani waliokuwa wanajaribu kukusanyika nje ya jumba la Mikutano ...
20/03/2023

Maofisa Polisi nchini Kenya, wamewak**ata wafuasi wa upinzani waliokuwa wanajaribu kukusanyika nje ya jumba la Mikutano la KICC kwa Maandamano yaliyoitishwa na upinzani.

Maofisa Polisi waliweka kambi katika maeneo tofauti jijini Nairobi, huku barabara zinazoelekea Ikulu zikiwa zimekekwa vizuizi, kabla ya Maandamano ya Muungano wa Azimio la Umoja yaliopangwa kufanyika leo.

Polisi nchini Kenya jana Jumapili walipiga marufuku upinzani kufanya Maandamano kuhusu mfumuko wa bei, wakisema maombi ya Maandamano hayo yaliwasilishwa kwa kuchelewa, lakini waandalizi waliapa kuendelea na mikutano hiyo.


Klabu ya soka ya Singida Big Stars leo Machi 20, 2023 imeingia makubaliano na Klabu ya US Monastir ya Tunisia kwa ajili ...
20/03/2023

Klabu ya soka ya Singida Big Stars leo Machi 20, 2023 imeingia makubaliano na Klabu ya US Monastir ya Tunisia kwa ajili ya kushirikiana masuala mbalimbali ya soka.

Katika makubaliano hayo yaliyowekwa saini jijini Dar es Salaam, yatagusa mambo ya kiutawala ambapo klabu ya Us Monastir watawapa Singida Big Stars uzoefu wa masuala ya uendeshaji, maandalizi ya msimu (Pre-Season) ambapo klabu ya Singida Big Stars itakuwa ikiweka kambi nchini Tunisia.

Makubaliano hayo pia yatagusa wachezaji wa timu kubwa na ile ya U20.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana .chana amesema Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Mil...
20/03/2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana .chana amesema Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 endapo timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) itafuzu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Barani Afrika (AFCON) mwaka 2024 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20,2023 jijini Dar es Salaam ambapo amesema Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma ataongoza Watanzania wa hapa nchini na waishio nchini Misri kuishangilia Taifa Stars.

"Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wa tarehe 24, Machi 2023 dhidi ya Uganda (The Cranes) ambao utakaochezwa katika mji wa Isimailia nchini Misri na mchezo wa marudiano utachezwa Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamini Mkapa" amesema Mhe. Chana.

Aidha, amewataka wadau wa mchezo huo ikiwemo Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na mashabiki kumuunga mkono Kocha wa Timu hiyo Bw. Adel Amrouche, huku akiwasistiza wachezaji wajitume ili waweze kufanya vizuri katika nashindano hayo.


“Simba hatujapokea barua yoyote na wala Wachezaji wetu hawajatuma barua TFF kwamba wasiitwe Taifa Stars, lakini Sisi tum...
14/03/2023

“Simba hatujapokea barua yoyote na wala Wachezaji wetu hawajatuma barua TFF kwamba wasiitwe Taifa Stars, lakini Sisi tumefurahi maana wanabaki kuisaidia Simba itimize malengo yake kuingia ROBO FAINALI” -Ahmed Ally

Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika katika mechi za hatua ya Makundi ya mzunguk...
14/03/2023

Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika katika mechi za hatua ya Makundi ya mzunguko wa 4, Mwamba wa Lusaka ndani!

Kura yako unampa nani?


Jina halisi ni Constantinos Tsobanoglou lakini wengi mnamtumba kwa jina la Costa Titch ni rapa, dancer na mwimbaji wa Af...
13/03/2023

Jina halisi ni Constantinos Tsobanoglou lakini wengi mnamtumba kwa jina la Costa Titch ni rapa, dancer na mwimbaji wa Afrika Kusini, maarufu kwa nyimbo nyingi zikiwemo Nkalakatha na Activate.

Titch alizaliwa mwaka wa 1995 huko Nelspruit Mpumalanga, Afrika Kusini.

Alianza kupendezwa na mu*iki katika umri mdogo na alikuwa akipenda burudani kila wakati,
Ingawa aliingia katika eneo la burudani akiwa na umri mdogo sana, alianza kazi yake k**a dancer alipojiunga na kikundi cha dance cha New Age Steez.

Kundi hilo lilikua ni kundi maarufu na baadhi ya wanachama walikua maarufu wakiwemo Phantom Steeze na Tumi Tladi walikua wakisumbua sana SA lakini pia kwa kazi hiyo ya kudance Costa alishaonekana kwenye baadhi ya video za wasanii kutoka bongo k**a;

Wanjera ya Usiende mbali ya na Game ya .

Mnamo mwaka 2014, alihamia Johannesburg na kuendelea na kazi yake ya kurap ambapo alipata bahati ya kufanya kazi na wasanii wakubwa akiwemo Cassper Nyovest.

Mafanikio yake ya mu*iki yalifuatia kutolewa kwa wimbo wake wa ,

Costa ni miongoni mwa waanzilishi wa mu*iki wa trap wa Kiafrika na pia ameathiri wasanii wengine wa aina hiyo.

Costa pia alikua akitunga mistari ya Isizulu katika rap zake na mara nyingi rapu zake zilikua nyepesi moyoni.

Nyimbo zake mara nyingi zilielekezwa kwa sakafu ya dance. ‘Nkalakatha’ na 'Phezulu' feat. Bioty, rapa kutoka Afrika Kusini ndo nyibo ambazo zilimjengea jina katika anga za burudani ndani na nje ya nchi na alipata collaborations nyingi na wasanii k**a ndani na nje ya SA ambapo hapa bongo alifanya na pamoja na

February 8 mwaka huu ilisemekana Costa amesainiwa katika record label ya Konvict Kulture inayomilikiwa na msanii Akon tetesi hizi zilionekana kuwafurahisha mashabiki wa Costa lakini sasa hivi ndoto za msanii huyo zimezimika tayari hii ni baada ya dunia na tasinia ya mu*iki kupokea taarifa mbaya kupitia page ya
Rapa huyo wa Afrika Kusini alianguka jukwaani alipokuwa akitumbuiza wakati wa Tamasha kuu la Jumamosi, Machi 11, 2023 katika ukumbi wa Expo center huko mjini Johannesburg.

Jan March 12 kifo chake cha kushangaza kimethibitishwa na familia yake.

R.I.P 🙏

UKIACHA ‘SUBS’ ZA NABI, YANGA INASHINDA KUTOKANA NA ‘FITNESS’ KUBWA ZA WACHEZAJI - Edo kumwembe “Watu wengi wanasifia Ma...
13/03/2023

UKIACHA ‘SUBS’ ZA NABI, YANGA INASHINDA KUTOKANA NA ‘FITNESS’ KUBWA ZA WACHEZAJI - Edo kumwembe

“Watu wengi wanasifia Mabadiliko (substitutions) anazofanya Kocha Nabi lakini mie pia naona Kocha wa Viungo Yanga amewafanya Wachezaji kuwa na Fitness kubwa sana”

“Hebu angalia namna wachezaji wa Yanga wanavyocheza, namna wanavyo ‘react’ mchezoni, hata goli la Mzize ile reaction yake ni kutokana na utimamu wa mwili wake”

Klabu ya yanga imetoa taarifa juu ya mchezaji wake Kennedy Musonda kupokea Zawadi ya medali kutoka nchini Hispania.Taari...
13/03/2023

Klabu ya yanga imetoa taarifa juu ya mchezaji wake Kennedy Musonda kupokea Zawadi ya medali kutoka nchini Hispania.

Taarifa kamili kutoka hii hapa chini👇

Leo asubuhi mchezaji wetu Kennedy Musonda_ Jr] amepata nafasi ya kupokea zawadi ya medali kutoka kwa mtoto Lucas Gomez Usoz kutoka Spain.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 8 anayeishi mjini Madrid nchini Spain alituma Medali hiyo kupitia ubalozi wa Spain (TZ) na kukabidhiwa rasmi leo na Balozi Jorge Moragas mbele ya Rais wa Klabu yetu k**a sehemu ya kuvutiwa na uchezaji wa Kennedy Musonda_ Jr] baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi akiwa anaitumikia klabu yake ya zamani ya Power Dynamos FC ya nchini Zambia.

Hafla hii fupi iliyoandaliwa na balozi ilifanyika kwenye makazi yake eneo la Oyster bay, jijini Dar es salaam.

Wananchi wana jambo lao mchana huu.... Endelea kufatilia Manara Tv kwa taarifa zaidi.
13/03/2023

Wananchi wana jambo lao mchana huu.... Endelea kufatilia Manara Tv kwa taarifa zaidi.


Usha Subscribe  YouTube channel yetu ya  ??K**a bado kafanye hivyo sasa , ili uweze kushuhudia live stream tukio hili ku...
10/03/2023

Usha Subscribe YouTube channel yetu ya ??

K**a bado kafanye hivyo sasa , ili uweze kushuhudia live stream tukio hili kubwa la Haji Manara .

Follow social media zetu zote kwa Update mbalimbali za matukio yote hapo kesho .

"Tunachokifanya kwenye Simba Beach Party ni kuufanya mchezo kuwa Live , kuvutia zaidi ili Watu tuanze kuishi tarehe 7 ka...
05/03/2023

"Tunachokifanya kwenye Simba Beach Party ni kuufanya mchezo kuwa Live , kuvutia zaidi ili Watu tuanze kuishi tarehe 7 kabla ya haijafika, hii ni k**a FIESTA hivi kuna matukio mengi kuelekea siku ya ya tukio"

"Sasa hivi tayari msafara umefika Coco Beach Watu wanakula burudani , kuna Kigoma cha , mwisho ni michezo ni k**a FIESTA flani la Kibonanza hivi" -

Afisa habari wa Simba SC


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwasalimia Wananchi wa USA River Jijini Arusha leo amesema hawachukul...
05/03/2023

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwasalimia Wananchi wa USA River Jijini Arusha leo amesema hawachukulii Wapinzani k**a Maadui bali anawachukulia kuwa ni Watu wanaomuonesha changamoto ili aweze ku*itatua.

“Mtanzania yeyote awe Chama chochote cha siasa tunachotofautiana ni mawazo tu na fikra lakini pia Mimi sichukulii Wapinzani k**a Maadui, nawachukulia k**a Watu watakaonionesha changamoto zilipo nizitekeleze ili CCM iimarike”

“Kwahiyo Mdogo wangu (Lema) amerudi ameniambia ‘Mama nataka kurudi’ nikamwambia rudi, akasema ‘Mama nina kesi’, nikamwambia nazifuta rudi, amerudi tuimarishe siasa si ndio?”

“Mwanaume ni yule anayejiamini, Mwanamke ni yule anayejiamini, kwahiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini tupo vizuri na tutakwenda vizuri, nawashukuru Watoto wangu wa Bodaboda, Bodaboda mpooo, wamenisindikiza toka Mjini mpaka hapa, mwendo ni huohuo mpaka 2025, nawatambua”


Kesho ni marejeo ya shauri la FEISALI SALUM  na Yanga SC mbele ya k**ati ya sheria, haki na hadhi za wachezaji ya TFF. H...
01/03/2023

Kesho ni marejeo ya shauri la FEISALI SALUM na Yanga SC mbele ya k**ati ya sheria, haki na hadhi za wachezaji ya TFF.

Hii inakuja baada ya upande wa feisal kutoridhia maamu*i ya k**ati baada ya kikao cha hapo awali.

AMEANDIKA HAJI MANARA Kupitia Instagram acc yake......" Why leo ndio ionekane aliteseka sana? Aliteswa Kwa njia gani? Ha...
01/03/2023

AMEANDIKA HAJI MANARA
Kupitia Instagram acc yake......

" Why leo ndio ionekane aliteseka sana? Aliteswa Kwa njia gani? Hakulipwa haki zake gani za mkataba? Aliwahi kudhulumiwa chochote alichostahili?

Aliwahi kunyimwa Chakula kambini au Bonus wanazopewa wengine? Kuna Mshahara wowote au hata posho yoyote aliyowahi kunyimwa?

Na kwa nini hizi Clips mara nyingi zinatembea siku k**a ya leo? Nini dhamira yake?

Hivi baina ya pande mbili nani anaestahili kulalamika na nani aliyemdhulumu mwenzie hyo haki ?

Mungu tunaemlilia anazijua nafsi zetu na anatujua tuliyoyafanya, tumlilie kwa misingi sahihi, sio kutafuta huruma siku moja kabla ya hukumu.

Ni kutoa shinikizo tu kwa Mamlaka bila sababu na kuna Watu hii imekuwa desturi zao ila ajue mwisho unakaribia na kwa kesho tuache vyombo vifanye maamu*i yake bila shinikizo la huruma na kuonekana kuna Mtu aliwahi kuteswa.

Unateswa vipi kwa mkataba uliousaini mwenyewe ? Kisa una ofa nyingine ndio leo ionekane Mtu aliteseka?
Mungu gani tunaemlilia ?

Ittaqi llah Ittaqi lllah, haki ina pande mbili za Shilingi na tunapoidai tufahamu na wale wa upande mwingine nao wanastahili haki.

Nimalize kwa kuweka wazi, unapopata sehemu nyingine yenye maslahi kwako ni vema ukafata taratibu za kisheria , kuja mitandaoni kusema uliteseka sana bila kutaja hayo mateso kisa huko kwingine may be kuna ahadi kubwa ni kutowatendea hiyo haki tunayoililia kwa Muumba wetu."........

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi ratiba ya safari yao kuelekea nchini Uganda leo jioni kwa...
23/02/2023

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi ratiba ya safari yao kuelekea nchini Uganda leo jioni kwa ajili ya kucheza na Vipers ya nchini humo Jumamosi.

Simba SC inatarajiwa kuwafuata Vipers fc kunako jiji la Kampala kucheza mchezo wa Klabu bingwa Afrika, huku ikiwa haina alama hata moja baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza.

Ahmed kupitia akaunti yake ya Instagram ametoa taarifa inayosema kwamba.

"Kikosi chetu kinatarajiwa kuondoka leo jioni kuelekea Uganda kuwafuata Vipers. Huu ni mchezo muhimu kwetu, ambao utatoa taswira ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa msimu huu.

" Mechi hii inatuhitaji Wanasimba kuunganisha nguvu ili kufanya vizuri.

Hatuna namna zaidi ya kushik**ana na kupambana kila idara ili tupate matokeo yatakayofufua matumaini yetu. Njia pekee ya kufanikiwa kwenye nyakati ngumu ni kuwa wamoja na kutazama mbele.

" Inawezekana kuchukua alama tatu Uganda. Twendeni Wanasimba💪 Haijaisha mpaka iisheeeeee🦁🦁"
_________________________

Simba🎉
04/11/2022

Simba🎉

Address

Chunya
Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Manara tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Manara tv:

Share