BADO KUNA Tumaini

BADO KUNA Tumaini Purpose of this page is Preaching word of God and prayer online.

22/07/2023
09/10/2022

Sifa time ndani ya Talitha Cumi

17/07/2022

Karibu uabudu nasi

Mambo yote kwa Yesu
25/06/2022

Mambo yote kwa Yesu

15/06/2022

Mafanikio yoyote yanasababu

USISAHAU  KUMBUKA Maneno hayo mawili ni maneno muhimu sana katika mfumo wa maisha ya kila siku.. Wahenga walikuwa na man...
23/05/2022

USISAHAU KUMBUKA
Maneno hayo mawili ni maneno muhimu sana katika mfumo wa maisha ya kila siku.. Wahenga walikuwa na maneno ya hekima sana k**a 👉Usisahau ubaharia kwa sababu ya unaodha. Maana yake kumbuka ulikotoka.
Neno Usisahau ni neno la muhimu sana pia ni neno hatari sana. K**a kusahau kusingekuwepo leo hii dunia ingelikuwa ni bonde la hofu, kushindwa na kufadhaika. Mfano unamkuta mama akiwa katika hali ngumu kipindi anakaribia kujifungua uchungu mkubwa usioweza kubebeka mpaka kwa hudhuni anadiriki kusema mimi sizai tena si kwamba amependa kusema maneno hayo amelazimishwa na hali au mkulima amewekeza ardhini mtaji mkubwa mno mwaka huo mvua hazinyeshi vizuri kila kitu kinaharibika. Au kuna watu waliofanyiwa mambo mabaya, visa, fitina au kupitia mateso mengi lakini baadaye anasahau na anasonga mbele. Ingawa unakuwa umepita hayo madhira na mateso fahamu yakuwa na hilo litapita kwani ndio daraja lako na kipimo cha kesho yako. Neno usisahau limeandikwa karibu mara mbili kwenye biblia ;

Kumbukumbu la Torati 25:19
[19]Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.
Kumbukumbu la Torati 9:7
[7]Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA.

Mungu anatukumbusha kuwa ingawa umefanikiwa leo lakini ni vema ukakumbuka njia uliyoipitia. Watu wengi leo wamesahau walikotoka. Ashibae hamjui mwenye njaa. Hivyo ulivyo leo si kwamba unaakili sana au mjanja kuliko wote. Kumbuka akili haukuzipata leo ulikuwa nazo tangu zamani lakini mwanzo hazikukusaidia maana yake si kwa akili zako upo jinsi ulivyo, bali ni kwa neema ya Mungu. Mungu anawaambia Wana wa Israeli.

Kumbukumbu la Torati 15:15
[15]Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa BWANA, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 8:18
[18]Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, k**a hivi leo.

Watu wengi leo hawakumbuki walikotoka njia uliuoipitia usiitie uchafu kuzuia wengine wasiipitie. Daraja ulilopitia wako wengine wanalisubiri ili liwavushe usiliondoe. Ubinafsi ni dhambi mbaya mno ambayo imewafunga wengi ni vizuri ukayatumia maneno haya mawili USISAHAU na KUMBUKA kujenga mustakabari wako sahihi . Jua k**a leo wewe umekula ukashiba wapo walio na njaa na k**a wewe leo ni mzima wapo wagonjwa hali hizi zikunyenyekeze ujuwe kuwa si kwa uweza wako hivyo ulivyo.
Kumbuka Tajiri alimuona maskini akiokota chakula jalalani akasema mimi sio k**a masikini huo ninakula ninashiba na ninasaza. Masikini akamuona mtu amepata ajali mbaya amevunjika miguu yote abakimbizwa hospital kwenye wodi ya mahututi akasema mimi sio k**a huyo asiyejiweza amekuwa kiwete mimi ingawa ninaokota makombo lakini nina viungo vyangu vyote. Yule majeruhi wodi akashuhudia waganga wakihangaikia maisha ya mgonjwa mwingine hatmaye alikufa akapelekwa Mochwari yule mahututi akasema afadhali mimi ingawa ni mahututi lakini mimi si k**a mtu yule amekwenda kwenye ukimya hawezi kufanya chochote ingawa mimi ni kilema nitatumia mdomo kuelekeza. Marehemu hand cha kufanya kila kitu anafanyiwa hata yale asiyoyapenda. Usidharau ulivyo ikiwa unauzima ndani yako kwani hujui kesho itakuaje. Tumia vizuri hali uliyonayo leo kwa faida ya kedho. Ukifanikiwa jitahidi kuwasaidia wengine na kuwawezedha usiondoe daraja. Wanyamwezi wanamsemo usemao Mapuri gagwiwochaga (Tembo hunyanyuana)
Heshima yako iko kwa wengine fahari ya mrefu kwa sababu kuna mfupi, heshima ya tajiri kwa sababu kuna masikini. Kipimo cha ulivyo kipo kwa wengine. Fanya uamuzi sahihi sasa na kubadilisha mtazamo. Amen

17/05/2022

Ibenge 🗣️Nilisha sema timu yeyote ambayo inafanikisha kuifunga klabu ya pili kwa kuwa na mashabiki wengi Africa klabu ya Simba Sc basi hiyo timu inaweza kwenda fainali ya michuano hii ya CAF

Wengi walinisema sana niliposema kuwa tutafika fainali baada ya mechi ya mwanzo kufungwa goli 1-0 dhidi ya TP Mazembe na leo tupo fainali

Jambo ambalo nalifikili muda wote ni sisi tulistahili kucheza fainali hii na Simba Sc kwa hakika Africa nzima ingesimama juu ya fainali hii iwapo tungecheza na Simba Sc

Simba ilikuwa ni moja ya timu bora sana katika michuano hii ila sijajuwa Orando walitumia mbinu gani kuitoa Simba Sc isifike nusu fainali na k**a ingefika nusu ingefika fainali mechi ingekuwa nzur sana hiyo fainali maana tungekutana tunaolijua soka sasa hapa tumeachiwa kombe ni letu Berkane hili

FT RS Berkane 4-1 Mazembe

Fainali
Orando Pirates vs Rs Berkane

Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye
12/05/2022

Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye

11/05/2022

Mchungaji wa kanisa la Talitha Cumi Daniel Amewaombea wanafunzi kidato Cha Sita kuelekea mitihani wa Taifa mwaka 2022 Jijini Dodoma.

11/05/2022

kanisa la Talitha Cumi limetoa msaada wa kadi za bima ya Afya kwa wanainchi wanaoishi katika mazingira magumu/makundi maalumu wapatao 75 kutoka kata ya Tambu...

Address

Railway
Dodoma
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BADO KUNA Tumaini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Category


Other TV Channels in Dodoma

Show All