10/09/2024
NZI HATUI KWENYE CHUNGU CHA MOTO
"The boiling pot, flies come not".
Rafiki yangu salamu! Leo njoo tutete jambo kubwa, watu waliofanikiwa ni wasomaji wazuri wa vitabu. Hawasomi vitabu wanavyovipenda tu, bali husoma vitabu hasa vile vigumu kuvielewa na havisomwi na watu wengi. Kwa kuwa umejitoa kufanikiwa wekeza kwenye kusoma vitabu. Kumbuka siyo wote wanaosoma vitabu wanafanikiwa bali wote waliofanikiwa wanasoma vitabu. Baada ya utangulizi naomba twende tujifunze kauli hiyo iliyowahi kutumiwa sana na moja ya waasisi na mwandishi wa Taifa la Marekani bwana Benjamin Franklin karne ya 18.
Nzi hatui kwenye chungu cha moto, ni kauli inayosadifu maisha yetu leo. Tupo kwenye ulimwengu wa mvurugo,kelele nyingi na ushindani. Watu wanahangaika na ushindani kwenye biashara, vyeo, na hata fursa. Ajira zimekuwa haba, watu kukicha wanahitimu pasipo kujua wapi wanakwenda. Elimu imekuwa ikiwaahidi mafanikio makubwa na wakitoka shuleni wanagundua walikuwa wanatapeliwa. Biashara zinaanza na kufa, zinakabiliwa na ushindani mkali. Watu wanaigana kila leo. Kwenye muziki usiseme. Kauli za anawaibia nyota ndo zimepewa kipaumbele.
Jamii imehamia kwenye kuwasema vibaya watu wanaofanikiwa, waliotajirika wanaitwa Freemasons kwamba wamepata utajiri kwa njia za kutoa kafara za damu, watu waliofanikiwa kupanda vyeo wanasemwa wametoa rushwa ya ngono, wengine ndugu na maboss, ukiajiriwa watasema kuna namna umefanya. Shule zikifaulisha sana zinasemwa wameiba mitihani. Mafelia wana kelele nyingi. Wengine wanatoa shuhuda za uwongo ili tu kuihadaa jamii, mara nimetumia mafuta ya upako sasa ninauza laki tano kwa siku, ila nyie. Nilikuwa sivuni mazao ya kutosha tangu nianze kutumia maji haya ya mtume sasa navuna gunia nyingi. Kuna mmoja kaibuka na sauti mbaya k**a Kamera chura, anadai mwimbaji aliyefariki wa Zabron Singers alikuwa Freemasons. Watu wanahadaika kirahisi sana.
Kauli ya Benjamin Franklin inatuambia ili ufanikiwe kuudhibiti ushindani hakikisha unakuwa chungu cha moto. Nzi ni wapinzani wako, washindani wako au marafiki wanaokupotezea muda wa kufokasi na malengo yako. Ukiwa chungu cha moto hakuna nzi atatua. Kwenye makala ya "TAI HA