JAGO TV

JAGO TV This is official JAGO TV page, for more informations,educations and entertainment please follow us,

Baada ya tuhuma zinazomkumba mfanyabiashara Niffer pamoja na Mtangazi Diva the bawse za kuchangisha michango ili kusaidi...
20/11/2024

Baada ya tuhuma zinazomkumba mfanyabiashara Niffer pamoja na Mtangazi Diva the bawse za kuchangisha michango ili kusaidia waliokumbwa na maafa ya kuangukiwa na Ghorofa kariakoo, hatimaye wawili ao wanaandika barua za kuomba msamaha kwa kujutia walichokifanya.

Una maoni yoyote kuhusu u*i mpya wa Yanga sc, tukutane kwenye comments.
20/11/2024

Una maoni yoyote kuhusu u*i mpya wa Yanga sc, tukutane kwenye comments.

RONALDO ATUPIA TENA .Na Ignas MyovelaNyota wa time ya taifa ya Ureno na klabu ya Al Nasr ya Saudi Arabia ameendeleza mak...
16/11/2024

RONALDO ATUPIA TENA .

Na Ignas Myovela

Nyota wa time ya taifa ya Ureno na klabu ya Al Nasr ya Saudi Arabia ameendeleza makali yake baada ya kutupia mabao mawili katika michuano ya kimataifa .Cristiano Ronaldo aliifungia timu yake ya Ureno katika mchezo dhidi ya Poland ya Lewandowski

Katika ushindi huo Ureno waliibuka na mabao matano kwa moja huku Cristiano Ronaldo akifunga mabao haya katika dakika ya 72’ kwa mkwaju wa penati na kisha dakika ya 87’ akipokea asisti kutoka kwa Vitinha .

Baada ya ushindi huo Ureno wamefanikiwa kukusanya jumla ya alama 13 katika kundi la kwanza wakifuatiwa na Croatia mwenye alama 7 ,Poland 4 na Scotland ambao wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 4.

Kwa upande wa Cristiano Ronaldo kufunga mabao hayo kunamfanya afikishe jumla ya mabao 910 kwenye maisha yake ya soka huku hesabu zake zikiwa na kuyafikia mabao 1000 ili kuendelea kuilinda rekodi yake ya ufungaji

SIMBA NI MWENDO WA DOZI TU !!!Klabu ya simba  sports club  imeibuka na ushindi  mnono wa mabao manne (04) kwa sifuri (0)...
06/11/2024

SIMBA NI MWENDO WA DOZI TU !!!

Klabu ya simba sports club imeibuka na ushindi mnono wa mabao manne (04) kwa sifuri (0)dhidi ya klabu ya KMC mabao ya Simba yamewekwa Kambani na aliekuwa mchezaji wa zamani wa KMC Awesu Awesu 25’ ,Ahoua J.C 38’ ,69’na Balua 67’.
Baada ya ushindi huu klabu ya simba inafikisha alama 25 katika michezo kumi na kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC huku KMC ikisalia katika nafasi ya saba na alama kumi na nne .
Cc:

Donald trump ashinda uchagu*i Marekani. *i  *imarekani
06/11/2024

Donald trump ashinda uchagu*i Marekani.
*i *imarekani

🔥🔥
26/10/2024

🔥🔥

SUBSCRIBE YOUTUBE JAGO TV
26/10/2024

SUBSCRIBE YOUTUBE JAGO TV

MGOMBEA URAIS JELA MIAKA 12 TUNISIAZammel ambaye ni mbunge wa zamani na mfanyabiashara anaongoza chama kidogo cha kilibe...
02/10/2024

MGOMBEA URAIS JELA MIAKA 12 TUNISIA
Zammel ambaye ni mbunge wa zamani na mfanyabiashara anaongoza chama kidogo cha kiliberali na amekuwa ni mmoja kati ya wagombea wawili walioidhinishwa na Tume ya Uchagu*i ya Tunisia kupambana na Rais Kais Saed katika uchagu*i huo wa rais.

Wakili wa Ayachi Zammel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba bado mwanasiasa huyo anabakia kuwa mgombea katika uchagu*i huo wa rais unaofanyika siku ya Jumapili (Oktoba 6).
Tume ya uchagu*i imewazuia kiasi cha wagombea wengine 14 kuwania kwenye uchagu*i huo.

IRAN YAISHAMBULIA MAKOMBORA 180 ISRAEL KULIPA KISASI  Iran Jumanne imefanya shambulizi kubwa la makombora dhidi ya Israe...
02/10/2024

IRAN YAISHAMBULIA MAKOMBORA 180 ISRAEL KULIPA KISASI Iran Jumanne imefanya shambulizi kubwa la makombora dhidi ya Israel, hatua ambayo inaashiria kusambaa kwa mzozo kati ya Israel na mataifa ya Kiislamu ya kieneo.

Jeshi la Israel limesema kuwa kombora la kwanza kutoka Iran lilirushwa saa moja na nusu jioni kwa saa za huko, na kisha kuendelea kwa takriban nusu saa. Ripoti zimeongeza kusema kuwa Iran ilirusha takriban makombora 180.

Chombo cha habari cha serikali ya Iran, IRNA, kilionyesha video ya mashambulizi hayo kupitia ukurasa wake wa Telegram.

Pia taarifa ilitolewa kwamba jeshi la Iran na Revolutionary Guard Corps, IRGC, lilishambulia “ malengo ya kiusalama na kijasusi” ndani ya Israel, k**a njia ya kulipiza kisasi kutokana na mauaji ya Julai, ya kiongozi wa Hamas wa Kipalestina, Ismail Haniyeh mjini Tehran, pamoja na mauaji ya karibuni ya mak**anda wengine wa Hezbollah nchini Labanon.

Ijumaa iliyopita, Israel iliua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah kwenye kituo cha kundi hilo kusini mwa Beirut. Brigedia Jenerali wa jeshi la Iran Abbas Nilforoushan pia aliuwawa wakati wa shambulizi hilo. Kufikia sasa, Israel haijakiri wala kukana kuhusika kwenye kifo cha Haniye.
Iran imesema kuwa shambulizi la Jumanne dhidi ya Israel liliidhinishwa na Baraza la Usalama la Kitaifa la Iran, lililopo chini ya ofisi ya kiongozi wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei.

   wamethibitisha kumsajiri kiungo mshambuliaji raia wa DRC CONGO Elie Mpanzu (22) kwa mkataba wa miaka 2.Ikumbukwe Mpan...
30/09/2024

wamethibitisha kumsajiri kiungo mshambuliaji raia wa DRC CONGO Elie Mpanzu (22) kwa mkataba wa miaka 2.

Ikumbukwe Mpanzu kabla ya kwenda majaribio katika klabu GENT ya ubelgiji na kufeli majarbio hayoo alkua katika kikosi Cha AS VITA CLUB na kufanikiw kumalza msimu k**a mfungaji Bora

Usjili🔥🙌

tunalalamikaa Leo au kesho😂🔥

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya...
28/09/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Taifa katika ukumbi wa Parokia ya Bombambili, Wilaya Songea Mkoani Ruvuma, leo tarehe 28 Septemba, 2024.

Msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki, maarufu k**a Nay wa Mitego,  amesh*takiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata...
28/09/2024

Msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki, maarufu k**a Nay wa Mitego, amesh*takiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa makosa manne yanayohusiana na wimbo wake wa 'Nitaserna."

Nay aliwasili nje ya ofisi za Basata jijini Dar es Salaam mchana wa jana, 27 Septemba 2024, ambapo wakili wake, Jebra Kambole, alizungumza na vyombo vya habari, akisema, Basata imemshtaki kwa makosa manne.

Aidha aliweka wazi kuwa sh*taka la kwanza linadai kuwa Nay aliachia wimbo huo bila kibali cha Basata na kwamba amevunja kifungu cha 25 cha kanuni za Basata.

Huku sh*taka la pili likihusu madai ya kuwa wimbo wa 'Nitasema' unachochea machafuko ikidai kuwa serikali inahusika na utekaji nyara na mauaji. "Wanasema kuna sehemu za wimbo huo zinazochochea machafuko kwa kudai kuwa Serikali inahusika na utekaji nyara na mauaji," alisema.

Kambole alifafanua kuhusu sh*taka la tatu, akibainisha kuwa linahusisha kauli potofu zinazoashiria kuwa Serikali imeanzisha miradi lakini imeshindwa kuitekeleza, jambo ambalo Basata linatafsiri k**a ukosoaji wa utendaji wa serikali. "Walisema kosa la tatu linaonesha kuwa serikali haijatekeleza baadhi ya miradi," ameeleza.

Hata hivyo, sh*taka la nne linamtuhumu Nay kukashifu mataifa mengine kwa kutaja nchi za Rwanda na Congo katika mistari ya wimbo wake.


  Mkurugenzi wa klabu ya Manchester United Omar Berrada ameweka wazi kuwa lengo la klabu ya Man United kutwaa kombe la L...
28/09/2024

Mkurugenzi wa klabu ya Manchester United Omar Berrada ameweka wazi kuwa lengo la klabu ya Man United kutwaa kombe la Ligi kuu ya England (EPL) ni mwaka 2028.

Ambapo mwaka huo (2028) Man United itakuwa inaadhimisha Miaka (150) tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1878.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Manchester United kutwaa kombe la Ligi kuu ilikuwa msimu wa 2012-13 ikiwa chini ya Kocha Sir Alex Ferguson.

Mashabiki wa UNITED furahaa mpaka 2028😀😀


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa ametaja chanzo cha ajali iliyoua watu 12 na kujeruhi 23, akisema ni ...
28/09/2024

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa ametaja chanzo cha ajali iliyoua watu 12 na kujeruhi 23, akisema ni dereva kushindwa kuchukua tahadhari kwenye mteremko na kusababisha gari kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea jana Septemba 27, 2024 baada ya gari aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likitokea Mbalizi kuelekea kwenye mnada katika kijiji cha Jojo, Kata ya llembo wilayani Mbeya kuacha njia na kupinduka.

Hii ni ajali ya tatu ndani ya mwezi huu, ikitanguliwa ile ya Septemba 4, iliyohusisha basi la kampuni ya Shari Line iliyoua watu tisa na kujeruhi wengine 18 huko Kata ya Chimala wilayani Mbarali na kampuni ya A-N Classic iliyoua 12 na kujeruhi 44, Septemba 6.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 28, 2024, Kamanda Siwa amesema ajali hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi.

"Dereva alikimbia baada ya ajali, Polisi inaendelea kumsaka wakati majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Afya Illembo.

"Tunatoa wito kwa madereva ku*ingatia sheria za usalama na kuacha kupakia abiria kwenye magari ya mizigo," amesema Kamanda Siwa.


Mfanyabiashara Maarufu katika Falme za Kiarabu Dubai anayefahamika kwa jina la Jamal Nadak ameamua kumnunulia mke wake S...
27/09/2024

Mfanyabiashara Maarufu katika Falme za Kiarabu Dubai anayefahamika kwa jina la Jamal Nadak ameamua kumnunulia mke wake Soudi Nadak kisiwa kilichopo Asia chenye thamani ya dola milioni 50 kwaajili ya kumfurahisha.

Nadak Mwenye umri wa miaka 26 ni Miongoni mwa Wanawake wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii ambapo alichapisha habari hizo kupita ukrasa wake wa Instagram ambapo aliandika.

"Ulitaka kuvaa bikini ili mume wako milionea akununulie kisiwa."

Thamani halisi ya kisiwa hicho haijawekwa wazi kwa sababu za faragha na usalama, lakini Soudi alitaja kuwa kiko Asia na kiligharimu dola milioni 50.

"Kwa sababu za faragha hatushiriki eneo halisi lakini ni Asia na ilikuwa dola milioni 50," alisema.


Muonekano wa shule ya sekondari ya wasichana inayotambulika kwa jina la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Su...
27/09/2024

Muonekano wa shule ya sekondari ya wasichana inayotambulika kwa jina la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Ujenzi wa shule hiyo yenye uwezo kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 kwa mkupuo umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 4, 643.

Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan mpaka sasa ina wanafunzi 548 ambao kati yao 420 ni wa kidato cha tano na sita, na 128 ni kidato cha kwanza. Ina mabweni tisa yakiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila bweni, ikiwa pia na bwalo la kulia chakula lenye uwezo wa kuchukua watu 1000 na likitumika pia k**a ukumbi wa mkutano.

Uandaaji wa chakula katika bwalo hilo unatumia mfumo wa gesi uliowekwa na Wizara ya Nishati na wadau wengine ili kuondokana na changamoto ya kutumia mkaa na kuni.


Baada ya miaka zaidi ya mitano kupita leo, septemba 27 Wakili Tundu Lissu anaongoza kesi inayomhusu mteja wake Askofu ma...
27/09/2024

Baada ya miaka zaidi ya mitano kupita leo, septemba 27 Wakili Tundu Lissu anaongoza kesi inayomhusu mteja wake Askofu maxmilliam Machumu maarufu k**a Askofu Mwanamapindu*i mkoa wa Singida.


Hija Harnis Msumi (16) Mwanafunzi ya Kidato cha Tatu, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti, mkoa wa k...
27/09/2024

Hija Harnis Msumi (16) Mwanafunzi ya Kidato cha Tatu, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti, mkoa wa kipolisi Rufiji, amehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 12, kwenye makalio mbele ya mahak**a kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la Nne mwenye umri wa miaka 12.

Mahak**a imemuamuru msh*takiwa huyo kumlipa muhanga fidia ya Shilingi laki 5, kwa madhara ambayo amemsababishia mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mahak**a imesema msh*takiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya mwezi Agosti na Novemba, 2023, huko Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti.


Address

Dodoma

Telephone

+255659842457

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JAGO TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to JAGO TV:

Videos

Share

Category