Torch Tv tz

Torch Tv tz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Torch Tv tz, TV Channel, Dar es salaam, Dar es Salaam.

*HATIMAE FAMILIA YA MAMA AMINA MOHAMED MUGHENYI YAPOKEA HUNDI YA FIDIA SHANTA* Familia ya Mama amina mohamed mghenyi wa ...
21/09/2022

*HATIMAE FAMILIA YA MAMA AMINA MOHAMED MUGHENYI YAPOKEA HUNDI YA FIDIA SHANTA*

Familia ya Mama amina mohamed mghenyi wa kitongoji cha taru kijiji cha Mang'onyi kata Mang'onyi jimbo la singida mashariki wamefikia muafa na ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa kuridhia kupokea hundi ya fedha ikiwa ni fidia ya malipo ya eneo lao ambalo limechukulia na kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Shanta kwa ajili ya upanuzi wa mgodi huo

Akizungumza mara baada ya kupokea hundi Bi. Amina Mohamed Mughenyi amesema ameridhishwa na mchakato w tathmini na kiwango alicholipwa mara baada ya kueleweshwa kwa kina na vielelezo na yeye kupata muda wa kushauriana na familia yake na hatimae kukubali kupokea hundi hiyo

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameshukuru kuona mazungumzo aliyoyasimamia kwa zaidi ya miezi kadhaa yamefikia mwisho kwa pande zote kuridhiana hatua ambayo amesisitiza imeongeza ushirikiano baina ya mwekezaji na wananchi wanaozunguka mgodi

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama imefanya kikao kazi chenye lengo la kutengeneza mpango kazi wa kuh...
20/09/2022

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama imefanya kikao kazi chenye lengo la kutengeneza mpango kazi wa kuhamasisha na kutoa elimu juu ya uchangiaji wa damu wa hiari kwa wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali Nchini.

Mpango huu utawezesha Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu salama kuwa na idadi kubwa ya wachangiaji damu wa hiari na kuwezesha ukusanyaji wa damu utakaokidhi Nahitaji ya nchi.

Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na maafisa habari, maafisa utumishi na rasilimali watu kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali, Binafsi na za Dini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Philip Mpango amesema katika kuelekea mwaka 2030, mataifa yan...
20/09/2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Philip Mpango amesema katika kuelekea mwaka 2030, mataifa yanapaswa kujitoa upya na kuazimia kuongeza uwekezaji zaidi katika sekta ya elimu kwa nia kuhakikisha Watoto wanapata elimu iliyo bora na ya uhakika.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akitoa hotuba katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliobeba ajenda ya Mageuzi katika sekta ya elimu ulioshirikisha wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali, wakuu wa taasisi na mashirika pamoja na wadau wa elimu.

19/09/2022

Serikali kupitia waziri wa Michezo Mohamed Mchengerwa ameipongeza klabu ya Simba kwa ushindi mnono waliyo upata baada ya kuifanga Nyasa Big Bullet 2-0 hapo katika uwanja wa taifa.

Mwili wa Malkia Elizabeth II utapumzishwa hii leo baada ya siku kadhaa za kuaga, mwili utasafirishwa Westminster Abbey k...
19/09/2022

Mwili wa Malkia Elizabeth II utapumzishwa hii leo baada ya siku kadhaa za kuaga, mwili utasafirishwa Westminster Abbey kwa ibada ya kidini mbele ya maelfu ya watu, na kisha kupelekwa Kasri la Windsor kwa ibada ya kifamilia na watu wa karibu na hatimaye kuzikwa kibinafsi.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Malkia El...
19/09/2022

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza aliyefariki Septemba 08, 2022. Rais Samia amesaini kitabu hicho katika jengo la Lancaster (Lancaster House), London, Uingereza.

Surua au kwa Kiingereza “measles” ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. Ugonjwa wa surua unaweza kumpata mtu wa rika lolo...
19/09/2022

Surua au kwa Kiingereza “measles” ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. Ugonjwa wa surua unaweza kumpata mtu wa rika lolote ila huathiri zaidi watoto. Dalili za awali za surua ni koo kuuma, kikohozi , homa na madoa ya rangi ya kijivu au nyeupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. Baada ya siku chache, upele mwekundu hutokea.

Hamna tiba maalum ya surua ingawa kupumzika na kunywa maji ya kutosha ni muhimu sana. Homa inaweza kudhibitiwa kwa dawa ikiwa inamfanya mtu kujihisi mgonjwa. Watu wenye surua wanaweza kuwaambukiza wengine wanapoanza kuwa na dalili za awali hadi siku 3 - 4 baada ya upele kutokeza. Watu wengi wenye surua hupata nafuu ndani ya wiki moja toka dalili za awali kujitokeza.

16/09/2022
Wafanyakazi wa Kurugenzi ya Ufundi Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga wamejumuika pamoja kusherekea sherehe ya kuwaaga ...
16/09/2022

Wafanyakazi wa Kurugenzi ya Ufundi Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga wamejumuika pamoja kusherekea sherehe ya kuwaaga waliokuwa wafanyakazi katika kurugenzi hiyo ambao wamestaafu.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji Prof. Lawrence Museru, ambaye aliwashukuru wastaafu hao sita akiwemo aliyekuwa Mkurugugenzi wa Ufundi Mhandisi Gaudence Aksante kwa utumishi mwema uliotukuka huku akiwatakia maisha mema nje ya utumishi wa umma.

16/09/2022

Jeshi la polisi Tanzania limepiga marufuku kupita kwenye bara bara ya mwendokasi isipokuwa mabasi yenyewe ya mwendokasi tu.

Hii imekuja Baada ya kusambaa video ikionyesha polisi wakizozana na walinzi/wafanyakazi wa Mwendokasi wakizuia gari la polisi lisipite kwenye bara bara la mwendokasi.
tanzania

Kitengo cha magonjwa ya saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda  leo Septemba 15, 2022, wameadhimisha siku ya uelewa...
16/09/2022

Kitengo cha magonjwa ya saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda leo Septemba 15, 2022, wameadhimisha siku ya uelewa wa magonjwa ya saratani kwa watoto kwa kufanya matembezi kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuelekea eneo la rock city mall jijini Mwanza.

Aidha maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa wazazi na jamii ya wakazi wa kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla Ili kueneza ujumbe kuwa saratani kwa watoto inatibika iwapo tu ukiwahi vipimo na matibabu mapema.

Dkt Bingwa na bobezi wa magonjwa ya saratani kwa watoto, Hironima Kashaigili amesema, watoto wengi wanaokuja katika Hospitali ya Bugando kutibiwa saratani wakiwa katika hali ngumu kutibika, hivyo anashauri kuwahi mapema hospitali kwaajili ya uchunguzi. Pia ametaja dalili kubwa za ugonjwa wa saratani ni kuvimba tumbo, kupata maumivu makali mwilini, kupungua uzito na mboni ya jicho kuwa nyeupe.

Sambamba na hayo Dkt. Hironima Kashaigili amesema, tafiti mbalimbali zinaendelea kufanyika Ili kubaini chanzo na tatizo la saratani kueneza kwa kasi hasa kwa Kanda ya ziwa.

Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF leo imetangaza kumpunguzia adhabu Msemaji wa Yanga Haji Manara kutok...
15/09/2022

Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF leo imetangaza kumpunguzia adhabu Msemaji wa Yanga Haji Manara kutoka milioni 20 ya faini aliyotakiwa kuilipa hadi milioni 10 huku hukumu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili ikibaki palepale.

Mwenyekiti wa k**ati ya rufaa ya Maadili ya TFF Richard Mbaruku amesema hii ni baada ya kupitia rufaa ya Haji Manara ambayo hata hivyo wameona haina mashiko lakini wakatumia busara ya kumpunguzia faini hiyo.

July 21 2022 Haji Manara alitangazwa kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na faini ya milioni 20 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF Wallace Karia wakati wa mechi ya fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal Union Arusha July 2 2022.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameendelea na zoezi la utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Mhe. Kasim Maja...
14/09/2022

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameendelea na zoezi la utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa ya kumaliza migogoro sugu ya ardhi kwa baadhi ya wananchi wilaya ya Ikungi

Dc Muro amekutana na kufanya mazungumzo na familia ya Mama amina mohamed mghenyi wa kitongoji cha taru kijiji cha Mang'onyi kata Mang'onyi jimbo la singida mashariki kumuomba aridhie kupokea fidia ya kupisha uendelezaji wa eneo la mradi wa ujenzi wa mgodi mpya wa dhahabu wa shanta mradi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 80

Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa sugar umemalizika ambapo yanga imetoka na ushindi wa 3 kwa 0 na matokeo haya kunaip...
13/09/2022

Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa sugar umemalizika ambapo yanga imetoka na ushindi wa 3 kwa 0 na matokeo haya kunaipelekea Yanga kuwa kileleni kwa point 9 huku simba akiwa na point 7 ambapo kesho watashuka dimbani dhidi ya Tanzania prison katika uwanja wa Sokaine Mbaya.

Kikosi cha Taifa stars kitakachoingia Kambini kucheza michezo ya kirafiki.
13/09/2022

Kikosi cha Taifa stars kitakachoingia Kambini kucheza michezo ya kirafiki.

Hiki hapa kikosi cha Stars kitakachoingia kambini kucheza michezo ya kirafiki.
13/09/2022

Hiki hapa kikosi cha Stars kitakachoingia kambini kucheza michezo ya kirafiki.

William Ruto ameapishwa kuwa Rais wa tano wa Taifa la Kenya.Ruto ameapishwa kuwa Rais wa Kenya kufuatia ushindi alioupat...
13/09/2022

William Ruto ameapishwa kuwa Rais wa tano wa Taifa la Kenya.

Ruto ameapishwa kuwa Rais wa Kenya kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 9 mwaka huu akitokea muungano wa Kenya Kwanza.

Jaji Mkuu wa Kenya, Martha Koome ndiye aliyemuapisha Ruto pamoja na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Marais kutoka nchi 16 za Afrika akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania wanashiriki katika sherehe za kuapishwa kwa William Ruto katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Mbunge Tamima Haji Abass akiapa kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa Mkutano wa ...
13/09/2022

Mbunge Tamima Haji Abass akiapa kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa Mkutano wa Nane Kikao cha kwanza cha Bunge leo tarehe 13 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi

Mkuu wa Mkoa wa Njombe ametoa rukhsa kwa Walimu kufundisha Wanafunzi katika muda wao wa ziada ili kupandisha viwango vya...
13/09/2022

Mkuu wa Mkoa wa Njombe ametoa rukhsa kwa Walimu kufundisha Wanafunzi katika muda wao wa ziada ili kupandisha viwango vya taaluma katika Mkoa huo pamoja na kukuza vipato vyao.

Mtaka ametoa rukhsa hiyo katika kikao cha uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa bila kuvunja sheria huku akidai kuwa haoni haja ya kuwazuia kuwa na Tuition binafsi Walimu wakati Kada nyingine wakiwemo Madaktari wamekuwa wakiongeza vipato vyao kwa kuwa na maduka ya dawa.

“Walimu wa Njombe unapomaliza muda wangu wa Serikali nenda kwenye ratiba yako binafsi ili tugawane namna ya kuwaondolea Watoto ujinga kwenye vichwa vyao, fundisheni Mimi nimewapa rukhsa, wakiwauliza waambieni RC ametoa rukhsa sio Afisa Elimu”

Mtaka amesema hataki kuona Mwalimu akifa Masikini kwakuwa Madaktari wamekuwa na maduka ya dawa, zahanati na wanatibu zaidi ya Hospitali mbili hivyo haoni haja ya kuwazuia walimu kuwa na Tuition ili kujiongezea vipato vyao.

Kutoka Mwanza, Septemba 13, 2022.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata...
13/09/2022

Kutoka Mwanza, Septemba 13, 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Jengo la Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Jijini Mwanza leo tarehe 13 Septemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango , mkewe Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na...
13/09/2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango , mkewe Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Afya Mhe Dkt wakishiriki ibada maalum iliofanyika kabla ya uzinduzi wa Jengo la Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Jijini Mwanza leo tarehe 13 Septemba 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo K...
13/09/2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Kenya Mhe. William Samoei Ruto tarehe 13 Septemba, 2022.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Marais 20 kutoka Afrika ambao watahudhuria sherehe ya kuapishw...
12/09/2022

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Marais 20 kutoka Afrika ambao watahudhuria sherehe ya kuapishwa Rais mteule wa nchi hiyo, Dk William Ruto.

Hafla hiyo itafanyika kesho Jumanne Septemba 13, 2022 katika uwanja wa MISC Kasarani ambapo Ruto atakabidhiwa rasmi madaraka ya kuliongoza taifa hilo.

Kamati ya Wabunge wa  yapitisha Wagombea Wa nane Ubunge wa Afrika Mashariki. Wamemrejesha  kwa takriban 95% ya kura!Dr. ...
12/09/2022

Kamati ya Wabunge wa yapitisha Wagombea Wa nane Ubunge wa Afrika Mashariki. Wamemrejesha kwa takriban 95% ya kura!

Dr. Makame amesema "Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa Neema na Rehema zake. Tunakishukuru kwa kunilea na kunipa tiketi ya kuwakilisha taifa letu. Tunawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kuniamini. Ni heshima kubwa nimepewa, zaidi ya 90%, Tunashukuru, asanteni sana". Dk. Makame

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amemsimamisha Kazi Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijini RUWASA wilaya ...
12/09/2022

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amemsimamisha Kazi Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijini RUWASA wilaya Karagwe, Mhandisi Magai Kakuru kwa kushindwa kusimamia miradi ya Maji inayoendelea kutekelezwa Wilayani Karagwe.

Ametoa agizo hilo leo septemba 11, 2022 wakati alipoambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kukagua mradi wa maji wa Chanika/Omululama ulipo wilayani humo na kutoridhishwa na hali ya utekelezaji wa mradi huo.

“Mhandisi huyu anajitahidi kufanya kazi lakini haiendani na kasi inayohitajika kwahiyo ataenda kusaidia kwenye kazi nyingi, hapa karagwe nitaleta Meneja Mwingine anayeendana na kasi tunayoitaka” amesema Aweso

Waziri Aweso amesema alipokuja wilaya karagwe alitoa maelekezo mahususi kuhusu miradi ya maji, lakini leo baada ya kuona na kupata taarifa amegundua wakandarasi wanachezea fedha za miradi.

Ikulu ya Buckingham imetoa mwaliko maalum kwa Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake pekee bila msafara wa wajumbe wake,...
12/09/2022

Ikulu ya Buckingham imetoa mwaliko maalum kwa Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake pekee bila msafara wa wajumbe wake, kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II Septemba 19, 2022 . Afisa wa Ikulu ya White House amethibitisha kuwa Biden amekubali mwaliko huo.

MASHINDANO ya mbio fupi za magari ya Sao Hill Misitu Auto Cross ambayo yamefanyika kwa mara kwanza katika Shamba la Miti...
12/09/2022

MASHINDANO ya mbio fupi za magari ya Sao Hill Misitu Auto Cross ambayo yamefanyika kwa mara kwanza katika Shamba la Miti Sao Hill lililopo wilayani Mufindi mkoani Iringa yamefana kwa kiwango kikubwa huku washiriki wa mashindano hayo wakiomba mashindano hayo yafanyike kila mwaka pamoja na kuandaliwa mashindano makubwa ya Bara la Afrika.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mashindano hayo katika Shamba la Miti Sao Hill linalomikiliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Mhifadhi Mkuu wa Shamba hilo Lucas Sabida amesema ndio mara ya kwanza kwa Wakala huo kuandaa mashindano hayo ikiwa ni utalii mpya ambao wameutambulisha kwenye sekta ya utalii nchini.

“Katika shamba la Sao Hill fursa ziko nyingi , tunazalisha bidhaa zinatokana na mbao , asali na tunazo fursa za uwekezaji .Lakini sasa tumekuja na utalii wa michezo kwenye maeneo yetu ya hifadhi za misitu ya asili na ile misitu ya kupanda k**a Sao Hill k**a ambavyo leo tumeanza na mbio fupi za magari.

Najua kuna wengine wanaweza kuchanganya mabadiliko katika matamshi ya hatua za Caf Interclub. Katika kuwekana sawa, ngoj...
10/09/2022

Najua kuna wengine wanaweza kuchanganya mabadiliko katika matamshi ya hatua za Caf Interclub. Katika kuwekana sawa, ngoja nitoe ufafanuzi.

Zamani watu wanajua hatua ya Awali ni Preminary Round sasa inaitwa 1st Preminary Round

Nyingine inayofuata zamani iliitwa hatua 1st Round (hatua ya pili), sasa inaitwa 2nd Preminary Round.

Hatua zote hizi ni kabla ya Group Stage. Tukumuke kuwa, sasa hivi Qualification ni Preminary, ambako katika Champions League zipo hatua mbili na katika Confederation zipo hatua tatu, Mbili Preminary na ya Tatu Mtoano/ Playoff ambayo ni mchangayiko wa Timu zilizoshinda Confederation dhidi ya Timu zizoshindwa Champions league.

Tanzania imeanza vizuri michuono ya kimataifa ikiwa timu zote zimeanzia ugenini Ambapo Zolan fc ya Sudan ya kusini imech...
10/09/2022

Tanzania imeanza vizuri michuono ya kimataifa ikiwa timu zote zimeanzia ugenini Ambapo Zolan fc ya Sudan ya kusini imecheza katika uwanja wa taifa Benjamini Mkapa wao wakiwa wenyeji na Yanga kushinda 4 bila.

Tanzania imeanza vizuri michuono ya kimataifa ikiwa timu zote zimeanzia ugenini Ambapo Nyasa big Bullet ya Malawi waliku...
10/09/2022

Tanzania imeanza vizuri michuono ya kimataifa ikiwa timu zote zimeanzia ugenini Ambapo Nyasa big Bullet ya Malawi walikuwa wenyeji ambapo wamepoteza kwa mbili bila.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Eli...
10/09/2022

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Elizabeth II kilichotokea September 08,2022 nchini Uskochi.

Maombolezo hayo yataanza leo Jumamosi September 10, 2022 hadi September 14,2022, katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye Balozi
Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Kiongozi wao nchini humo.

Tff yatoa orodha ya makocha wenye leseni A.
09/09/2022

Tff yatoa orodha ya makocha wenye leseni A.

Malkia Elizabeth II, malkia aliyehudumu muda mrefu zaidi nchini Uingereza, amefariki akiwa Balmoral akiwa na umri wa mia...
08/09/2022

Malkia Elizabeth II, malkia aliyehudumu muda mrefu zaidi nchini Uingereza, amefariki akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa miaka 70.
Familia yake ilikusanyika katika kasri yake ya Uskoti baada ya wasiwasi kuongezeka juu ya afya yake mapema Alhamisi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Ali Abdalla Ali kuwa Mku...
08/09/2022

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Ali Abdalla Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika leo 8-9-2022 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

Serikali imetangaza kulegeza masharti ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19, ambapo kuanzia sasa hakutakuwa na ulazima wa ...
08/09/2022

Serikali imetangaza kulegeza masharti ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19, ambapo kuanzia sasa hakutakuwa na ulazima wa kuvaa barakoa isipokuwa kwa mtu mwenye mafua pale itakapomlazimu sambamba na kwenye misongamano ya watu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya kufuatia kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini na duniani.

TANZANIA KUTUMIA FURSA YA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA.Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na U...
08/09/2022

TANZANIA KUTUMIA FURSA YA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka amefanya ziara ya siku nne (4) nchini Qatar kwa lengo la kuweka mikakati ya kutumia fursa ya Mashindano ya Kombe la Dunia kutangaza utalii wa Tanzania. Mashindano hayo yanatarajia kufanyika nchini Qatar kuanzia tarehe 20 Nov hadi 18 Des 2022.

Katika ziara hiyo Prof. Sedoyeka ameongozana na Wakurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw.Rich Wandwi, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Felix John na Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bi. Hafsa Mbamba.

Timu ya Simba imemtangaza kocha Juma Mgunda kuwa kocha mkuu Wa muda kwenye club hiyo hasa kwenye kipindi hiki Cha mpito ...
08/09/2022

Timu ya Simba imemtangaza kocha Juma Mgunda kuwa kocha mkuu Wa muda kwenye club hiyo hasa kwenye kipindi hiki Cha mpito Cha club hiyo.

Taarifa ya Simba inasema inaishukuru coastal union Kwa kumruhusu kocha wao ajiunge na Simba kwenye kipindi hiki Cha Cha mpito huku tukiendelea kumtafuta kocha mkuu , Mgunda ana leseni inayofaa kwenda kwenye mashindano ya Cuf

Mgunda anaungana na kocha msaidizi Matola kuelekea kwenye mechi ya hatua ya kwanza ya mabingwa wa ligi kuu Africa itakayofanyika nchini Malawi dhidi ya Nyasa Big Bullets siku ya jumamosi.

Msimu uliopita Liverpool walikaribia kabisa kutwaa makombe manne makubwa. Miezi minne baada ya kushindwa kwenye fainali ...
08/09/2022

Msimu uliopita Liverpool walikaribia kabisa kutwaa makombe manne makubwa. Miezi minne baada ya kushindwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa, Jurgen Klopp sasa anauliza k**a timu yake inahitaji "kujipanga upya".

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Torch Tv tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share


Other Dar es Salaam media companies

Show All

You may also like