Vibe la wadau wakati 'Wakimwaga wese na kujenga afya' kupitia Passion FM Jogging Club. Hakikisha wakati mwingine haupitwi na hili vibe la kibabe.
#passionfmjoggingclub
#mwagawese
#jengaafya
Mtagi rafiki yako mwenye Vibe kama Hilo
MIAKA YA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR; Passion Fm Tumezungumza na Ally Saleh Mwanasiasa Mashuhuri na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha ACT Wazalendo ambaye pia Msemaji wa Sekta ya Mawasiliano, Teknolojia Habari na Uchukuzi wa Chama hicho aliyegusia Mambo Mbalimbali Kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Unafikiri kwanini Watoto hao walikuwa Makini Kwa kiasi hiki
Timu ya Ihefu imesitisha rekodi ya Yanga ya kutofungwa kwa muda mrefu baada ya kupata ushindi wa goli 2-1.
Kabla ya mchezo huu wa leo mara ya mwisho Yanga walifungwa na Azam Fc goli 1-0, April,25 mwaka jana.
Baada ya ushindi wa leo Ihefu wamefikisha alama 11 na wamepanda mpaka nafasi ya 13.
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kimeelekeza wataalamu wa ndani kushirikiana na wale wa kutoka nje kufanya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision iliyotokea katika ziwa Victoria tarehe 6 Novemba,2022.
Aidha, Msemaji huyo wa Serikali amebainisha kuwa kikao hicho kimeelekeza vitengo vyote vinavyohusika na majanga nchini viimarishwe ili viweze kusaidia wakati wa majanga.
Katika kikao hicho cha dharura cha Baraza la Mawaziri, Serikali imewaomba wananchi kuwa watulivu wakati taratibu za kiuchunguzi zikiendelea.
📷 @maelezonews
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji Saini wa mikataba na hati za makubaliano ya kimkakati 15 akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping.
Miongoni mwa mikataba hiyo iliyolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili na pia umeshuhudia China ikiipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la thamani ya Shilingi bilioni 31.4.
Watanzania wawili Ibrahim na Fadi Ramadhani (The Ramadhani Brothers ) wamewaacha watazamaji wa 'Austalia Got Talent' vinywa wazi huku wengine wakiwa wameshika vichwa kutokana na onesho lao la kipekee.
Watanzania hao wameupiga mwingi na kuwashawishi majaji kuwatunuku 'Golden Buzzer' tuzo ambayo haitolewi mara kwa mara na hutolewa kwa wanaofanya vizuri zaidi.
Video hii ni sehemu tu ya walichokifanya wanasarakasi hao.
Video ya Mtandao.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete ameipongeza Passion Fm kwa kazi nzuri ya kuhabarisha umma.
Kiongozi huyo alitoa pongezi hizo baada ya kutembelea studio ndogo iliyokuwa ikirusha matangazo mubashara kwenye Maonesho ya Uwekezaji na Biashara yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani.
Aidha, Rais Mstaafu Kikwete ameiomba Passion Fm kuendelea kufanya kazi kubwa ya kupasha habari kwa jamii.
Maonesho ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani yalifunguliwa rasmi na Dkt.Jakaya Kikwete Oktoba 6, 2022 na yalifungwa Oktoba 10, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mikataba yote itakayoingia serikali ni lazima kuishirikisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akizindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na mfumo rasmi wa Kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS) katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali jijini Dodoma.
Video credit: Ikulu Tanzania
Mandonga haishiwi maneno😂safari hii ametoa tahadhari kwa bondia atakayepandanae ulingoni kuwa atapigwa ngumi mchomoko kama kamchukulia mke wake. Bondia Karim Mandonga atapigana Pambano la utangulizi kabla ya bondia Twaha Kiduku kupanda ulingoni kuzichapa na bondia Abdo Khaled kutoka Misri Jumamosi Septemba 24 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa bunge litapitisha sheria ya bima ya afya Kwa wote na kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa hiyo mara baada ya sheria hiyo kupitishwa.
Baada ya kupoteza Pambano lake kwa TKO raundi ya nne dhidi ya Muingereza Liam Smith, Mtanzania Hassan Mwakinyo amesema kuwa kuna vitu havikuwa sawa kabla ya Pambano hilo na kudai kuwa kuna hujuma alifanyiwa.
Je, nini maoni yako?
Video courtesy: @salim_kikeke
Baada ya wananchi wengi kulalamika kuhusu masuala ya tozo Serikali kupitia kwa Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amesema kuwa wamepokea maoni ya wadau na yanafanyiwa kazi.
Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakilalamikia kukosa huduma kutoka kwa baadhi ya vituo vya afya/hospitali na wengi wakiambiwa kuwa bima zao haziwaruhusu kupata baadhi ya huduma.
Majibu ya changamoto hiyo yametolewa na Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi NHIF-Temeke Dkt.Ngalela Kateule kwenye Mahojiano maalumu kupitia kipindi cha Drive Home Show cha Passion Fm.
Kupitia Passion Fm Bondia Shaban Kaoneka amesisitiza kuwa ngumi ndio mchezo anaoutegemea kuendesha maisha yake na ameendelea kuonesha mshangao namna Mandonga anavyozidi kupata madili alafu yeye anazidi kula msoto kitaa, Kaoneka anasema eti kuna muda anakosa hata hela ya kula.......
Eti anasema kama mwenzake nyota zimeng'aa basi angalau na yeye apate hata nyota moja.
Una lipi la kumwambia Kaoneka kwenye kazi yake.
Hakikisha unaendelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa zaidi na vilevile Follow ukurasa wetu wa Instagram @passionfmtz