10/09/2021
Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa msingi, kuta na sakafu hufuatia aina ya ezeko litalowekwa na namna ya uwekaji wake
Kuna aina nyingi ya maezeko ya materials tofauti tofauti na kila moja ina faida na hasara zake kulingana na hali ya hewa ya eneo husika, bajeti, upatikanaji na wepesi wa uwezekaji wake
Ezeko linatakiwa kulinda eneo la ndani ya nyumba kutokana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa k**a jua, mvua, joto, baridi na umande hivo kuruhusu uhifadhi wa joto wakati wote, lidumu kwa muda unaotakiwa ili kupunguza gharama ya marekebisho ya mara kwa mara na kuipa nyumba muonekano stahiki unaohitajika kwasbb ezeko ni sehemu ya kuliremba jengo
Lakini kila aina ya ezeko hufanya kazi fulani kwa ubora kuliko aina nyingine na hivo hivo kila mtindo wa kuezeka hutofautiana katika kudumu na wepesi wa uwezekaji wake
Ili kufanya maamuzi sahihi inapaswa kuzingatia yafuatayo
1) Mtindo wa uwezekaji pamoja na faida na hasara zake kwa kuzingatia mazingira na hali ya hewa ya eneo husika (yaani uwezo wake wa kuhimili changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ya mahali husika) na gharama ya aina ya ezeko husika
2) Materials yanayohitajika kwa kila mtindo, upatikanaji na uimara wake
3) Namna ya kuandaa michoro yake na jinsi ya kuezeka
4) Mvuto, usalama wake kwa afya na urafiki wake kwa mazingira
NB: Unatarajia kuezeka nyumba yako hivi karibuni?! Basi zingatia hayo!!! Umeshaezeka nyumba yako?! Unapitia changamoto ipi?! Au ulifanya maamuzi sahihi?!
Tupe uzoefu!!!
[email protected]
0718600290