Jenerali Sylvain Kyenge: Msemaji wa Gavana wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, kupitia tangazo la msemaji wa Gavana wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini, limesema kua halitoacha hata sehemu ya ardhi ya Congo kwa yeyote,.
Sultani MAKENGA ,kamanda wa jeshi la M23 ajitosa hadharani mbele ya watoto wa masomo akiwahakikishia kuwa yeye akingali haï licha ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii kua ameuawa kwenye mapigano ya Runyonyi.
Msemaji wa M23, Meja Willy Ngoma.
DRCONGO: Rutshuru/ Kivu Kaskazini - M23/ by Madiba Mahoye.
M23, YASITISHA MASHAMBULIO NA KURUDI NYUMA.
"''"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Uasi wa M23, umesitisha mashambulizi dhidi ya jeshi la serikali na kurudi nyuma katika ngome zake ambazo zinapatikana katika vilele vya milima ya Runyonyi na Canzu. Hatua hiyo imo katika tangazo ambalo limesomwa na msamaji wa M23, jumapili hii tarehe 10 April 2022, ambapo waasi hao wamesema kua wanajiondoa katika miji na vijiji ambavyo walikua tayari kuvidhibiti tangu warudi tena kupambana na FARDC. Wanarudi katika vijiji ambavyo viko chini ya milki yao,ikiwa ni Bugusa, Canzu na Runyonyi kwa kusubiria mazunguzo na serikali ya Kongo.
<> limejulisha hivo tangazo ambalo amelisaïni msemaji wa waasi hao wa M23, meja
Willy Ngoma.
Kulingana na raïa m'moja ambae hakupenda kutajwa jina lake, amesema kua wakati waasi walipokua wakirudi nyuma wameonekana wakipora mali madukani, vituo vya afya na maduka vimeporwa.
Raïa huyo ameïomba serikali ifanye mashambulizi makali dhidi ya waasi hao na iwafurushe. Amesema kua yeye hayuko tayari kwa serikali kufanya mazunguzo na waasi hao.
Vidéo ya Antoine Gabriel Kyungu Wa Kumwanza, enzi za uhayi wake.
DRCONGO: Haut Katanga/ Lubumbashi
MGOGORO WA KUWANIA MADARA NDANI CHAMA CHA UNAFEC, WAÏBUKA BAADA YA KIFO CHA KYUNGU WA KUMWANZA/ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Vijana wa chama cha kisiasa " Union Nationales des Fédéralistes du Congo (UNAFEC) " wameandamana mbarabarani kwa kupaza sauti wakilalama kuhusu nani atakae rithi mikoba ya muhasisi wa chama hicho Gabriel Kyungu Wa Kumwanza. Wakati vijana hao wakiandamana kwa hasira wamechoma moto picha ya raïs wa jamuhuru Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika manispaa ya Kenya Lubumbashi katika jimbo la Haut - Katanga, vurugu hizo zimetokea jumainne hii tarehe 05 April 2022.
Mgogoro huo umezuka ndani ya chama hicho , baada ya kifo cha baba wa Katangu Gabriel Kyungu Wa Kumwanza ambapo na fasi alio kua akiishikilia katika chama hicho hajapatikana mrithi wake.
Maandamano hayo yameutikisa mji wa Lubumbashi. Duru za mahali za eleza kua shughuli za kibiashara zilesimama. Vijana wa chama cha UNAFEC, wamesikika wakipaza sauti wakiwash*tumu magwiji na mabwanyenye wa chama hicho ambao hataki kutoa mwanya kwa vijana kupata na fasi za uongozi katika chama hicho na kumtafuta atakae rithi mikoba ya Antoine Gabriel Kyungu Wa Kumwanza.
Tuwajulishe kua mzozo huo wakuwania madaraka ndani ya chama cha UNAFEC umeibuka baada ya kifo cha Kyungu Wa Kumwanza. Baada ya Gabriel Kyungu Wa Kumwanza kuiaga dunia ambae alieteuliwa kushikilia nafasi hiyo kwa mpito ni Jean Lungange Umba, ila amekua akipingwa vikali na katibu mkuu wa chama hicho kwa kusukumwa na Lama Mukalay.
Upande mwengine, wizara ya mambo ya ndani inamtambua Bertin Kanunu kama mwenye kiti wa UNAFEC, kutokana na makada wengi wa UNAFEC kumtambua kama alie kua akishikilia wazifa kama makamu wa kwanza wa Kyungu Wa Kumwanza.
Ameteuliwa kushikilia wazifa huo mpaka pale mkutano mkuu wa chama utakapo itishwa wa kuchagua wakuu wa UNAFEC.
Raïs Paul KAGAME wa Rwanda akihutubia mawaziri wa pya.
RDCONGO - RWANDA/ Usalama na Diplomasi/ by Madiba Mahoye
JE, RAÏS PAUL KAGAME WA RWANDA, ATAMANI KURUDISHA MAJESHI YAKE NCHINI CONGO?
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Raia wa Congo wameingiwa na wasiwasi kuhusu usalama wao baada ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kutishia kupeleka vikosi vyake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kupambana na waasi Rwanda wa kundi la FDLR
Kagame aliyasema hayo mjini Kigali mwanzoni mwa wiki wakati akiwaapisha mawaziri wapya. Katika matamshi yake Rais wa Rwanda Paul Kagame, alionyesha kwamba kuwepo kwa waasi kinyarwanda wa FDLR pamoja na waganda wa ADF mashariki mwa Kongo kunaendelea kuiweka hatarini nchi yake, na kusisitiza kuwa kuna wakati wa kujadiliana na wakati wa kuamua na kupata suluhisho bila kuomba ruhusa kwa yeyote yule.
Kinachowahuzunisha zaidi wakongomani ni kwamba kamati ya bunge la kitaifa inayohusika na ulinzi na usalama iliwahi kuitolea serikali mapendekezo ili kutatua suala la usalama mashariki mwa nchi hii, lakini hadi sasa hali inaendelea kuzorota katika eneo hilo licha ya kuwekwa utawala wa kijeshi tangu sasa miezi tisa.
Akizungumza na DW, mbunge wa bunge la taifa Gratien de Saint Nicolas Iracan alisema ni muhimu sana kwa waziri mkuu kujieleza bungeni kuhusu jambo hilo.
Inatupatia woga na ingekuwa vizuri serikali ya Kongo kutueleza namna gani hali ya usalama ilivyo upande wa kwetu. Tuweze kujua serikali inatayarisha kitu gani, tunaogopa kuona leo au kesho jeshi kutoka Rwanda likiingia Kongo kwa sababu hakuna namna ya kulinda usalama. Basi ni vizuri tuweze kujua mambo yanavyoendelea."
Kuna uwezekano majeshi ya Rwanda na Uganda kukutana tena kwenye ardhi ya Kongo, na hii ni moja ya sababu za wasiwasi kwa Wakongomani. Nicoles Kavira, mratibu wa kitaifa wa harakati ya hasira kuhusu usalama wa Kongo, anapinga kabisa mradi wa rais Kagame.
"Tunasikitika sana na tunashangaa kuona kiongozi wa nchi nyingine akisema kwamba anataka kuingia tena katika nchi yet
WAKIMBIZI WA LWEBA WAÏNGIYA BARAKA
DRCO: Kivu Kusini/ Usalama / Baraka/ By Madiba Mahoye
RAÏA WA LWEBA WAKIMBIA KUTOKANA NA HOFU YA KUSHAMBULIWA NA MAKUNDI YA WANAMGAMBO WENYE KUMILIKI SILAHA.
""""""""''"""""""""""""""'''"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Wimbi la wakimbizi wa ndani kutoka katika vijiji na pembezuni mwake wameïngi jioni ya leo jumatano mjini Baraka wakihofia Usalama mdogo unao tipotiwa Bibokoboko kutokana na milio ya silaha za rashasha na mizinga mizito ambayo imeanza kuskika tangu umajira ya saa mbili usiku katika marneo hayo.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa awali na kamanda wa Sekta ndogo ya operesheni Sokola ya pili kanali David Ipanga amesema kua ni kundi la wanamgambo wa Maï Maï ambao hawajulikana ndio walikua wamevamia mabanda ambayo yanafugwa ngombe na kuchukua baadhi ya mifugo hiyo, ila askari jeshi wamekua wakikabiliana nao.
Duru nyingine ambazo hazikupenda kutajwa kwa sababu za kiusalama, zimeliambia shirika la habari la Canal Tanganyika Média kua wanamgambo wa Maï Maï TORONTO ndio wameendesha shambulio hilo na kusababisha maafa ya wachunga ngombe watatu (3).
Raïa hao wamekimbia kijiji cha Lweba kinacho patika katika kitongoji cha Bashimunyaka Kaskazini, Sekta ya Tanganyika kutokana na kuendelea kuskika kwa zana nzito nzito za vita ambazo zimeendelea kuskika hadi jioni majira ya saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili. Kwa upande mwengine taarifa zaeleza kua wanakijiji hao wamekua na hofu ya kushambuliwa na wanamgambo wa Gumino kutokana na kinacho daïwa kuwa kutakua na ulipishaji kisasi cha mauaji ya Meja Kaminzobe wa Kabila la wanyamulenge wanadaïwa kua na asilii ya Rwanda, ambae aliuawa kikatili kijiji hicho cha Lweba.
Vikosi vya Usalama vimetumwa Lweba kuhakikisha hali ya Usalama inasalia tulivu.
Kijiji cha Lweba kimebaki bilan raïa hâta mmoja duru zimeendelea kutaja. Wamekimbilia Baraka na wengine wameelekea Lusenda na kwengineko.
Raïa hao ambao wamekimbia wanakabiliwa na hali ya mvua ambayo imeanza kuonesha dalili. Usiku huu watakua
VIKOSI VYA JESHI LA CONGO VIKIKABIANA NA M23 RUTSHURU.
RDCONGO: Kivu - Kaskazini/ Usalama: JESHI LA JAMUHURI YAKIDEMOKRASIA YA CINGO ( FARDC) LAZIDISHA MASHAMBULIZI DHIDI YA UASI WA M23 KATIKA WILAYA YA RUTSHURU/ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Vikosi vya jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vimekua vikikabiana na waasi wa M23 ambao wamevivamia vijiji vya kiyongoji cha Kisigari tarani Rutshuru jimboni Kivu Kaskazini.
WASIYA WA MW.JULIUS K.NYERERE.
Mw.Julius K. NYERERE na ushauri wa mwezi huu!
WANAJESHK WA BURKINA FASO ,WAMTIMUA MADARAKANI RAÏS ROCH MARC CHRISTIAN KABORÉ .YAMEKUA SASA MAPINDUZI YA KIJESHI YA MARA YA SITA TANGU NCHI HIYO IJIPATIE UHURU.
TANGAZO LA KIJESHO,BAADA YA JARIBIO LA MAPINDUZI.
Burkina Faso:
Tangazo la wanajeshi walio fanya jaribio la mapinduzi.
Kanali Paul - Henri Sandaogo akitangaza jaribio hilo la mapinduzi.
Radio Télé Tanganyika 24
Vikosi vya Jeshi la Kenya vya anza mazoezi ya kivita kwa kukabiliana na makundi ya uasi mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Hatua hiyo imekuja baada ya raïs Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kutangaza hali ya isio ya kawaïda katika majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini.
Raïa wa mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waandamana dhidi ya mauaji na usalama mdogo unaoripotiwa mashariki mwa nchi hii.
Maandamano hayo yameïtishwa na muungano wa mashirika ya Kiraïa. Shirika la Kiraïa la NDSC - CHUMVI YA CONGO.