HMG

HMG Dunia yetu ni nzuri sana, ungana na HMG AFRICA kila siku ili kupata kujua historia ya ulimwengu huu
(5)

Karibu ndani ya HMG hapa tutajadili makala mbalimbali kuhusu dunia yetu na viumbe wapatikanao ndani ya dunia yetu pia tutajadili habari na makala za uchunguzi pamoja na makala kuhusu maeneo yaliyovunja record duniani bila kusahau historia yake tutajadili teknolojia ya dunia pamoja na viumbe wa ajabu wanaotishia dunia

BREAKING - Iran imeripotiwa kupokea mifumo ya makombora ya balestiki ya Iskander kutoka Urusi.  "Iskander-M" ni kombora ...
05/08/2024

BREAKING - Iran imeripotiwa kupokea mifumo ya makombora ya balestiki ya Iskander kutoka Urusi. "Iskander-M" ni kombora la masafa mafupi la hypersonic na lina takriban masafa ya kilomita 480-500 (maili 250-310.

Ndege ya usafiri ya L-76, inayojulikana kwa kusafirisha silaha nzito na vifaa, imetua Tehran, Iran kutokea Moscow Urusi 🇮🇷 🇷🇺

Haya yanajiri baada ya Uran kuapa kuwa muda mfupi itaishambulia Israel moja kwa moja

Ukristo barani Afrika una historia ndefu inayokaribia miaka elfu mbili.Ukristo uko Afrika katika wingi wa madhehebu yali...
30/07/2024

Ukristo barani Afrika una historia ndefu inayokaribia miaka elfu mbili.
Ukristo uko Afrika katika wingi wa madhehebu yaliyopatikana katika historia ya Kanisa, baadhi katika bara hilo, baadhi katika mabara mengine.
Kwa sasa ndiyo dini kubwa zaidi barani, hasa Kusini kwa Sahara, pamoja na Uislamu ambao unaongoza Kaskazini kwa jangwa hilo.
Leo karibu nusu ya Waafrika wote ni Wakristo. Lakini asilimia ya Wakristo inaweza kuwa ndogo katika nchi kadhaa na kubwa katika nchi nyingine. Katika Afrika Kaskazini Wakristo ni wachache. Kumbe ni wengi kwa theluthi mbili za bara kusini kwa Sahara.
Mwaka 1900 katika eneo la Tanzania ya leo Wakristo walikuwa elfu kadhaa tu. Ongezeko lilikuja haraka sana. Leo hii wako zaidi ya milioni 20. Wakati ule kati ya Watanganyika 100, Wakristo walikuwa 2 tu. Leo zaidi ya 50 kati ya Watanzania 100 ni Wakristo.
Tuna habari nyingi juu ya Wakristo kule Misri na Karthago (magofu yake yako nchini Tunisia) wakati wa karne ya 2. Habari hizo zinaeleza maisha na mateso yao. Hao na Wakristo wa kwanza walio wengi waliishi chini ya serikali ya Roma. Kwa jumla hiyo iliwaruhusu watu wote kuendelea na desturi na dini zao. Serikali iliona ni muhimu kuabudu miungu yote kwani ingekuwa hatari mungu fulani angesahauliwa hata kusababisha akasirike.
Katika karne ya 3 mateso yalikuwa makali hasa kule Misri. Katika miji mikubwa k**a Aleksandria watu wengi walikuwa Wakristo. Machoni pa wakuu wa serikali hali hiyo ilikuwa uasi. Wakaona ni lazima kuzima uasi huo.
Kati ya miaka 302 na 308 B.K. maelfu wakauawa kule Aleksandria. Wakakatwa vichwa na maaskari, wakapelekwa katika kiwanja cha michezo mbele ya wanyama mwitu, wakachomwa moto. Lakini idadi ya Wakristo waliokuwa tayari kufa ilizidi uwezo wa serikali wa kuwaua.
Kumbe mwaka 312 ilikuwa k**a ukombozi kwa mji wa Aleksandria. Kaisari mpya, kwa jina Konstantino Mkuu akatangaza mwisho wa mateso. Akatoa sheria ya kuwa Ukristo ni dini halali katika Dola la Roma.
Misri ilikuwa kitovu muhimu cha Ukristo wa kale. Uhodari wa Wakristo wake ulishinda dhuluma za serikali ya Kiroma. Katika mapambano hayo Wakristo Wamisri wakaunda silaha mbili ambazo zimekuwa muhimu katika Kanisa zima mpaka leo: 1. Elimu ya Kikristo 2. Utaratibu wa umonaki.
Jiji la Aleksandria lilikuwa na maktaba kubwa kuliko zote duniani. Wakati ule haikujulikana jinsi ya kupiga chapa vitabu. Kila kitabu kiliandikwa kwa mkono kikawa na bei kubwa sana. Kununua kitabu kulikuwa na gharama zinazofanana na ile ya kununua gari leo. Kwa hiyo elimu ilikuwa na thamani kubwa, na maktaba kubwa ilikuwa na thamani kupita kiasi. Wataalamu toka pande zote za dunia walifika Aleksandria, mji wa elimu, ili kusoma na kunakili vitabu. Si ajabu kwamba Agano la Kale lote lilitafsiriwa kwa mara ya kwanza katika lugha ya Kigiriki huko Aleksandria mwaka 150 hivi K.K.
Mnamo mwaka 203 B.K. aliishi mama kijana mwenye miaka 22 kwa jina Perpetua katika mji mkubwa wa Karthago. Perpetua alitokea familia tajiri na kuwa na mtoto wa kiume. Wazazi wake walikuwa wanaheshimiwa sana.
Kumbe Perpetua akashtakiwa kuwa Mkristo akak**atwa. Baba akamwendea mkuu wa mkoa wakapatana Perpetua atoe sadaka mbele ya sanamu ya Kaisari ili shtaka lifutwe. Kutoa sadaka maana yake ilikuwa kushika nafaka kidogo na kuitupa kwenye karai ya mkaa uliowaka mbele ya sanamu. Baba akamweleza mtoto wake gerezani alivyopatana na mkuu wa mkoa. Perpetua akakataa. Baba akamsihi akamwomba asilete aibu juu ya wazazi wake na amhurumie mtoto wake mdogo. Perpetua akamjibu baba ya kuwa tendo hilo halipatani na imani yake.
Felista alikuwa msichana Mkristo na wanawake hao wawili walikuwa marafiki ingawa Felista alikuwa mtumwa. Akafungwa pamoja na Perpetua na vijana watatu. Walipokataa kutoa sadaka wakapewa wote adhabu ya kifo.
Hao vijana Wakristo watano wakapelekwa katika uwanja wa michezo wa Karthago. Watu wengi wakatazama. Kuua wakosaji kulikuwa k**a mchezo au burudani kwa wakazi wa miji. Walizoea kutazama maonyesho ya kuua wakosaji wenye hukumu ya mauti. Vijana Wakristo waliposimama uwanjani milango ya chini ikafunguliwa. Wanyamapori wakali waliokuwa wanahifadhiwa katika vyumba vya chini katika uwanja huo, wakiwekwa tayari ili kuwararua Wakristo wakatokea. Kuwatupa Wakristo mbele ya wanyama wakali ilifanywa k**a onyesho la kuburudisha halaiki. Hao vijana wakashambuliwa na wanyama; wengine wakawaua na wengine wakajeruhiwa vibaya. Mwishoni wote waliojeruhiwa waliuawa kwa upanga.
SIMULIZI YA UKRISTO BARANI AFRICA INAENDELEA HAPA KWA NJIA YA SAUTI NA VIDEO BONYEZA LINK https://youtu.be/4bziVxbeBes

𝗦𝗔𝗙𝗔𝗥𝗜 𝗡𝗗𝗘𝗙𝗨 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗗𝗘𝗚𝗘 𝗗𝗨𝗡𝗜𝗔𝗡𝗜..Kwa sasa, Shirika la Ndege la Singapore ndilo linalofanya safari ndefu zaidi ya nde...
28/07/2024

𝗦𝗔𝗙𝗔𝗥𝗜 𝗡𝗗𝗘𝗙𝗨 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗗𝗘𝗚𝗘 𝗗𝗨𝗡𝗜𝗔𝗡𝗜..

Kwa sasa, Shirika la Ndege la Singapore ndilo linalofanya safari ndefu zaidi ya ndege ya moja kwa moja duniani.
Safari hiyo ni kati ya Uwanja wa Ndege wa Changi nchini Singapore na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK mjini New York, Marekani.

Shirika hilo la ndege la Singapore hutumia Airbus A350-900ULR (Utra Long Range) iliyoundwa mahususi kwa safari ndefu zaidi.

Umbali uliokokotolewa wa safari ya ndege ya Singapore hadi New York ni kilomita 15,349km (9,537mi), jumla ya takriban saa 19 za kuruka bila kusimama.

Safari ya ndege inahitaji mipango makini ya marubani, ambayo inajumuisha usimamizi sahihi wa mafuta, hali ya hewa na mapumziko ya wafanyakazi ili kuhakikisha usalama na ustawi wa abiria.

Rwanda: Kabla ya UkoloniAsili rasmi kabisa ya watu wa kwanza kuishi katika eneo ambalo leo tubalitambua k**a nchi ya Rwa...
27/07/2024

Rwanda: Kabla ya Ukoloni
Asili rasmi kabisa ya watu wa kwanza kuishi katika eneo ambalo leo tubalitambua k**a nchi ya Rwanda ni watu wa kabila la ‘Twa’ (Watwa). Kabila hili la wawindaji si la kibantu bali ni sehemu ya makabila yanayotambulika na wanahistoria k**a ‘pygmy’ ambao sifa yao kuu ni ufupi. Mtu mzima anayetoka makabila ya namna hii anakadirwa kuwa na wastani wa urefu chini ya sentimita 150. Watwa waliishi Rwanda enzi za kale sana miaka ya 8000 BC na 3000 BC.

Kuanzia miaka ya 700 BC mpaka 1500 AD makabila ya Kibantu kutoka maeneo ya jirani yalianza kuhamia eneo hili.

Kuna nadharia mbali mbali kuhusu ni namna gani haswa makabila haya ya kibantu yalihamia hapa na baadae kupelekea kutokea Makabila ya sasa ya Wahutu na Watusi.

Nadharia ya kwanza inadai kwamba; Wahutu ndio walikuwa wa kwanza kuhamia eneo hili na kuanzisha shughuli za kilimo. Baadae watu wenye asili ya Ukushi (Watusi wa sasa) nao wakahamia kwenye eneo hili na kulitawala.

Nadharia ya Pili inadai kwamba; kuna uwezekano kwamba Watusi si wakushi bali ni wahamiaji tu kutoka maeneo ya jirani kipindi hicho cha kale ambao walihamia na kujichanganya na jamii waliyoikuta hapo (Wahutu) lakini wao walikuwa wafugaji. Chini ya nadharia hii inadai kwamba kuibuka kwa Wahutu na Watusi hakukutokana na kuwa na utofauti wa kinasaba au asili ya mababu bali ulitokana na utofauti wa kimadaraja/matabaka ya kijamii.

Tabaka la wale walio wa daraja la juu ambao walikuwa wafugaji walijitanabaisha k**a Watusi wakati ambapo tabaka la chini ambao walikuwa wakulima walijitanabasha k**a Wahutu.

Makabila haya yote matatu, Watwa, Wahutu na Watusi wanazungumza lugha moja na kwa wote kwa pamoja wanajulikana k**a ‘Banyarwanda’.

Idadi ya watu ilipoongezeka katika eneo hili walianza kujitambua kupitia makundi madogo madogo yaliyoitwa ‘Ubwoko’ au ‘koo’ kwa kiswahili. Ilipofika katikati ya miaka ya 1700 koo nyingi ziliungana na kuunda ‘Falme’.

Moja ya Falme ambazo zilikuwa imara zaidi ulikuwa ni ‘Kingdom of Rwanda’ ambayo watawala wake wote walitokea katika koo ya Kitusi ya Nyiginya.

Ufalme huu ulifikia kileleni kipindi cha utawala wa Mfalme Kigeli Rwabugiri chini ya falsafa yake ya kujipanua na kuteka falme nyingine na kuzifanya sehemu ya Kingdom of Rwanda.

Chini ya Mfalme Rwabugiri alianzisha mfumi wa kiuchumi wa ‘ubuhake’ na baadae ‘uburetwa’.

Katika mifumo yote hii miwili, iliwanufaisha zaidi Watusi na kuwafanya Wahutu k**a vijakazi wao kuwafanyia kazi za uzalishaji na kuwa askari vitani kwa ujira wa kupata fursa ya kumiliki mifugo na kutumia ardhi.

Watusi walipaa juu zaidi na kuwa raia daraja la kwanza ma Wahutu kubakia kuwa tabaka la chini kabisa ndani ya Kingdom of Rwanda.
simulizi kamili ipo hapa bonyeza link https://youtu.be/JmfzvQFzSlU

ma unasoma ujumbe huu, muda huu… uko mpweke! Pengine ushahidi pekee uliobakia ni kijipande hiki cha maandishi. Sijui k**...
27/07/2024

ma unasoma ujumbe huu, muda huu… uko mpweke! Pengine ushahidi pekee uliobakia ni kijipande hiki cha maandishi. Sijui k**a kuna yeyote kati yetu aliyesalimika kufika kizazi chenu mwaka huu mtakaosoma andishi langu. Sijui hata k**a tumeshinda au tumeshindwa vita tunayopigana sasa hivi. Sijui, lakini naamini mwaka huu mliopo nyinyi sasa mwaweza kuwa na jibu sahihi. Vyovyote vile lakini jambo lililo dhahiri ni kwamba hakuna yeyote wa kizazi chetu mliye naye sasa hivi kwenye miaka yenu muusomapo ujumbe huu. Kwa hiyo wacha niwaeleze sisi tulikuwa akina nani, na kwa namna gani tulipambana mpaka tone la mwisho la damu mwilini mwetu ili kutetea kizazi chetu kisifutwe juu ya uso wa dunia. Wacha niwaeleze namna ambavyo japo tulikamuliwa damu mpaka kutiririka kufanya mifereji lakini lakini tulisimama kutetea kizazi chenu na ninyi watoto wetu. Wacha niwaeleze kisa kilichotikisa ulimwengu. Wacha niwaeleze kuhusu mifereji ya damu kwenda Ethiopia.!”

March 21, 1994 maeneo ya Uganda ambayo yanapakana na Rwanda, katika ziwa viktoria serikali ilituma vikosi vya jeshi kudhibiti eneo hilo kwa hali ya dharura. Agizo hili la serikali kutuma jeshi halikuwa kwa ajili ya kidhibiti eneo hilo kutoka kwa adui bali agizo lilikuwa ni kudhibiti eneo hilo dhidi ya maiti, maiti za binadamu. Sio maiti mbili au tatu, si mamia bali maelfu ya maiti za binadamu ambazo zilikuwa zinaingia ziwani Victoria zikiletwa na maji ya mto Kagera.

Maiti hizi zilikuwa nyingi kwa maelfu kiasi kwamba mapaka zilikuwa zinafanya maji yatoe harufu. Serikali ya Uganda ilituma jeshi eneo hili ili kudhibiti eneo hili maji yake yasitumiwe na wananchi kwa matumizi ya nyumbani au shughuli za uvuvi. Lakini jeshi lilikuwa eneo hili ili kuhakikisha kuwa taharuki iliyozuka baada ya maelfu ya miili hii kuonekana haigeuki na kuvuruga amanai katika eneo hili. Lakini pia jeshi lilikuwa hapa ili kubaini miili hii ilikuwa inatoka wapi.

Kadiri ambavyo jeshi la Uganda lilivyokuwa linafuatilia kwa kurudi nyuma kufuata mto Kagera ndivyo ambavyo walizidi kubaini kwamba maiti hizo zinaletwa na maji kutoka tawi la mto Kagera lililopita kusini mwa Rwanda. Na kadiri ambavyo walizidi kufuata chanzo cha maiti hizo zinakotoka ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia Rwanda na maji ya mto rangi yake kuwa nyekundu zaidi.

Wanajeshi wa Uganda ambao walishiriki kwenye ukaguzi huu wa mto huu wanakiri kwamba licha ya baadhi yao kupigana mstari wa mbele kwenye vita mbali mbali lakini hakuna yeyote kati yao ambaye aliwahi kushuhudia ukatili mkubwa wa kiasi hiki.

Siku hii jeshi la Uganda linakisia kwamba waliokota si chini ya miili elfu kumi ya binadamu na yote ilionekana kuletwa na maji ya mto Kagera kutoka nchini Rwanda.

Ajabu ni kwamba miili yote hii ilikiwa inamfanano fulani. Maiti zote zilikuwa za watu warefu, wembamba, wenye nyuso ndefu na pua za kuchongoka. Haikuhitaji kufikiria sana kufahamu kuwa maiti hizi zilikuwa za watu wa kabila la Tusi (Tutsi).

Miezi kadhaa baadae ndipo ambapo jeshi la Uganda na ulimwengu wote walikuja kuelewa kwa nini maiti zilikuwa zinatupwa mto Kagera. Ni ujumbe gani ambao ulikuwa unajaribu kutumwa.

Kwamba Watusi nchini Rwanda walikuwa waapenda kujisifu kuwa mababu zao wana asili ya nchi ya Ethiopia. Kitendo hiki cha watesi wao kuwatupa mtoni, walikuwa wanawaua na wakiwa wanatupa maiti zao mto wanawaambia kwamba “wanawasafirisha warudi kwao Ethiopia ambako wamekuwa wakijisifu ndio asili yao.”

Sio kwamba jeshi la Uganda hawakuwa na taarifa juu ya hali tete iliyopo Rwanda kwa muda wa karibia wiki nzima iliyopita bali hawakujua k**a hali hiyo tete ilikuwa ni ya kinyama kiasi hicho.

Wanajeshi hawa wa Uganda walikuwa wameshikwa na bumbuwazi na vihoro vilivyo wapasua mioyo kwa kuona miili hii elfu kumi ya binadamu isiyo na uhai. Kitu ambacho walikuwa hawakijua na hakuna ambaye alidhahania ni kwamba ndani ya siku mia moja zijazo ulimwengu ulikuwa unaenda kushuhudia moja ya tukio la kikatili zaidi tangu kuubwa kwa ulimwengu. Karibia maiti za binadamu milioni moja zikiwa zimetapakaa mitaani nchini Rwanda iking’ong’wa na nzi na kuliwa na mbwa. makala hii isikilize hapa yote bonyeza link https://youtu.be/JmfzvQFzSlU

LAANA YA MIZIMU NA HATARI KATIKA MAISHA YETU HAKIKA NYOTA ZETU ZIPO KUZIMUIfahamike kuwa kila kabila lina utawala wake w...
23/07/2024

LAANA YA MIZIMU NA HATARI KATIKA MAISHA YETU HAKIKA NYOTA ZETU ZIPO KUZIMU

Ifahamike kuwa kila kabila lina utawala wake wa mizimu ambapo utawala huo huwa unateua kuhani wa kuongoza shughuli zao..

Ila kutokana na Mwamko wa Elimu na dini mpya zilizoingia habari za mizimu zimeendelea kupoteza nguvu na wafuasi na taratibu Elimu hii imekuwa ikipotea.. Lakini usumbufu wa mizimu bado umeendelea kuwepo kwa kiwango kikubwa katika maisha ya wanadamu bila wanadamu wenyewe kujua..

Watu husema mizimu haipo hasa wafia dini lakini wanasahau kwamba sauli alikwenda kwa muaguzi akasema anataka amuinulie roho ya samuel ambaye ni marehemu na ile roho ilivyokuja ikawa inasema mbona unanitaabisha?

Mfano kabila la wahaya huwa wana nyumba maalum (mishonge) hii kwa kilugha zinaitwa (nyaruju), huwa zinakaa zikiwa zimefungwa milango yake.

Kwa lugha nyingine mahali zilipo panaitwa (omukikare) kiswahili inaweza kuwa imaya kizungu (empire). Hapo ukoo wote huwa unajua ndio asili yao ilipo na ndipo roho za wazee (ancestors) zilipo.

katika page yetu ya dream zone tuna makala hizi nyingi na tiba zake, tu follow link hii

https://www.facebook.com/dreamzonetz?mibextid=ZbWKwL

Mizimu inawatesa wengi

1: wengine wamevaa bangili za chuma mikononi sababu ya mizimu
2: kuna watoto wameacha shule, kila wakienda shule hawaoni ubaoni, wanaona mauza uza kisa mizimu
3: Mizimu ipo tangu enzi na enzi waoati mwingine ikisaidia na wakati mwingine ikiharibu

Lakini kumbuka kuna mizimu ambayo ni mashetani huvaa mwili wa marehemu ama mtu aliye hai na kuwatokea watu huku ukijifanya mzimu mwema ama mbaya na mzimu huu hukopi kila kitu cha marehemu aliyekuwa hai halo awali kila kitu hukopi na kujifanya ni yeye na mzimu hii inaishi hadi miaka elfu hivyo inazo taarifa zote za mtu tangu yupo tumboni na kufahamu vyema maisha yako yote kwamba atakuwa nani hadi atakapokufa.

Generation nzima ya familia tree yako kuanzia chimbuko la ukoo au kabila fulani mjzimu inazo taarifa zote ndiyo maana wakati mwingine ukikutana na mtu katika tendo la ndoa basi mnaweza kushare mizimu yenu sasa hapo ni balaa lingine maana kuna watu wamaishi na mizimu ya wengine kwa kukutana nao kimwili na mizimu hii imewaletea matatizo makubwa na maumivu yiyopelekea wengine kupoteza maisha.

Tatizo la mizimu haitaki maendeleo, watu wakiendelea watoto watapa elimu na wakipata elimu awatokumbuka kutambika mizimu hapo ndipo shida ya mizimu.

Kuna bangili ukivaa mkononi tu basi mizimu hukukimbia ama majini hukukimbia hii ni kwa sababu mfano kuna binadamu kuna vitu hawapendelei na wakiviona kwako hawasogei mfano k**a unafuga nyoka na mwingine hapendi nyoka basi hasogei kwako ndivyo ilivyo kwa majini, wachawi nk kuna vitu navyo awapatani navyo hivyo ili kuwazuia wasikuvae unavaa unatumia vitu wasivyovipenda mfano miti,mimea, vyakula,kemikali,madini.

Mizimu huweza kuvamia na kuzuia nyota yako kufanya kazi ama kuzuia maendeleo yako yoyote ama kukutupia ugonjwa wowote.

Mizimu ambayo mnshare yaani ile mizimu ambayo umeitoka kwa kukutana na mtu kimapenzi hii ni mibaya sana kwani huingia ndani yako na ikiwa haijakupenda basi ni taabu juu ya taabu.

Kwanini kuwa na laana tu za ukoo na sio mafanikio ya ukoo?

Asili yetu wote ni hizi koo ambazo zimetokea kwenye miungu kabla hawajapokea Dini za Mungu mmoja. Hata walipopokea hizi dini za Mungu mmoja haikuwa rahisi kuwatoa kabisa kwenye imani hizo na zinaendelea hadi leo pamoja na kuelimika kijamii na kidini!

Kimsimgi hakuna kitu kinachokosa chanzo na mara nyingi ikiwa ni mababu na wazazi wetu, matambiko na maagano. ..kuna mahali kuna kitu kilikosewa na hakuna akiyekirebisha aidha kwa makusudi au kwa kutojua sometimes ishu za uchawi na ushirikina vikichangia.

Cha kuleta faraja ni kwamba huinuliwa mmoja katika familia kuja kurekebisha hali hiyo..yeye atakuwa tofauti na wengine yeye ataangaziwa kuiona hali ilivyo na atataka kuchukua hatua...huwa ni mmoja tu katika familia.

Sababu ya laana ya mizimu kuna familia moja iliteketea yote na kubaki mama tu!,

Baba aliangukiwa na ukuta na kufa hapo hapo, kaka aliugua kisukari na kufa na mdogo alipata ajali ya boda boda wote walikufa mwaka mmoja.

Mtu akipata matatizo akashindwa kabisa kuyatatua kwa njia yeyote ile basi njia ya mwisho huwa ni kwenda kwenye makaburi ya wazazi/wapendwa wake waliotangulia na kuwaomba wamsaidie,wengi husaidiwa.

Lakini kumbuka chanzo kikubwa cha laana ni dhambi. Hukumu ya dhambi ni mauti (kiroho na kimwili)

Mizimu wakati mwingine huacha maagano katika ulimwengu wetu huu kwa maana mizimu ni jamaa zetu waliotangulia mbele za ha...
23/07/2024

Mizimu wakati mwingine huacha maagano katika ulimwengu wetu huu kwa maana mizimu ni jamaa zetu waliotangulia mbele za haki

Lakini wakati mwingine mizimu ni roho za kishetani ama kijini zinazojitokeza katika umbile la ndugu zetu waliokufa hasa k**a mtu huyo alifunga mikataba na majini ama mashetani na mikataba hiyo ni k**a kupata utajiri wa kafara fulani ama kupata mali kwa kuingia mikataba basi mtu huyo anapofariki majini ama mashetani huwatokea ndugu za marehemu kwa umbile la marehemu na wengi wakidhani wametokewa na mzimu wao.

Hivyo kuna mizimu ambayo ni mashetani ya kijini yanayokuja kwa wajihi wa watu ambao walishakufa na watu wakadhani ndio wenyewe.

Unakuta mtu anamuona mtu wake wa karibu k**a baba, mama, mke, mume, mtoto, dada, kaka, au rafiki ambaye kashafariki au kusikia sauti yake kabisa, akadhani ni mzimu, kumbe ni shetani wa kijini na anamtokea kwa lengo fulani k**a ni agano ama kuja kumdhulu ama kumlaghai.

Kila binadamu aliyepo duniani ana watangulizi wake k**a vile Baba, Mama, Babu, Bibi na kuendelea.. Watangulizi hawa wanaacha alama kwa kizazi chao kinachofuata. Unaweza ukawa na sura yao, tabia zao, Jina lao na hata kufanana kwa makundi ya damu.. Watangulizi hawa wanaweza kukuachia alama ambazo huwezi kuziona kwa macho wala kufananisha, mfano kutembea na hata kucheka au kutabasamu..

Watangulizi hao ambao tunawaita mizimu kawaida wana uhalali mkubwa sana kwetu na wana nafasi kubwa sana katika maisha yetu hapa duniani.. Wewe uliyepo hapa duniani huna nafasi ya kuishinda mizimu ya kwenu mpaka pale utakapovunja muunganiko wako na mizimu hiyo.

Makala hii imeandikwa na dream zone secreat..unaweza kupata makala k**a hizi kwa wingi wewe follow page yetu link hii hapa... 🍇
https://www.facebook.com/dreamzonetz?mibextid=ZbWKwL

Binadamu anapozaliwa moja kwa moja anakuwa mali ya mizimu hiyo. Mizimu ina uwezo wa kuzuia mafanikio yako. Mizimu inaweza kikupa mafanikio pia. Mizimu inaweza kukuchagulia kazi ya kufanya na pia inaweza kukuzuia kufanya kazi fulani. Mizimu inaweza kukuepusha na majanga na pia kukuletea majanga. Hii itatokana na ufahamu wako kuhusu mambo hayo na maagano ambayo mizimu hiyo imeacha kwenu.

Kutokujua habari za mizimu sio suluhisho la wewe kuokoka na nguvu za mizimu.

Mizimu ipo na ina nguvu kubwa sana katika kuathiri maisha ya mtu aliye hai ikiwa mizimu yako iliacha agano fulani hapa duniani basi litaathiri vizazi na vuzazi hadi kufa kwenu na ikiwa ilkacha mambo mazuri basi itanufaisha vizazi vyenu.

Waafrika marehemu wetu tunawaita mizimu Wazungu marehemu wao wanawaita watakatifu sasa hapo itategemeana na kile mizimu iliacha.

Katika ulimwengu kuna tawala nyingi sana.. Zipo tawala zinazoonekana na tawala zisizoonekana.. Tawala zinazoonekana ni hizi za marais, wakuu wa mikoa, wilaya nk.. Tawala zisizoonekana ndio utakuta yapo majini, mapepo mizimu na kuna tawala ikiyo kuu kuliko zote.. Mwanadamu ndio mtawala wa dunia hii.. Toka kuumbwa kwa mwanadamu, Mwanadamu amepewa mamlaka ya kutawala vyote vilivyopo ulimwenguni.. Lakini kwa sababu ya kukosa maarifa k**a ilivyoandikwa basi mwanadamu huyu ameshindwa kutawala na amekuwa akitishwa na kuendeshwa na Majini, mizimu na nguvu tofauti za giza..

Na hawa wote wanafahamu wazi kuwa mwanadamu ndio mtawala wao.. Hivyo basi wanapigana usiku na mchana kuhakikisha kuwa mwanadamu huyu hapati maarifa ya kuwatawala.. Vita hii inapiganwa kwa kuwatumia mawakala wao ambao ni wanadamu au kwa kutumia Roho chafu zinazowaingia wanadamu na kufanya uharibifu.. Wanafanya hivyo kwa sababu wana uwezo wa kuona mafanikio ya mwanadamu hata miaka hamsini mbele.

Jiulize tu kwa nini mimba inashambuliwa toka kutungwa kwake (sio mimba zote)

Jilize tu ni kwa nini mtu ambaye hajafanikiwa kwa chochote kimaisha na bado anahangaika anasumbuliwa na wachawi na nguvu za giza.

Jibu ni kuwa nyota yake imeshaonekana na tishio lake kwa ulimwengu wa giza limeshaonekana hivyo anazuiwa kabla hajakomaa.

Ulimwengu wa Roho pamoja na mizimu una nafasi kubwa sana katika maisha ya mwanadamu aliye hai.

Wanaweza kukupa mafanikio, matatizo, magonjwa balaa na hata mikosi kutegemeana na nguvu walizo nazo kwa mwanadamu pamoja na uhalali au uhusiano walionao kwa mwanadamu huyo.

Mara nyingi mizimu huwa inachagua mzaliwa wa kwanza au wa pili katika familia.. Ifahmike kuwa kila kabila lina utawala wake wa mizimu ambapo utawala huo huwa unateua kuhani wa kuongoza shughuli zao..

Ila kutokana na Mwamko wa Elimu na dini mpya zilizoingia habari za mizimu zimeendelea kupoteza nguvu na wafuasi na taratibu elimu hii imekuwa ikipotea na watu hujikuta wakiangamia na kusingizia wachawi kumbe mizimu yao.

Lakini usumbufu wa mizimu bado umeendelea kuwepo kwa kiwango kikubwa katika maisha ya wanadamu bila wanadamu wenyewe kujua.. kwa ah 10000 tu k**a ofa njoo tukutazame mizimu ya ukoo kwako kwa kutumia macho na sura yako...

ITAENDELEA KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK LINK https://www.facebook.com/dreamzonetz?mibextid=ZbWKwL

Hili ndilo jengo kubwa la ghorofa la Regent International linalopatikana huko Hangzhou, China, ndilo jengo kubwa zaidi l...
22/07/2024

Hili ndilo jengo kubwa la ghorofa la Regent International linalopatikana huko Hangzhou, China, ndilo jengo kubwa zaidi la makazi ulimwenguni na hupokea zaidi ya wakazi 20,000!

🌍🏙 Hapo awali jengo hili lilijengwa k**a hoteli, lakini maajabu haya ya usanifu ya jengo hili la ghorofa 36 yalibadilishwa na kuwa jumuiya inayojitosheleza, inayojivunia vyumba vya makazi vya hali ya juu, bwalo kubwa la chakula, mabwawa ya kuogelea, saluni, maduka makubwa na zaidi.

Jengo hili lilibuniwa na Alicia Loo, mbunifu mkuu. Jengo hili lenye umbo la S lina urefu wa mita 206 na lilizinduliwa mwaka wa 2013.

Katika jengo hili ni nyumbani kwa jumuiya mbalimbali, kuanzia wataalamu wachanga hadi washawishi na biashara ndogo ndogo.

Jengo la Regent International lina urefu wa zaidi ya mita za mraba 260,000, likitengeneza upya anga na kufafanua upya maisha ya mijini nchini China. 🏠

Kichwa chake na nywele zake zilikua nyeupe k**a sufu/cotton/pamba na macho yake yalikua k**a miale ya moto iwakayo .. mi...
22/07/2024

Kichwa chake na nywele zake zilikua nyeupe k**a sufu/cotton/pamba na macho yake yalikua k**a miale ya moto iwakayo .. miguu yake k**a shaba/copper nyeusi iliyochomwa kwenye moto. Kati ya hizo picha ipi inaendana na hayo maandiko ya biblia..

20/07/2024
Jiji la kale la Ninawi lililoitwa “jiji la umwagaji wa damu”Ninawi lilikuwa jiji kuu la Milki ya Ashuru. Lilikuwa jiji k...
20/07/2024

Jiji la kale la Ninawi lililoitwa “jiji la umwagaji wa damu”

Ninawi lilikuwa jiji kuu la Milki ya Ashuru. Lilikuwa jiji kubwa lenye mahekalu na maeneo yenye kuvutia, barabara pana, na kuta ndefu. Nabii Myahudi Nahumu aliliita “jiji la umwagaji wa damu.

Hii ni kwa sababu michoro ya ukutani katika jumba la mfalme Senakeribu huko Ninawi inathibitisha ukatili huo. Mchoro mmoja unaonyesha mtesaji aking’oa ulimi wa mfungwa aliyepigiliwa ardhini. Maandishi ya ukutani yanasema kwamba mateka walifungwa kwa minyororo iliyokuwa na kulabu zilizoingizwa puani au midomoni. Maofisa waliotekwa walidhihakiwa kwa kufungwa shingoni vichwa vya wafalme wao waliouawa.

Vichwa vya wanadamu vilipangwa k**a piramidi kwenye barabara ya mshindi; wavulana na wasichana walichomwa wakiwa hai au kuwekwa kando ili wateswe baadaye; wanaume walitundikwa, walichunwa ngozi wakiwa hai, walipofushwa, au kukatwa mikono na miguu, masikio na pua.”

🍇Ninawi ni mji uliokuwepo kaskazini mwa Taifa la Iraq kwasasa. Mji huu kwasasa haupo, ila mahali pale ulipokuwepo mpaka leo pako!. Na mji huu ndio uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru.

Ashuru ilikuwa ni nchi iliyokuwepo maeneo ya Iraq, Uturuki, na Syria..Mataifa haya matatu yamechangia sehemu ya nchi hiyo ya Ashuru, lakini kwasasa duniani hakuna Taifa linaloitwa Ashuru. Kwani baada ya mataifa hayo matatu kuzaliwa Taifa hilo la Ashuru likafa.Ninawi ndio mji ambao Nabii Yona aliambiwa akahubiri Injili, lakini kinyume chake akakimbilia Tarshishi.

Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanon.

Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israel (na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanon haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)

Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI.

Wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote.

Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU nyingi za kibiashara kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara

Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi

Kwa nyongeza tu Lebanon ndipo alipotoka mwanamke katili Jezebel mke wa Ahab kwenye Biblia.

Mwanama huyu aliogopwa kwa Ukatili na alileta Miungu yake ya Baal Israel. Alimpelekesha sana Nabii Elijah.

Alitokea mji wa Sidon kusin mwa Lebanon sasa hivi ngome kuu ya Hezbollah.

Lebanese walijulikana zamani k**a Phoenician wafanyabiashara wakubwa sana.

Kivutio cha Lebanon ni miti aina ya Cedar. Hii miti ni mingi sana Lebanon enzi na enzi na ni nembo yao ya taifa hata kwenye bendera yao ipo.

Mji wa Ninawi haukuwa mji wenye watu wengi sana lakini ulikuwa umeendelea sana. Kipindi Nabii Yona anatumwa kwenda kuhubiri huko, biblia inarekodi mji ule kuwa na watu 120,000 tu!.video hapa https://youtu.be/4A8TiSxVqfo

Masimulizi katika vitabu mbalimbali hasa vitabu vitakatifu yanasema

Watu wa Ninawi walikuwa wameitikia wito wa mahubiri ya Yona na wakageuka kutoka kwa njia zao mbaya kumtumikia Bwana Mungu Yehova. Lakini miaka 150 baadaye, Ninawi ikarudi kuabudu sanamu, vurugu na kiburi. Kwa mara nyingine tena Mungu akatuma mmoja wa manabii wake Ninawi kuhubiri hukumu katika uharibifu wa mji na kuwaonya watubu. Cha kusikitisha, watu wa Ninawi hawakutilia maanani onyo za Nahumu na mji ukawekwa chini ya utawala wa Babeli.

Habari za kuangamizwa kwa mji wa Ninawi ni miongoni mwa nabii za kushangaza ambazo maelezo yake yanapatikana katika Biblia. Habari hizi zilitabiriwa na Nabii Nahumu mwaka 700 K.K. Katika utabiri wake alitabiri kuwa mji mkubwa huu, utaangamizwa kabisa na hautajengwa tena.

Unabii huu ulitimizwa mwaka 606 K.K, wakati Wamedi walipouharibu na kuuteketeza. Sawasawa na maneno ya Nabii Nahumu, mji huu haujawahi kujengwa.

Anasema Mike Tyson "Mwanangu Mkubwa Aliniambia Kwamba Anataka Kuwa Bondia K**a Mimi, Nikamwambia Umeshatembea Ulaya Na D...
16/07/2024

Anasema Mike Tyson "Mwanangu Mkubwa Aliniambia Kwamba Anataka Kuwa Bondia K**a Mimi, Nikamwambia Umeshatembea Ulaya Na Dunia Yote Unasoma Shule Za Binafsi Na Maisha Mazuri Huwezi Kuwa Bondia. Unataka Ukapigane Na Watu Wenye Hasira Wanyama K**a Mimi? Nimevumilia Kupigwa Maumivu Na Mateso Makali Ili Wanangu Wasije Wakaishi Maisha K**a Yangu, Kazi Ya Ubondia Ni Ya Watu Mafukara Wenye Hasira Na Tabu Ambao Wanatafuta Kula Yao, Watu Hawa Huwa Wanyama Sana Unapokutana Nao Hivyo Unapotaka Kukabiliana Nao Ujue Unakabiliana Na Wanyama Watu Wabaya K**a Nilivyo Mimi Baba Yenu"

Wakazi wa msitu wa Amazoni huamini kwamba msitu huo umejaa nafsi zinazozurura usiku, roho zinazosababisha magonjwa, na M...
15/07/2024

Wakazi wa msitu wa Amazoni huamini kwamba msitu huo umejaa nafsi zinazozurura usiku, roho zinazosababisha magonjwa, na Miungu inayojificha ndani ya mito ikisubiri kuwanasa watu.

Fikiria kuhusu Kabila la Aguaruna moja kati ya makabila makubwa zaidi nchini Peru.

Kabila hilo la Aguaruna wanaabudu miungu mitano tofauti:

“Baba Shujaa wa Vita,” “Baba wa Maji,” “Mama wa Dunia,” “Baba wa Jua,” na “Baba wa uganga.”

Watu wa kabila hilo wanaamini kwamba wanadamu wanabadilishwa kuwa mimea na wanyama. Kwa kuwa wanaogopa kuwakasirisha viumbe wa roho, wenyeji huepuka kuwaua wanyama fulani nao huwawinda wengine inapohitajika tu.

Waganga ndio husimamia maisha ya kidini na ya kijamii. Wao hutumia mimea kujipumbaza akili. Watu fulani katika maeneo hayo huwatazamia waganga hao watibu magonjwa, watabiri jinsi uwindaji na mavuno yatakavyokuwa, na kutabiri matukio ya wakati ujao.

Tazama hapa makala bora kuhusu msitu wa Amazom bonyeza link https://youtu.be/devMBwi0of4

ASILI YA JINA LA MSAIDIZI WA DEREVA KUITWA "TANDIBOI"Katika kipindi cha kabla ya enzi ya ukoloni, na hata ukoloni ulipoi...
11/07/2024

ASILI YA JINA LA MSAIDIZI WA DEREVA KUITWA "TANDIBOI"

Katika kipindi cha kabla ya enzi ya ukoloni, na hata ukoloni ulipoingia nchini Tanganyika, aina hiyo ya magari ndio yalikuwa vyombo vikuu vya usafiri nchini.

Magari hayo hayakuwa ya kuwasha kwa funguo (ignition key/starter). Yaani yalikuwa yanawashwa kwa kuzungusha "hendeli" kwa mikono....😀

Ukiangalia kwa makini ama ukizoom, unaweza kuona kuna kimtalimbo ambacho kimechomoza kwa mbele, chini kidogo ya taa. Kwa hivyo ili kuwasha injini ilibidi uzungushe hio hendeli kwa dakika kadhaa, k**a wafanyavyo wasaga unga katika mashine za kusagia za kizamani.

Wakati hio kilikuwa na vijana wa kiume wenye msuli kidogo ambao ndio waliokuwa wakifanya kazi hiyo.

Na dereva, aghalabu alikuwa mzungu, akishaingia ndani ya gari alikuwa anampigia kelele kijana wa kuwasha gari: "OK! Turn Boy! turn boooy!! Yaani zungusha (hendeli) kijana! Zungusha kijana.

Nasi Wamatumbi k**a ilivyo kawaida yetu tukisikia neno lazima tulitohoe kivyetu. Hivyo hata baada ya magari ya kuwashwa kwa hendeli yalipotoweka na kuja ya kuwasha kwa funguo, hadi leo msaidizi yeyote wa dereva, hasa wa lori, anaitwa "Tandiboi" ikimaanisha "Turn boy...."

Uyoga wa Kichawi: Uyoga wa Kichawi ni dawa ya kulevya yenye alkaloidi za kiindole, iliyoanza kutumika katika kipindi cha...
05/07/2024

Uyoga wa Kichawi: Uyoga wa Kichawi ni dawa ya kulevya yenye alkaloidi za kiindole, iliyoanza kutumika katika kipindi cha kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo Mwana wa Mungu (miaka 9,000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo), iliyokuwa ikitumika katika matambiko ya kifalme na kidini hata kabla ya kuandikwa kwa historia. Dawa hii husababisha furaha iliyochanganyikana na uwendawazimu, na ndiyo iliyoipa ushindi Denmaki katika vita yake ya Viking dhidi ya Uingereza mnamo mwaka 1016. Dawa hii imetumika katika kitabu cha Kolonia Santita, ikiwa mojawapo ya dawa za kulevya zilizolimwa na zilizosafirishwa na Kolonia Santita ulimwenguni kote.

Address

Mbeya

11000

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HMG posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share