Zanzibar young journalist

Zanzibar young journalist WANAHABARI WACHANGA AMBAO TUNA MALENGO YA KUISAIDIA JAMII KUONDOKANA NA MATATIZO AMBAYO YAMEJIFICHA KWA LENGO LA KULETA USAWA KATIKA JAMII.

Tafsiri ya misamiati ya lugha ya Kiswahili.
23/07/2024

Tafsiri ya misamiati ya lugha ya Kiswahili.

Abaya kinapatikana dukani kwetu.
30/03/2024

Abaya kinapatikana dukani kwetu.

Baada ya baadhi ya wananchi visiwani Zanzibar kushindwa kufuata sheria na taratibu za nchi na kupelekea mijadala tofauti...
30/03/2024

Baada ya baadhi ya wananchi visiwani Zanzibar kushindwa kufuata sheria na taratibu za nchi na kupelekea mijadala tofauti. Ikulu ya Zanzibar yatoa taarifa.

"Pamoja na ugumu wa utumiaji wa dawa za Pressure kwa wagongwa hao na dawa zinazotolewa zinataka kupitiwa upya kubaini us...
16/02/2024

"Pamoja na ugumu wa utumiaji wa dawa za Pressure kwa wagongwa hao na dawa zinazotolewa zinataka kupitiwa upya kubaini usahihi wake" Haji Fundi meneja wa mwenvuli wa taasisi zinazotoa huduma za maradhi yasiyoambukiza Zanzibar.

MAISHA NI POPOTE PALE AMBAPO FURSA INAPATIKANA.Ninachotaka kusema kwamba, Kung'ang'ania sehem moja kwa hisia na tumaini ...
12/08/2023

MAISHA NI POPOTE PALE AMBAPO FURSA INAPATIKANA.

Ninachotaka kusema kwamba, Kung'ang'ania sehem moja kwa hisia na tumaini kuwa utatoka siku moja maana tumejaribu sana ila bado mambo hayaendi kiukweli sio ustaarabu katika mifumo ya Maisha, inabidi tuamke na kufikiria wapi kwingine tunaweza kujipata au kuna fursa zaidi.

Hii picha imebeba zaidi ya maneno 1000 kwangu nimeipa Caption ya MAISHA NI POPOTE PALE AMBAPO FURSA INAPATIKANA.

OFFICIAL: Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ally Saleh Kiba 'Alikiba' KING KIBA amehama rasmi kutoka Yanga SC 🇹🇿 na kuji...
02/08/2023

OFFICIAL: Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ally Saleh Kiba 'Alikiba' KING KIBA amehama rasmi kutoka Yanga SC 🇹🇿 na kujiunga na watani wao,Simba SC 🇹🇿.

Alikiba amekabidhiwa kadi rasmi ya Uanachama wa Simba mda mfupi uliopita.

Alichokisema KING KIBA

"Kila mtu anapenda kwenda sehemu ambayo anakuwa Appreciated (Thaminiwa)"

07/01/2023

Jitahidi kuvuruga fedha uipatayo wakati babaako na mama ako aliekulea kwa mazingira ya shida sana anaishi maisha haya.
Je umetafakari kesho yako?

01/11/2021

Nchi za G20 zaahidi kupunguza uchafuzi wa gesi ya kaboni duniani

Viongozi wa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani wameahidi kupunguza viwango vya gesi ya kaboni inayochafua mazingira ,wakati wa mkutano wa kilele wa siku mbili ambao utaweka msingi wa kongamano la Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi mjini Glasgow, Scotland.Kwa mujibu wa taarifa, viongozi hao wa kundi la G20 pia wamekubaliana kusitisha ufadhili wa miradi ya uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe japo hawakuweka muda wa mwisho wa kuondokana na utegemezi wa nishati ya makaa ya mawe kwenye nchi zao, hatua hiyo ikiwa ahueni kwa China na India zinazotumia nishati ya makaa ya mawe.Uingereza ilitaraji kuwepo kwa ahadi thabiti za kufikisha mwisho matumizi ya nishati ya makaa ya mawe kuelekea mkutano wa Glasgow.Kundi la G20 linawakilisha zaidi ya robo tatu ya nchi zinazoongoza kwa kutoa gesi chafu duniani, wakati mwenyeji wa mkutano huo Italia ikitarajia kuwepo kwa malengo thabiti ya jinsi ya kupunguza utoaji wa hewa ukaa pamoja na kuzisaidia nchi maskini kukabiliana na ongezeko la joto.Waziri Mkuu wa Italia Mario Dradhi amewaambia viongozi kwenye mkutano huo wa mjini Rome kuwa wanahitaji kuweka malengo ya muda mrefu na mfupi ili kusaidia kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

https://www.facebook.com/108926914834162/posts/114949237565263/MHE. HEMED AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WANAOGHUSHI NYAR...
02/09/2021

https://www.facebook.com/108926914834162/posts/114949237565263/

MHE. HEMED AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WANAOGHUSHI NYARAKA

Uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi umetakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wananchi wanaofika kupata huduma katika Idara ya Usafiri na Leseni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani iliyopo Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Unguja.

Alisema Serikali inahitaji mapato katika uendeshaji wa kazi zake hivyo mamlaka hiyo ina jukumu la msingi la kuweka utaratibu imara utakaosaidia kuingizia serikali mapato, ili kusaidia kukuza uchumi wa Nchi.

Akizungumzia juu ya suala la kughushi nyaraka feki Mhe. Hemed alimuagiza Mkurugenzi Mkuu Mamlaka Usafiri ya na Usalama barabarani kuchukua hatua kali dhidi ya watu watakaobainika kufanya vitendo hivyo ikiwemo kuwafikisha mahak**ani ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Katika hatua nyengine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo kuangalia namna bora ya kuimarisha ulinzi katika eneo la maegesho ya magari kwa kufunga Kamera za usalama ili kudhibiti uhalifu unaojitokeza mara kwa mara.

Aidha, aliwataka wananchi wanaofika kupata huduma katika mamlaka hiyo kujenga tabia ya uaminifu na kauchana na vitendo vya utapeli ikiwemo kughushi nyaraka za Serikali ili kujenga mashirikiano mazuri na wafanyakazi wa idara hiyo.

Akijibu baadhi ya changamoto zilozotolewa na wananchi Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri na Usalama barabarani Haji Ali Zubeir alisema mamlaka anayoisimamia imekuwa ikichukua hatua kwa wananchi wanaokiuka taratibu ili kuondosha vitendo vya kihalifu ikiwemo kughushi nyaraka feki za Leseni.

Alieleza kuwa, mamlaka ya Usafiri na Usalama barabarani imekuwa ikisimamia sheria kwa wanafunzi wanaojifunza udereva kwa kutumia gari za manual badala ya automatic ili kuwajengea umahiri wanafunzi hao na kupunguza idadi ya ajali na athari mbali mbali wanapokuwa Barabarani.

Wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Hemed Suleiman Abdulla alifanya ziara katika ukarabati wa ujenzi unaoendelea wa nyumba ya mnadani Darajani unaosimamiwa na Shirikia la Nyumba Zanzibar unaofanywa na kampuni ya Yassin and Son Co. Limited.

Akimkaguza kuangalia ukarabati wa ujenzi huo Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Zanzibar Mwanaisha Said alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa, Shirika la Nyumba limeamua kufanya marekebisho kwa baadhi ya nyumba zake ili kuiongezea mapato serikali.

Mkurugenzi Mwanaisha alisema kukamilika kwa ukarabati wa ujenzi huo kutasaidia kuingizia Serikali jumla ya Shilingi Millioni 18 (18,000,000) kwa mwezi badala ya shillingi Milioni tatu laki nane (3,800,000) kwa mwezi kabla ya ukarabati wa jingo hilo.

Alibainisha kwamba, mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ujenzi huo unaofanywa na kampunzi ya Yassin and son CO. Limited jengo hilo litatumika kwa ajili ya biashara ambapo fremu za milango ya chini zitatumika k**a maduka kwa ajili kukodishwa wafanyabiashara na ghorofa ya juu itatumika kwa ajili ya kukodishwa kwa matumizi ya ofisi.

Nae, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuagiza mkandarasi aliepewa dhamana ya ukarabati wa wa jengo hilo kuzingatia viwango na ubora katika kukamilisha ukarabati wa ujeniz huo.

Pamoja na mengine Mhe. Hemed alimtaka mkandarasi kumaliza kazi hiyo mapema ili kutoa fursa kwa Shirika la Nyumba kuweza kufanya biashara kwa lengo la kuingizia Serikali mapato, ili ziweze kusaidia ujenzi wa shughuli za kijamii.

Wakati wa mchana, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikutana na viongozi wa Jumuiya ya wakimbiza mwenge Tanzania (TAUTA) Afisini kwake Vuga na kubadilishana nao mawazo.

Katika kikao hicho Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Ndugu Erica Segela amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa TAUTA imepanga kufanya ukarabati wa Bweni la Karume lililopo Wilaya ya Chato, ili kuunga Mkono juhudi za Serikali kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wana Jumuiya hiyo kuendelea kufanyakazi kwa pamoja na kuishauri Serikali katika ujenzi wa taifa, na kuwapongeza kwa kuona umuhimu wa kuanzisha Jumuiya hiyo, ili kusaidia maendeleo Nchini.

Mhe. Hemed alifurahishwa na uamuzi wa Jumuiya hiyo wa kuamua kujiimarisha kiuchumi kwani kufanya hivyo kutasaidia kuijiendesha na kuondokana na utegemezi.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Septemba 02, 2021.

18/06/2021

Address

Mwanakwerekwe Zanzibar
Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar young journalist posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Zanzibar young journalist:

Videos

Share