Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Ukurasa rasmi wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar

10/09/2024
Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA) inawataarifu wateja wake na Jamii kwa ujumla kuwa Mfumo wa Usajili Mtandaon...
09/09/2024

Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA) inawataarifu wateja wake na Jamii kwa ujumla kuwa Mfumo wa Usajili Mtandaoni (ORS) sasa upo tayari kwa huduma ya usajili wa majina ya Biashara na Makampuni.
Mfumo huo umefanyiwa marekebisho ya kiufundi ya MongoDB na kuruhusu mfumo wa Database kufanya kazi kiufanisi zaidi. Aidha BPRA inawakaribisha wateja wake kutumia mfumo huo kwa lengo la huduma za usajili wa majina ya Biashara na Makampuni.

Meli ya mizigo ya AMU 2 kutoka Mombasa Kenya, iliwasili katika Bandari ya Mkoani Pemba, Septemba 3, 2024, ikiwa imebeba ...
06/09/2024

Meli ya mizigo ya AMU 2 kutoka Mombasa Kenya, iliwasili katika Bandari ya Mkoani Pemba, Septemba 3, 2024, ikiwa imebeba jumla ya Makontena matupu 40, ambapo Makontena yenye urefu wa Futi 40 ni 25 na ya Futi 20 ni 15

Makontena hayo matupu yameshushwa katika Bandari ya Mkoani Pemba, kwa ajili ya kukabidhiwa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) kwa lengo la kupakia Karafuu za Zanzibar zitakazosafirishwa kwenda katika masoko ya nje. Hali hii itaisaidia Shirika la ZSTC kupunguza gharama ya TZS milioni 100 endapo Shirika hilo lingetumia bandari ya Malindi, Zanzibar

Aidha, Mpango huu ni miongoni mwa utekelezaji wa sera ya Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kuifungua Pemba kiuchumi na kibiashara baina ya kisiwa cha Pemba na nchi nyengine.

Aidha, utaratibu wa ZSTC kwa mkulima wa zao la Karafuu, ni kuhakikisha kuwa anauza karafuu zake kwa Shirika hilo akiwa na kibali cha sheha wa shehia na kuziuza katika kituo cha ununuzi wa karafuu kilicho karibu naye.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Dkt. Said Seif Mzee amesema lengo ya mafunzo ya Urasimi...
04/09/2024

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Dkt. Said Seif Mzee amesema lengo ya mafunzo ya Urasimishaji wa Wafanyabiashara ni kuwawezesha Wajasiriamali kufanya urasimishaji wa Biashara zao, kuweza kutumia fursa zinazopatikana za Biashara na fursa za mikopo zinazotolewa na Taasisi za kifedha kwa lengo la kukuza Biashara zao, na jinsi ya kuweka kumbukumbu ya Biashara zao ambapo kwa upande wa Wizara itahakikisha inawawezesha Wajasiriamali pale fursa zinapotokea.

Ameyasema hayo, Septemba 4, 2024 wakati akifungua mafunzo ya Urasimishaji wa Wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda na Tume ya Mipango Zanzibar katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Tumekuja, Wilaya ya Mjini Unguja.

Aidha, Mafunzo hayo ya siku tatu (3) yamehudhuriwa na washiriki mia mbili (200) kutoka Wilaya ya Mjini ambapo Wizara imewashirikisha wawezeshaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA) Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA), Manispaa ya Mjini na Taasisi za Kifedha (NMB na CRDB) katika utoaji wa elimu kwa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo.

Nao, Wafanyabiashara hao, Abrahman Ali Dadi na Saadati Juma Suleiman wamesema mafunzo yaliyotolewa kwa kiasi kikubwa yatawasaidia umuhimu wa ulipaji kodi, umuhimu wa upatikanaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara, umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Hiari wa ZSSF na utambuzi wa sheria zilizo wekwa na Mamlaka husika ili kufanya Biashara kwa ufanisi.

Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Zanzibar (ZWCC) leo Septemba 2, 2024 wamefika...
02/09/2024

Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Zanzibar (ZWCC) leo Septemba 2, 2024 wamefika katika Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda kwa lengo la kujitambulisha na kuitambulisha bodi hiyo, pia walifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Fatma Mabrouk Khamis.

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda amewapongeza Wajumbe kwa ujio wao na amesema kuwa, Wizara itashirikiana na Bodi hiyo katika upatikanaji wa fursa za Biashara pamoja na kuangalia changamoto za kisera na kiutendaji zitakazojitokeza kuweza kutatuliwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Biubwa Omar Khamis ameishukuru Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda kwa mapokezi mazuri na ameiomba kuwaunga mkono katika kuwawawezesha na kuwaendeleza katika upatikanaji wa fursa za kibiashara ili Bodi hiyo iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma Mabrouk Khamis amesema Wizara inatekeleza maeneo makuu ...
30/08/2024

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma Mabrouk Khamis amesema Wizara inatekeleza maeneo makuu matatu ya Viwanda ambayo ni Dunga, Chamanangwe na Pangatupu.

Aliyasema hayo katika siku ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Mtaa wa Viwanda Dunga zuze Agosti 7, 2024, ambapo pia alifanya mahojiano na vyombo vya habari na kufafanua kuwa Wizara imekamilisha Ujenzi wa Barabara zenye urefu wa Kilomita 7.83 katika Mtaa wa Viwanda Dunga zuze ambayo ilianza Disemba 2023 chini ya Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) Iliyogharimu TZS. Bilioni 23.37 na ujenzi huo umefikia 75% na unatarajiwa kukamilika ifikapo Disema 22, 2024.

Aidha, alisema, Wizara inaendelea na ujenzi wa Miundombinu ya maji unaojumuisha ujenzi wa Mnara wa Tangi la maji lenye ujazo wa lita milioni moja, uchimbaji wa visima vitatu na utandazaji wa bomba za maji kwenye eneo la Viwanda lenye ukubwa wa ekari 173 unaotekelezwa chini ya Mkandarasi Simba Developer Limited kwa gharama ya TZS. Bilioni 3.467 na Umefikia 60%.

Pia alifafanua, kwa mwaka wa fedha 2024-2025, Wizara imeidhinishwa matumizi ya TZS. Bilioni 40.32 kwa lengo la kuyaendeleza Maeneo matatu ya Viwanda kwa ujenzi wa Ukuta wa uzio na Majengo ya Viwanda pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya umeme katika eneo la Viwanda Dunga na Chamanangwe, ujenzi wa Miundombinu ya maji na barabara za ndani katika eneo la Viwanda Chamanangwe na kuandaa Mpango Mkuu wa Ardhi (Masterplan), Uchunguzi na Upembuzi yakinifu katika eneo La Viwanda Pangatupu.

Kamati maalumu kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imekutana kwa ajili ya kujadili utafiti wa Viwanda unao...
28/08/2024

Kamati maalumu kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imekutana kwa ajili ya kujadili utafiti wa Viwanda unaotarajiwa kufanywa ili kubaini changamoto zinazoikabili Sekta ya Viwanda hapa Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha uwekezaji katika Sekta ya viwanda unaimarika na unadumu.

Kikao hicho kimefanyika leo Ogasti 28, 2024 katika ukumbi wa Wizara Kinazini na kuwakutanisha Wajumbe kutoka Idara zilizo chini ya Wizara hiyo, Wajumbe kutoka Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imesaini Hati ya Makubaliano na Kampuni ya Niajiri Platforms kwa lengo la kua...
27/08/2024

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imesaini Hati ya Makubaliano na Kampuni ya Niajiri Platforms kwa lengo la kuandaa mifumo ya kieloktroniki, uandaaji wa Takwimu na upatikanaji wa Taarifa zinazohusiana na soko la ajira la pamoja kwenye Sekta zilizo chini ya Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.

Aidha, Makubaliano hayo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yametiwa saini na Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Bi. Fatma Mabrouk Khamis na kwa upande wa Kampuni ya Niajiri Platforms saini hiyo imewekwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Lillian Madeje. Hafla iliyofanyika Agosti 26, 2024 katika Ukumbi wa Wizara Kinazini, Wilaya ya Mjini Unguja.

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imekamilisha utiaji saini wa Hati za Makubaliano ya Ujenzi wa Viwanda kwa Kam...
26/08/2024

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imekamilisha utiaji saini wa Hati za Makubaliano ya Ujenzi wa Viwanda kwa Kampuni tatu (3) na Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ambazo zitajenga Viwanda na Maabara katika Mtaa wa Viwanda Dunga-Zuze.

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma Mabrouk Khamis amesaini Hati hizo na kushuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi katika Siku ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Mtaa wa Viwanda Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 7, 2024

Aidha, Kampuni zilizosaini Hati hizo ni pamoja na SK Medicine ambayo itajenga kiwanda cha dawa za Binadamu, Afro Bio Chem itajenga kiwanda cha dawa na chanjo mbalimbali za Binadamu, Taasisi ya Viwango Zanzibar ( ZBS) itajenga Maabara na Kampuni ya Nanji 2020 ambayo itajenga kiwanda cha kuunda Magari

23/08/2024

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akitoa ufafanuzi kuhusu Eneo la kimkakati la Mtaa wa Viwanda Dunga Zuze, ambalo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha Mradi huu, kwa lengo la kuvutia Uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Viwanda na kuona mitaji inakuja kupitia uwekezaji wa eneo hilo.

Ifahamike kuwa tarehe 7 Agosti, 2024, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi aliweka Jiwe la Msingi katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Makala hii fupi, Mhe Waziri anafafanua zaidi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dkt. Said Seif Mzee, amesema utekelezaji wa falsafa ya Kaiz...
21/08/2024

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dkt. Said Seif Mzee, amesema utekelezaji wa falsafa ya Kaizen nchini Tanzania ulianza mwaka 2015 na kuleta matokeo chanya ambapo Makampuni 350 yamenufaika na kwa Zanzibar, Mradi wa Kaizen umeanza kutekelezwa rasmi mwaka 2023 ambapo kwa sasa kampuni tisa (9) zimenufaika kupitia mafunzo hayo.

Aidha, Dkt. Said amesema wanufaika wa Mradi huu ni pamoja na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Lootah Group of Company (Drop of Zanzibar), Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC), Inaya Limited, Zanto, Kiwanda cha Maji Amos Pemba, YYTZ, Agro Processing Limited, Kiwanda cha Mabati Metal Man na Tantex.

Ameyasema hayo, leo 21 Agosti,2024 katika Ufunguzi wa Warsha ya Uhamasishaji wa Matumizi ya Falsafa ya Kaizen katika Ukumbi wa Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) ambapo Wakufunzi kutoka YYTZ Agro Processing Limited, Inaya Limited na Karume Institute of Science and Technology (KIST) waliwasilisha mada mbalimbali kwa wajumbe na pia Wajumbe hao walijufunza na kuchangia mambo tofauti yaliyowasilishwa katika warsha hiyo.

21/08/2024

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akihutubia katika Kongamano la 19 la Biashara kati ya India na bara la Afrika lililoandaliwa na Shirikisho la wenye Viwanda katika mji wa New delhi, nchini India

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban leo tarehe 21 Agosti, 2024  ameshiriki na kuhutubia ko...
21/08/2024

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban leo tarehe 21 Agosti, 2024 ameshiriki na kuhutubia kongamano la 19 la Biashara kati ya India na bara la Afrika lililoandaliwa na Shirikisho la wenye Viwanda Newdelhi, Jamhuri ya India.

Katika hotuba yake, amesisitiza umuhimu wa India na Afrika kutumia fursa na rasilimali zilizopo katika kukuza wigo wa ushirikiano wa kiuchumi kwa maslahi ya pande mbili.

Aidha, Mhe. Omar ameeleza kuwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zina fursa nyingi za uwekezaji na amewahakikishia kuwa Zanzibar itaendelea kuthamini mchango na uhusiano ambao Serikali ya Jamhuri ya India wanautoa katika ukuzaji wa Biashara na Viwanda uliodumu kwa muda mrefu.

Kongamano hilo la siku tatu (3) limehudhuriwa na Makamu wa Rais 6, Mawaziri wa Biashara na Viwanda 42, pamoja na Wajumbe 789 kutoka nchi 46 za Afrika.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania ...
16/08/2024

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Balozi Fatma Ahmed Rajab.

Mazungumzo hayo yalilenga kukuza ushirikiano na mahusiano mazuri ya kihistoria na kindugu kati ya Zanzibar na Oman ili kukuza masuala ya biashara na uwekezaji

Aidha, Mhe. Omar amesema Wizara imejipanga kuweka sera na mikakati imara ya kiutendaji ili kutangaza fursa za kibiashara na uwekezaji kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa bidhaa ili kuifungua nchi kiuchumi.

Aidha, Waziri amempongeza Balozi kwa ushirikiano baina yao na kuhakikisha kuwa Wizara itashiriki katika mualiko wa kongamano la Biashara litakalofanyika tarehe 26-28 Septemba,2024 nchini Oman

Nae, Balozi Fatma amemshukuru Mwenyeji wake kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuwa wataendelea kukuza ushirikiano na uhusiano mzuri uliopo kati ya Zanzibar na Oman kwa lengo la kukuza uchumi wa pande zote.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara, Kinazini, tarehe 16 Agosti, 2024

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda   imetiliana saini na Serikali ya Jiji...
13/08/2024

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imetiliana saini na Serikali ya Jiji la Weihai la nchini China kutokana mahusiano mazuri yaliopo baina yao.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Omar Said Shaaban na Naibu Meya wa Manispaa ya Jiji la Weihai, Bwana Zhai Baogang katika ukumbi wa Wizara, Kinazini tarehe 12/08/2024, kwa lengo la kuimarisha Mashirikiano ya kimkakati kati ya Zanzibar na Jiji la Weihai (China) na kupatikana kwa fursa za kibiashara na uwekezaji, kuimarisha sekta za uzalishaji viwandani, baharini pamoja na kuendeleza uhusiano mzuri baina ya nchi hizo.

Aidha, Mhe. Waziri Shaaban amewashukuru Wageni wake na amewaalika Wafanyabiashara wenye viwanda kuja kuwekeza na kuzalisha bidhaa ambazo zinahitajika kwa wingi hapa nchini ili kupunguza gharama za bidhaa kutoka nje.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah leo tarehe 08/08/2024 ametembelea mabanda mbalimbali na...
08/08/2024

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah leo tarehe 08/08/2024 ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea hali ilivyo katika siku ya kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nane nane) yanayoendelea katika viwanja vya Dole Kizimbani, Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka  udongo na  kuweka maji kwenye ...
08/08/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo na kuweka maji kwenye Mti uliopandwa katika Mtaa wa Viwanda Dunga Zuze katika siku ya uwekaji wa Jiwe la Msingi, hafla iliyofanyika jana tarehe 7/08/2024

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika hafla ya Uzinduzi wa ...
06/08/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika hafla ya Uzinduzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto katika Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), iliyofanyika leo tarehe 6/8/2024. Maruhubi.

05/08/2024
04/08/2024

Vijana wametakiwa kutumia fursa zinazojitokeza katika sekta ya kilimo ili kujifunza mbinu mpya za kilimo biashara kwa lengo la kujikwamua kiuchumi, katika Mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda kwa kushirikiana na Chuo cha kilimo cha China yaliyofanyika katika ukumbi wa ZBS, Maruhubi tarehe 2 Agosti, 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa, kilimo ndio uti wa mgong...
03/08/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa, kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu ambapo asilimia 40 ya Wananchi wamejiajiri moja kwa moja kupitia Sekta hiyo, huku takwimu za mwaka 2023 zinaonesha Sekta ya Kilimo imechangia asilimia 24.9 ya Pato la Taifa hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo, leo tarehe 03 Agosti, 2024 katika hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya saba ya Kilimo ya Nane nane kwa mwaka 2024 yanayo fanyika Dole Kizimbani Wilaya ya Magharibi A, Unguja yenye kauli mbiu Kilimo ni utajiri kila mtu atalima.

Aidha Dk. Mwinyi amefafanua kuwa, ni dhahiri Kilimo kinaunganisha Sekta nyingi muhimu ikiwemo Biashara,Viwanda, Utalii, Maji na Nishati hivyo kikiboreshwa kitaleta matokeo chanya kwa uchumi mzima wa nchi yetu, ambapo pia Dk. Mwinyi alitembelea Mabanda mbali mbali ya Taasisi za Umma.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea n...
29/07/2024

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na jitihada kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya Nchi kwani Zanzibar bado inafursa nyingi zakimaendeleo zikiwemo za kiuchumi pamoja na uwekezaji.

Ameyasema hayo, jana katika majadiliano kuhusu Biashara na uwekezaji kati ya Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na China katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege na kuhudhuriwa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China, Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wawekezaji pamoja na Wadau mbali mbali.

Aidha alisema, fursa hizo, zinahitaji mitaji, uwekaziji kutoka Mataifa ya kigeni na Makampuni kutoka nje ambayo yanauwezo kuweka mitaji pamoja na kuleta ujuzi sambamba na wafanyabiashara wa ndani, wawekezaji kuweza kukutana na wenziwao ambao wanaweza kushirikiana katika kukuza Biashara na uwekezaji baina ya China na Zanzibar na Mataifa mengine.

Kituo cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF) ni eneo lililopo Wilaya ya Magharibi ‘B’ Dimani na ni kituo ...
26/07/2024

Kituo cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF) ni eneo lililopo Wilaya ya Magharibi ‘B’ Dimani na ni kituo cha Uwekezaji chenye eneo lenye ukubwa wa ekari 11 na masafa ya umbali wa kilomita 14.8 kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Aidha, eneo hilo linasimamiwa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo na hutumika katika Maonesho ya Biashara ambayo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka ambapo hushirikisha Taasisi za Umma, Taasisi Binafsi, Makampuni, Wafanyabiashara na Wajasiriamali.

Eneo hilo hutumika katika Mikutano ya Kimataifa, Mikutano ya Taasisi za Umma na Taasisi binafsi, sherehe za harusi, na Mahafali kwa Taasisi za elimu ya juu na kwa Wahtimu wa elimu ya lazima.

Hivyo, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda inawakaribisha Wadau wote kulitumia eneo hilo kwa mustakbali wa maendeleo ya Nchi, unaweza kuwasiliana na Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa namba +255656444784/ 0777567965 au fika katika Ofisi za Wizara Kinazini, Ghorofa ya kwanza katika Idara ya Biashara na Masoko.

Watendaji kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda wamefanya ziara ya kikazi kukagua Mradi wa Ujenzi wa Barabar...
23/07/2024

Watendaji kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda wamefanya ziara ya kikazi kukagua Mradi wa Ujenzi wa Barabara unaoendelea kujengwa katika eneo tengefu la Viwanda Dunga Zuze Wilaya ya kati ambao Mradi huo umejumuisha Barabara kuu
(Access roads) na Barabara za ndani (Internal roads).

Aidha, Ziara hiyo imejumuisha kampuni husika ya ujenzi ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Washauri elekezi kutoka Nimeta, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS) Mhandisi Safia J. Ameir na Maafisa mbali mbali wa Wizara ya Biashara ambapo ziara hiyo imeambatana na kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za CCECC zilizopo Kisauni na kujadili ajenda za kikao kilichopita pamoja na muendelezo wa hatua iliyofikiwa ya Mradi huo.

Mradi wa ujenzi wa Barabara yenye urefu wa kilomitia 7.83 umefikia asilimia 75% na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo tarehe 22 septemba, 2024 na kwa sasa hatua inayoendelea ni uwekaji wa kingo za mawe (kerbstone) pamoja na miundombinu ya nishati na maji.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Taasisi zinazosimamia b...
14/07/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Taasisi zinazosimamia biashara na uwekezaji, Bara na Zanzibar kuhakikisha wanaondoa urasimu na kuwawezesha wafanyabiashara zaidi.

Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 13 Julai 2024, alipofunga Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba, Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali zote mbili zina nia thabiti katika kuboresha mazingira ya biashara kwa kuelekeza taasisi za Serikali kusomana katika mifumo , kuondoa kodi na tozo kwenye maeneo ya kimkakati.

Address

46 BARABARA YA MALAWI, GHOROFA 1 And 5
Zanzibar
S.L.P601,[email protected]

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda:

Videos

Share



You may also like