15/04/2024
Kwenye mashambulizi ambayo waliyafanya Iran kwenda nchini Israeli, takribani makombora 9 ya balistiki yalifanikiwa kuzifumua kambi kadhaa za kijeshi zilizopo nchini Israeli.
Shambulio moja lilitua kwenye kituo cha anga cha Nevatim kilichopo kwenye Mji wa Negev ambacho kilipigwa makombora 5 ya balestiki.
Makombora hayo yalifanikiwa kuharibu njia kuu ya ndege,
ndege ya usafirishaji ya C-130, na vifaa kadhaa vya kuhifadhi silaha.
Shambulio lingine lilifanyika kwenye kituo cha anga cha Ramon, ambacho pia kipo kwenye Mji wa Negev.
Kituo hiki Kilipigwa na angalau makombora 4 ya balestiki na
Kusababisha uharibifu ambao haujajulikana mpaka sasa.
Taarifa hizi zimetolewa na wachambuzi wa masuala ya kivita
wa Marekani kwa kupitia kituo cha habari cha ABC News.
Kwa upande wa Israeli,
Wizara ya Ulinzi imetoa picha na video za ukarabati wa sehemu iliyoharibika kwenye njia ya ndege iliyopo kwenye
kambi ya Nevatim ambayo ilipiga na makombora ya Iran.
Kwa lugha rahisi ni kwamba, ndege zisizo na rubani ambazo zilitumwa na Iran ndizo ambazo zilidunguliwa na Israeli,
Kwa upande wa Makombora machache ya Balestiki na Hypersonic ambayo waliyatuma, yalifanikiwa kugonga kwenye maeneo husika.
Huku Taifa la Israel wakiendelea kuficha uharibu zaidi ulio tokea lakini taarifa zimeanza kuvujishwa ndani ya maeneo husika.
Credit to siasa makini