Habari za Zanzibar

Habari za Zanzibar Twitter:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
24/11/2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UWANJA WA AMAAN KUKABIDHIWA KWA SERIKALI DISEMBA MWISHONI MWAKA HUURais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi...
24/11/2023

UWANJA WA AMAAN KUKABIDHIWA KWA SERIKALI DISEMBA MWISHONI MWAKA HUU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12 zitafanyika katika uwanja wa Amaan.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo leo alipokagua maendeleo ya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Amaan, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 24 Novemba 2023.

Aidha Rais Dk. Mwinyi amempongeza mkandarasi kampuni ya Orkun kwa kazi nzuri ya kuukarabati uwanja huo ambapo wametumia miezi sita tu.

Mkandarasi huyo ameahidi kuikabidhi Serikali uwanja huo mwishoni mwa mwezi wa Disemba mwaka huu.

✍️📸 - Ikulu Zanzibar.

Jummah Mubarak 📆 24 Nov, 2023.
24/11/2023

Jummah Mubarak

📆 24 Nov, 2023.

📍 Ikulu Zanzibar
09/11/2023

📍 Ikulu Zanzibar

Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) ametembelewa na Marafiki zake kutoka Mbeya.Awali a...
08/11/2023

Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) ametembelewa na Marafiki zake kutoka Mbeya.

Awali akiwa anazungumza na wageni hao, Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Biteko(Mb) alikuja kuwasalimu na kuwapa moyo waendelee kumuombea Spika wa Bunge.

Wageni hao wamefika Leo tarehe 08 Novemba 2023, Bungeni Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Eng. Zena Ahmed Said pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi ...
08/11/2023

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Eng. Zena Ahmed Said pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, katika Ufunguzi wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha India (Tawi la Zanzibar) Mkoa wa Mjini Magharibi, tarehe 06 Novemba 2023.

Top Indian university opens first offshore campus in Africa.
08/11/2023

Top Indian university opens first offshore campus in Africa.

Spika wa Bunge na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kuzungumza na Balozi wa Qatar nchini...
08/11/2023

Spika wa Bunge na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kuzungumza na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 06 Novemba, 2023.

Balozi huyo amempongeza Mhe. Dkt. Tulia kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa IPU na kumuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa upande wake Mhe. Dkt. Tulia amemuomba Balozi huyo amfikishie shukrani zake kwa Wabunge wa Bunge la Qatar kwa jinsi walivyomuunga mkono wakati wa uchaguzi.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada maalum ya kuaga mwili wa Mare...
07/11/2023

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada maalum ya kuaga mwili wa Marehemu Issa Juma Nangalapa ambaye ni Kaka wa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa iliyofanyika Ruangwa Mkoani Lindi, tarehe 6 Novemba, 2023.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameku...
07/11/2023

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ndg. Ruth Zaipuna walipomtembelea leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamempongeza Mhe. Spika kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Kwa upande wake Mhe. Spika aliishukuru Benki hiyo kwa kujitoa kwake kulisaidia Bunge katika shughuli mbalimbali hususan michezo.

📍Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Tangazo la Kupokea maoni kuhusu Mswada.
07/11/2023

📍Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Tangazo la Kupokea maoni kuhusu Mswada.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kufungua Taasisi ya Chuo c...
06/11/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kufungua Taasisi ya Chuo cha Teknolojia cha India Madras - Tawi la Zanzibar, leo tarehe 06 Oktoba, 2023. Bweleo, Wilaya ya Magharibi B - Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Hayati Dkt. John Po...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla fupi ya kukabidhi nyumba ya kuishi iliyopo wilaya ya Kinondoni ambayo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufunguo mjane wa Hayati Dkt. John ...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufunguo mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli ikiwa ni ishara ya kukabidhi nyumba mpya ya kuishi kwa familia ya Dkt. John Pombe Magufuli iliyopo wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambayo amejengewa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe k**a ishara ya uzinduzi wa nyumba mpya ya...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe k**a ishara ya uzinduzi wa nyumba mpya ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, na kuikabidhi kwa Mama Janeth Magufuli, nyumba hiyo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Maja...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alimpotembelea nyumbani kwake kumpa pole ya kufiwa na Kaka yake Issa Juma Ngalapa aliyefariki alfajiri ya leo, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Uganda ukiong...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Uganda ukiongozwa na Waziri wa Nishati wa Uganda Balozi Ruth Nankabirwa mara baada ya kuwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni. Wengine ni Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki katika makabidhiano hayo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Mhe. Y...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambao umewasilishwa kwake na Waziri wa Nishati wa Uganda Balozi Ruth Nankabirwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Nishati wa Uganda ...
05/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Nishati wa Uganda Balozi Ruth Nankabirwa baada ya kuwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Salamu za Pongezi
04/11/2023

Salamu za Pongezi

Jummah Mubarak
03/11/2023

Jummah Mubarak

Imetimia miaka Mitatu tangu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kuingia Ma...
02/11/2023

Imetimia miaka Mitatu tangu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kuingia Madarakani kuiongoza Zanzibar ambapo amefanikiwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alizowaahidi Wazanzibari wakati wa kampeni kwa kuboresha miundombinu ya Elimu, Afya, Maji na Utalii.

Aidha kwa kipindi cha miaka mitatu Rais Dk. Mwinyi amefanikiwa kuboresha na kuimarisha miundombinu ya Barabara, Mawasiliano, Ujenzi wa Masoko ya Kisasa, Viwanda pamoja na kuwawezesha Wananchi kiuchumi.

Hongera Dk. Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu ya Uongozi wako ambapo Zanzibar imepiga hatua kwa kila sekta kwa Maendeleo.

TAMASHA LA KABILA LA WAMATENGO KUFANYIKA KILA MWAKANa Shamimu NyakiTamasha la Utamaduni wa kabila la Wamatengo Mkoani Ru...
31/10/2023

TAMASHA LA KABILA LA WAMATENGO KUFANYIKA KILA MWAKA

Na Shamimu Nyaki

Tamasha la Utamaduni wa kabila la Wamatengo Mkoani Ruvuma litafanyika kila mwaka ili kutangaza utamaduni wa kabila hilo na Mkoa wa Ruvuma ndani na nje ya Tanzania.

Hayo yameelezwa Oktoba 30, 2023 na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akifungua tamasha hilo katika kijiji cha Makumbusho Mtama Wilayani Mbinga.

"Matamasha haya yanatangaza Utamaduni, Mila na Desturi zetu watanzania, tamasha hili lifanyike kila mwaka ili kukumbushana maisha yetu ya asili, na nitoe rai kwa makabila mengine kuwa na Matamasha k**a haya katika maeneo yao" amesema Mhe. Ndumbaro.

Tamasha hilo lilishereheshwa na burudani mbalimbali na kupambwa na maonesho ya tamaduni zenye asili ya kabila hilo.

Kwa kipindi cha miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mw...
30/10/2023

Kwa kipindi cha miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, sekta ya Uwekezaji imefanikiwa kusajili miradi 15 ya Uwekezaji katika visiwa vidogo vidogo yenye thamani ya mtaji wa Dola za Kimarekani 384,500,000.

Uamuzi wa Rais Dk. Mwinyi kuvikodisha visiwa hivyo kwa wawekezaji ni pamoja kuviendeleza ili kuinua uchumi Zanzibar ambapo kwa muda mrefu vilikuwa havitumiki.

📍Kisiwa cha Pamunda, Unguja

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari M...
29/10/2023

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye Oktoba 28, 20203 Jijini Dar es Salaam wameshiriki mchezo wa Gofu katika viwanja vya Lugalo.

Kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mw...
29/10/2023

Kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanikiwa kujenga Matangi 10 ya maji Unguja na Pemba ambayo yanatarajiwa kumaliza kero za maji safi na salama.

Kukamilika kwa ujenzi wa matangi ya Kwarara Kidutani yenye ujazo wa Lita milioni 43.5 yatahudumia wakaazi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

📍KWARARA KIDUTANI

RAIS DK. MWINYI AWATEMBELEA WAZEERais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi baada...
27/10/2023

RAIS DK. MWINYI AWATEMBELEA WAZEE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi baada ya sala ya Ijumaa amewatembelea Wazee na kuwajulia hali akiwemo Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Mstaafu, Mwalimu Sheikh Machano Makame Machano nyumbani kwake Mwembe Makumbi Wilaya ya Mjini , Mkoa wa Mjini Magharibi .

Pia alimtembelea Mzee Alawi Suleiman Khatib nyumbani kwake Makadara, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

🗓️27 Oktoba 2023

📍Mkoa wa Mjini Magharibi.

Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais wa Zanzinar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, Wizara ya ...
27/10/2023

Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais wa Zanzinar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imefanikiwa kuimarisha mazingira ya Skuli kwa kujenga madarasa 2,273 na hivyo kupunguza changamoto ya uhaba wa madarasa kutoka madarasa 5600 hadi kufikia 3327.

MHE. NDUMBARO APIGIA “DEBE” FILAMU ZA TANZANIA KIMATAIFANa Brown JonasWaziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Dam...
27/10/2023

MHE. NDUMBARO APIGIA “DEBE” FILAMU ZA TANZANIA KIMATAIFA

Na Brown Jonas

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 27, 2023 Jijini Dar es Salaam ameungana na Raia wa Uturuki wanaoishi hapa nchini kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwa taifa hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, Tanzania itendelea kushirikiana na nchi hiyo katika maeneo mbalimbali hususani kuendeleza Sanaa ya Tanzania hasa filamu ili ziweze kufika kiwango cha juu.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Mabalozi Pamoja na viongozi wengine wa kidiplomasia.

42 Bagamoyo Festival.
26/10/2023

42 Bagamoyo Festival.

📍Lusaka Zambia🇿🇲HER EXCELLENCY SAMIA SULUHU HASSAN, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAADDRESSING THE NATIONAL ...
25/10/2023

📍Lusaka Zambia🇿🇲

HER EXCELLENCY SAMIA SULUHU HASSAN, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

ADDRESSING THE NATIONAL ASSEMBLY OF ZAMBIA

📅 25 October, 2023.

Moja ya Mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la...
25/10/2023

Moja ya Mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ni kurejesha mchezo wa ngumi za kulipwa ambao ulipigwa marufuku Zanzibar kwa zaidi ya miaka 50.

Uamuzi wa Rais Dk. Mwinyi kuruhusu mchezo wa ngumi za kulipwa ni kufungua fursa za ajira kwa vijana pamoja na kutangaza utalii wa Zanzibar.

“Sina budi kumshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kurejesha Ndondi, tumepata ajira za uhakika ambapo hapo awali tulikuwa tunacheza kwa kujificha” amesema Miraji Iddi Juma (38) Mkaazi Kianga, Unguja.

WAZIRI MKUU AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI WAZINGATIE SHERIA- Asisitiza kuwa ukiwa dereva wa Serikali haimaanishi uko juu ...
24/10/2023

WAZIRI MKUU AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI WAZINGATIE SHERIA

- Asisitiza kuwa ukiwa dereva wa Serikali haimaanishi uko juu ya sheria

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka madereva wa Serikali kuwa mfano wa kuzingatia sheria zote kwa sababu kuendesha gari ya Serikali haimaanishi wamepewa rungu la kuvunja sheria bali wanapaswa kuwa mfano wa kuzizingatia hasa zile za usalama barabarani.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, “ukiwa dereva wa Serikali haimaanishi kuwa uko juu ya sheria bali kila dereva anatakiwa kuwa mfano wa kuzingatia sheria zote. Aidha, madereva wa vyombo visivyo vya Serikali wanapaswa kujifunza kutoka kwenu madereva wa Serikali.”

Pia, Waziri Mkuu amesema madereva hao wanapaswa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya taaluma ya madereva wa Serikali ambayo yanawataka madereva hao kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani. “Madereva wa Serikali hakikisheni mnakuwa kioo cha jamii.”

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 24, 2023) alipofungua Kongamano la Chama cha Madereva wa Serikali, katika Ukumbi wa Hoteli ya Morena mkoani Morogoro. Kongamano hilo limebeba kauli mbiu isemayo; “Dereva wa Serikali bila ajali inawezekana. Kazi iendelee”

Akizungumzia kauli mbiu hiyo, Waziri Mkuu amesema ni kweli inawezekana kuendesha magari ya Serikali bila kusababisha ajali iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake kwa kuzingatia sheria zilizopo, hivyo amewasisitiza madereva hao wahakikishe wanafuata sheria.

“Ninawapongeza sana kwa kuwa kaulimbiu hii pia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020/2025, Ibara ya 105 (K) ambayo inailekeza Serikali kuliwezesha Jeshi la Polisi pamoja na mambo mengine kuendelea na jukumu la kudhibiti ajali za barabarani.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeshafanya jitihada kubwa katika kutatua kero za watumishi wa kada hiyo ya udereva na bado inaendelea kuzitatua changamoto zinazojitokeza kwa kushirikiana na Chama chao.

Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara zenye dhamana husika bila kuathiri shughuli na majukumu yake ya kila siku ya kiutumishi, imebadilisha muundo wa ajira na kuondoa kigezo cha cheti cha ufundi (trade test) katika kuwapandisha madaraja na ngazi za mshahara kwa mwaka wa fedha uliopita.

Waziri Mkuu amewahakikishia madereva hao kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya tisa inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi zinaendelea kutekeleza azma yake ya kulinda maslahi ya madereva wa Serikali pamoja na kuyafanyia kazi maombi na ushauri utakaotolewa.

Naye, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewahakikishia madereva hao kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kupitia Chama Cha Madereva wa Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuongeza tija katika utendaji kazi Serikalini.

Pia, Waziri Bashungwa amesema suala la stahiki za madereva linapewa msisitizo mkubwa na Serikali. K**a ilivyoelekezwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, waajiri wote wahahakikishe kuwa madereva wote wanapatiwa barua za kuthibitishwa hususan kwa wale ambao bado hawajapewa barua hizo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongoz...
24/10/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma hatua ambayo imechangia kuleta maendeleo kwa haraka.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameongeza maslahi ya wafanyakazi Serikali kwa kuwaongezea kima cha mishahara.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongoz...
24/10/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma hatua ambayo imechangia kuleta maendeleo kwa haraka.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameongeza maslahi ya wafanyakazi Serikali kwa kuwaongezea kima cha mishahara.

ZIARA YA KITAIFA YA RAIS SAMIA JAMHURI YA ZAMBIA KWA MWALIKO WA RAIS MHE. HAKAINDE HICHILEMA
23/10/2023

ZIARA YA KITAIFA YA RAIS SAMIA JAMHURI YA ZAMBIA KWA MWALIKO WA RAIS MHE. HAKAINDE HICHILEMA

WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA WATUMIE VIZURI FURSA ZA UWEKEZAJI- Awataka watoe ushirikiano kwa wawekezaji wanaoonesha n...
22/10/2023

WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA WATUMIE VIZURI FURSA ZA UWEKEZAJI

- Awataka watoe ushirikiano kwa wawekezaji wanaoonesha nia ya kuwekeza nchini.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania walioshiriki katika Jukwaa la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia wahakikishe wanatumia vizuri fursa walizozipata kutoka kwenye jukwaa hilo, ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji na wafanyabiashara walioonesha nia ya kuja kuwekeza nchini.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeondoa tozo na urasimu uliokuwepo awali kwa lengo la kurahisisha shughuli za biashara na uwekezaji nchini.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi wahakikishe Taifa linanufaika kwa kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vya uwekezaji pamoja na kuwashawishi wawekezaji kutoka katika nchi wanazoishi waje kuwekeza Tanzania.

Ameyasema hayo Ijumaa, Oktoba 20, 2023 katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kushirikiana na Benki ya NMB kwa lengo la kuwatambua wafadhili na washiriki wa Jukwaa la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia.

Waziri Mkuu ambaye yuko Italia akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023, Rome nchini Italia, aliwasisitiza Watanzania waheshimu sheria za nchi husika.

Mheshimiwa Majaliwa alisema kupitia jukwaa hilo wafanyabiashara na wawekezaji wengi kutoka nchini Italia wameonesha nia ya kuja Tanzania kwa ajili ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo, hivyo amewataka viongozi na watendaji wa wizara zinazohusika na masuala ya uwekezaji kuchangamkia fursa hiyo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wafugaji nchini wakubali kubadilika na wafuge kwa kutumia teknolijia ya kisasa ili waweze kujinufaisha zaidi na shughuli hiyo. “Tubadilike tupate manufaa zaidi, ufugaji ni uchumi, ufugaji ni maisha na ufugaji ni kazi, hivyo tubadili mfumo wa ufugaji wetu kwa ajili ya kujiongezea kipato zaidi.”

WAZIRI NDUMBARO ATETA NA WAANDAJI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI AFLNa Shamimu NyakiWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. D...
21/10/2023

WAZIRI NDUMBARO ATETA NA WAANDAJI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI AFL

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Black Engineering kutoka nchini Italia Massimo Fogliati ambao ndio walioandaa sherehe za Ufunguzi wa African Football League Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamefanyika Oktoba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Waziri amewashukuru kwa kufanikisha ufunguzi huo, pamoja na kutoa ajira na fursa kwa watanzania ambao walihusika katika Ufunguzi huo.

Mhe. Ndumbaro amewakaribisha wawekezaji hao kufungua tawi hapa nchini kwakua tayari wana matawi Saud Arabia na Dubai.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji huyo, Bw. Massimo amepokea pongezi hizo na kushukuru Serikali na Wadau wote wa michezo kwa ushirikiano, ambapo ameahidi kurudi nchini kwa ajili ya kutafuta fursa zaidi na uwekezaji.

Makamu Mwenyeki wa K**ati ya Kudumu ya Bunge, Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Florent Laurent Kyombo (katikati) akiwa kat...
21/10/2023

Makamu Mwenyeki wa K**ati ya Kudumu ya Bunge, Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Florent Laurent Kyombo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa K**ati hiyo Mhe. Salum Mohamed Shaaf (Kulia) na Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) kabla ya kuingia katika Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Oktoba 20, 2023 Arusha.

WAZIRI NDUMBARO ASHUHUDIA TANZANIA IKIICHAPA BENIN MPIRA WA KIKAPUWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas ...
20/10/2023

WAZIRI NDUMBARO ASHUHUDIA TANZANIA IKIICHAPA BENIN MPIRA WA KIKAPU

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshuhudia mchezo wa Ligi ya Kikapu kwa vilabu vya Afrika Kundi C, ambapo Timu ya Pazi kutoka Tanzania imeibuka na ushindi wa Vikapu 78 dhidi ya 65 vya Timu ya Elan Cotton ya nchini Benin.

Mchezo huo umechezwa Oktoba 19, 2023 katika viwanja vya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika Jijini Dar es Salam.

Kundi C linaundwa pia na timu ya Dymano kutoka Burundi na KPA kutoka Kenya.

Address

Kaunda Street
Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari za Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share



You may also like