Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi atawasili nchini Julai 01, 2024 kwa ziara ya Kitaifa hadi julai 04, 2024 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Atakapowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Nyusi atapokelewa na viongozi waandamizi wa Serikali na mapokezi rasmi yatafanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam Julai 02, 2024.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba alisema pamoja na mambo mengine, Rais Nyusi atakuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam maarufu, Sabasaba siku ya tarehe 03 Julai, 2024.
Mhe. Waziri Makamba alieleza kuwa ziara hiyo ya Rais Nyusi nchini itakuwa ziara ya mwisho kama kiongozi wa nchi kutokana na kumaliza mihula miwili ya uongozi wake mwezi Oktoba 2024. Hivyo, ziara hiyo ataitumia kumuaga Rais Samia na Watanzania kwa ujumla.
Aidha, Waziri Makamba alisema Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Msumbiji kukabiliana na changamoto za kiusalama. Alitolea mfano wa Tanzania kuwa moja kati ya nchi 11 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zilizochangia vikosi vya kulinda amani nchini Msumbiji kufuatia mashambulizi ya vikundi vya kigaidi Kaskazini mwa nchi hiyo, hasa katika majimbo ya Cabo Delgado, Niassa na Nampula.
Rais Samia na Mgeni wake, Rais Nyusi watashiriki mazungumzo ya faragha na rasmi ambayo yanatarajiwa kujikita katika kukuza biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama. Viongozi hao pia watashuhudia uwekaji saini wa makubaliano mbalimbali ya ushirikiano katika maeneo ya ulinzi, elimu na afya kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Julai 02, 2024.
Rais Nyusi ataondoka nchini Julai 04, 2024 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aman Abeid Karume baada ya kumaliza ziara binafsi mjini Zanzibar.
Kampuni ya Magic Builders International Ltd, kama kawaida jana waliandaa Semina ya Mafundi Ujenzi Jijini Mwanza iliyofanyika katika ukumbi wa Kwa Tunza na Mafundi Takriban 15000 walihudhuria katika Semina hiyo. Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Angeline Mabula ndiye alikuwa Mgeni rasmi na alitoa vyeti vya semina hiyo kwa Mafundi pamoja na kugawa zawadi za Simu kwa Mafundi walijibu kwa ufasaha maswali ya Bidhaa zinazozalishwa na Magic Builders International Ltd na Pikiki kwa mafundi walioshida kwa kupakua coupon nyingi zaidi zinazopatikana kwenye kila mfuko wa whiteskim wallputty.
Mwanga kaskazini wananchi Wanamlilia Diwani Wao Wa Zamani @officialbabalevo
Katibu wa UWT @jokatemwegelo baada ya kukanyaga Ardhi ya nyumbani kwa mara ya kwanza Tangu ateuliewe.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda @baba_keagan ametuma Salamu kwa Mawaziri Leo alipokuwa akizungumza hii Leo baada ya Makabidhiano ya kijiti kutoka kwa Mwenezi aliepita.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda @baba_keagan amesema tangu ateuliwe kuna Watu wamehamaki wengi wao wakiwaza kuwa Makonda ataenda kulipa kisasi huku wengine wakiwataja baadhi ya Watu na kuwaambia ‘Utaona sasa usiyemtaka kaja’, ambapo Makonda amesema hajaja kulipa kisasi kwa yeyote.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam baada ya kupokelewa na Viongozi na Wanachama wa CCM, Makonda amesema “Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupitapita kwenye mitandao, nimesoma maoni ya baadhi ya Watu, wengi wanahamaki na wengi wana bashasha lakini wanaohamaki wengi wao wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi, nimeona na wengine wanaanza kuwataja Watu wengine kwamba ‘Utaona sasa usiyemtaka kaja’, naomba niseme Mimi sina kisasi kwa Mtu yoyote, na asiwepo Mtu yoyote yule akafikiri lengo langu ni kumkandamiza, au nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikiri wamenitenda mabaya”
“Mnaohisi kuna jambo halikuwa sawa Mimi naelewa Mungu aliwatumia kunisaidia kumjua Mungu zaidi, naamini Mungu aliwatumia ili kuniandaa kwa kazi kubwa zaidi msiwe na hofu, naomba ushirikiano na umoja wenu na wala Dkt. Samia hajaniteua kuja kuhangaika na mambo ya Makonda bali uenezi wa CCM na wala Dkt. Samia na Kamati Kuu haikukaa kwenye kikao kumtafuta Mtu wa kwenda kulipa kisasi, walimtafuta Mtu atakayeongeza nguvu katika kujenga imani ya Watanzania kwenye CCM”
Makonda alivyowasili Lumumba na Bodaboda
Nunu mfuko wa #WhiteSkimWallPutty kutoka @magic_builders_international na ujishindie kuanzia Shilingi 500-15000 za Kitanzania
Ukinunua mfuko wa White Skim Wall Putty ndani ya mfuko utakuta Vocha. Ikwangue kisha ingia kwenye uwanja wa meseji kwenye simu yako Andika neno SKIM Acha nafasi kisha andika namba zilizopo kwenye vocha yake kisha tuma kwenda namba 15320
White Skim Wall Putty ni Putty bora inayopatikana kwenye maduka yote ya ujenzi Tanzania
@officialbabalevo Amemuwakilisha Mke wake @salma_mdoli kwenye Dili la Ubalozi wa Duka la Mikoba la @munystylish_tz kwa sababu ya Ujauzito wake.
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ameendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuwafikia Wananchi katika huduma za Maji. Afya, Umeme, Elimu na Miundombinu katika Jimbo la MorogoroKusiniMashariki.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Gwata kijiji cha Gwata, amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kupeleka huduma muhimu kama ilivyoahidiwa na kwa kuanza Wananchi wameanza kunufaika kupitia ujenzi wa miradi ya maji , Elimu,Afya na Miundombinu. @babutale
Ali Kamwe na Privadinho wakitamba na Shombo baada ya Kupata Mualiko wa Ikula Kula chakula cha Jioni na Rais
YANGA WAALIKWA IKULU KULA CHAKULA NA RAIS BAADA YA MAPAMBANO
Burundi Traditional Dance 'Amazing'
Burundi Traditional Dance 'Amazing'
Babuu kijana alieuza Nyumba zake 2 na Kuacha kazi ili kwenda China na Kuanza Biashara
Babuu kijana alieuza Nyumba zake 2 na Kuacha kazi ili kwenda China na Kuanza Biashara
Manara Afunguka baada ya kulikosa Kombe
Neema mfanyabiasha alieachana na kazi yenye mshahara mkubwa na kuuza mtumba
Neema mfanyabiasha alieachana na kazi yenye mshahara mkubwa na kuuza mtumba
Nilianza na miaka 15/Nikiwa nafanya kazi zandani kwa Wahindi/Wateja wasumbufu napata
Nilianza na miaka 15/Nikiwa nafanya kazi zandani kwa Wahindi/Wateja wasumbufu napata
Malaika: Alianza na mtaji wa laki nne kwa sasa anamtaji wa milion 80
Malaika: Alianza na mtaji wa laki nne kwa sasa anamtaji wa milion 80
Asimulia alivyonusurika ajali ya Bas la #MAJINJA, 42 walipoteza Maisha
Asimulia alivyonusurika ajali ya Bas la #MAJINJA, 42 walipoteza Maisha