09/12/2024
ASANTE KWA TAFUU IMANI KAJULA 📌
Repost ..
Hongereni Gen C - Miaka 25 ya Mapinduzi !
Tuna haki na sababu kubwa sana ya kuwapongeza Clouds FM kwa kutimiza miaka 25
- Ni miaka 25 inayoonyesha dhamira huweza kuumba, na uthibitisho kuwa ukijitafuta unajipata.
- Miaka 25 ya maamuzi ya vijana walioamua kugeuza mtazamo hasi kuwa muziki ni uhuni hadi kufanya muziki kuwa ni ajira kwa vijana na kuwapa mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania.
- Miaka 25 iliyothibitisha kuwa muziki ni bidhaa ambayo inaweza kutangaza Nchi nje ya mipaka yake. Bongo Flavour na Artist wake ni Moja ya Identity ya Tanzania.
- Miaka 25 ya kuthibitisha kuwa Media ikitumika vizuti inakua mlango mkubwa sana wa fursa hususani kwa vijana.
- Miaka 25 iliyokipa kizazi chetu identity ya "Bongo Flavour" generation na kutupa hit songs nyingi zinazobaki kwenye maktaba yetu ya kichwani milele.
Kwangu Mimi Clouds wamekua sehemu ya maisha yangu. Ni furaha kuona marafiki wakipiga hatua na kuleta mapinduzi kwenye media na entertainment industry na kuwawezesha vijana wengi.
Hongereni sana kwa miaka 25 ya Mapinduzi makubwa, ahsanteni sana kwa support ya nguvu na mara zote kuwa tayari kuwa jukwaa la fursa na udiriki.
Cheers to Many Successful years ahead!