Vfm Radio Zanzibar

Vfm Radio Zanzibar KARIBU KWENYE UKURASA WETU RASMIN WA V FM RADIO ZANZIBAR 92.01 ULIPO TUPO

Waliohamia kwa hiari Msomera, mkoani Tanga wameanza kujionea fursa zilizopo katika kilimo na kulima mazao ya aina mbalim...
19/04/2023

Waliohamia kwa hiari Msomera, mkoani Tanga wameanza kujionea fursa zilizopo katika kilimo na kulima mazao ya aina mbalimbali , tofauti na hali ilivyokuwa awali ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro

Baadhi ya wakazi hao wanaoishi Msomera kwa sasa, wanasema awali walipokuwa ndani ya hifadhi hawakuruhusiwa kulima wala kufanya shughuli zozote katika eneo hilo, lakini walipofika Msomera, Novemba 2022 mambo ni tofauti.

Mkazi wa Msomera, Jackson Kipuyo anasema katika eneo hilo analima, kwani eneo hilo wana amani, uhuru na mipaka kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo cha umwagiliaji na cha kawaida kinachowapa mazao ya kutosha.
“Tumebadilika kimawazo na mtazamo maana hapa tunalima na kuvuna kule Ngorongoro haturuhusiwi kulima kwa sababu ya uhifadhi na kilimo hiki kimesaidia watoto kujua maana halisi ya mazao mbalimbali yanavyolimwa, kupandwa na kuvunwa na tumefurahi sana sana kuona mazao halisi shambani,” amesema.

Baadhi ya watoto wakizungumza na HabariLEO kwa kwanyakati tofauti, ambao ni Meshack Joshua na Theresia Ndemgei wamesema wakiwa Ngorongoro hawakuwa wakilima wala kujionea uhalisia wa mazao yanavyoandaliwa mashambani na kupandwa hadi kuvunwa, lakini sasa wamejionea.

“Tulipokuwa Ngorongoro hakujua hata kushika jembe au kulima kilimo cha umwagiliaji, lakini hapa Msomera tunalima kwa mikono yetu wenyewe na kujionea aina mbalimbali za mazao yanayovunwa ambayo hatukuwahi kuyaona awali,” amesema.

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema kuwa serikali imenunua magari 528 ya wagonjwa yat...
19/04/2023

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema kuwa serikali imenunua magari 528 ya wagonjwa yatakayogawiwa kwa halmashauri zote 184 nchini na kila halmashauri itapata magari mawili.

Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki amesema hayo bungeni Dodoma wakati akijibu hoja zilizotolewa na wabunge waliochangia katika hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Kairuki alisema awali serikali ilipanga kununua magari 407 lakini baadaye ikaamua kuongeza idadi hiyo hadi kufikia magari 528 kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Unicef, hivyo wameokoa magari zaidi ya 121 ambayo k**a wasingetumia mbinu waliyoitumia magari hayo yasingepatikana.

Alisema kila halmashauri itapata magari mawili ya kubebea wagonjwa na gari moja kwa ajili ya usimamizi na uratibu wa miradi ya afya katika halmashauri.

Kairuki alisema tangu Aprili 7, mwaka huu magari yameanza kuwasili nchini hususani bandarini na mengine yaliwasili Aprili 14 na mengine yataingia Aprili 21 na yaliyobaki yataendelea kuja hadi yote 528 yatimie.

“Mpaka sasa yapo katika ukomboaji magari 55 zikiwepo Landcruiser hardtop 30 na ambulance 25, kikubwa kuliko yote ni kwamba kila mmoja atapata kwa ajili ya kuhudumia wananchi wetu,” alisema Kairuki.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo ya kutambua noti halali kwa makundi maalumu wakiwamo wenye ulemavu.Akizungumz...
19/04/2023

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo ya kutambua noti halali kwa makundi maalumu wakiwamo wenye ulemavu.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Arusha, Meneja Msaidizi Sarafu BoT, Joyce Saidimu alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwawezesha kupata uelewa wa kutosha wa kujua alama za usalama kwenye sarafu.

Alisema elimu waliyowapa itawawezesha kugundua fedha halali kwani ni makundi ambayo yamekuwa yakisahaulika katika masuala ya kijamii.

“Sisi k**a BoT, ni utaratibu wetu kutoa mafunzo k**a hayo shuleni, sokoni na kwenye maeneo mbalimbali ya biashara, ila kwa awamu hii tumeamua kutoa elimu kwa watu wa makundi maalumu ili waweze kupata uelewa wa kutosha na kutambua noti halali,” alisema.

Aliongeza: “Mafunzo haya yatakuwa endelevu na tutakuwa tukiyatoa mara kwa mara ili waweze kupata uelewa wa kutosha juu ya masuala haya na kuepuka kushikishwa fedha bandia kwani tayari wana uelewa wa kutosha.”

Aidha, BoT imetoa mafunzo ya namna sahihi ya kutunza fedha kwa ajili ya matumizi yao huku akiwataka kuwa mabalozi wazuri wa kufundisha wenzao namna ya kutunza fedha.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Jamii na Viziwi (DCPO), Jafari Shabani alisema waliomba kupatiwa mafunzo hayo kwa watu wenye ulemavu kutokana na changamoto mbalimbali walizokuwa wakikabiliana nazo katika kutambua noti bandia na halali.

Alisema jumla ya watu wenye mahitaji maalumu 70 walipatiwa mafunzo hayo.

Jafari alisema watu hao wenye mahitaji maalumu walikuwa wakikabiliwa na changamoto hiyo na hata kusababisha wengi wao kupelekwa katika vyombo vya usalama wanapokutwa na noti bandia kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya utambuzi wa alama za usalama kwenye sarafu.

Kwa upande wake, mshiriki wa semina, Emmanuel Benjamin aliishukuru Benki Kuu kwa mafunzo hayo.

Alisema aliwahi kupewa noti bandia katika biashara yake ya kuendesha bajaji na sasa baada ya kupatiwa elimu, ataweza kuchukua tahadhari mapema.

Aliomba mafunzo hayo kuwa endelevu huku akiomba serikali kutoa mafunzo zaidi kwa watu wenye ulemavu kwani ni hatua ya kundi hili kushirikishwa na kuondoa dhana ya kubaguliwa.

Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (Chadema) na wenzake 18, itaendelea kusikilizwa M...
19/04/2023

Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (Chadema) na wenzake 18, itaendelea kusikilizwa Mei 17 na 18, 2023 baada ya kuahirishwa kwa kile kilichoelezwa kuwa Jaji anayeendesha kesi hiyo, Cyprian Mkeha, yuko kwenye majukumu mengine.

Kesi hiyo iliahirishwa jana katika Mahak**a Kuu Masjala Kuu na Msajili wa mahak**a hiyo, Veronika Mteta aliyetoa taarifa ya kutokuwepo jaji huyo.

Itakaporejea mahak**ani Mei 17, mawakili wa upande wa watoa maombi (Mdee na wenzake) wataendelea na maswali ya dodoso kwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema, Dk Lucy Mollel ambaye anahojiwa baada ya kumaliza kuhojiwa mjumbe wa kwanza, Profesa Azaveli Lwaitama.

Wabunge hao wa viti maalumu walifungua shauri kuomba mapitio ya kimahak**a wakipinga uamuzi wa kikao cha Baraza Kuu la Chadema wa kufukuzwa uanachama.

Awali, wakili wa wajibu maombi wa kwanza (Chadema), Peter Kibatala aliomba mahak**a iruhusu wabunge tisa kati ya 19 waliomo katika kesi hiyo waitwe mahak**ani kwa ajili ya mahojiano. Wabunge wanne walifanyiwa mahojiano kabla ya Kibatala kuwasilisha hoja ya kusitisha mahojiano.

Wabunge waliohojiwa ni Hawa Mwaifuga, Cecilia Pareso, Nusrat Hanje na Jesca Kishoa huku wengine akiwemo Halima Mdee, Esther Bulaya na Esther Matiko wakiachwa.

Baada ya Chadema kusitisha mahojiano, mawakili wa watoa maombi waliomba kuwahoji Profesa Lwaitama na Dk Mollel ambapo walimaliza kumhoji Profesa Lwaitama na wanatarajia kumhoji Dk Molel.

Katika shauri hilo, wabunge hao pamoja na mambo mengine, waliiomba mahak**a ipitie mchakato na uamuzi huo wa Chadema kuwafukuza uanachama, kisha itoe amri tatu.

Wabunge hao wanaomba mahak**a itengue mchakato na uamuzi wa kuwavua uanachama. Pia wanaomba iwalazimishe Chadema kuwapa haki ya kuwasikiliza.

Vilevile wanaomba mahak**a itoe amri ya zuio dhidi ya Spika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua hatua yoyote mpaka malalamiko yao yatakapotolewa uamuzi.

Wakazi wa Kijiji cha Nakapanya, Halmashauri ya Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, wamekumbushwa umuhimu wa kutumia vyandarua ...
19/04/2023

Wakazi wa Kijiji cha Nakapanya, Halmashauri ya Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, wamekumbushwa umuhimu wa kutumia vyandarua vyenye viuatilifu na kudumisha usafi wa mazingira kwenye maeneo wanayoishi kuepuka mazalia ya mbu wanaoeneza malaria.

Wito huo ulitolewa jana na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Abdallah Shaib Kaim, wakati akizindua ugawaji wa vyandarua kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito wilayani Tunduru.

Aliwataka wananchi kuachana na imani potofu kuwa vyandarua vyenye dawa ni hatari kwa afya zao na kuwahakikishia kwamba vimetolewa na serikali, ni salama na havina madhara kwa binadamu.

Kaim ameonya wakazi wa Wilaya ya Tunduru kutumia vyandarua hivyo kwa ajili ya bustani, kufugia mifugo na kuvulia samaki, badala yake watumie kujikinga na maambukizi ya malaria hasa usiku.

Alipongeza Wilaya ya Tunduru kwa jitihada inazofanya katika kutokomeza ugonjwa huo unaotajwa kuwa ni kati ya magonjwa hatari na yanayoongoza kupoteza maisha ya watu wengi nchini.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Tunduru, Chiza Marando alisema serikali kwa kushirikiana na wahisani Global Fund imetumia Sh 54,280,000 kununua na kusambaza vyandarua vyenye dawa.

Kwa mujibu wa Marando, kuanzia mwaka 2020 hadi Machi mwaka 2023, halmashauri hiyo imegawa zaidi ya vyandarua 176,747 kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito k**a mkakati wake wa kukabiliana kuenea kwa ugonjwa wa malaria.

Marando alisema mwaka 2020 waligawa vyandarua 51,409, mwaka 2021 vyandarua 60,792, mwaka 2022 vyandarua 59,847 na hadi kufikia Machi 30, mwaka huu wametoa vyandarua 4,699.

Alisema kutokana na jitihada na mikakati inayofanywa na halmashauri hiyo, takwimu za wagonjwa wa malaria zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka kutoka wagonjwa 102,628 mwaka 2020/2021 sawa na asilimia 44 ya wagonjwa 228,991 waliopimwa ugonjwa huo hadi wagonjwa 81,248 mwaka 2021/2022.

JeshiI la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu 10 wakiwemo wazee wa kimila maarufu k**a Ndagashida na viongozi wa ul...
19/04/2023

JeshiI la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu 10 wakiwemo wazee wa kimila maarufu k**a Ndagashida na viongozi wa ulinzi wa jadi maarufu sungusungu kwa tuhuma za kuchukua mifugo kwenye familia za watuhumiwa wa kesi ya mauaji na kugawana.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mkoani humo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Simiyu, Blasious Chatanda amesema Februari 2023 kulitokea tukio la mauaji ya mfanyabiashara, William Fumbuka (39) katika Kijiji cha Bukundi, wilayani Meatu.

Chanzo cha kifo chake kilibainika kuwa kulikuwepo na mgogoro wa umiliki wa ardhi inayokadiriwa kufikia ekari 2,500 ambayo ilielezwa kuwa Fumbuka alizitumia kuzikodisha.

Kamanda Chatanda alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo walifanikiwa kuwak**ata watuhumiwa sita na kuwafikisha katika Mahak**a ya Wilaya ya Meatu ndipo viongozi hao wakarudi na kuchukua mifugo katika familia hizo na kugawana kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

“Kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo katika familia hiyo, watuhumiwa walipanga mipango ya kumuua Fumbuka na walitekeleza tukio hilo na hadi sasa tayari watuhumiwa wa tukio hilo wako mikononi mwa Jeshi la Polisi tayari kwa taratibu za kuwafikisha mahak**ani zikiendelea,” alisema.

Mwili wa mkazi wa Usule ambaye ni dereva wa bajaji, Shaban Mangi (40) umekutwa umefukiwa katika shimo baada ya kudaiwa k...
19/04/2023

Mwili wa mkazi wa Usule ambaye ni dereva wa bajaji, Shaban Mangi (40) umekutwa umefukiwa katika shimo baada ya kudaiwa kuuawa na msaidizi wake kwa tuhuma za wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Richard Abwao alisema tukio hilo lilitokea Aprili 15, mwaka huu majira ya saa 9:00 alasiri katika Kitongoji na Kijiji cha Utusini, Kata ya Misha, Manispaa ya Tabora mkoani hapa.

Alisema mtuhumiwa ambaye jina lake limehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi alimpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha kifo chake.

Kamanda Abwao alisema Mangi aligundulika ameuawa kisha kufukiwa kwenye shimo na mtuhumiwa huyo huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Alisema mtuhumiwa alishirikiana na watu wengine ambao Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka.

Kamanda Abwao alisema mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu dereva wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mpenzi wake.

Mwili wa dereva huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete kwa ajili ya uchunguzi zaidi na mtuhumiwa amek**atwa na atafikishwa mahak**ani baada ya upelelezi kukamilika.

Serikali imesema itatoa vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa  kwenye mwaka 2023/2024.Katika mwaka ...
19/04/2023

Serikali imesema itatoa vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa kwenye mwaka 2023/2024.

Katika mwaka 2022/2023, Serikali ilitoa vibali vya ajira mpya 30,000 na vibali vya ajira mbadala 7,721 kwa waajiri kutoka katika taasisi mbalimbali vimetolewa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Aprili 19, 2023 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.
“Itashughulikia vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa katika Ik**a,”amesema.

Amesema pia watahakiki na kuidhinisha madai ya malimbikizo ya mishahara na kusahihisha taarifa zinazohusiana na masuala ya kiutumishi na mishahara ya watumishi kwa taasisi 433.

Aidha watakagua orodha ya malipo ya mshahara katika taasisi 150.

Katika mwaka 2023/2024, ofisi hiyo imeliomba Bunge kuwaidhinishia Sh1 trilioni kwa ajili ya mafungu yake sita ya bajeti.

Mafungu hayo ni Ofisi ya Rais Ikulu, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Sekretarieti ya katika Utumishi wa Umma.

Mafungu mengine ni Tume ya Utumishi wa Umma na idara ndogo ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawatafuta sungusungu zaidi ya 30 waliohusika kumcharaza viboko hadharani na kumsabab...
19/04/2023

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawatafuta sungusungu zaidi ya 30 waliohusika kumcharaza viboko hadharani na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini, Manka Mushi (26) mkazi wa Kijiji cha Ikoma Kata ya Itilima Halmashauri ya Kishapu kwa madai ya kuiba Sh420, 000 za mteja wake.

Akizungumzia tukio hilo lilitokea Aprili 14, 2023 na kumsababisha binti huyo kulazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Janeth Magomi amesema baada ya sungusungu hao wa jeshi hilo la jadi kufanya tukio hilo kwenye uwanja uliopo katika kijiji hicho walikimbia.

Akisimulia mkasa uliomkuta, Manka aliyekuwa akifanya kazi baa na nyumba ya kulala wageni kijijini humo amesema ilikuwa Saa sita usiku ambapo mteja aliyefahamika kwa jina la Julius Tarimo aliagiza kupelekewa shuka, baada ya kumpelekea ghafla alimkaba koo akimtaka kurudisha Sh420, 000 alizohisi binti huyo kachukua.

Manka amesema alikataa kuhusika na wizi huo na kupiga kelele za kuomba msaada kisha Julius kumtishia kuwa atamtambua baada ya binti huyo kumkataa kimapenzi na baadaye alifanikiwa kutoka ndani ya chumba hicho.

“Kufuatia hatua hiyo niliambiwa na k**anda wa sungusungu twende uwanjani na baada ya kufika nilikuwa mwanamke pekee yangu nikaambiwa ni lale chini katikati ya wanaume zaidi ya 30 ukaletwa mzigo wa fimbo wakaanza kunicharaza viboko kwa zamu nikijaribu kuinuka wengine wanapiga mgongoni na kichwani,” amesema Manka

Amesema aliwapa namba ya mama yake mzazi ambaye anaishi jijini Arusha, walimpigia na kuzungumza naye kisha kumtaka atume hela lakini aliwaomba wampeleke polisi na baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya walimpeleka ofisi ya Kata kutoa maelezo hakupokelewa.

Mkazi wa Kitongoji cha Utusini Kata ya Misha mkoani Tabora, Benedicto Modest (40) ameuawa kisha mwili wake kufukiwa kwen...
19/04/2023

Mkazi wa Kitongoji cha Utusini Kata ya Misha mkoani Tabora, Benedicto Modest (40) ameuawa kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema Benedicto ambaye alikuwa dereva bajaji alipigwa na kitu kizito kichwani na kisha kufukiwa kwenye shimo na msaidizi wake aliyekuwa akishirikiana naye kwenye kazi hiyo.

Amesema chanzo cha mauaji hayo yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita ni wivu wa mapenzi akidai mtuhumiwa alikuwa anamuhisi mwenzake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake.

Abwao amesema msaidizi huyo aliwahi kumuonya bosi wake mara kadhaa pasipo mafanikio na ndipo alipoamua kujichukulia sheria mkononi kwa kumuua na kisha kumfukia shimoni.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete kwaajili ya uchunguzi,”amesema

Abwao amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo atafikishwa Mahak**ani baada ya upelelezi kukamilika.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashikilia watu 21 mkoani humo kwa tuhuma za kuiba miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora (Tuwasa).

Abwao amesema watu hao wamek**atwa kutokana na msako unaofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na watumishi wa Tuwasa, halmashauri na vyombo vingine vya usalama.

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha amekemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea nchini na kuomba waumini wa din...
19/04/2023

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha amekemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea nchini na kuomba waumini wa dini ya Kiislamu kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Njalambaha ameyasema hayo usiku wa juzi Jumatatu Aprili 17, 2023 wakati wa futari iliyoandaliwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia Trust iliyohusisha waumini wa dini ya Kiislamu, viongozi wa Serikali na wadau zaidi ya 1,000 walioshiriki.

“Vitendo viovu vya utatili wa kijinsia, ulawiti, na watu kujinyonga vinatokana na jamii kukosa mafundisho ya Mungu na kwenda kinyume umefika wakati viongozi wa dini kutoa elimu ili waweze kurejesha kwenya imani za dini na kujua vitabu vinasema nini katika kumcha Mungu,” amesema.

Ameshukuru Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwa kuwakusanya waumini wa dini hiyo kupitia taasisi yake jijini humo ikiwa ni mara ya saba mfululizo.

Akizungumza kwa niaba ya Dk Tulia, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amesema k**a viongozi wa Serikali wataendelea kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu katika mfungo wa kuelekea sikukuu ya Eid el Fitr.

Mahak**a ya Mwanzo Kariakoo imemuhukumu, Pastory Meza (25) kifungo cha miezi 10 jela baada ya kukiri kutenda makosa ya k...
19/04/2023

Mahak**a ya Mwanzo Kariakoo imemuhukumu, Pastory Meza (25) kifungo cha miezi 10 jela baada ya kukiri kutenda makosa ya kuvunja nyumba na kuiba vitu vyenye thamani ya Sh790, 000 mali ya Rukia Magere.

Hukumu hiyo imesomwa leo Aprili 18, 2023 na Hakimu, Gladness Njau, akisema pia msh*takiwa alikutwa na baadhi ya vitu alivyoiba ikiwemo televisheni, redio pamoja na pasi.

Njau amesema kwa kuwa mahak**a hiyo imemtia hatiani hivyo inamuhukumu kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuvunja na miezi minne kwa kosa la wizi.

"Adhabu hizo zitakwenda tofauti na mshtakiwa anaweza kukata rufaa k**a hajaridhika na hukumu," amesema Njau.

Awali akisoma mash*taka mahak**ani hapo Karani, Linda Kivaju alidai mahak**ani hapo kuwa April 5, 2023 nyuma ya ukuta wa shule ya sekondari ya Azania iliyopo Upanga mshtakiwa huyo alivunja mlango wa nyumba ya, Rukia Magere na kuingia ndani.

Maafisa Lishe wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wameanza kupewa mafunzo ya jinsi ya uandaaji pamoja na namna ya ulaji sah...
19/04/2023

Maafisa Lishe wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wameanza kupewa mafunzo ya jinsi ya uandaaji pamoja na namna ya ulaji sahihi wa chakula, ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya lishe bora ni mtaji.

Akifungua mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku nne mkoani humo leo Aprili 18, 2023 Magret Natai Ofisa Kilimo Mkuu na mratibu wa masuala ya lishe wa Wizara ya kilimo, amesema mafunzo hayo wanayotoa yatawasaidia maofisa lishe kuutumia mwongozo kuihamasisha jamii juu ya ulaji unaofaa.

Natai amesema kulingana na mafunzo hayo ya ulaji, makundi yote katika jamii k**a wamama wajawazito, watoto, wazee na watu wa rika zote watakuwa na watatambua jinsi ya kuaandaa pamoja na namna sahihi ya ulaji chakula.

"Baada ya mafunzo jamii kupitia kwa maafisa lishe ambao ndio watekelezaji wa mradi itaanza kuelewa juu ya uandaaji sahihi pamoja na ulaji wa chakula unaofaa," amesema Natai.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Maafisa Lishe kutoka Mikoa sita ya nyanda za juu kusini ambayo ni Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Katavi na Ruvuma.

Akizungumza na Mwananchi Ofisa Lishe wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) nchini Tanzania, Stella Kimambo amesema watatumia mwongozo wa chakula na utafiti utakaofanywa juu ya usalama wa chakula ikiwa ni mikakati ya kufikisha elimu kwa jamii.

Serikali imetangaza kupeleka magari ya kubebea wagonjwa mawili na gari moja la uendeshaji kwa kila Halmashauri nchini na...
19/04/2023

Serikali imetangaza kupeleka magari ya kubebea wagonjwa mawili na gari moja la uendeshaji kwa kila Halmashauri nchini na tayari baadhi ya magari yameshashuka bandarini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Angela Kairuki leo Jumanne April 18, 2023 wakati akijibu Hoja za wabunge kwenye maombi ya fedha kwa Wizara yake.

Kairuki amesema magari 528 yameagizwa na yanaingia kwa awamu ambapo baadhi yameshafika kazi iliyopo ni kuyakomboa tayari kwa kuanza kuyasambaza kwenye maeneo mbalimbali.

Waziri amesema idadi ya magari hayo yamefikiwa kutokana na namna ambayo waliitumia Tamisemi kwani awali walikuwa na bajeti ya kuagiza magari 407 kabla ya kutumia alichokiita namna wakaongezewa magari 121.

“Hivi ninavyozungumza kila siku napiga simu, hata juzi magari mengine yaliingia nchini na mengine yako njiani yanaletwa, niwahakikishe wabunge kwamba kila halmashauri inapata mgao wa magari mawili ya wagonjwa na gari moja la uendeshaji mapema iwezekanavyo,” amesema Kairuki.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, tayari magari 25 ya kubebea wagonjwa yameshalipia gharama zilizotakiwa na sasa yanapelekwa kwenye maeneo husika.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Butiama mkoani Mara, Ni**od Mkono amefariki dunia akiwa nchini Marekani alikokuwa akitibiwa tan...
19/04/2023

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Butiama mkoani Mara, Ni**od Mkono amefariki dunia akiwa nchini Marekani alikokuwa akitibiwa tangu mwaka 2018.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Aprili 18, mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema kimetokea Florida nchini Marekani.

“Taarifa ni za kweli, hata mimi nimezungumza na binti yake na mkewe wamesema kuwa amefariki leo (jana) saa za aubuhi huko Amerika. Alikuwa anatibiwa nchini Marekani katika jimbo la Florida miaka minne iliyopita na sasa unaingia mwaka wa tano,” amesema.

Amesema Mkono alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

“Nimeongea na ndugu kule wanasema mwili utaletwa kuzikwa Tanzania, japo utachelewa,” amesema.

Mkono, aliyezaliwa Agosti 18, 1948, Busegwe Mkoani Mara alikuwa mwanasheria na mwanasiasa maarufu.

Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye maarufu Namba tatu amesema kuwa chama hicho kimepoteza kada mtiifu na mpenda maendeleo wa kweli.

Serikali ya Afrika Kusini imesema ilitumia kiasi cha Sh175 milioni (R1.4 milioni) ili kukodi ndege kwa ajili ya maafisa ...
19/04/2023

Serikali ya Afrika Kusini imesema ilitumia kiasi cha Sh175 milioni (R1.4 milioni) ili kukodi ndege kwa ajili ya maafisa kumrejesha Thabo Bester na mpenzi wake Dk Nandipha Magudumana waliok**atwa jijini Arusha Aprili 7, mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi ameiambia Kamati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwamba walilazimika kufikia uamuzi huo sababu hawakuwa na ndege.

Motsoaledi amesema, maofisa 14 waliokuwa wanahitajika kwa operesheni hiyo walilazimika kusafiri kibiashara kwa sababu Idara ya Mambo ya Ndani haina ndege yake.

Ameongeza kuwa kwa bei hiyo ndiyo ilikuwa chaguo nafuu zaidi kwa wao na vilevile walilazimika kukodi mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Arusha, kwenda na kurudi.

Ikumbukwe Thabo Bester na mpenzi wake Dk Nandipha Magudumana walik**atwa Aprili 7 na Polisi wa Tanzania kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini na Jeshi la Polisi la kimataifa (Interpol).

Bester ni mfungwa aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji na mauaji, alikuwa akitafutwa baada ya kutoroka huko Bloemfontein Mei 2022 ambapo awali aliaminika alijiua kwa kujichoma moto.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja sababu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TT...
19/04/2023

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja sababu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupata hati chafu mfululizo kuwa ni urithi wa matatizo ya hesabu za kifedha yaliyoanza wakiwa na mbia wao kabla Serikali haijarudishiwa umiliki wa shirika hilo.

Nape alisema hayo jana jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika wilaya 23 nchini, ikiwa ni takribani wiki moja imepita tangu Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 kuwasilishwa bungeni na kuonyesha dosari kadhaa kwa TTCL.

Miongoni mwa kasoro alizozibaini CAG, Charles Kichere ni TTCL lilikuwa na madeni ya Sh21 bilioni ambayo uongozi haukuweza kutambua wadaiwa husika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, TTCL ni kati ya mashirika yaliyo na deni kubwa kuliko mtaji walionao, kwani ripoti ilieleza shirika lina jumla ya deni la Sh349.9 bilioni huku likiwa na mtaji wa Sh227.8.

Serikali imesema itaanza kutoa chanjo ya Marburg kwa majaribio endapo usalama wa chanjo hiyo utathibitishwa na wataalamu...
19/04/2023

Serikali imesema itaanza kutoa chanjo ya Marburg kwa majaribio endapo usalama wa chanjo hiyo utathibitishwa na wataalamu wa ndani.

Majaribio hayo ni wito wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kutaka majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo yafanyike hapa nchini.

Wito huo umetolewa ikiwa mwezi mmoja tangu ugonjwa huo ulipuke katika Mkoa wa Kagera na kuua watu watano na wengine kadhaa kulazwa huku wengine wakiwekwa karantini kuzia usisambae.

“Bado hakuna chanjo ya Marburg, lakini ipo inayofanyiwa majaribio, tumepata ombi kutoka WHO wakituomba turidhie majaribio ya chanjo ya Maburg, hili nimepeleka kwa wataalamu wanishauri tukubali au tusikubali.

“Jambo la kusisitiza pale ambapo chanjo imethibitishwa rasmi na WHO na k**ati yetu itaona ni salama, Tanzania si kisiwa tutaikubali,” alisema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam katika hafla ya kupokea msaada wa majokofu ya kuhifadhi chanjo, vifaa vya mnyororo wa baridi na maboresho ya majengo mbalimbali, iliyotolewa na Taasisi ya Clinton Health Access Innitiative ya Marekani (CHAI), Kampuni ya Vodacom pamoja na Serikali ya Japan.

Serikali imesema hakuna Mtanzania aliyezurika katika mapigano yanayoendelea nchini Sudani.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushi...
19/04/2023

Serikali imesema hakuna Mtanzania aliyezurika katika mapigano yanayoendelea nchini Sudani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax ameliambia Bunge leo Jumatano April 19, 2023 wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu mapigano nchini Sudan.

Mapigano yalizuka mwishoni mwa wiki iliyopita nchini humo na hadi leo Dk Tax amesema yameshasababisha vifo vya watu 185 na majeruhi zaidi ya 1000 ingawa kwa sasa yamesimama kwa muda wa saa 24.

Chanzo cha mapigano hayo ambayo yalianzia mji mkuu wa Khartoum, ni vikosi vya jeshi chini ya utawala wa Jenerali Abdul Fattah al-Burhan ambaye sasa ni Rais na wanachama wa kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces (RSF).

“Mapigano hayo yamerudisha nyuma jitihada zinazoendelea kutafuta amani, Tanzania inaunga mkono tamko la Baraza la Amani la Umoja wa Afrika kwenye lililotolewa kwenye mkutano wa April 16, 2023 na inalaani mapigano hayo ikitaka pande mbili zinazofadhiana kusitisha mapigano,” amesema Dk Tax.

Waziri amesema Serikali inafanya mawasiliano ya mara kwa mara na ubalozi wake ili kujua hali za Watanzania 210 wanaoishi nchini humo ambao kati yao 171 ni wanafunzi na wengine ni maofisa wa ubalozi na raia wengine.

“Tunampongeza na kumshukuru Balozi wetu nchini Sudan, Silima Kombo Haji kwa kuendelea kufuatilia hali za Watanzania lakini Serikali inawahakikishia kuwa inachukua hatua stahiki za kuwarejesha ikibidi,” amesema.

Kwa mujibu wa Waziri, kusitishwa kwa mapigano hayo kwa muda wa saa 24 kuanzia jana saa kumi jioni, ni kutoa fursa kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu lakini akasema upo uwezekano wa kusitisha na mapigano na kuruhusu mazungumzo ya njia kwa amani.

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo ameiibua ufisadi mwingine katika Jiji la Arusha akisema anajitoa ‘kafara’ kwa...
19/04/2023

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo ameiibua ufisadi mwingine katika Jiji la Arusha akisema anajitoa ‘kafara’ kwa ajili ya wananchi. lakini kwa vyovyote ni lazima aseme namna fedha zinavyotafunwa.

Gambo amesema Jiji la Arusha kuna changamoto na ubadhirifu wa fedha za umma mkubwa ambao unahitaji kufanyiwa uchunguzi maalumu kwa sababu hali ni mbaya.

Mkuu huyo wa mkoa wa zamani wa Arusha aliibua tuhuma hizo jana bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ya mwaka wa fedha 2023/24.

Alitolea mfano ujenzi wa jengo la utawala katika la ghorofa sita ambalo viongozi wa halmashauri walimpa mjenzi rafiki yao bila kutangaza zabuni, kila wakati kumekuwa na ongezeko la fedha ambazo haijulikani zinaliwa na wajanja.

“Fedha zilitengwa Sh199 milioni, lakini kuna manunuzi ya Sh132 milioni ya vifaa ambavyo havijafika eneo la ujenzi, hali ambayo ni mbaya na sura ya wizi. Pia kuna Sh17 milioni za ununuzi wa nondo, nazo zimeliwa,” alisema Gambo.

Alisema uzembe wa wataalamu umesababisha Sh21 milioni kwa malipo ya ziada kwa mjenzi huku kukiwa na risiti za kughushi za mashine za kilelekroniki ambazo walizichukua Hoteli ya Arusha zenye thamani ya Sh30 milioni.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Abdallah Ulega amesema wizara  imeanzisha vituo atamizi vya kuwafundisha vijana ufugaji wa k...
19/04/2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara imeanzisha vituo atamizi vya kuwafundisha vijana ufugaji wa kisasa wa mifugo na samaki lengo likiwa ni kujibu changamoto ya ajira kwa vijana. Waziri ameyasema hayo katika Kongamano la Tisa la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu maswala ya sera linalofanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2023.
“Tunamshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuturidhia kuanzisha programu hii kwa ajili ya kuandaa vijana kufanya ufugaji wa kibiashara ambapo kwa mwaka huu tumeanzisha vituo atamizi nane vya kuwafundisha vijana ufugaji kwa tija”, alisema
Amesema kila mwaka takribani vijana 1600 wanahitimu ngazi mbalimbali za elimu katika vyuo vya mifugo na kati ya hao 150 tu ndio hupata nafasi katika mfumo rasmi wa ajira hivyo lengo la ubunifu huu tulioufanya ni kuwezesha vijana wanaobaki kujiajiri kupitia unenepeshaji na uuzji wa mifugo yake ndani nan je ya nchi.
“Mipango yetu katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 ni kuwa na vituo atamizi 30 ambavyo vitakuwa na vijana wasiopungua 30 na kutufanya kuwa na vijana 900 ambao watakuwa wamepata mafunzo hayo na kuweza kujiajiri wenyewe kupitia mitaji watakayokuwa wameipata wakati wa mafunzo hayo”,alifafanua
Kauli mbiu na dhima ya Kongamano hilo ni “Ushindani wa Tanzania Katika Soko Huru Barani Afrika (AfCFTA): Changamoto na Fursa Katika Sekta ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi.

Jamii imeshauriwa kutumia mlo kamili ili kuepuka maradhi yasioambukiza ambayo yameshika kasi katika jamii. Afisa kutoka ...
19/04/2023

Jamii imeshauriwa kutumia mlo kamili ili kuepuka maradhi yasioambukiza ambayo yameshika kasi katika jamii. Afisa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Hafidh Abdurahman Seif ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa wagonjwa wa maradhi yasioambukiza katika hafla ya wa utoaji wa huduma za Afya kwa ngazi ya jamii Koani Wilaya ya Kati Unguja.

Ameeleza maradhi ya kuambikiza yamekua yakiongezeka kwa kasi zaidi kutokana na jamii kutokuwa tayari kufanya mabadiliko ya mfumo wa chakula. Alisema ulaji usiozingatia makundi ya mlo ni sababu inayopelekea maradhi hayo kuongezeka hivyo ameishauri jamii kupunguza matumizi ya vyakula vya uwanga na kutumia matunda kwa wingi.

"Nibora Kula chakula Bora na sio Bora chakula, tuachane na vyakula vya kusindikwa vimekosa virutubisho ,sasa tutumie vyakula vyetu vya asili ambavyo hata gharama yake nindogo"alishauri
Alifahamisha kuwa kiafya kwa siku inatakiwa kutumia uwanga ujazo wa mkono , mboga mboga kwa wingi na mafuta yasiozidi vijiko viwili vya chakula hivyo ameiasa jamii kuwa na Utamaduni huo ili kupunguza ongezeko la maradhi hayo.

"Kitu chochote kinapoongezeka katika mwili ni sumu, si uwanga,mafuta ,sukari wala chumvi ivyo tujitahii kupunguza matumizi ya vitu hivi kwani ni miongoni mwa sababu za maradhi haya"alifahamisha

Makamu wa Rais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. Philip Mpango, amesema serikali inaendelea na mchakato wa...
19/04/2023

Makamu wa Rais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. Philip Mpango, amesema serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ambavyo vimeendelea kukithiri na kuathiri watoto na vijana.

Dk. Mpango alitoa kauli wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Buswelu katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza baada ya kukutana na wananchi waliobeba mabango wakiiomba serikali kudhibiti vitendo hivyo vinavyokiuka maadili ya kitanzania. Alisema kuwa wakati serikali ikiendelea na mchakato juu ya udhibiti wa jambo hilo, haiwezi kukubali hali ikaishia hapo na kuacha jamii ikiendelea kutafunwa na janga hilo huku akitaka jamii kuweka mkono wake ili kuzuia vitendo hivyo.

“Nimeona mmenyanyua mabango hapa, mnasema hamtaki ushoga, usagaji. Kadhalika mmesema mnaomba zitungwe sheria haraka ili kuokoa taifa. Ninyi ni watu wazuri, niwaombe nanyi wazazi wenzangu kurudi katika familia zenu kuhakikisha mnafuatilia maendeleo yao ya elimu shuleni hususani katika madaftari yao kujua wanajifunza nini,” alisema. Pia alizitaka taasisi za serikali na dini kupinga vikali matendo hayo kwa kutoa elimu na kuhubiri maadili mema kwa jamii.

Pia amesema serikali itachunguza mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) hususani zile zinazopeleka maombi ya usajili serikalini ili kuhakikisha hazileti miradi yenye viashiria vya mapenzi ya jinsia moja.

Address

Mazizini Unguja
Unguja

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vfm Radio Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Vfm Radio Zanzibar:

Videos

Share

Media/News Company

Radio HITS FM private radio station in the Tanzanian Isles, Zanzibar. It was officially it went on transmission and extensive programs research, programming and recruiting process from 22nd September 2009. It was officially given the license by Zanzibar Broadcasting Corporation on the 15th of September 2009.

Management offices and studio is located at Airport Street, Migombani Zanzibar. Both are on air and other production studios are located here.

We have well-researched and tailored programs to meet different ages and ethnic groups and at large, we have grasped the hearts and minds of the youth of ages 15 years to adults of up to 45 years and above.


Other Unguja media companies

Show All