Ihsaan Fm Radio

Ihsaan Fm Radio Ihsaan Fm Radio broadcasting live from Tanga Tanzania

02/01/2025

DAY 3 | MKUTANO MKUU WA 28 WA MWAKA | ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE - 28TH DEC, 2024

Cc: Tv Imaan Tanzania

01/01/2025

DAY 2 | MKUTANO MKUU WA 28 WA MWAKA | ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE - 28TH DEC, 2024

Cc: Tv Imaan Tanzania

01/01/2025

DAY 1 | MKUTANO MKUU WA 28 WA MWAKA | ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE - 27TH DEC, 2024

Cc: Tv Imaan Tanzania

SHEIKH SALIM BARAHIYAN AKALIFISHWA TENA KUONGOZA AMYCTanga, TanzaniaKufuatia Mkutano Mkuu wa 28 wa Mwaka wa Taasisi ya A...
29/12/2024

SHEIKH SALIM BARAHIYAN AKALIFISHWA TENA KUONGOZA AMYC

Tanga, Tanzania
Kufuatia Mkutano Mkuu wa 28 wa Mwaka wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre (AMYC) uliofanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 27 hadi 29, 2024, Sheikh Salim Barahiyan amechaguliwa tena kuwa Mudir wa Taasisi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Katika uchaguzi huo, nafasi mbalimbali za uongozi zilijazwa, ambapo Sheikh Ally Nassor alichaguliwa tena kuwa Naibu Mudir, Al Akh Seif Ally Babu kuwa Mweka Hazina, na Al Akh Fuad Barahiyan alirudi tena kaika nafasi ya Naibu Mweka Hazina.

Pia, wajumbe 10 wa Bodi ya Wadhamini walichaguliwa katika mkutano huo. Wajumbe hao ni Eliamani Mgallah, Badru Issa Badru, Muhammad Bawazir, Fuad Barahiyan, Mbarak Ahmed, Edha Al Obthan, Bakari M. Bakari, Sheikh Salim Barahiyan, Sheikh Salim Bafadhil, na Muhammad Hussein.

Kabla ya zoezi la uchaguzi, ripoti muhimu ziliwasilishwa, ikiwa ni pamoja na Ripoti za Utendaji na Ripoti ya Fedha kutoka kwa Majimbo yote pamoja na Markaz Kuu. Ripoti hizi zilijadiliwa kwa kina, na maoni pamoja na mapendekezo yalitolewa kwa lengo la kuimarisha utendaji wa taasisi.

Aidha, mipango ya kimkakati na kimaendeleo yaliazimiwa, yakitarajiwa kuanza kutekelezwa rasmi kuanzia Januari 2025. Maazimio hayo yanajumuisha juhudi za kuimarisha elimu ya dini, kueneza Da’wah ya Haki, kuendeleza ustawi wa jamii, kujenga uchumi madhubuti, na kukuza matumizi ya teknolojia za kisasa.

Tunamuomba Allah Subhanahu wa Ta’ala aibariki Taasisi ya AMYC, awaongoze viongozi wake wapya, na aisahilishie kufanikisha malengo yake kwa mafanikio na baraka.



🥀 *VIONGOZI 14 WACHAGULIWA KUIONGOZA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE KWA MIAKA MINNE IJAYO* 🥀Jumla ya viongozi 14 ...
29/12/2024

🥀 *VIONGOZI 14 WACHAGULIWA KUIONGOZA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE KWA MIAKA MINNE IJAYO* 🥀

Jumla ya viongozi 14 wamechaguliwa kuingoza Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre kwa ngazi ya Markaz kuu katika uchaguzi uliofanyika mchana wa leo Jumapili Disemba 29,2024 ndani ya mkutano Mkuu uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha Ummu Salama jijini Tanga.

Nafasi zilizochaguliwa ni Wadhamini 10, Mudir ,Naibu Mudir ,Mweka Hazina na Naibu Mweka hazina ambapo wajumbe wajumbe wa Mkutano Mkuu wamewachagua viongozi hao watakaohudumu kwa muda wa miaka mine kuanzia mwaka 2025 hadi 2028.

MATOKEO YA UCHAGUZI AMYC 1446H/2024M

01. Eliamini Shaban
Mgallah -
Mdhamini - amepata kura 100 kati ya kura 106

02. Saalim Awadhi
Bafadhili -
Mdhamini -amepata kura 102 kati ya kura 106.

03. Awadhi Muhammd
Bawaazir -
Mdhamini - amepata kura 101 kati ya kura 106.

04. Mubaaraka Ahmed - Mdhamini - amepata kura 102 kati ya kura 106.

05. Muhammad Hussein - Mdhamini - amepata kura 102 kati ya kura 106.

06. Fuad ‘Abdulrahiym
Barahiyaan -
Mdhamini - amepata kura 103 kati ya kura 106.

07. Saalim ‘Abdulrahiym
Barahiyaan -
Mdhamini - amepata kura 103 kati ya kura 106.

08. Edha Saidi
Mubaaraka -
Mdhamini - amepata kura 102 kati ya kura 106.

09. Badru ‘Iysa Badru - Mdhamini - amepata kura 102 kati ya kura 106.

10. Bakari Muhammad
Bakari -
Mdhamini - amepata kura 102 kati ya kura 106

11. Saalim ‘Abdulrahiym
Barahiyaan -
Mudir - amepata kura 104 kati ya kura 106.

12. ‘Ally Naasor ‘Ally - Naibu Mudir - amepata kura - 106 kati ya kura 106.

13. Seif ‘Ally Babu - Mweka Hazina - amepata kura 104 kati ya kura 106.

14. Fuad ‘Abdulrahiym
Barahiyaan -
Naibu Mweka
Hazina - amepata kura
106 kati ya kura 106.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

🥀 *VIONGOZI WAKUU WA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE WANACHAGULIWA HII LEO* 🥀Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Taasisi ya...
29/12/2024

🥀 *VIONGOZI WAKUU WA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE WANACHAGULIWA HII LEO* 🥀

Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre wapo katika uchaguzi kuwachagua viongozi wa Taasisi hiyo katika ngazi ya Markaz kuu.

Uchaguzi huo unafanyika leo jumapili Tar. 29.12.2024 ikiwa ni hatua ya mwisho ya chaguzi mwaka huu katika Taasisi hiyo ambapo mwezi Septemba na Oktoba zilianza chaguzi za Matawi na Majimbo ndani na nje ya Tanzania.

Nafasi zinazochaguliwa katika mkutano huo Mkuu ni Wadhamini, Mudir, Naibu Mudir, Mweka hazina na Naibu Mweka hazina ambapo kwa mujibu wa k**ati ya uchaguzi matokeo ya uchaguzi yatatangazwa Jumapili ya leo mara baada ya Swalah ya adhuhuri.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

VIONGOZI WAKUU AMYC WANACHAGULIWA HII LEO
29/12/2024

VIONGOZI WAKUU AMYC WANACHAGULIWA HII LEO

🥀 *SHEIKH BARAHIYAAN AIZUNGUMZA HATARI YA BAADHI YA MASHEIKH WA SUNNAH KUSHIRIKI VIPINDI KATIKA RADIO ZA MAIBADHI* 🥀Mudi...
29/12/2024

🥀 *SHEIKH BARAHIYAAN AIZUNGUMZA HATARI YA BAADHI YA MASHEIKH WA SUNNAH KUSHIRIKI VIPINDI KATIKA RADIO ZA MAIBADHI* 🥀

Mudir Markaz kuu Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Sheikh Saalim Barahiyaan amewakemea baadhi ya Masheikh wa Sunnah ambao wamekuwa wakiyaunga mkono makundi mapotovu yaliyo kinyume na itikadi sahiyh ya kiislamu ikiwa ni pamoja na kushiriki vipindi katika Radio zao.

Akizungumza katika mkutano Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre unaofanyika kwa siku ya tatu leo Jumapili Tar. 29.12.2024 katika ukumbi wa chuo cha Ummu Salamah jijini Tanga Tanzania amesema kuna hatari kubwa katika Da’awah kushirikiana na watu wa makundi mapotovu.

“Katika makundi mapotovu ni pamoja na Maibadhi ambao wanaonekana hivi sasa wanauadui mkubwa, Kuna baadhi ya Masheikh wetu wa Sunnah wanashiriki vipindi katika Radio Nuwr, kweli hawauzungumzi uibadhi lakini kushiriki vipindi ni kuifanya jami ya kawaida iwaone wale hawana neno” Amesema Sheikh Barahiyaan.

Katika Mihaadhara yake mbalimbali Muhaadhiri huyu wa Kimataifa amekuwa akitekeleza malengo ya Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre kwa kuitahadharisha jamii ya kiislamu juu ya hatari ya makundi mbalimbali mapotovu ikiwemo Mashi’a, Matakfiyr, Quraaniynna,Maibadhi na kundi jipya la Kijadiydah.

🥀 *IMETOLEWA NA KAMATI YA HABARI MKUTANO MKUU AMYC 1446H/2024* 🥀

🥀 *SHEIKH ALLY ZUBEIR : SISI BASUTA TUNAFANYA KAZI KILA SIKU* 🥀Kaimu Amiri wa Baraza kuu la Taasisi za Sunnah Tanzania B...
29/12/2024

🥀 *SHEIKH ALLY ZUBEIR : SISI BASUTA TUNAFANYA KAZI KILA SIKU* 🥀

Kaimu Amiri wa Baraza kuu la Taasisi za Sunnah Tanzania BASUTA Sheikh ‘Ally Zubeir amekiri kuwa Baraza hilo lenye jumla ya Taasisi 16 za sunnah linafanya kazi kila siku tofauti na baadhi ya watu wanavyodai kuwa halifanyi kazi.

Akiufungua mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha Ummu Salamah jijini Tanga leo Disemba 29, 2024M Sheikh Ally Zubeir amesema baraza hilo ni tendaji kwa kila siku hivyo amekanusha madai ya baadhi ya watu kuwa halionekani utendaji wake Zaidi ya kutangaza mwezi pekee.

Sheikh Zubeir amezitaja baadhi ya kazi kubwa zinazofanywa na baraza hilo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano tendaji ya Taasisi za baraza, kuziwakilisha Taasisi za Sunnah katika mikutano na vikao vya kiserikali, kuzisemea Taasisi hizo katika masuala mbalimbali kwa ujumla pamoja na kushauri utendaji na uwajibikaji bora wa Taasisi hizo.

“Wapo wanaosema hatufanyi kazi, si kweli uwepo wangu hapa pia nipo kazini na mimi ni Kaimu wa BASUTA, tunahudhuria mikutano k**a hii, wakati mwingine tunaalikwa na Serikali k**a Baraza mwakilishi kuziwakilisha taasisi hizi” amesema Sheikh Zubeir.

Aidha kiongozi huyo anayekaimu nafasi ya Uamiri wa BASUTA ameiomba serikali kuendelea kuliamini Baraza hilo na kulipa haki sawa k**a mabaraza mengine mengi ya wasiokuwa waislamu.

“Wasiokuwa sisi wana mabaraza Zaidi ya matano, sasa sisi tuna baraza moja, tunaomba uadilifu na sisi tupewe nafasi kwa baraza letu, tunaamini serikali yetu ni sikivu itatusikiliza katika hili” amesema Sheikh Zubeir.

Katika kalimah yake hiyo ya kuelekea uchaguzi mkuu wa Taasisi ya Ansaar Muslim youth Centre amewaasa wajumbe wa mkutano huo kufanya uchaguzi wa Amani na uadilifu k**a ilivyo katika Shariyah ya kiislamu inavyosisitiza huku wakijiepusha na fitna.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA TANZANIA* 🥀

🥀 *TAASISI YA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE MAADUI WAKE* 🥀AMYC ni Taasisi ya kisunnah yenye makao yake Makuu jijini Tanga n...
28/12/2024

🥀 *TAASISI YA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE MAADUI WAKE* 🥀

AMYC ni Taasisi ya kisunnah yenye makao yake Makuu jijini Tanga nchini Tanzania ambayo ina jumla ya Majimbo 29 ndani na nje ya Tanzania.

Katika katiba ya Taasisi hii moja ya malengo yake ni kuratibu na kusimamia utoaji wa elimu ya dini ,mazingira na ufundi kwa vijana na waislamu kwa ujumla ili kujenga ummah wenye kujitegemea bila kuchanganya mila potofu, uzushi au ushirikina ,yaani uislamu k**a ulivyotekelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam) kwa ufahamu wa wema waliotangulia.

Kwa malengo haya Taasisi hii kwa Zaidi ya miaka 30 sasa imekuwa ikipambana na kila kundi ambalo linakwenda kinyume na itikadi hii tukufu, kumeanzishwa vitengo mbalimbali ili kulisimamia lengo hili ipasavyo.

Katika mikutano miwili mikuu ya Taasisi hii iliyofanyika mwaka 2020 na 2021 kumeshuhudiwa Ripoti nyingi za majimbo ya Taasisi hii zikieleza juu ya mfumuko mpya wa makundi mbalimbali yalio kinyume ,yanayofanya uadui kwa Taasisi ikiwa ni pamoja na Majadiydah ( Wanasunnah wanaoasi), Mashi’a , Matakfiri na makundi mengine.

Mambo yamekuwa Tofauti kwa Mkuutano mkuu wa Mwaka huu unaofanyika leo Jumamosi kwa siku ya pili katika ukumbi wa chuo cha Ummu Salamah jijini Tanga ambapo Ripoti nyingi za majimbo hazina maelezo ya changamoto hii huku mengine yakieleza mafanikio makubwa ya Da’awah katika majimbo yao.

Radio Ihsaan FM ikazungumza na Naibu Mudir Markaz kuu wa Taasisi hiyo Sheikh ‘Ally Nassor ambaye ameeleza namna walivyopambana na makundi haya yaliyofanya uadui na Taasisi hii.

“Tupo imara ,tunawajua vizuri na ndio maana ripoti za majimbo ni nzuri, wajua ukimjua adui yako vizuri na kumsoma unajua namna ya kupambana nae, mipango yetu ni thabiti na ndio maana huwasikii tena wakileta changamoto” amesema Sheikh Nassor.

Mkutano mkuu wa Taasisi unaendelea katika ukumbi wa Ummu Salama jijini Tanga ikiwa leo Jumamosi upo katika siku yake ya Pili.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

*MKUTANO MKUU AMYC UNAENDELEA*"Alla awafanyie wepesi katika Mambo yao wote walioshiriki na kufuatilia Mkutano huu Mwanzo...
28/12/2024

*MKUTANO MKUU AMYC UNAENDELEA*

"Alla awafanyie wepesi katika Mambo yao wote walioshiriki na kufuatilia Mkutano huu Mwanzo mpaka hivi sasa"

Mkutano mkuu wa Taasisi unaendelea katika ukumbi wa Ummu Salama jijini Tanga ikiwa leo Jumamosi upo katika siku yake ya Pili.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

🥀 *SHEIKH KIROBOTO NA MATUMAINI MAPYA YA JIMBO LA MUHEZA AMYC BAADA YA KIFO CHA SHEIKH ANUWARY* 🥀Jimbo la Muheza Taasisi...
28/12/2024

🥀 *SHEIKH KIROBOTO NA MATUMAINI MAPYA YA JIMBO LA MUHEZA AMYC BAADA YA KIFO CHA SHEIKH ANUWARY* 🥀

Jimbo la Muheza Taasisi ya Ansaar Muslim Yoouth Centre limepata matumaini mapya sasa baada ya kuchaguliwa uongozi Mpya wa kuliongoza jimbo hilo lenye matawi 14.

Jimbo hili ambalo awali lilikuwa likiongozwa na Sheikh Anuwary Khatwiyb ambaye alifariki Dunia kwa ajali Tarehe 30 Julai 2024M, kwa sasa linaongozwa na Sheikh Amiri Kiroboto , mwanaharakati Mkongwe wa jimbo aliyechaguliwa katika uchaguzo uliofanyika Tarehe 19 Oktoba 2024.

“Kwa sasa nimekalia Mwenyewe kiti cha uongozi baada kura kutosha mimi kushika nafasi hii, Sheikh Anuwary (Allaah amrehemu) tulimsomesha sisi ,tulimuona kijana ameshakuwa na ana elimu ,tukasema anafaa kutuongoza, kufariki kwake ni mtihani kwetu na sasa tunaliamsha jimbo tena k**a ilivyo zamani” amesema Sheikh Kiroboto.

Ni matumaini mapya yaliyotolewa na Kiongozi huyo wa sasa jimboni humo akizungumza na Radio Ihsaan FM nje ya kidogo ya Mkutano Mkuu wa Taasisi ya AMYC jijini Tanga akieleza hatua madhubuti wanazozifanya kwa kushirikiana na Markaz kuu kurudisha uhai wa Jimbo k**a ilivyo zamani kwa kuhakikisha kila kitengo ambacho kiliporwa na waasi kukirejesha katika himaya yao.

Jimbo hili hapo awali lilikutana na changamoto ya uasi ambayo baadhi ya wanachama wa Jimbo hili katika Tawi la Ngwaru waliweza kung’atuka na kupora baadhi ya vitengo ikiwemo misikiti na Shule za Swafaa ambapo kesi ya kurejesha vitengo hivyo ipo katika muendelezo wa kutatuliwa.

Mudir Markaz kuu Sheikh Salim Barahiyaan amesema “hawakuwa Majadiydah wala Makundi mengine ya Kitakfiri bali tamaa ya mali iliwafanya wakafanya uasi”.

Sheikh Kiroboto amesema wapo mbioni kushinda kesi zote na muda si Mrefu wanavirejesha vitengo vyote vya Taasisi vilivyoporwa.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA TANZANIA* 🥀

🥀*MUDIR WA MARKAZ JIMBO LA MARAMBA AWATAJA MASHIA KUVAMIA MAENEO YA WAISLAMU*🥀Mudir wa Markaz jimbo la Maramba chini ya ...
28/12/2024

🥀*MUDIR WA MARKAZ JIMBO LA MARAMBA AWATAJA MASHIA KUVAMIA MAENEO YA WAISLAMU*🥀

Mudir wa Markaz jimbo la Maramba chini ya Taasisi ya Ansaar Muslim youth Centre (AMYC) Ambaye Ripoti yake imesomwa na Mjumbe Ndugu Ismail Juma, ameonesha kutoridhishwa na baadhi ya mapote yanayojinasibisha na uislam kuvamia maeneo yanayomilikiwa na Ahlusunna waljamaa na kueneza itikadi zao.

Ameyazungumza hayo siku ya pili katika mkutano wa 28 wa taasisi hiyo wakati akitoa ripoti ya jimbo lake na kueleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni kuvamiwa katika misikiti ya Ahlusunna waljamaa na mapote yanayojinasibisha na Uislam na kutangaza itikadi zao potofu.

Hata hivyo Mudir wa markaz hiyo ameeleza juu ya mafanikio waliyoyapata ya kufanya daawa katika jimbo lake na kuwafanya waaminiwe na kuendeleza majukumu na mipango ya kuundeleza Uislamu.

Aidha amesema wamefanikiwa kupitia daawa hizo kupata vituo viwili ambavyo ni Muangalieni na Bantu ambavyo vinaweza kufikia sifa ya kuwa markaz tawi.

Mkutano mkuu wa Taasisi unaendelea katika ukumbi wa Ummu Salamah jijini Tanga ikiwa leo ijumaa upo katika siku yake ya kwanza.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

"MKUTANO UNAENDELEA VIZURI ALHAMDULILLAH""SIKU YA PILI" 🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀
28/12/2024

"MKUTANO UNAENDELEA VIZURI ALHAMDULILLAH"

"SIKU YA PILI"

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

"SIKU YA PILI"Naibu Mudir Markaz kuu Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre (AMYC) Sheikh Ally Nassoro  amefungua  Mkutan...
28/12/2024

"SIKU YA PILI"

Naibu Mudir Markaz kuu Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre (AMYC) Sheikh Ally Nassoro amefungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 28 Taasisi ya AMYC unaofanyika kwa siku tatu Ijumaa ,Jumamosi na Jumapili katika ukumbi wa Chuo cha Ummu Salamah barabara ya 19 jijini Tanga.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

🥀 *SHEIKH SAALIM BARAHIYAAN : HATUWEZI KUWA CHINI YA BAKWATA, WAPO KINYUME NA ITIKADI ZETU* 🥀Mudir Markaz kuu Sheikh Sal...
27/12/2024

🥀 *SHEIKH SAALIM BARAHIYAAN : HATUWEZI KUWA CHINI YA BAKWATA, WAPO KINYUME NA ITIKADI ZETU* 🥀

Mudir Markaz kuu Sheikh Salim Barahiyan Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre amesema kuwa Taasisi hiyo haiwezi kujiunga wala kuwa chini ya Baraza la BAKWATA kwani wao wana tofautiana na baraza hilo kiitikadi.

Akizungumza na Radio Ihsaan FM pembeni ya Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha Ummu Salamah jijini Tanga Sheikh Barahiyan amesema kuwa Taasisi ya Ansaar AMYC imejikita katika itikadi sahihi ya Qur’aan na Sunnah ,kupinga shirki na bid’ah katika dini hivyo haiwezekani kuwa chini ya baraza ambalo lina tofauti na wao katika itikadi hiyo.

Kiongozi huyo katika ngazi ya Markaz kuu amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi wa Serikali ikiwemo msajili wa Taasisi za Dini na wadhamini ambao wanakwenda kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwalazimisha kuwa chini ya BAKWATA k**a Taasisi mama jambo ambalo halikubaliki.

‘’Sisi tunasema ni watu tulio na muelekeo maalum, tunaajiita watu wa Sunnah kwa hiyo hatuwezi kuwa chini ya Taasisi ambayo haiendani na malengo yetu , Baraza linapinga mambo yetu ,tutakuwaje chini ya Baraza ambalo linapinga mifumo na mielekeo ya itikadi zetu ,kwa nini tuwe chini ya watu ambao wanatufanyia uadui’’ ameuliza Sheikh Barahiyan.

Hata hivyo Sheikh Salim Barahiyan amesema Taasisi pekee walio tayari kuwa chini yao ni Taasisi ya Baraza la Sunnah Tanzania BASUTA ambayo Taasisi ya AMYC ni mwanachama wake ,akisema hiyo ndio Taasisi pekee wanayoiamini katika kuendana na itikadi sahiyh ya Ahlu Sunnah wal Jamaa’ah.

‘’Nataraji kwamba serikali hii ya mama ni sikivu inaweza ikaja kukubali haya maombi yetu na tupate uhuru wa ‘ibaada k**a vile inavyotakiwa katika katiba ya jamhuri’’ amesema Sheikh Barahiyaan.

Mkutano mkuu wa Taasisi unaendelea katika ukumbi wa Ummu Salamah jijini Tanga ikiwa leo ijumaa upo katika siku yake ya kwanza.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANG

🥀 *JIMBO LA SINGIDA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE MBIONI KUWA NA ZAHANATI* 🥀Jimbo la Singida Taasisi ya Ansaar Muslim Youth...
27/12/2024

🥀 *JIMBO LA SINGIDA ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTRE MBIONI KUWA NA ZAHANATI* 🥀

Jimbo la Singida Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre lipo mbioni kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwa ajili kurahisisha huduma za matibabu kwa wanajamii jimboni.

Akijibu Swali la Mudir wa Jimbo la Pangani Sheikh Salim Amar katika mkutano mkuu wa Mwaka Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Katibu wa Jimbo la Singida Ustadh Hashimu Rashid Sinda amesema ujenzi huo ka upo katika renta tayari kwa umaliziwaji.

‘’Kwa sasa dispensary yetu ipo katika hatua renta’’ amesema Ustash Sinda.

Akisoma Ripoti ya Jimbo hilo Ustadh Sinda ametaja maendeleo makubwa ya jimbo hilo katika elimu, da’awah.

Mkutano mkuu wa Taasisi unaendelea katika ukumbi wa Ummu Salama jijini Tanga ikiwa leo ijumaa upo katika siku yake ya kwanza.

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA.* 🥀

🥀 *MUDIR MARKAZ KUU AMYC ASISITIZA WAISLAMU KUFANYA SHUWRAH KATIKA MAMBO YAO ILI KUPATA MAENDELEO*🥀Mudir Markaz kuu Taas...
27/12/2024

🥀 *MUDIR MARKAZ KUU AMYC ASISITIZA WAISLAMU KUFANYA SHUWRAH KATIKA MAMBO YAO ILI KUPATA MAENDELEO*🥀

Mudir Markaz kuu Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Sheikh Salim Barahiyaan amesema suala la kushauriana katika dini ni jambo muhimu sana na inapaswa kwa waislamu wawe na tabia ya hiyo ili kupatikana kwa maendeleo ya Duniani na Aakhera.

Hayo ameyasema leo Ijumaa akitoa neno la ufunguzi katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa 28 Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Cente unaofanyika kwa siku tatu Ijumaa ,Jumamosi na Jumapili katika ukumbi wa Chuo cha Ummu Salamah barabara ya 19 jijini Tanga.

Sheikh Barahiyan amesema moja ya mambo ya msingi yanayoruhusiwa kishariyah yanayotengeneza maendeleo ni suala la kushauriana na ndio maana wao Taasisi wanafanya mikutano mbalimbali ikiwemo mkutano mkuu wa mwaka 2024M.

‘’Mkutano mkuu ni katika amri kuu, tumekaa kwa ajili ya kushariana na pia tumekaa kwa ajili ya amri ya Allaah Subhaanahu Wata’ala’’ amesema Sheikh Barahiyaan.

Hata hivyo kiongozi mkuu huyo huyo wa Taasisi ametaja uimara wa Taasisi katika matumizi ya teknolojia za kidijitali hivi sasa kwa kuanza na Shuwrah za Markaz kuu ambazo ambazo pia zitawakutanisha viongozi wakuu wa majimbo.

‘’Kwa mara ya kwanza mwaka huu tunaingia katika mfumo wa kidijitali, Shuwrah ya sasa itakuwa na wakuu wa majimbo pia, na Shuwrah ya kwanza tutaifanya kwa njia ya Mtandao katika kila mwezi’’

🥀 *IMETOLEWA NA RADIO IHSAAN FM 102.1 TANGA* 🥀

Address

1542
Tanga
21105

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ihsaan Fm Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ihsaan Fm Radio:

Videos

Share