Dreams Tz

Dreams Tz Dreams Media is your ultimate source for news and trending topics, seven days a week.
(2)

CRDB Bank Federation Cup 2024/2025. 72’ Young Africans 3️⃣-0️⃣ Copco FC⚽️Sheikhan Ibrahim⚽️Prince Dube ⚽️Maxi Nzingeli  ...
25/01/2025

CRDB Bank Federation Cup 2024/2025.

72’ Young Africans 3️⃣-0️⃣ Copco FC
⚽️Sheikhan Ibrahim
⚽️Prince Dube
⚽️Maxi Nzingeli


Singida Black Stars imewabadilisha uraia wachezaji wake watatu wa kigeni na kuwa raia wa Tanzania, Singida imefanya hivy...
22/01/2025

Singida Black Stars imewabadilisha uraia wachezaji wake watatu wa kigeni na kuwa raia wa Tanzania, Singida imefanya hivyo ili kukidhi kanuni ya kuwa na wachezaji 12 wa kigeni.
✅ E. Keyekeh (27) 🇬🇭 ➡️ 🇹🇿
✅ Arthur Bada (22) 🇨🇮 ➡️ 🇹🇿
✅ Damaro Camara (21) 🇬🇳 ➡️ 🇹🇿
Golikipa Amas Obasogie (25) ambaye alikuwa raia wa Nigeria 🇳🇬 nae ni miongoni mwa wachezaji wa Singida Black Stars waliobadili uraia na kuwa Mtanzania.
➡️ Obasogie amejiunga na Singida Black Stars akitokea Fasil Kenema ya Ethiopia 🇪🇹

*“Watumishi mnanaotaka kugombea nafasi za kisiasa zingatieni taratibu za kiutumishi” Mhe. Mchengerwa*Waziri wa Nchi, Ofi...
22/01/2025

*“Watumishi mnanaotaka kugombea nafasi za kisiasa zingatieni taratibu za kiutumishi” Mhe. Mchengerwa*

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka watumishi wa umma wanaohudumu chini ya ofisi yake kutojiusisha na shughuli za siasa k**a ambavyo Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma zinavyoelekeza.

Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo hayo leo Januari 22, 2025, wakati akijibu hoja za baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayoendelea na vikao vyake vya kawaida jijini Dodoma chini ya mwenyekiti wake Mhe. Justine Nyamoga.

“Kwa mujibu wa Kanuni F.21 (b) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la Mwaka 2009 mtumishi wa umma harusiwi kujihusisha na shughuli za kisiasa wakati akiendelea kutekeleza majukumu yake ya kiutumishi, hivyo ofisi yangu haitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wanaokiuka kanuni hiyo,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewaelezea wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa, Ofisi yake haiungi mkono watumishi wanaoacha kutekeleza majukumu yao ya msingi na badala yake wanajishughulisha na masuala ya kisiasa ambayo yanaathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, uwepo wa baadhi ya watumishi wanaotumia rasilimali za Serikali kufanya shughuli zao za kisiasa ni jambo ambalo hawezi kulifumbia macho na kueleza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI kufuatilia kwa ukaribu madai hayo ili hatua stahiki zichukuliwe.

“Taratibu ziko wazi k**a kuna mtumishi anahitaji kuingia kwenye siasa anapaswa kuzingatia taratibu za kiutumishi ikiwepo kumfahamisha mwajiri wake na kwa baadhi ya nyadhifa mtumishi anapaswa kujiudhuru ili aingie moja kwa moja kwenye siasa, hivyo ninashauri watumishi wa umma kuzingatia Kanuni, Sheria, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma iliyopo,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Kupitia ukurasa wake wa X (Twitter), Mwanasiasa, Freeman Mbowe amempongeza na kumtakia heri Tundu Lissu licha ya kuwa ma...
22/01/2025

Kupitia ukurasa wake wa X (Twitter), Mwanasiasa, Freeman Mbowe amempongeza na kumtakia heri Tundu Lissu licha ya kuwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa CHADEMA hayajatangazwa

Mbowe ameandika “Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.”

Baada ya andiko hilo, John Heche akajibu “Asante sana Mwenyekiti, umetujenga na kutulea, umeonesha Demokrasia kwa kuongoza timu kusimamia uchaguzi wa wazi, huru na haki. Historia ya Tanzania itakukumbuka, k**a mtu uliejenga Demokrasia na kuleta mageuzi makubwa kwenye Nchi na chama chetu.”

"Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Ja...
22/01/2025

"Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la uongozi wa chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele chama chetu." - Freeman Mbowe

 : Kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, Freeman Mbowe aliandika“Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa ...
22/01/2025

: Kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, Freeman Mbowe aliandika
“Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu”-Freeman Mbowe, Mwenyekiti anaemaliza muda wake ChademaTaifa.

Wizara ya fedhaa, imeahidi kuendelea kutekeleza azma yake ya kuhakikisha elimu ya fedha inawafikia wananchi wote ili kuh...
21/01/2025

Wizara ya fedhaa, imeahidi kuendelea kutekeleza azma yake ya kuhakikisha elimu ya fedha inawafikia wananchi wote ili kuhakikisha kuwa wanaelimika kuhusu masuala ya fedha, mikopo, uwekezaji ili kuwawezesha wananchi kutumia huduma sahihi za fedha.

Akizungumza jijini Arusha, Afisa Mwandamizi, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, wakati akitoa elimu ya fedha kwa wajasiliamali na wananchi wa Mtaa wa Muriet jijini Arusha, alisema Wizara iliona umuhimu wa kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wote ili kuwajengea nidhamu ya matumizi ya fedha.

Bw. Kimaro alisema kuwa wananchi wengi wanashindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na uelewa mdogo juu ya matumizi sahihi ya fedha, kukosa usimamizi mzuri wa fedha zao pamoja na kutokuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza hali inayosababisha baadhi ya wananchi fedha wanazopata kutobadilisha maisha yao kiuchumi.

“Imekuwa ni kawaida kusikia vilio vya wananchi wakiwa wamepata changamoto za mikopo wanakopa kwa watu wasio rasmi kutokana na kukosa uelewa wa wapi wanapaswa kukopa na namna ya kutumia hiyo mikopo jambo linalowaletea madhara” alisema Bw. Kimaro

Akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya uwekezaji, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani Arusha, Bw. Josephat Komba, aliwataka wajasiriamali kuwekeza sehemu sahihi ili kuepuka kupoteza fedha zao.

‘’Nawasihi kuwekeza kwenye maeneo ambayo fedha zenu zitakuwa salama na mtapata faida, karibuni kuwekeza NSSSF, kwakuwa kwa kila kiasi cha fedha zako unachoweka utapata akiba na utapata bima ya afya’’ alisema Bw. Komba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Muriet, Bw. Rashid Juma, aliwataka watoa huduma za fedha katika mtaa huo kufuata sheria na taratibu za huduma ndogo za fedha k**a mafunzo yalivyotolewa na timu ya wataalam wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha.

‘’Natoa onyo kwa watoa mikopo mtaani kwangu, ni marufuku kumfuata mtu usiku wa manane kudai pesa, wengine wanaingia kwenye matatizo wanaitiwa wezi wanapigwa kumbe sio wezi wameenda kudai mikopo, kopesheni kwa kufuata taratibu zilizowekwa’’ alisema Bw. Juma.

 : Wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia Taasisi za Fedha zilizosajiliwa amb...
21/01/2025

: Wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia Taasisi za Fedha zilizosajiliwa ambazo zinazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika huduma za fedha ili kujiepesha na watoa huduma za fedha wasio sajiliwa.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Mhe. Dadi Kolimba, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha waliofika wilayani hapo kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Fedha, ili kuwawezesha wananchi kuwa na uelewa wa masuala ya fedha.

Mhe. Kolimba alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya taasisi zinazotoa mikopo kwa wananchi ambayo haifuati Sheria hivyo kusababisha malalamiko ya mara kwa mara na kusababisha wananchi kupoteza mali zao ambazo wameweka dhamana.

‘‘Tulishazungumza na watoa huduma za fedha na taasisi za fedha hapa wilayani na tukasisitiza kuwa mikopo wanayotoa isiwaumize wananchi na endapo tukigundua wanaenda kinyume na Sheria tutawachukulia hatua za kisheria na tunasisitiza wananchi kutumia watoa huduma rasmi za fedha ili kuepuka mikopo isiyofuata Sheria’’, alisisitiza Mhe. Kolimba.

Akizungumza kuhusu elimu inayoenda kutolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha wilayani humo, alisema kuwa elimu hiyo itasaidia wananchi kupata uelewa wa haki na wajibu wa mtoa huduma katika utoaji wa mikopo ili kuwasaidia kuondokana na mikopo umiza.

Mhe. Kolimba alisema kuwa ana imani elimu itakayotolewa kwa wananchi itawaongezea uelewa zaidi wa kutambua haki zao ikiwemo kufahamu taratibu za mikopo ikiwemo kiasi cha riba watakachotozwa na taasisi ya fedha katika mikopo wanayochukua kabla ya kuchukua mkopo.

‘Natoa pongezi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo haya ya kutoa elimu kwa wananchi na pia nimpongeze Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo haya kuhakikisha kuwa elimu hii ya fedha inawafikia wananchi ili kuondokana na changamoto za kiuchumi‘’, aliongeza Mhe. Kolimba.

 : Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi a...
21/01/2025

: Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM , uliofungwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Januari 2025 katika Ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Aidha, Dk.Mwinyi amethibitishwa na Mkutano huo Mkuu Maalum kuwa Mgombea wa Urais pekee wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu mwaka huu.

Vilevile, Mkutano huo umemchagua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea pekee wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na Dk.Emmanuel John Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza.

Donald Trump ameapishwa k**a Rais wa 47 wa Marekani na Jaji Mkuu John Roberts.Aidha, JD Vance ameapishwa leo k**a Makamu...
21/01/2025

Donald Trump ameapishwa k**a Rais wa 47 wa Marekani na Jaji Mkuu John Roberts.

Aidha, JD Vance ameapishwa leo k**a Makamu wa Rais, ambapo Jaji Brett Kavanaugh aliendesha kiapo hicho.

PWANI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumk**ata  mtu mmoja ambaye anadaiwa kuhusika k...
21/01/2025

PWANI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumk**ata mtu mmoja ambaye anadaiwa kuhusika katika kutengeneza picha za mjongeo ambazo za utupu zenye maudhui machafu ambayo ni kinyume kabisa na maadili na sheria za nchi na kuamua kuzisambaza katika mitandao mbali mbali ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salim Morcase amesema kwamba mtuhimiwa huyo baada ya kufanya uchunguzi na kwamba alitengeneza picha hizo za utupu kwa kutengengeneza na kuunganisha na baadhi ya picha za majengo ya shule ya sekondari Baobab kwa lengo la kuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vimefanyika shuleni hapo kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo.

Kamanda huyo pia alisema kuwa picha hizo chafu na zisizo za kimaadili waliotengeneza na kuzisambaza waliziunganisha na baadhi ya picha za wanafunzi ambazo zilitumika kipindi cha nyuma wakati wa mahafari.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shule ya sekondari Baobab Shani Swai amekanusha vikali na kusema kwamba kwamba wamesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya watu kuamua kuwachafua taasisi yao kwa kusamabaza picha hizo za utupu katika mitandao ya kijamii na kusababisha kuleta hali ya sintofahamu kubwa kwa wananchi katika maeneo mbali mbali hasa kwa wazazi na walezi.

Naye Kaimu mkuu wa shule taalamu Alphonce Kamisa na Mwenyekiti wa Bodi ya Talaamu wa shule ya hiyo wamesema kutokana na jambo hilo limeweza kuleta taharuki kubwa licha ya kwamba wanafunzi tayari wamesharipoti shule kwa ajili ya kuanza na masomo yao.

Rais wa Marekani Baada ya Kuapishwa jioni ya Leo amesema Katika Sheria anazoenda kuanza Nazo ni pamoja na Kufuta utambuz...
21/01/2025

Rais wa Marekani Baada ya Kuapishwa jioni ya Leo amesema Katika Sheria anazoenda kuanza Nazo ni pamoja na Kufuta utambuzi wa jinsia tofauti na Mwanaume na Mwanamke Nchini humo

“Nasaini leo rasmi kuwa Marekani inatambua jinsia mbili pekee ambazo ni Mwanaume na Mwanamke, tutaongozwa na miongozo yote ila kubwa zaidi hatutamsahau Mungu wetu”- Donal Trump, Rais wa Marekani wakati anaapishwa leo hii.

Wengi wa watu wazima Nchini marelani (97.3%) wanajitambulisha k**a cisgender humu Asilimia nyingine 1.52 hawatambui kuwa ni wanaume, wanawake, au waliobadili jinsia - watu hawa wanaweza kutumia maneno k**a vile (Non Binary) au Wasiofuata jinsia kuelezea utambulisho wao wa kijinsia.

🚨🇸🇦 Al-Hilal are targeting moves for both Mohamed Salah and Rodrygo as they seek replacements for Neymar. (Rudy Galetti)...
21/01/2025

🚨🇸🇦 Al-Hilal are targeting moves for both Mohamed Salah and Rodrygo as they seek replacements for Neymar. (Rudy Galetti)

🇧🇷 Neymar is close to a sensational loan return to Santos. Final details are being discussed with Al-Hilal, and the loan bid has been submitted. Santos and Neymar are now awaiting the green light from the Saudi club. (Fabrizio Romano)

🇧🇷 Saudi Arabia are reportedly pushing to sign Vinícius Jr. from Real Madrid. While the Brazilian superstar prefers to stay in Madrid, he has not ruled out a move to Saudi Arabia. (Jose Felix Diaz)

🇧🇷 Manchester City are considering a move for Douglas Luiz. Juventus prefer either a straight sale or a loan with an obligation to buy, but Manchester City are only interested in a loan. (David Ornstein)

🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Following rumors about Marcus Rashford’s potential move to Milan, Dortmund are now leading the race for the English striker. (Bild)

Klabu ya Simba SC inatinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi dhidi ya CS Constantine, Mn...
20/01/2025

Klabu ya Simba SC inatinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi dhidi ya CS Constantine,
Mnyama anafikisha alama 13 na kuwa kinara wa Kundi A akishinda michezo minne, sare moja huku akipoteza mchezo mmoja kati ya sita aliyocheza katika hatua ya makundi.

Simba SC 2️⃣ -0️⃣ CS Constantine

⚽ Kibu Denis 61'
⚽ Lionel Ateba 79'


MICHEZO: Timu ya Simba imeingia Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuongoza Kundi A baada ya kuifun...
20/01/2025

MICHEZO: Timu ya Simba imeingia Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuongoza Kundi A baada ya kuifunga CS Constantine ya Algeria kwa Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa

Magoli yaliyofungwa na Kibu Denis na Leonel Ateba yamepeleka furaha kwa wenyeji licha ya mchezo huo kutokuwa na mashabiki, ambapo Simba imefikisha pointi 13 ikifuatiwa na Constantine yenye alama 12

CS Sfaxien ya Tunisia imeshika mkia Kundini ikiwa na alama 3 licha ya kushinda Magoli 4-0 dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola

Simba SC ipo dimbani hii leo kumenyana dhidi ya CS Constantine ya Algeria, mchezo huo unaotarajia kupigwa majira ya saa ...
19/01/2025

Simba SC ipo dimbani hii leo kumenyana dhidi ya CS Constantine ya Algeria, mchezo huo unaotarajia kupigwa majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa ikumbukwe Simba inacheza bila uwepo wa mashabiki wake kutokana na adhabu waliyopewa na CAF.

Mnyama tayari ameshafuzu hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika kikubwa anachohitaji ni kupata ushindi aweze kuongoza kundi A.

Ratiba ya mechi za kombe la Shirikisho Afrika.

16:00 | CS Sfaxien 🆚 Bravos do Maquis
19:00 | Al Masry 🆚 Black Bulls
19:00 | Zamalek 🆚 Enyimba
22:00 | ASEC Mimosas 🆚 Orapa United
22:00 | RS Berkane 🆚 Stellanbosch
22:00 | Stade Malien 🆚 CD Lunda Sul
22:00 | USM Alger 🆚 Jaraaf

CAF: Safari ya Timu ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/25 imefikia tamati kwa kuishia Hatua ya Makundi baada y...
18/01/2025

CAF: Safari ya Timu ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/25 imefikia tamati kwa kuishia Hatua ya Makundi baada ya kulazimishwa matokeo ya 0-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ishike nafasi ya tatu katika Kundi A nyuma ya Al Hilal ya Sudan yenye alama 10 ikifuatiwa na MC Alger yenye alama 9, hivyo timu hizo mbili za juu zimefuzu kucheza Robo Fainali

Timu ya TP Mzembe ambayo imeshika mkia licha ya kushinda magoli 4-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa mwisho, ina pointi 5 ikiwa imeshinda mchezo mmoja

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kukamilisha usajili wa aliyekuwa Kiungo mshambuliaji Al Hilal Serge Pokou, mw...
17/01/2025

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kukamilisha usajili wa aliyekuwa Kiungo mshambuliaji Al Hilal Serge Pokou, mwenye umri wa miaka 24 ambaye pia aliwahi kucheza Asec Mimosas.

Address

Singida

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dreams Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dreams Tz:

Videos

Share