Radio farajatz

Radio farajatz Ukurasa rasmi wa Radio Faraja FM Stereo I 91.3 Mhz Shinyanga


Radio faraja ni chombo cha habari kinacholenga kutoa elimu na kusaidia jamii kwa nyakati mbalimbali,
Pia kinaendeshwa na kutoa mahudhui ya Dini ya kikristo kutoka dhehebu la Roman Catholic katika Jimbo la shinyanga Mjini, Ngokoro.

jamii

03/02/2025

WANAWAKE DODOMA WAIUNGA MKONO SERIKALI KUSAIDIA MAKUNDI MAALUMU

Taasisi ya kikundi cha wanawake ya Jijini Dodoma ijulikanayo k**a WE CAN imetoa msaada wa mahitaji muhimu kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri yenye Wanafunzi Wasioona pamoja na wenye ulemavu wa ngozi.

Akizungumza leo tarehe 02 Februari 2025 mara baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bi. Emmah Kelvin Komba amesema wametoa misaada hiyo ikiwa ni kuunga jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuyashika mkono makundi maalumu ya watu wenye uhitaji ikiwamo watoto, walemavu na hata Wazee.

Kwa Upande wake Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Samwel Sospeter ameishukuru taasisi kwa kuwakumbuka watoto hao kwa kuwapatia mahitaji muhimu k**a nguo chakula na kuchangia kuboresha miundombinu ikiwemo taa za umeme.

Kadhalika Mkuu huyo amesema wanajivunia kuwa na Viongozi katika Ngazi za juu za Serikali waliosoma katika Shule hiyo akiwamo Dkt. Abdallah Saleh Possi ambaye ni Mwakilishi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa mjini Geneva.

Vilevile Wanafunzi wa Shule hiyo wameishukuru Taasisi hiyo kwa mchango na kuwaomba wawe mabalozi kwa wadau wengine katika kuwasadia watoto Hao.

SIMBA SC WARUDI KILELENI  BAADA YA KUWAKUMBATIA NYUKI WA TABORA.Simba SC wanarejea kileleni  baada  ya ushindi wa goli 3...
02/02/2025

SIMBA SC WARUDI KILELENI BAADA YA KUWAKUMBATIA NYUKI WA TABORA.

Simba SC wanarejea kileleni baada ya ushindi wa goli 3-0 na kumshusha mtani wao Yanga SC aliyekaa kileleni kwa masaa machache.

HUU HAPA MSIMAMO BAADA YA MICHEZO 16

1️⃣ Simba SC - 43 pts
2️⃣ Yanga SC - 42 pts
3️⃣ Azam FC - 36 pts
4️⃣ Singida Black Stars - 33 pts
5️⃣ Tabora United - 25 pts

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu kesho Jumapili tarehe 02.02.2025, atatimiza miaka ...
01/02/2025

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu kesho Jumapili tarehe 02.02.2025, atatimiza miaka 10 tangu Baba Mtakatifu Fransisko alipomteua na kumtangaza rasmi kuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga.

Askofu Sangu aliteuliwa na kutangazwa kuwa Askofu wa Jimbo la Shinyanga mnamo Februari 2 mwaka 2015, wakati akifanya utume katika idara ya Uinjilishaji wa watu huko Vatican.

Askofu Sangu aliyewekwa wakfu na kusimikwa rasmi kuliongoza Jimbo la Shinyanga mnamo Aprili 12 mwaka 2015, anatimiza miaka 10 ya kuteuliwa kwake kuwa Askofu wa Shinyanga huku akiwa amefanya juhudi kubwa za kusogeza huduma za kiroho kwa waamini, ambapo mpaka sasa ameongeza Parokia mpya 14 na kulifanya Jimbo la Shinyanga kuwa na jumla ya Parokia 40 kutoka 26 alizozikuta.

Jimbo Katoliki Shinyanga lilianzishwa mnamo mwaka 1956, ambapo Askofu wake wa kwanza alikuwa Hayati Edward Aloysius McGurkin wa shirikia la Maryknoll aliyehudumu kuanzia mwaka 1956 mpaka mwaka 1975.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1996, Jimbo la Shinyanga liliongozwa na Askofu wa kwanza mzalendo Hayati Askofu Castory Sekwa, ambapo baada ya kifo chake, aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Geita wakati ule Hayati Aloysius Balina alihamishiwa katika Jimbo la Shinyanga, ambapo aliliongoza katika kipindi cha kuanzia mwaka 1997 mpaka alipofariki dunia mnamo Novemba 6 mwaka 2012.

Baada ya kifo cha hayati Askofu Balina, Baba Mtakatifu Fransisko alimteua na kumtangaza Askofu Liberatus Sangu kuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga ambaye analiongoza mpaka hivi sasa.

HII HAPA RATIBA YA MICHEZO YA NBC CHAMPIONSHIP ROUND YA 17.Stand United Chama la watakuwa ugenini kuvaana na Transt Camp...
31/01/2025

HII HAPA RATIBA YA MICHEZO YA NBC CHAMPIONSHIP ROUND YA 17.

Stand United Chama la watakuwa ugenini kuvaana na Transt Camp ✅

Transt Camp vs Stand United

📅: 03/2/2025
⏰: 10: 00 jioni
🏟️: Mabatini

Baba Mtakatifu Fransisko, amemteua Padre Romanus Elamu Mihali, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Iringa, baada ya ku...
28/01/2025

Baba Mtakatifu Fransisko, amemteua Padre Romanus Elamu Mihali, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Iringa, baada ya kuridhia ombi la kustaafu kwa mujibu wa sheria za Kanisa kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC, Padre Chesco Msaga, Padre Mihali ameteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Iringa leo Jumanne tarehe 28.01.2025.

Askofu Mteule Romanus Mihali alizaliwa mnamo Juni 10 mwaka 1969 katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Baada ya kumaliza masomo yake ya kipadre, alipewa Daraja takatifu la Upadre mnamo Julai 13 mwaka 2000, ambapo alihudumu katika nafasi mbalimbali Jimboni Iringa.

Alijiendeleza kielimu katika chuo kikuu cha Kerala nchini India na kutunikiwa shahada ya Uzamili katika Sayansi ya wanyama mwaka 2010.

Mpaka kuteuliwa kwake, alikuwa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mafinga.

Aidha kufuatia Askofu Ngalalekumtwa kukubaliwa ombi lake la kustaafu, kwa sasa ataendelea kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la Iringa mpaka Askofu mteule Mihali atakapowekwa wakfu na kusimikwa kuliongoza Jimbo hilo.

Waamini wa Jimbo Katoliki Shinyanga wakiongozwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, wanamtakia matashi mema na kumwombea kwa Mungu ili ampe nguvu na neema Askofu mteule Mihali pale anapojiandaa kupokea jukumu alilopewa na Kanisa la kuliongoza Jimbo la Iringa.

Lipi ni kundi lako humu kuelekea michuano ya AFCON 2025 ? 😁
28/01/2025

Lipi ni kundi lako humu kuelekea michuano ya AFCON 2025 ? 😁

HILI HAPA KUNDI LA TANZANIA MICHUANO YA AFCON 2025.Droo imefanyika wapinzani wamefahamika je, tutapenya kwenda robo fain...
27/01/2025

HILI HAPA KUNDI LA TANZANIA MICHUANO YA AFCON 2025.

Droo imefanyika wapinzani wamefahamika je, tutapenya kwenda robo fainali ?

Je, tutafanikiwa kumaliza nafasi ya kwanza au ya pili ? 😁

Radio Faraja FM inakutakia Heri ya siku ya kuzaliwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
27/01/2025

Radio Faraja FM inakutakia Heri ya siku ya kuzaliwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mzaliwa wa tarehe 27.1.1960 ✅

STAND UNITED CHAMA LA WANA WAREJEA TOP FOUR LIGI DARAJA LA KWANZA.Vita ya kupanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao 2025...
26/01/2025

STAND UNITED CHAMA LA WANA WAREJEA TOP FOUR LIGI DARAJA LA KWANZA.

Vita ya kupanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao 2025/2026 imeendelea kupamba moto na kunogeshwa na matokeo ya michezo mbalimbali hii hapa top four ya msimamo huo.

1️⃣ Mtibwa Sugar - 41 pts
2️⃣ Mbeya City - 34 pts
3️⃣ Geita Gold - 33 pts
4️⃣ Stand United - 32 pts

Je, timu zipi unazipa nafasi ya kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili ili kupanda ligi kuu Moja kwa moja ? 🔥ANDIKA MAONI YAKO KWENYE COMMENT🔥

WABUNGE SHINYANGA WAIMWAGIA SIFA RUWASANa Moshi NdugulileMkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka wananchi Mk...
25/01/2025

WABUNGE SHINYANGA WAIMWAGIA SIFA RUWASA

Na Moshi Ndugulile

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka wananchi Mkoani Shinyanga kuwa wazalendo katika jukumu la kutunza miradi ya maji inayowekezwa na serikali, badala ya kuhujumu miundombinu hiyo, kwani kwa kufanya hivyo ni kuitia hasara serikali.

Ameyasema hayo kwenye hafla ya utiaji saini mikataba tisa ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ,kati ya RUWASA na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo ya maji.

RC Macha amesema serikali imeendelea kutekeleza wajibu wake wa kujenga na kuboresha miundombinu ya maji katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha upatianaji wa huduma hiyo,hivyo wananchi wanapaswa kutunza rasilimali hizo.

RC Macha ameiagiza RUWASA kutoa taarifa ya utekelezaji wa mradi kila tarehe 15 ya mwezi ili serikali iweze kujua maendeleo ya miradi hiyo,ikiwa ni hatua ya kuepuka kukwama kwa utekelezaji huo

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, amesema Miradi hiyo itajengwa katika Wilaya za Kahama, Kishapu na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na kwamba ujenzi wa miradi hiyo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita.

Mhandisi Payovela amefafanua kuwa, katika utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Shinyanga, vijiji vingi sasa vimepata huduma ya maji, na kwamba serikali imeongeza fedha za ujenzi wa visima 20 vya maji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kumaliza changamoto ya ukosefu wa maji.

Akizungumza katika hafla hiyo mbunge wa jimbo la Msalala wilayani kahama Mhe. Idd kassim ameipongeza serikali chini ya jemedari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kutekeleza miradi hiyo ikiwa ni juhudi zilizolenga kuondoa changamoto za kijamii kwa wananchi

“ tunakupongeza sana mheshimiwa mkuu wa Mkoa, wewe pamoja na timu yako,kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kwenye mkoa wetu wa Shinyanga, ambayo mmeendelea kuifanya, nitakuwa mchoyo wa fadhila pia k**a nisipomshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan,Mama na Rais wetu,kwa kazi kubwa na nzuri anayoendelea kuifanya ya kutuletea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji kwenye majimbo yetu, Mimi mbunge wa jimbo la Msalala nimekuwa shuhuda wa miradi mikubwa ya maji ambayo Dkt Saia Suluhu Hassan ndani ya miaka mine,tunaenda mwaka wa tano sasa, imetekelezwa katika jimbo la Msalala,ambapo tunayo miradi mikubwa kadha wa kadha uiwemo mradi unaotoka Mangu-Ilogi,ambao umekamilika,lakini tuna mradi mwingine wa Busangi-Ntobo ambao umekamilika kwa gharama ya shilingi Bil.11,lakini ipo miradi inayoendelea kutekelezwa ukiwemo ule wa kanda ya Mwalugulu,kanda ya Jana na kanda ya Mwamkima na maeneo mengine.

Lakini tuna fedha nyingine ambazo Rais Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan ametupatia kwa ajili ya usambazaji wa maji kwenye kata ya Bugarama na Bulyanhulu ambao tayari umekamilika na wananchi wananufaika na huduma ya maji ya ziwa Victoria”ameeleza Mbunge Idd Kassim

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe. Emanuel Cherehani ameipongeza RUWASA ambayo ameitaja kuwa imeendelea kutatua changamoto ya maji kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa

Ameomba kila mdau wa maji atambue wajibu wa kudhibiti upotevu wa maji na kwamba iwe ni kipaumbele cha kushughulikia,ambapo amewataka wakandarasi wanaopewa kazi hiyo kuhakikisha vifaa vyao vinakuwa imara na vyenye ubora wenye kiwango

Hafla ya utiaji saini mikataba tisa ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kati ya RUWASA na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali na Chama tawala CCM, wabunge,wakuu wa wilaya,k**ati ya ulinzi na usalama ya Mkoa.

Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) itaanza utekelezaji wa ujenzi wa miradi tisa ya maji yenye thamani ya zaidi Shilingi Bilioni 4.7 utakaonufaisha vijiji 16 katika wilala za Kishapu,Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2020/2025 YAWASILISHWA JIMBO LA SHINYANGA MJINI.Mbunge wa jimbo la Shinyanga...
25/01/2025

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2020/2025 YAWASILISHWA JIMBO LA SHINYANGA MJINI.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe Paschal Patrobas Katambi amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 .

Katika taarifa yake hiyo ametaja mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika kipindi hicho ikiwemo ujenzi wa shule na chuo hali ambayo italeta mapinduzi makubwa ya kiuchumi

Ametaja maboresho mbalimbali yaliyofanyika ikiwemo kuboreshwa kwa miundombinu ya Barabara,madaraja na karavati zilizokuwa changamoto kwa wananchi,katika kata mbalimbali za jimbo la Ucaguzi Shinyanya Mjini

Akizungumzia barabara inayounganisha kata ya mjini kupitia kata za Ndala,Masekelo kwenda katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ameiomba serikali kuona namna ya kuondoa changamoto hiyo,ambayo imekuwa kero kwa wakazi wa mji wa Shinyanga

24/01/2025

TAZAMA KILICHOZUNGUMZWA NA WANACHAMA WA CHADEMA KANDA YA SERENGETI BAADA YA KUWASILI NA KUPOKELEWA MKOANI SHINYANGA.

⛔ Ni wajumbe wa mkutano mkuu ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti wakipiga shangwe baada ya kuwasili Mkoani Shinyanga na kupokelewa na baadhi ya wanachama wa Chama hicho.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZA MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI PASCHAL PATROBAS KATAMBI AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKE...
24/01/2025

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZA MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI PASCHAL PATROBAS KATAMBI AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2020/2025 KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM JIMBO LA SHINYANGA MJINI

⛔ Mgeni rasmi kwenye mkutano alikuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi taifa Ndugu Ally Hapi ambao mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Paschal Patrobas Katambi, kesho Ijumaa tarehe 24.01.2025, atasoma taarifa ya utekelez...
23/01/2025

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Paschal Patrobas Katambi, kesho Ijumaa tarehe 24.01.2025, atasoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha mwaka 2020/2025.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Mbunge, Katambi atawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika Jimbo la Shinyanga mjini kupitia Mkutano mkuu wa chama Jimbo (Wilaya ya Shinyanga mjini) ambao utafanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga (NSSF ya zamani) kuanzia saa tatu asubuhi.

Mgeni rasmi katika Mkutano huo atakuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi Taifa Ndugu Ally Hapi.

Mkutano huo utarushwa mubashara (Live) Redio Faraja 91.3 MHz na kupitia ukurasa huu wa Facebook.

RASMI: JUMA HUSSEIN NI KOCHA MPYA WA STAND UNITED CHAMA LA WANA ✅
23/01/2025

RASMI: JUMA HUSSEIN NI KOCHA MPYA WA STAND UNITED CHAMA LA WANA ✅

Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Nhobola Kata ya Talaga katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, amelazwa katika Hos...
23/01/2025

Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Nhobola Kata ya Talaga katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali kinachotajwa kuwa ni Mshale, na watu anaowataja kuwa ni wakazi wa kijiji hicho.

Mwanaume huyo aitwaye M***a Ngasa mwenye umri wa miaka 39, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 12 jioni Jumatatu wiki hii baada ya watu hao sita kumvamia wakati akitoka shambani na mke wake, ambapo walimshambulia kwa mshale na kumjeruhi katika ubavu wake wa kulia, ambapo alisaidiwa na wasamaria wema kukimbizwa katika Hospitali ya Kolandoto kabla ya kupewa rufaa kwenda katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga-Mwawaza, ambapo Madaktari walimfanyia upasuaji ili kuokoa maisha yake.

Amelieza tukio hilo kuwa linatokana na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati yake na watu hao ambao wamekuwa wakimshambulia mara kwa mara, baada ya kuwashinda kesi katika baraza la Ardhi la Kata na Baraza la ardhi la wilaya.

Amewashukuru Madaktari wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga-Mwawaza kwa namna ambavyo wamefanya juhudi kuokoa maisha yake.

Ngasa ameiomba Serikali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama wamsaidie kulinda usalama wake na familia yake ambao uko hatarini, kwa kuwa matukio ya kushambuliwa na watu hao yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikiwemo tukio jingine la kukatwa panga kichwani na mkononi na kwamba, wamekuwa wakiapa kupoteza uhai wake ili wapate uhalali wa kumiliki mashamba hayo ambayo aliyanunua, licha ya kuwashinda kwenye vyombo vya sheria.

Amesema kwa sasa amefungua kesi nyingine ya shambulio alilofanyiwa na watu hao na watu hao na kuuguza majeraha kwa muda mrefu, lakini kabla haijaanza kusikilizwa wamemshambulia tena kwa mara ya nne.

Daktari bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Matinde Joseph Dotto, amesema walimpokea majeruhi kutoka katika Hospitali ya Kolandoto akiwa na hali mbaya, lakini baada ya kumfanyia upasuaji na kukitoa kitu alichochomwa kwenye ubavu wake wa kulia karibu na ini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa, mpaka sasa mtuhumiwa mmoja kati ya wanane wanaotafutwa amek**atwa na wengine saba wanaendelea kutafutwa.

WACHEZAJI WATATU WA SINGIDA BLACK STARS RAIA WA KIGENI WAPEWA URAIA WA TANZANIA.Idara ya uhamiaji imethibitisha taarifa ...
23/01/2025

WACHEZAJI WATATU WA SINGIDA BLACK STARS RAIA WA KIGENI WAPEWA URAIA WA TANZANIA.

Idara ya uhamiaji imethibitisha taarifa za wachezaji watatu wa klabu ya Singida Black Stars raia wa kigeni kupewa Uraia wa Tanzania.

1️⃣ Emmanuel Kwame Keyekeh raia wa Ghana
2️⃣ Josephat Arthur Bada kutoka Ivory Coast
3️⃣ Mohammed Damaro Camara kutoa Guinea

NECTA YATANGAZA MATOKEO KIDATO CHA NNE UFAULU WAZIDI KUPANDA.Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya ...
23/01/2025

NECTA YATANGAZA MATOKEO KIDATO CHA NNE UFAULU WAZIDI KUPANDA.

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne uliofanyika mwezi November 2024 ambapo jumla ya watahiniwa 477,226 wamefaulu kwa kupata daraja I - IV kati ya wanafunzi 516,695 walifanga mtihani huo.

Katibu mtendaji NECTA Dkt. Said Mohamed ametangaza matokeo hayo leo January 23 , 2025 Jijini Dar es Salaam ambapo amesema mwaka 2023 watahiniwa waliofaulu walikuwa 471,427 ambazo ni sawa na 89.36% ikiwa ufaulu umeongezeka kwa 3.01% na kwamba kati ya watahiniwa 477,262 waliofaulu wasichana ni 249,078 sawa na 91.72% ya wasichana wote wenye matokeo huku wavulana 228,184 sawa na 93.08% ya wavulana wote wenye matokeo.

Watahiniwa 15,703 wa kujitegemea wamefaulu mitihani hiyo sawa na 62.51% ambapo mwaka 2023 watahiniwa wa kujitegemea 13,396 waliofaulu mitihani yao ambayo ni sawa na asilimia 52.44% hivyo ufaulu wa watahiniwa wa kujitegemea umepanda kwa 10.07 % ikilinganishwa na mwaka 2023.

Address

Shinyanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio farajatz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio farajatz:

Videos

Share

Category