22/12/2024
MTWANGO KUNUFAIKA NA BARABARA ZA LAMI
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mh Edwini Enosy Swalle Amesema Tayari Ujenzi wa Barabara kwa Kiwango cha Lami yenye thamani ya zaidi shilingi bilioni moja Inayo fika Katika Kituo cha Afya Mtwango Umeanza Rasmi Huku Mkandarasi akiwa na Mkataba wa Miezi Sita ya Kuhakikisha Barabara Hiyo Inakuwa Imekamilika.
Swalle Amesema Hayo Mara Baada ya Kutembelea Mradi Huo na kuukagua akiwa ameongozana na Baadhi ya Viongozi Ili Kuona Maendeleo ya Mradi Huo Ambao Unatekelezwa Kwa Fedha za Mapato ya Ndani Huku Akiwataka Wananchi Kuwa na Subira Pindi Miradi Hiyo Inapo Tekelezwa Kwenye Maeneo Yao.
Aidha Amemuagiza Mkandarasi Aliye Pata Tenda Hiyo Kuhakikisha Barabaraba hiyo Inakuwa na Karavati za Uhakika Kutokana na Thamani ya Fedha Iliyo Tolewa na Serikali.
Kutokana na Hali Hiyo Kituo Hiki Kimezungumza na Mkandarasi Mzawa Aliye pata Tenda Hiyo ambapo Amekiri Kwenda Kufanya Kazi na Kukamilisha Barabara Hiyo Kwa Mujibu wa Mkataba.
Akiwa Katika ziara ya Kikazi Katika Kata ya Mtwango Moja ya Changamoto Ambazo Wananchi Waliomba Serikali zipatiwe Ufumbuni ni Pamoja na Miundombinu ya Barabara ikiwemo Barabara hii ya kuelekea kituo Cha afya cha kata ya Mtwango.