21/06/2023
⚠️"Nilikuwa naumwa sana, nililazwa Muhimbili kwa muda wa wiki mbili na nusu, Sikukuu ya Pasaka ilinikuta Muhimbili, Sikukuu ya Eid ilinikuta Muhimbili, Meimosi ilinikuta pale nikiwa nimelazwa na hata Birthday yangu ya mwaka huu ilinikuta kitandani, kwahiyo mwaka huu kwangu umekuja na mazonge k**a mwaka jana alipoondoka binti yangu 'Maunda Zoro'" - amesema Zahir Zoro msanii mkongwe wa muziki nchini na kuongeza
"Nilianza kuumwa ile siku aliyofariki Maunda, tarehe 13 April ndiyo nilianza kujisikia naumwa hadi baadae ambapo ilikuwa too much, nilikuwa natapika sana nyongo na uchafu mwingine, namshukuru Mungu, namshukuru Banana Zorro na Mwana FA ambao walipambana kwa kusimamia vipimo na gharama, wamenipigania sana kwasababu wakati nimelazwa Muhimbili nilikuwa siwezi kula nilikuwa naweza kula tu matunda k**a tikitimaji na juice kwa muda wa wiki mbili"
"Namkumbuka mwanangu kwa kila kitu, naweza nikawa naangalia movie kwenye simu au kwenye TV, nikiona mtu anambembeleza mtoto analia namkumbuka mwanangu Maunda Zorro kwasababu watoto wangu nimewalea mwenyewe tangu wakiwa wadogo sana, nimewalea mimi mwenyewe kwa mikono yangu na nilikuwa natoka jeshini nikiondoka nilikuwa nawafungia ndani kwenye chumba changu"
"Niliporudi kutoka hospitali nilikuta watoto wangu wametoa makochi yote sebreni, wamesafisha nyumba, naona walijua k**a nitakufa sitarudi, nilishtuka sana, sijui walifikiria nini ila nawashukuru kwa yote, tangu Maunda afariki nimesitisha kufanya kazi za muziki, nimejikita kwenye kumuombea dua, namuombea dua kila siku"- Zahir Zorro, baba mzazi wa wasanii Banana Zoro na Maunda Zoro