26/03/2022
Hifadhi ya Taifa Mikumi, ni moja ya hifadhi kubwa na mashuhuri nchini. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapakana na hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinashamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mraba 3,230 na ipo umbali wa kilomita 283 magharibi mwa Dar es Salaam.
Aidha hifadhi hii iko kaskazini mwa mbuga ya Selous na iko njiani unapoelekea au kutoka hifadhi za Udzungwa na Ruaha.
Unaweza kuunganisha safari ya hifadhi hii pamoja na hifadhi za Udzungwa, Selous na Ruaha kwa barabara kutoka Dar es Salaam. Hifadhi hufikika pia kwa ndege za kukodi kutoka Dar es salaam, Arusha na Selous.
Sehemu za malazi ni pamoja na hoteli za kitalii, nyumba za wageni hifadhini na maeneo ya kupiga makambi/mahema.
KARIBU MIKUMI, FAHARI YA TANZANIA
Credit: Mikumi National Park
Credit: Tanzania Tourism
Application