Maneno mazito kutoka kwa Dada wa Taifa @thea_tanzania. Sikiliza mpaka mwisho.
Tanzania ni Nchi ambayo ukipata Stress umetaka wewe na sio vinginevyo!!
Majina mapya
Emmanuel Keyeke 'NTANDU"
Mohamed Cumaro "HANGO"
Josephate BADA "KINGU"
NB..... Hata waitwe kina MAKOYE bado hayavutii😁
FT | Tabora United 0 - 3 Simba SC
Kwa ushindi huu tumpe Simba SC kombe mapema au bado.?
YANGA KILELENI BAADA YA USHINDI WA LEO | NANI WA KUMSHUSHA?
Yanga wamerudi kwa kishindo kwenye ligi kuu baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Yanga chini ya Kocha Mjerumani Sead Ramovic imeingia kwa nguvu sana katika mechi hiyo katika uwanja wa KMC ambao ni uwanja wa nyumbani wa Yanga.
Kagera Sugar wameonekana kukosa utulivu toka mechi inaanza. Wamekuwa na makosa mengi kuanza beki, viungo na washambuliaji.
Kagera Sukari wamekosa utulivu wakiwa na mpira kitendo ambacho kimewapa Yanga uzuri wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.
Kidogo Yanga wamerudishwa ile kujiamini ingawa Master Azizi Ki yeye bado ana ugomvi na penalty maana leo amepoteza penalti ya pili.
Kwa matokeo ya leo, Yanga anakalia usukani wa ligi kwa kufikisha pointi 42 huku hasimu wake Simba SC wakitarajia kucheza kesho Jumapili uwanja wa Ally Hassan Mwinyi dhidi ya Tabora United.
Nb... Kafungwa Kagera Sugar ila vilio vinasikika msimbazi😁
Huyu ndio @goodluckgozbert mdogo wangu ninayemfahamu....
Mwanamuziki John Lennon aliamua kumuacha mke wake Cynthia na kwenda kuanzisha mahusiano mapya na Yoko Ono ambae ni msanii mkubwa mwenye asili ya Japan mwaka 1966, na kweli mwaka 1969 akamuoa Yoko Ono.
Mke wake Cynthia alibaki na mtoto wao wa kiume mwenye miaka mi 5 tu anaeitwa Julian Lennon (ambae ni mwanamuziki mkubwa kwa sasa na Baba yake baada ya kuuwawa 1980 ilikua hajamuweka Julian kwenye wosia wa urithi, yani hakurithishwa chochote) lakini tuachane na hilo ni stori nyingine.
Basi Cynthia alibaki na mtoto wake Julian na maisha yakawa magumu sana kwa upande wake akafikiria nini afanye? Akaamua aziuze kumbukumbu zake zote za mapenzi ya miaka mingi tangu utoto (teens) na John Lennon ambae alikua ni msanii mkubwa wakati huo, akauza barua zote za mapenzi na michoro waliyokua wanapeana kabla hajaachwa na John Lennon.
Barua zilizokua zimebeba ujumbe wa hisia kama "Nakupenda Cynthia" fikiria ni maumivu kiasi gani Cynthia kubaki na barua zenye kumbukumbu kama hizi, Cynthia alifanikiwa kuziuza kumbukumbu hizo kwa gharama kubwa kwakua Ex-husband wake alikua ni msanii mkubwa.
Lakini baada ya muda Cynthia alishangaa ametumiwa zawadi kupitia mail alipopokea zawadi hizo zilikua zimetoka kwa Paul McCartney ambae ni msanii mkubwa rafiki wa mume wake waliekua wanaimba wote kwenye bendi moja na alipofungua ndani kuangalia zawadi hizo alikuta ni zile barua zake za kumbukumbu alizoziuza na zilikuja na karatasi ya ujumbe kutoka kwa McCartney aliyokua ameandika "Daima usiuze kumbukumbu zako"
Hivyo ndivyo ilivyo Kumbukumbu zote zinafaa kutunzwa kwa matumizi ya baadae iwe mbaya au nzuri, kama ni nzuri zitunze kama kielelezo cha furaha na kama ni mbaya zitunze kama funzo. Hii ni entertainment plus education.
Hawa ndio MTIBWA SUGAR... wanataka kurudi Ligi Kuu NBC. Weka mbali na watoto.
Ahmed Ally @ahmedally_ mbona ulifurahi sana hapa!! Au ndio Ubaya Ubwela.
Mkutano Mkubwa wa Injili Mwanza, CCM Kirumba 24-28 Julai 2024 kuanzia saa 2 asubuhi hadi 11 jioni.
Ni Pasta Ezekiel kutoka Kenya ambaye Bwana anamtumia kwa ishara na miujiza mikubwa atahubiri na kufanya maombi na maombezi kwa wagonjwa na wote wenye shida mbalimbali.
Njoo upokeee muujiza wako kutoka kwa Mungu Mtenda miujiza.
0717583492
0785514127
Khalid Aucho amempiga kiviko Ibrahim Ajibu kwenye mechi ya NBC Premier League baina Coastal Union vs Yanga. Mwamuzi Emmanuel Mwandembwa amempa Aucho kadi ya njano kutokana na mchezo usio wa kiungwana.
Kitendo kama hiki kwenye mechi huwa kikitokea mwamuzi anatakiwa atoe kadi ya njano au kadi nyekundu au atoe msamaha? Karibu tuyajenge.
#NBCPL Namba 10
Analysed by @sistiinho
Kwenye #MzizimaDerby leo nimeondoka na Perfomance bora ya namba 10 wa pande zote;
- Stephanie Aziz Ki (Yanga Sc)
- Feisal Salum (Azam Fc)
🔥 Kwenye STRUCTURE za timu zao walitumikia nafasi zinazofanana
• Aziz kwenye 4-2-3-1 ya Yanga alicheza;
- Mbele ya viungo wawili wa kati, Aucho na Mudathir (double Pivot)
- Katikati ya viungo wawili wa pembeni, Pacome na Max
- Nyuma ya Mzize (Zone 14)
• Feisal kwenye 4-2-3-1 ya Azam alicheza;
- Mbele ya viungo wawili wakati, Bajana na Akamiko (double pivot)
- Katikati ya viungo washambuliaji wa pembeni, Sillah na Sopu
- Nyuma ya Dube (zone 14)
🔥 Wote kwa pamoja walifanya MAJUKUMU yanayofanana kiuchezaji uwanjani
👉 Majukumu ya Aziz Ki
• Yanga ikishambulia
- Alikuwa anaji-position nyuma ya viungo wa Azam, Akamiko na Bajana
- Pia kuna nyakati Azam walikuwa wakitengeneza rest defence ya 2+3, mabeki wao wawili wa pembeni huingia ndani kuungana na Bajana mbele ya mabeki wawili wa kati, Ki Aziz alikuwakukabana nao
- Alikuwa na jukumu la kusaidia timu kupenya
• Yanga ikizuia
- Wakianza kuzuia kuanzia mbele na muundo wa 4-2-3-1, Aziz Ki huwa kwenye mstari wa pili wa uzuiaji nyuma ya mshambuliaji, dhidi ya kiungo wa chini wa Azam
- Kama Azam wakijenga shambulizi na viungo wawili wa chini Mudathir husaidia kuongengezeka usawa wa Ki (4-1-4-1)
- Yanga wakizuia kwenye nusu yao, Ki huungana na Mzize kwenye mstari wa kwanza wa uzuiaji (4-4-2 low & mid block)
👉 Majumukumu ya Feisal
• Azam ikishambulia
- Anaji-position nyuma ya viungo wa Yanga, dhidi ya Aucho na Muda
- Pia kuna nyakati Yanga walikuwa wakitengeneza rest defence ya 2+1, Muda husogea mbele, Lomalisa na Job hupanda, Fei alikuwa dhidi ya Aucho mbele ya CB's
- Alikuwa na jukumu la kusaidia timu kupenya
• Azam ikizuia
- Wakianza kuzuia kuanzia mbele na muundo wa 4-2-3-1, Fei huwa kwenye mstari wa pili wa uzuiaji nyuma ya mshambuliaji, dhidi ya kiungo wa chini wa Yanga
- Azam ikizuia kwenye nusu yao muundo huwa
Mwamba huyu hapaaaa.....Anapasuka mweupe mweupe.....