07/01/2026
Anaandika Dkt, Sebastian Ndege
“Kila ninaporudi katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Dkt, Chacha (CF), hukumbushwa kwa nini tiba siyo tu taaluma, bali ni wito wa maisha. Kuwepo hapa kunanirudisha kwenye kumbukumbu za thamani za rafiki yangu wa karibu na mlezi wangu, marehemu Dkt. Emmanuel Chacha (RIP).
Alikuwa akinisisitizia mara kwa mara umuhimu wa kujiendeleza kielimu, kuwa na nidhamu, na kubaki mwaminifu kwa maadili ya taaluma ya tiba.
Leo, naenzi urithi wake kwa kuendelea kujifunza, kuboresha ujuzi wangu, huku nikiendelea na majukumu yangu mengine mbalimbali, na kutoa huduma kwa ubora wa hali ya juu.
Natoa shukrani zangu za dhati kwa Dkt. Frank kwa kunipa fursa ya kurejea na kuimarisha zaidi utendaji wangu wa kitabibu.
Mwenye shukrani Daima. Nimejitoa Daima. 🩺🙏chacha.memorial.hospital_