05/03/2024
π ππππ π πͺπ π¦π’ππ ππ π§ππ‘πππ‘ππ β Young Africans Sports Club
Popote ulipo mwananchi Yanga unakila sababu ya kujivunia historia nzuri ya timu yako kuwa ni moja ya timu bora ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kwa mafanikio ambayo Yanga wanajivunia.Chukua haya madini ambayo ulikuwa hujui kuhusu Yanga kimataifa..
Mnamo Mwaka 1968 Yanga ndio walikuwa Mabingwa wa Ligi kuu ndio timu ya kwanza kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye mashindano ya klabu bingwa barani afrika 1969.Katika kuhakikisha wanafanya vyema kwenye mashindano haya ya klabu bingwa Afrika.Yanga walienda nchini Romania kufanya pre season ya mwezi mzima kitu kilichowafanya kufanya vizuri sana kwenye mashindano
Hatua ya awali.
Yanga walikutana na FITARIKANDRO ya Madagascar Yanga walishinda 4-0 na marudiano yanga wakafungwa 2-0 kuendelea
Raundi ya kwanza.Yanga walikutana na SAINT GEORGE ya Ethiopia wakatoka 0-0 mechi ya kwanza na mechi ya pili wakaipiga bila huruma saint george 5-0 na kuingia robo fainali moja kwa moja.
Hapa Yanga ikawa timu ya kwanza nchini Tanzania kuingia Robo fainaliβ
π₯π’ππ’ ππππ‘πππ 1969
Yanga walianzia nyumbani na kukutana na Asante Kotoko kutoka nchini Ghana na wakatoka sare 1-1 Katika mechi zote mbili yaani Home and Away hatimaye ikaamuliwa irushwe shilingi ili iamue nani aende nusu fainali.
Makapteni wote wawili wakishuhudia shilingi ikarushwa hata hivyo kapteni wa Asante kotoko alifanya udanganyifu kwani kabla shilingi haijatua alijifanya kushangilia na kumfanya kapteni wa Yanga Abdulrahaman kuamini kuwa shilingi imeangukia upande wake.Ndipo Yanga ikadhulumiwa nafasi ya kuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainal
KITWANA MANARA β½ akaingia kwenye orordha ya wafungaji bora akiwa mfungaji bora namba tisa mwenye magoli mawili.
π¨1970
Timu ya Wananchi Yanga ikafuzu tena kwa Mara nyingine kuiwakilisha nchini kimataifa na safari hii wakakutana tena na Mabingwa kutoka nchini Ghana Asante Kotoko Katika hatua ya robo fainali.Yanga walianza kutupa karata Yao nyumbani dhidi ya Asante Kotoko na kulazimishwa sare ya goli 1-1.Na mchezo wa raundi ya Pili uliochezwa nchini Ghana Kumasi mechi ikaisha tena kwa sare ya 1-1 mchezo ambao ulilazimika kuisha kabla ya muda wa dakika 9 kutokana na vurugu ndipo mchezo ukapelekewa Addis Ababa na Yanga wakapoteza kwa magoli 2-0 na kutupwa nje ya mashindano.
π¨1998
Timu ya Wananchi Yanga ikafuzu tena kwa mara nyingine kucheza hatua ya robo fainali na safari hii wakakutana na mabingwa kutoka nchini Ivory coast ASEC Mimosas.Yanga walianzia nyumbani mchezo wake wa kwanza wa Robo ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi B dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Novemba 8, mwaka 1998 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam uliomalizika kwa wageni kushinda 3-0.
π¨2024
Huu ndio mwaka ambao vijana wengi wameibuka na kutojua historia ya Yanga kwenye mashindano haya ya kimataifa baada ya Yanga kufuzu kwenda robo fainali mbele ya waarabu wawili ambao walikuwa kwenye kundi moja Yaani Al Ahly SC na CR Belouizdad
; KWENYE MASHINDANO YA CAF CONFEDERATION CUP YANGA IMEFUZU KUCHEZA HATUA YA MAKUNDI MARA TATU.
π¨2015,,,,π¨2018
π¨2023 Yanga ilifanikiwa kucheza fainali mashindano ya Caf Confederation Cup na Usm Alger ya nchini Algeria.Na kupoteza fainali kwa matokeo ya jumla ya goli 2-2 na Usm Alger kupata faida ya goli la ugenini.
π¬ππ‘ππ ππ ππ§π’π πͺπππ¨π‘ππππ ππ’π₯π ππͺππ‘π¬π π ππ¦πππ‘πππ‘π’ π¬π πππ.
π¨πππ ππππ π£ππ’π‘ πππππ¨π.MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuwa mfungaji bora wa michuano ya Afrika, baada ya kumaliza na mabao sita katika Ligi ya Mabingwa Afrka, ingawa timu yake haikufika hatua ya makundi.
Ngassa amefungana na Haythem Jouini wa Esperance ya Tunisia, Firmin Ndombe Mubele wa AS Vita ra DRC iliyofika fainali na El Hedi Belameiri wa Es Setif iliyoibuka bingwa kwa kufunga mabao sita kila mmoja.
Ngassa aliifungia Yanga SC mabao yote hayo katika hatua ya awali dhidi ya Komorozine ya Comoro kabla ya kutolewa na Ahly ya Misri katika hatua iliyofuata. Ahly nayo ilitolewa pia na kuangukia kwenye Kombe la Shiriksho, ambako ilifika Fainali.
π¨πππ ππ’π‘πππππ₯ππ§ππ’π‘ ππ¨π£: Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele aliibuka mfungaji bora wamashindano ya Caf confederation cup mwaka 2023.
NB;Yanga ndio timu ya kwanza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za CAF.Yanga waliteuliwa kugombania
-TUZO YA KLABU BORA YA MWAKA CAF (Waliishia 5 Bora)
-GOLIKIPA BORA WA CAF(Djigui Diarra)
-MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA(Fiston Kalala Mayele)
K**a Kuna timu inarekodi K**a hii Tz nitagβ