Sanuka Sports News

Sanuka Sports News Habari zote za michezo ulimwenguni utazipata hapa...

-Tanzania 🇹🇿

Call : +255622147696
(3)

🚨 :-Napenda kuomba radhi kwa familia nzima ya Simba Sc kwa kuwagharimu sana kwenye mechi mbili. Nawajibika kikamilifu kw...
13/01/2025

🚨 :-Napenda kuomba radhi kwa familia nzima ya Simba Sc kwa kuwagharimu sana kwenye mechi mbili. Nawajibika kikamilifu kwa makosa yangu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kufanya vizuri zaidi katika siku zijazo.

Samahani sana, Asante Simba,
Asanteni mashabiki kwa kunitia moyo kila mara licha ya kuwakatishwa tamaa.”

- Beki wa Simba SC, CHE MALONE FONDOH kwenye ukurasa wake wa Instagram.

🚨 :- Tumepoteza mchezo wetu wa kwanza kwenye mashindano haya ya CAF tumehuzunika sana kwasababu tulihitaji kushinda laki...
13/01/2025

🚨 :- Tumepoteza mchezo wetu wa kwanza kwenye mashindano haya ya CAF tumehuzunika sana kwasababu tulihitaji kushinda lakini mchezo wa mpira umeamua tofauti"

"Tulipoteza umakini kwenye mchezo na kupoteza nafasi nyingi za kufunga magoli lakini tunajipanga upya kushinda dhidi ya mchezo wetu na Tp Mazembe " Alisema kocha wa Al Hilal baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga"

🚨 :- Nyota wa kimataifa wa Burundi,Shassir Nahimana amejiunga na klabu ya Pamba Jiji ya mkoani Mwanza akitokea Bandari F...
13/01/2025

🚨 :- Nyota wa kimataifa wa Burundi,Shassir Nahimana amejiunga na klabu ya Pamba Jiji ya mkoani Mwanza akitokea Bandari FC ya Kenya.

Pamba wanaendelea kujiimarisha kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

🚨 :- Kitendo cha klabu ya AS Vita ya DR Congo kumnyemelea mchezaji Gibril Sillah, kimewafanya mabosi wa Azam FC kuwa na ...
13/01/2025

🚨 :- Kitendo cha klabu ya AS Vita ya DR Congo kumnyemelea mchezaji Gibril Sillah, kimewafanya mabosi wa Azam FC kuwa na haraka ya kumwandalia ofa ya mkataba mpya nyota huyo kutoka Gambia, ambaye mkataba wake na timu hiyo ya Chamazi utamalizika mwishoni mwa msimu huu, Juni 2025.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, inaelezwa kuwa kocha wa zamani wa Azam, Youssouph Dabo, ambaye sasa anainoa AS Vita, amependekeza kusajiliwa kwa Sillah, ambaye msimu wa 2023/24 alifunga mabao manane kwenye Ligi Kuu ya Tanzania akiwa na timu hiyo.

Sillah, ambaye anajulikana kwa kasi na uwezo mkubwa wa kiufundi, msimu huu amefunga mabao matatu na ameendelea kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha wa sasa wa Azam, Rachid Taoussi ambacho kinaendelea kujifua kwa ajili ya duru la pili la Ligi Kuu tangu Januari 6 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa Azam inataka kumfunga kwa mkataba mpya Sillah mapema ili kumzuia kujiunga na AS Vita au klabu nyingine yoyote kubwa inayomhitaji.

🚨 :- Katika malengo yetu msimu huu moja ni hilo la kubeba ubingwa wa Afrika na naamini kwa uwezo wa timu yetu, kwa nguvu...
12/01/2025

🚨 :- Katika malengo yetu msimu huu moja ni hilo la kubeba ubingwa wa Afrika na naamini kwa uwezo wa timu yetu, kwa nguvu ya timu yetu saivi na upambanaji wa wachezaji wenzangu mwanga upo wa kuona tunaweza kuchukua ubingwa wa CAF."

"Kwa Simba SC hatuna mechi ya nyumbani wala ugenini mechi zote tunahakikisha tunaweza kupata matokeo mazuri iwe sare au kushinda."

KIBU DENIS,Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Simba.

🚨 :- Nikiwa shabiki wa Simba Sports Club mimi nayajua maumivu ya mashabiki tunapopoteza.Nina nafasi ya kufanya mabadilik...
12/01/2025

🚨 :- Nikiwa shabiki wa Simba Sports Club mimi nayajua maumivu ya mashabiki tunapopoteza.

Nina nafasi ya kufanya mabadiliko ambayo yataleta matokeo chanya na lengo langu kuu ni kurejesha mataji yote msimbazi."

- Zubeda Sakuru
CEO Simba.
....

"As a Simba Sports Club fan, I know the pain of the fans when we lose.

I have the opportunity to make changes that will bring positive results and my main goal is to restore all the titles to the club."

Simba SC club CEO Zubeda Sakuru.

🚨 :- Leo tunakibarua kigumu sana, tena kizito haswa tumeingia kwenye kichaka cha Bravos na lengo letu ni kuteketeza kich...
12/01/2025

🚨 :- Leo tunakibarua kigumu sana, tena kizito haswa tumeingia kwenye kichaka cha Bravos na lengo letu ni kuteketeza kichaka hicho."

"Bravos ni mpinzani ambae amewekeza kila kitu kwenye mechi zake za nyumbani ndio maana haishangazi kuona hajapoteza hata mechi moja akiwa hapa Angola."

"Simba tunataka kumlazimisha Bravoz apate kitu kipya kwenye Uwanja wake wa nyumbani yaani kufungwa au kupata sare."

"Hatokubali na haitakua rahisi…
Hapo sasa ndio tunatakiwa kuonesha Usimba wetu, Tunatakiwa kumlazimisha, kumpelekea pumzi ya moto mpaka achanganyikiwe na atupe matokeo tunayotaka sisi."

"Inawezekana wana Simba twendeni kwenye mapambano.. l"

Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC.

📍Huu ni uwañja mpya wa timu ya Everton 🔥🔥Huu uwànja umejengwa kwenye mitaa ya Merseyside Huko Liverpool Everton wataanza...
12/01/2025

📍Huu ni uwañja mpya wa timu ya Everton 🔥🔥

Huu uwànja umejengwa kwenye mitaa ya Merseyside Huko Liverpool

Everton wataanza kuutumia huu uwànja wao mpya Msimu wa 2025/26

ila Msimu huu wa 2024/25 watamalizia kwenye uwanja wao wanaoutumia sasa ( Goodison park )

Uwanja wao mpya unaitwa Everton stadium Bramley moore park unabeba watu 52,088 ...utakuwa ni miongoni mwa viwanja 6 vikubwa pale England

Uwanja wao umejengwa Kwa gharama ya pound million 800

Uwanja wao upo pembezoni mwa bahari huko jijini Liverpool

🚨 :- Klabu ya Fountain Gate FC imetuma barua kwenda klabu ya Simba SC ili kupata saini ya beki wa kati Hussein Kazi kati...
11/01/2025

🚨 :- Klabu ya Fountain Gate FC imetuma barua kwenda klabu ya Simba SC ili kupata saini ya beki wa kati Hussein Kazi katika dirisha hili dogo la uhamisho

Fountain Gate FC inaungana na Namungo FC katika mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo kwa uhamisho wa mkopo.
....

- Fountain Gate FC have sent a letter to Simba SC to secure the signature of centre-back Hussein Kazi in this limited transfer window

🚨 :- Kabla David Beckham hajamuoa Victoria, siku moja Victoria alirudi kwa Beckham akiwa analia na anaomba waachane, Bec...
11/01/2025

🚨 :- Kabla David Beckham hajamuoa Victoria, siku moja Victoria alirudi kwa Beckham akiwa analia na anaomba waachane, Beckham alijitahidi kuongea nae lakini hakufanikiwa, Beckham alishangaa tatizo ni nini? Mbona hajakosea chochote na anamuonyesha mapenzi makubwa lakini Victoria anataka waachane?

Beckham alijipa muda mambo yatulie kwanza na baadae alimtafuta Victoria ili amuulize tatizo ni nini au kuna kitu kamkosea? Kweli walikutana na Victoria akamueleza Beckham kuwa hakuna chochote alichomkosea ila alienda kwa daktari na akagundulika ni Infertility yani hana uwezo wa kubeba mimba hivyo akamuomba Bekham atafute mwanamke mwingine.

Licha ya kuelezwa hivyo lakini David Beckham hakujali alipiga goti moja na akamuomba Victoria amkubalie kuwa mke wake, Victoria alishindwa kuzuia machozi yake na akakubali ombi la David Beckham kweli jamaa alimuoa kisha miujiza ya kweli ikatokea licha ya kuwa Doctor alitabiri kuwa Victoria hana uwezo wa kubeba mimba lakini Victoria alipata mimba na wakapata mtoto wao wa kwanza wakamuita Brooklyn.

Wakawa na furaha isiyo na mipaka na leo hii wana watoto wanne, siku moja Beckham alihojiwa kuhusiana na mapito haya na akajibu kwa kusema "K**a ningeondoa mapenzi yangu kwa mwanamke niliempenda wakati wa matatizo, ningepoteza amani ya moyo wangu"

Ni miaka 25 imepita tangu waoane na bado wapo pamoja, siku zote upendo wa kweli huwa unashinda wakati wa matatizo.

🚨 :- Vyanzo mbalimbali kutoka Afrika Kusini vimeripoti kuwa klabu ya Azam FC ilipokea na kuikataa ofa ya R8 million (Tsh...
11/01/2025

🚨 :- Vyanzo mbalimbali kutoka Afrika Kusini vimeripoti kuwa klabu ya Azam FC ilipokea na kuikataa ofa ya R8 million (Tshs Bilioni 1) kutoka Kaizer Chiefs 🇿🇦 wakihitaji saini ya Kiungo Feisal Salum

Azam FC wanahitaji Tshs Bilioni 5 ili kumuachia Kiungo Feitoto na bado wanaproject ya muda mrefu na mpaka sasa Azam FC imeshampa ofa kiungo huyo ya kuongeza mkataba mpya licha ya kubakiwa na mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
...

- Various sources from South Africa have reported that Azam FC received and rejected an R8 million (Tshs 1 billion) offer from Kaizer Chiefs 🇿🇦 for the signature of midfielder Feisal Salum

🚨 :- “Azma yetu ni kwenda robo fainali na tutashinda kila mechi, tutafuzu hapa hapa kwa Mkapa. Tufikishieni salamu kwa M...
11/01/2025

🚨 :- “Azma yetu ni kwenda robo fainali na tutashinda kila mechi, tutafuzu hapa hapa kwa Mkapa. Tufikishieni salamu kwa Mh. Rais.”

Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga SC.
...

“Our goal is to go to the quarter-finals and we will win every match, we will qualify right here in Mkapa. Please convey our greetings to the Hon. President.”

Eng. Hersi Said, President of Yanga SC.

🚨 :- Kushinda kwa MC Alger jana dhidi ya TP Mazembe kunaifanya mechi ya kesho ya Al Hilal na Yanga kuwa ngumu na klabu y...
11/01/2025

🚨 :- Kushinda kwa MC Alger jana dhidi ya TP Mazembe kunaifanya mechi ya kesho ya Al Hilal na Yanga kuwa ngumu na klabu ya Yanga inatakiwa kushinda mchezo wa kesho ili kuwa na asilimia kubwa ya kufuzu robo fainali

-Iwapo Yanga itafungwa kesho itakuwa imeshindwa kufuzu robo fainali na iwapo itatoa sare yoyote italazimika kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya MC Alger kwa tofauti ya magoli 2+.

🚨 :- Simba SC wapo katika mazungumzo ya mwisho na Coastal Union kwaajili ya kukamilisha uhamisho wa mlinzi wa kati  Lame...
10/01/2025

🚨 :- Simba SC wapo katika mazungumzo ya mwisho na Coastal Union kwaajili ya kukamilisha uhamisho wa mlinzi wa kati Lameck Lawi

According to baada ya dirisha dogo kufunguliwa, Yanga Sc walimpatia kiasi cha milioni 150Tsh kuihitaji huduma ya Mtanzania huyo kwa kufanya naye mazungumzo binafsi jambo ambalo liliisukuma Simba SC kwenda kuweka pingamizi kwenye k**ati ya sheria na hadhi za wachezaji iliyopo chini ya TFF.

K**ati hiyo ilitoa maamuzi kwa kuzitaka pande zote tatu kukaa Pamoja na kupata suluhisho juu ya nyota huyo na mpaka sasa Simba SC imepeleka ofa ya milioni 205 kwa Coastal Union kwa upande wa Yanga SC bado hawajapeleka ofa yeyote kwa wagosi wa kaya.

🚨 :- Huu sio mchezo muhimu kwetu,ni mchezo muhimu zaidi kwa wapinzani wetu ndio maana utakuwa mchezo mgumu,sisi tunafura...
10/01/2025

🚨 :- Huu sio mchezo muhimu kwetu,ni mchezo muhimu zaidi kwa wapinzani wetu ndio maana utakuwa mchezo mgumu,sisi tunafurahi kuona tulitumia nguvu kubwa katika michezo ya mwanzo ambayo imepelekea kufuzu mapema."

"Niwapongeze wachezaji wangu kwa kazi ngumu na kubwa waliyotumia katika michezo ya mwanzo naamini tulitumia nguvu na presha kubwa tofauti na michezo tunayoenda kucheza sasa haitakuwa na presha kubwa kwetu bali ni kwa wapinzani wetu."

"Michezo ya Ligi ya Mabingwa mara zote huwa ni migumu na k**a unapata matokeo basi unakuwa katika katika nafasi nzuri ya kufanikiwa."

Florent Ibenge, Kocha Mkuu wa Al Hilal Omdurman

🚨UPDATES:- “Sasa hivi Yanga anahitaji alama 6 kwenye mechi mbili zilizobaki, unajua unavyoijadili Yanga na michuano anay...
10/01/2025

🚨UPDATES:- “Sasa hivi Yanga anahitaji alama 6 kwenye mechi mbili zilizobaki, unajua unavyoijadili Yanga na michuano anayocheza ni tofauti na utakavyoijadili Simba kwa sababu ni michuano miwili tofauti yenye quality (ubora) tofauti”

Farhan Jr.

"Now Yanga needs 6 points in the remaining two matches, you know how you discuss Yanga and the tournament they play is different from how you discuss Simba because they are two different tournaments with different qualifications."

Farahan Kihamu Jr

🚨 :- Winga wa zamani wa klabu ya Yanga SC Skudu Mahlatse Makudubela amejiunga na klabu ya As Vita Club ya nchini Congo D...
09/01/2025

🚨 :- Winga wa zamani wa klabu ya Yanga SC Skudu Mahlatse Makudubela amejiunga na klabu ya As Vita Club ya nchini Congo DRC
.....

- Former Yanga SC winger Skudu Mahlatse Makudubela has joined As Vita Club in Congo DRC.

🚨 UPDATES:- Simba SC imefunga bao kila mchezo wa CAFCC kwenye hatua ya makundi msimu...haijawahi kumaliza dakika 90 bila...
09/01/2025

🚨 UPDATES:- Simba SC imefunga bao kila mchezo wa CAFCC kwenye hatua ya makundi msimu...haijawahi kumaliza dakika 90 bila bao.

Simba imepata clean sheet mbili katika mechi 4 ilizocheza na imefunga jumla ya mabao 5 na kufungwa mabao matatu.

Bravos de Maquis ameruhusu bao kila mechi aliyoingia uwanjani..Amefungwa jumla ya mabao (9) na kufunga mabao manne (4)

Simba akiwa ugenini amefunga jumla ya mabao mawili na kuruhusu mabao mawili kwenye mechi mbili.

Bravos do Maquis akiwa nyumbani amefunga mabao 6 na kufungwa mabao manne kwenye mechi mbili alizocheza.

Address

Mgulasi
Morogoro

Telephone

+255676440118

Website

http://News.com/

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sanuka Sports News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share