Mlimba tv

Mlimba tv MLIMBA TV ni tv ya mitandao ya kutoa habari na matukio kokote duniani tell the most difficult stories. Join us!

For more breaking news updates follow ,mlimba tv,


MAWASILIANO 0684495100, [email protected],

20/10/2024
14/10/2024

KUMBUKIZI YA NYERERE.

DC KILOMBERO AONGOZAMATEMBEZI MAALUM YA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA.Wananchi  mbali...
12/10/2024

DC KILOMBERO AONGOZAMATEMBEZI MAALUM YA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA.

Wananchi mbalimbali wa Halmashauri ya Mji Ifakara leo Jumamosi tarehe 12 Oktoba , 2024 wamejitokeza kushiriki Matembezi maalum kwaajili ya kuhamasisha Wananchi kushiriki Kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura.

Matembezi hayo yaliongozwa na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Mji ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya , Mbunge wa Kilombero Mhe. Abubakari Asenga na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi . Zahara Michuzi ambapo matembezi hayo yalianzia Round about ya Kibaoni hadi Viwanja vya Asante Afrika Lumemo.

Akizungumza wakati wa Matembezi hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya aliwasihi Wananchi hao kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura kwenye Mitaa na Vitongoji vyao Ili waweze kuchagua au kugombea nafasi za Uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba ,2024.

" Niwasihi Wananchi wote ambao bado hamjajiandikisha , zoezi hili limeanza tangu tarehe 11 Oktoba ,2024 na litakamilika tarehe 20 , Oktoba ,2024 hivyo ukishindwa kujiandikisha katika tarehe hizo hutakua na sifa za kushiriki Uchanguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Oktoba ,2024". Alisema Mhe. Wakili Kyobya

Nae Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Abubakari Asenga aliwasisitiza wananchi wote kuendelea kuhamasishana kushiriki Uchaguzi huo kwani ni haki ya kila mwananchi mwenye sifa .

" Niwaombe mtu yoyote ambaye ana umri wa miaka 18 au zaidi akajiandikishe kwenye Daftari la Mpiga kura Ili aweze kuchagua au kuchaguliwa" . Alisema Mhe. Asenga

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Zahara Michuzi aliwataka Wananchi hao kuendelea kudumisha amani katika kipindi chote cha kujiandikisha na hata itakapofika siku ya uchaguzi.

" Tuendelee kudumisha amani na utulivu tulionao, uchaguzi huu uende kwa amani na haki ,mtuletee viongozi watakao kuwa rahisi kuwafikia mnapowahitaji, viongozi ambao hawahamasishi vurugu". Alisisitiza Bi. Zahara

@ .kilombero

https://www.instagram.com/p/DBBmr3_MHhq/?igsh=MTh2dGUwNjJ4OHp1dQ==

28/09/2024

sangula bonde la kilombero .

28/09/2024

lizombe

24/09/2024
BASHE ATOA BEI ELEKEZI YA MAHINDI RUVUMAWaziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametangaza bei elekezi ya kununua mahindi Mkoani...
24/09/2024

BASHE ATOA BEI ELEKEZI YA MAHINDI RUVUMA

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametangaza bei elekezi ya kununua mahindi Mkoani Ruvuma, kuwa kilo moja ya mahindi itauzwa kwa bei isiyo pungua shilingi 550 kwa kilo moja.
Waziri Bashe amesema hayo alipokuwa anazungumza na maafisa kilimo, wafanya biashara ya mazao,mbegu na mbolea, maafisa ugani na wadau wengine wa kilimo; wilayani Songea.

Katika mkutano huo, Waziri Bashe alisisitiza umuhimu wa kufuata bei elekezi na kwamba wataalamu wa wizara watapita vijijini na wilayani kusajili mawakala ili kuhakikisha biashara ya mahindi inafanyika kwa ufanisi.

Waziri Bashe alisisitiza kuwa serikali inapotoa bei elekezi, inazingatia uhalisia wa soko, gharama za uzalishaji na gharama nyinginezo.

Aliongeza kuwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi wanaotaka kununua mazao lazima wapitie kwa wafanyabiashara wa ndani.

"Tenengenezeni umoja wenu wenye nguvu na serikali ipo tayari kufanya kazi na nyie,”alisema Bashe.

Alifafanua kuwa wafanyabiashara wanaonunua mahindi kwa niaba ya WFP walikuwa wakinunua kwa bei ya Shilingi 400 kwa kilo wakati serikali ilikuwa ikinunua kwa Shilingi 1000, lengo likiwa kuwasaidia wakulima kwa kupandisha bei ya ununuzi wa mahindi.

“Serikali imetoa muongozo kuwa itaendelea kununua mahindi mpaka yaishe na vituo havitafungwa,”.

“Pia Mahindi ambayo ni mabovu yaliyokuwa yakitupwa yatatumika k**a chakula cha mifugo.,”alisema.

Aidha serikali itatoa kibali kwa wafanyabiashara watakaokuwa tayari kujenga maghala ya kuhifadhia chakula.

Waziri Bashe alieleza kuwa mkakati wa kuboresha mifumo ya utoaji wa mbolea na mbegu unaendelea na mifumo hiyo itasimamiwa kikamilifu ili kuvutia wauzaji na wanunuzi.

Alisemaa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewekeza zaidi katika kilimo ikilinganishwa na awamu zilizopita, ikiwemo kuajiri wataalamu, ununuzi wa vifaa, na ujenzi wa miundombinu. Alisema serikali itaendelea kukabiliana na changamoto kadiri zitakavyojitokeza.

Kwa upande wa viwatilifu, Waziri Bashe alieleza kuwa kila aina ya kiuatilifu kitakachouzwa kwa mkulima kiwekewe alama ili serikali iweze kufuatilia changamoto zitakazojitokeza.

Aliongeza kuwa mamlaka husika zifanye uchunguzi na ufuatiliaji wa viuatilifu vinavyoingia kutoka nchi jirani ili kuthibiti ubora wake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea, William Ndile, ameomba wizara kutekeleza mpango wa kituo cha ambacho kitawakutanisha wataalam wa kilimo katika eneo moja, ili kuepusha adha kwa wakulima na kurahisisha utekelezaji wa mipango, malengo, sheria, kanuni na taratibu za wizara hiyo.

Mwisho

*WANANCHI WAFURIKA UWANJA WA MAJIMAJI KUMSIKILIZA RAIS SAMIA RUVUMA*Songea, RuvumaKatika hali ya hamasa kubwa, umati mku...
23/09/2024

*WANANCHI WAFURIKA UWANJA WA MAJIMAJI KUMSIKILIZA RAIS SAMIA RUVUMA*

Songea, Ruvuma

Katika hali ya hamasa kubwa, umati mkubwa wa wananchi wa Mji wa Songea umejitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Majimaji, kumshuhudia na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 23 Septemba 2024 katika kilele cha Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni, lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mkoani Ruvuma.

Mhe. Rais Dkt. Samia ni mgeni rasmi wa tamasha hilo, lililojikita katika kuonesha na kusherehekea utajiri wa urithi wa kitamaduni wa Tanzania.

Kabla ya hotuba yake, Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya utamaduni, ambapo alijionea kazi mbalimbali za sanaa na utamaduni, na hata kushiriki kucheza mchezo wa bao, jambo lililowafurahisha wananchi na wasanii waliokuwepo.

Shughuli hiyo inaendelea kwa shamrashamra, huku wananchi wakionesha shauku na furaha kubwa kwa ziara ya Rais katika eneo hilo, likiwa na umuhimu mkubwa kwa historia na utamaduni wa taifa.

23/09/2024

MKUU WA KITUO CHA POLISI KILOSA DONATI MHINA AKITOA ELIMU YA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO AMBAPO AMESISITIZA ULINZI WA MTOTO ,NA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANANCHI WA KATA YA ZOMBO WILAYA YA KILOSA MKOANI MOROGORO 20 SEPTEMBER 2024 .

Ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mkoani Morogoro.Septemba 23, 2024 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexande...
23/09/2024

Ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mkoani Morogoro.

Septemba 23, 2024 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Pastory Mnyeti (mb) amefanya ziara ya siku moja Mkoani Morogoro na kufungua Mkutano Mkuu wa 29 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA). Mkutano huo umefanyika katika Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro (MUM) kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Mhe. Naibu Waziri kabla ya kufungua Mkutano huo aliwasili Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kupokelewa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mali Dkt. Rozalia Rwegasira na kusaini kitabu cha wageni.

MWISHO.

Katika kuadhimisha miaka 60 ya jeshi la Polisi nchini jeshi hilo Mkoani Shinyanga limewataka askari wake kuendelea kusim...
17/09/2024

Katika kuadhimisha miaka 60 ya jeshi la Polisi nchini jeshi hilo Mkoani Shinyanga limewataka askari wake kuendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi pasipo kuleta malalamiko kwa jamii.
Kaimu K**anda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Kenedy Mgani amebainisha hayo wakati wa zoezi la usafi na kuchangia damu katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ulioshirikisha viongozi, maafisa na askari wa kawaida ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ambapo elimu mbalimbali zimetolewa ikiwemo elimu ya usalama barabarani na ukatili kwa jamii.
Amesema kwa sasa wamekuwa wakitoa elimu kwa askari wake kuhkikisha wanazinagaitai weledi wa kazi zake kwa kutotumia nguvu wakati wa uteklezaji wa majukumu yake jambo litakalosaidia jamii kuona uwepo wa jeshi hilo ni msitakabari kwao na jamii.
Aidha katika wiki ya kuadhmisha miaka 60 jeshi hilo limewezesha kufkia makundi ya watu tiofauti ikiwemo waendesha vyombo vya moto, pikipiki na Pamoja na makundi ya watu wenye mahitaji maalumu
Kwa uapnde wake mganga Mfawidhi wa hopsitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Pierina Mwaluko- amesema kuwa wamekuwa waksihrikiana na jeshi hilo katika Nyanja mbalimbali ikwiemo upiamaji, uchunguzi wa miili, na wale wanaokuwa wmaefariki kwa kukosa ndugu jamaa na marfiki smbamba na utoaji wa matibabu kupitia PF3
Dkt. Mwaluko amesema kuwa maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi la polisi yamekuwa na mafanikio tele ikiwemo mabadiliko mbalimbali ya kijamii
Nao baadhi ya askari walioshirki zoezi la usafi katika hospitali ya Mnaispa ya Shinyanga akiwemo koplo Daniel Bartazar na Mkaguzi Msaidizi Jane Mwazembe wamsema kuwa katika kipindi cha wiki moja wameweza kufikia makundi mbalimbali na kuwapatia elimu ya kukabiliana na uhalifu masuala ya usalama barbarani na jamii kujengewa uwezo wa kupaza sauti.

Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa kwenye maadhimisho ya maulid ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Geita katika viunga vy...
16/09/2024

Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa kwenye maadhimisho ya maulid ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Geita katika viunga vya shule ya sekondari wasichana Nyankumbu,wakimsubiri mgeni rasmi ambaye anatarajiwa kuwa waziri mkuu Kasaim majaliwa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan

Na MWANDISHI WETU  SERIKALI imewataka wananchi kuitambua na kuthamini uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo katika mae...
15/09/2024

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI imewataka wananchi kuitambua na kuthamini uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao na kuacha imani potofu katika utekelezaji wa miradi hiyo, hususani ujenzi wa Skimu za umwagilliaji na barabara kwa madai kuwa maeneo ya miradi ni ya matambiko hivyo isitishwe.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi akiwa Mkoani Tabora ambapo alitembelea eneo la mradi wa Umwagiliaji Mwasimbo Igunga, Mwampuli, Mwanzugi na Makomero.

Akiwa katika ziara hiyo ameahidi kurudisha ushirika katika eneo la mradi wa umwagiliaji Mwampuli, kujengwa fensi kuzunguka maeneo ya shamba kwa ajili ya usalama na kukarabati maghala ya mpunga.

Pia, kuanzisha kituo cha zana za kilimo ambacho kitakua na trekta na pawatila za serikali kwa ajili ya wakulima hao.

Waziri Bashe, ameelekeza kujengwa kwa bwawa upya, kujenga mashine za kukoboa mpunga na kukarabati za awali na kuweka mipaka katika eneo la umwagiliaji.

Waziri Bashe, amesema ameshangazwa na hatua ya wananchi wa Nzega vijijini kupinga utekelezaji wa miradi ya skimu za umwagiliaji unaohusisha ujenzi wa miundombinu ya bwawa la Nsembo, ujenzi wa barabara, madaraja madogo na mitaro ya kupitisha maji pembezoni mwa barabara.

Amesema, wananchi hao wanapinga miradi hiyo kwa imani potofu kuwa inapingana na mila na sehemu inapopita miradi hiyo ni maeneo ya matambiko hivyo iondolewe.

“Hii inashangaza sana ndugu zangu wa Nzega vijijini ipo haja sisi serikali kuongeza utoaji elimu, haiwezekani wananchi wanasimama na kudai hawataki barabara, hawataki miundombinu, wanachotaka ni ngoma za asili na matambiko, hivyo hatua zinazochukuliwa na serikali ni kuharibu mila,”amesema waziri Bashe

Akiwa wilayani Igunga Waziri Bashe, ameahidi kutuma timu ya wataalamu kufanya utafiti katika ujenzi wa bwawa la kukusanya maji, kutokana na maji mengi wakati wa mvua katika maeneo hayo, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalam wa Wizara hiyo watakapo fika kufanya utafiti.

"Ninawaomba ndugu zangu wataalam watakapofika muwape ushirikiano," aliomba.

Ameeleza kuwa bwawa litakapojengwa watawekewa maeneo ya kunyweshea mifugo lengo ni kuhakikisha mifugo haingii mashambani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa,amesema Tume ipo katika hatua za mwisho kuanza utekelezaji wa mradi wa skimu ya Mwamapuli iliyopo katika Kijiji cha Mwanzugi, kata ya Igunga wilaya ya Igunga -Mkoa wa Tabora.

Amesema skimu hiyo ilijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1968 hadi mwaka 1970 lakini bwawa lilikamilika mnamo mwaka 1986 hadi mwaka 1994, mifereji na miundombinu ya shambani ilijengwa na jumla ya hekta 630 zilianza kumwagiliwa Katika mwaka wa fedha 2024/2025.

“Serikali kupitia Tume imedhamiria kuboresha na kuendeleza skimu ya Mwampuli ambapo jumla ya hekta 1,557 zitajengewa miundombinu ya umwagiliaji na kufanya skimu kuwa na jumla ya hekta 2,187,”amesema Mndolwa

Mndolwa ameongeza kuwa mradi huo umeshatangazwa kwa ajili ya kumpata Mkandarasi atakaye fanya shughuli ya ujenzi.

Kwa upande wa mkazi wa eneo hilo, Jilala Shomba, amesema kuwa wapo tayari kwa miradi inayoletwa na serikali katika maeneo yao.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amewataka wananchi  Wilayani Kilombero kujitokeza kwa wingi kujia...
15/09/2024

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amewataka wananchi Wilayani Kilombero kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga Kura ifikapo tarehe 11 Oktoba hadi tarehe 20 Oktoba 2024.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua Bonanza la Uzinduzi wa Elimu ya Mpiga Kura katika Halmashauri ya Mji Ifakara lililofanyika siku ya Jumamosi tarehe 14 Septemba 2024 ambapo aliagiza viongozi wote kwa Makundi mbalimbali kuhakikisha kila mtu anahamasisha Elimu ya Mpiga Kura katika maeneo yao ili ifikapo tarehe 27 Novemba 2024 Wananchi waweze kuchagua viongozi watakaowaletea Maendeleo katika maeneo yao.

"Kwa Makundi yote ili uweze kuchagua kiongozi lazima ujiandikishe, nitoe wito kwa Wananchi wote kujiandikisha katika maeneo yenu ili tuweze kuchagua viongozi ambao watatusaidia kutatua kero zetu na kutuletea Maendeleo ". Alisisitiza Mhe. Wakili Kyobya.


https://www.instagram.com/p/C_7kJzGoDUh/?igsh=c205NGJvNW1uZmZn

SERIKALI imewataka wananchi kushiriki katikakuhifadhi Tabaka la Ozoni na kupunguza athari zamabadiliko ya tabianchi kwa ...
15/09/2024

SERIKALI imewataka wananchi kushiriki katikakuhifadhi Tabaka la Ozoni na kupunguza athari zamabadiliko ya tabianchi kwa kuepuka kuingiza nchinigesi zilizopigwa marufuku na vifaa vinavyotumia gesiharibifu k**a vile majokofu na viyoyozivilivyokwishatumika (mitumba).

Pia, imewataka kuepuka kutupa ovyo majokofu yazamani ama vifaa vya kuzima moto vyenye kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni au kusababishaongezeko la joto duniani.

Hayo yamesemwa Septemba 14,2024 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji wakatiakitoa taarifa kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifaya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni ambayo yanatarajiwakufanyika Septemba 16,2024.

Amesema kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imepangakutoa elimu kwa mafundi wa viyoyozi na majokofu katikajiji la Dodoma kwenye maadhimisho ya Siku yaKimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kuhusu namnabora ya kukarabati vifaa hivyo pasipo kuachia anganikemikali na hivyo kuharibu mazingira.

Waziri Kijaji amesema kupitia maadhimisho hayo pia wataendelea kutoa elimu kwa umma kupitia makalamjongeo kuhusu umuhimu wa kulinda tabaka la Ozonina kuendelea kuhimiza jamii kupunguza shughulimbalimbali za kibinadamu ambazo zinasababishamabadiliko ya tabianchi.

Amesema Tabaka la Ozoni linapoharibiwa huruhusumionzi ya jua kufika kwenye uso wa dunia na hivyokusababisha kuongezeka kwa magonjwa mbalimbaliyakiwemo saratani ya ngozi, mtoto wa jicho, upungufuwa kinga dhidi ya maradhi na kujikunja kwa ngozi.

"Baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwajoto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko yatabianchi. Kemikali hizo ni kemikali zinazotumika katik**ajokofu na viyoyozi, vifaa vya kuzimia moto, usafishajichuma, utengenezaji magodoro, ufukizaji wa udongokatika vitalu vya tumbaku na kilimo cha maua, hifadhi yanafaka katika maghala na kadhalika".

Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni mwaka huu ni Itifaki ya Montreal: Kupunguzaathari za mabadiliko ya tabianchi” Kauli mbiu hiiimechaguliwa ili kuendelea kujenga uelewa kwa ummawa namna ambavyo Itifaki ya Montreal imechangiakatika hifadhi ya tabaka la Ozoni na pia kuwa nyenzomuhimu katika kuchangia jitihada za kupunguza athariza mabadiliko ya tabianchi.

Misungwi,MwanzaWaziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza...
15/09/2024

Misungwi,Mwanza

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza kwa ziara rasmi ya kikazi na kupokelewa na Viongozi na wananchi wa wilaya hiyo. Katika ziara hiyo Mhe Dkt. Nchemba atakagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mwanza na kisha atazungumza na wananchi wa Misungwi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti Katika uwanja wa Amani, Misungwi Mjini.

Mhe. Dkt. Nchemba yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambayo imelenga kutembelea na kukagua, kuzindua na Kuweka mawe ya msingi katika Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.

▪️Jeshi la Polisi Nchini na Wataalam Wengine wa Uchunguzi inachunguza Kifo cha Daktari Dismas Chami.
15/09/2024

▪️Jeshi la Polisi Nchini na Wataalam Wengine wa Uchunguzi inachunguza Kifo cha Daktari Dismas Chami.

Address

MLIMBA TV
Morogoro
023

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mlimba tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mlimba tv:

Videos

Share