17/01/2025
“Tuna kazi kubwa ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi letu. K**a mnavyojua mchezo wetu tumezuiliwa kuingiza mashabiki kuingia uwanjani. Limekuwa tukio la kuumiza sana na wengine mpaka sasa bado hawajaamini, imetuchanganya pakubwa.”
“Adhabu hii ni mechi moja ambapo tukitumikia adhabu hii vizuri mechi ya robo fainali mashabiki wataingia uwanjani. Niwambe Wanasimba tuheshimu hii adhabu, mtu yoyote hata k**a ni mjanja kiasi gani wa kuingia uwanjani, niwaombe Wanasimba kukaa mbali na Uwanja wa Mkapa kuna watu ambao watakuwa wanaangalia k**a tumefata utaratibu.”
“Tuna idadi maalumu ya watu kuingia uwanjani hivyo hatazidi mtu hata mmoja. Kuna utaratibu tumepewa na CAF na sisi Simba tutaufata utaratibu huo. Kumekuwa na maoni mengi watu wakitaka tuweke screen kubwa kwenye uwanja wa Uhuru ili kelele zitakazopigwa ziwafikie wachezaji. Hairusiwi watu kukaa mita 1,000 kutoka uwanja wa Mkapa. Jambo hilo haliwezekani na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.”
“Asiyehusika yoyote atae mbali na Uwanja wa Mkapa, najua tunaumia hata mimi mwenyewe naumia.”
“Kwa kuwa watu wanataka kuiona timu yao pamoja k**a tulivyozoea, mdhamini wetu wa michuano ya kimataifa akaona atuandalie kitu cha kutuweka pamoja. Mo Cola ametutengea eneo maalumu la kukutana kuona timu yetu na eneo lenyewe ni Mwembe Yanga lililopo Temeke. Tutakuwepo pale kuanzia saa 5 asubuhi na kutakuwa na screen kubwa vibaya mno, hamjawahi kuiona.”
“Kutakuwepo na burudani mbalimbali siku hiyo k**a mwimbaji wa nyimbo ya Wivu ambaye ni Dj Mushizo lakini pia atakuwepo Dj Sinyorita.”
“Lakini pia wiki mbili ziliopita tulizindua kampeni ya Onja na Ushinde ukinywa Mo Cola. Hivyo siku ya Jumapili Januari 19, 2025 kutakuwa na zoezi la kugawa zawadi kwa washindi na wengine watashinda pale pale.”
“Mimi binafsi Jumapili sitaenda uwanjani, taenda Mwembe Yanga. Nimeshazoea kelele hivyo takuwa na Wanasimba wenzangu kufurahia.”
“Kampeni ya Tunawajibika Pamoja hadi sasa tuna milioni 47,141,024. Zoezi letu litafungwa mara tu baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo wa Jumapili. Tunaitafuta milioni 100 hivyo bado k**a milioni 53.”- Ahmed Ally. Instagram 👇👇
https://www.instagram.com/alpher_tv
YouTube 👇👇👇
https://youtube.com/