BANCE TV

BANCE TV Kisima cha burudani

12/06/2024

One of the best movie in the world.
. Uliangalia ukiwa wapi.

12/06/2024

Kazi zinaandaliwa,,, Mungu ni Mwingi wa Neema. Soon mizigo inapetwa sokoni YouTube ya bancetv stay tuned .

  Wananchi wa Kijiji cha Kambai Kata ya Kwezitu wilayani Muheza Mkoani Tanga wamechoma gari la Afisa Kilimo wa Kata jira...
04/04/2024

Wananchi wa Kijiji cha Kambai Kata ya Kwezitu wilayani Muheza Mkoani Tanga wamechoma gari la Afisa Kilimo wa Kata jirani ya Tongwe aina ya Suzuki pamoja na kumjeruhi Afisa huyo.

Wamechukua hatua hiyo wakituhumu kushindwa kusimamia maslahi ya wananchi na kupelekea wawekezaji kupewa eneo la zaidi ya ekari 500 bila tathimini ya kina kufanyika Wala wananchi kushirikishwa.

Akizungumzia tukio hilo baada ya kufika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah amethibitisha kutokea tukio hilo huku akielza baada ya kupokea taaarifa hiyo alilazimika kufika kujionea ili kufanya mkutano na wananchi kwa lengoa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Mkuu wa wilaya hiyo alisema halmshauri ina eneo la zaidi ya ekari 3000 lenye hatia kwa zaidi ya miaka 28 lakini ndani ya kipindi hicho cha miaka hiyo hawajaliendeleza na alipatikana mwekezaji wa kwanza mwaka 2020/21 akapewa ekari 500 pasipo tathimini ya kina kufanyika kuja kiwango cha uvamizi kilichofanyika kwenye eneo hilo.

Aidha alisema kwamba mwaka jana 2023 walipatikana wawekezaji wengine wanne nao pia tathimini ya kina haikufanyika.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Polisi wilaya ya Muheza (OCD) Hadija Soko alithibitisha kutokea kwa tukio Hilo ambapo alisema kwa sasa Afisa Kilimo huyo amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Muheza huku baadhi ya watu waliohusika na kuchoma moto gari wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano.

Cc

Ni Kawaida Sana kupita sehemu ukasikia tangazo la mtu kununua pesa za kigeni pesa  mbovu au pesa za zamani yes pesa hizi...
04/04/2024

Ni Kawaida Sana kupita sehemu ukasikia tangazo la mtu kununua pesa za kigeni pesa mbovu au pesa za zamani yes pesa hizi zinanunuliwa kulingana na thamani mfano elfu 10 mbovu atakupatia elfu 8 yeye akipeleka bank anapata elfu 10 Ile Ile na yeye anakuwa kapata faida ya shilingi elfu 2 maana bank hawakatai pesa eti Kisa mbovu

Je umewai kusikia kuwa pesa hizo (Mia tano) za zamani kuna watu wananunua na kuna wengine wanatangaza kuwa wananunua mpaka shilingi milioni Moja kwa noti Moja ?

Ngoja kwanza nikupe darasa kidogo

Ukweli ni kwamba hizo hela hazina Kazi yoyote na hakuna anaezinunua Ila wajanja wenzangu watoto wa town kila kukicha wanaamka na akili ya kupata pesa maana Ajira zenyewe hakuna na k**a unavyojua wajinga wa kuibiwa mjini huwa hawaishi

Wanachofanya anatokea mtu mmoja anatangaza ananunua hizo noti kwa shilingi elfu 2 kila Moja

Yoyote aliekuwa nazo atajitokeza tuu Kisha watakuja kununua kwako Kwa labda watasema wanataka noti 20 jumla watakupatia shilingi elfu 40 Kisha watakuacha unachelelea na wao watajifanya wajinga wanaondoka na hizo noti Kisha watachukua namba zako na kukuomba ukipata noti nyingine uwapigie

Baada ya siku 3 utapigiwa simu na mtu yoyote (kumbuka walichukua namba zako ) kisha atajitambulisha kuwa ni wale wanaonunua za zamani za Shilingi Mia 5 na wanaomba k**a ukipata nyingine uwaambie maana kwa sasa wamepata soko kubwa zaidi na watanunua kila noti kwa shilingi elfu 50 badala ya shilingi elfu 2 ya mwanzo

Kwanza ukiskia Hivi utawaamini maana walishakuja kwako kununua na hawana longo longo so kisaikorojia watakuwa wakekupa Kazi mbili

Kwanza kutafta hizo noti kwa udi na uvumba pili utakuwa tayari ata kwenda kukopa pesa ili ununue hizo noti mtaani Kisha uje kuwauzia hao matajiri

Baada ya kukata tuu simu Jioni ya siku hiyo eidha kuna kijana atakuja kwenu au pale mlipokutana na wateja wako wa mwanzo akiwa na noti za Mia 5 za kutosha tuu Kisha atakuulizia umsaidie kutafta soko k**a unajua zinaponunuliwa Itaendelea.....

Julius

04/04/2024

Shirikisho la Soka nchini (TFF) limeingia mkataba wa miaka mitatu na nusu na benki ya CRDB kwa ajili ya udhamini wa Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam na katika msimu huu wa 2023/24 CRDB itatoa milioni 255 na udhamini huo utaanza rasmi kuanzia hatua ya 16 bora hadi mwisho wa msimu.

Mkataba huo wenye thamani ya Bilioni 3.759 umesainiwa leo Jumanne Aprili 2, 2024 katika makao makuu ya benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam.

Akizungumzia udhamini huo wa Benki ya CRDB kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema “CRDB ndio anakuwa mdhamini wa kwanza wa kombe la Shirikisho”

Sasa itaitwa CRDB Bank Federation Cup” maneno ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza kwenye hafla ya kuingia mkataba wa kudhamini michuano ya FA.

.

Tau na MiquissoneK**a Soka ingekuwa ni uadui basi Luis Miquissone angekaa mbali na Percy Tau na asingetaka kumwona Kwa s...
30/03/2024

Tau na Miquissone
K**a Soka ingekuwa ni uadui basi Luis Miquissone angekaa mbali na Percy Tau na asingetaka kumwona Kwa sababu amekuwa kikwazo mbele yake .

Wakati Miquissone anatua Mamelodi Sundowns alikutana na Percy Tau akiwa anachipukia toka timu ya vijana mwamba akawasha moto Luis Miquissone akaishia kukaa benchi mwisho wa siku akatua Simba SC.

Luis Miquissone akaelekea Al Ahly Sporting Club lakini Percy Tau nae akatua ndani ya timu hii na kuendelea kuwa Chaguo la kwanza Kwa Kocha wa timu hiiii huku Miquissone akiendelea kula mbao ndefu kimya kimya .

✍️Hiii Picha ya Tau na Miquissone ni picha yenye historia kubwa katika Ulimwengu wa Soka walikutana Kwa mara ya kwanza mwaka January 2018 lakini Miquissone alishindwa kuvaa Viatu vya Percy Tau hata alipo ondoka kuelekea Brighton & Hove Albion.

👉 Wakati huo Percy Tau ana miaka 24 na Luis Miquissone ana miaka 23 .....Leo baada ya mechi wamekutana tena kupiga Stori.

Siku zote Soka siyo uadui ni furaha 🤚


ANAANDIKA FARHAN KIHAMUBado napata shaka kuamini kuwa Simba haina Wachezaji wazuri, ambao mnawaita QUALITY PLAYERS! Napa...
30/03/2024

ANAANDIKA FARHAN KIHAMU

Bado napata shaka kuamini kuwa Simba haina Wachezaji wazuri, ambao mnawaita QUALITY PLAYERS! Napata shaka kuamini hilo haswa kwa kutazama mechi kadhaa za Simba dhidi ya Al Ahly, haswa hizi tatu za mwaka huu, mbili zimeisha kwa sare na moja Simba kapoteza.

QUALITY ipi unaizungumzia? K**a timu imekupa game nzuri sana jana, kamzidi Al Ahly kila kitu kwenye dakika 90 za mchezo ukiachana na bao pekee lilotokana na makosa ya kimpira, sio sahihi kuiona Simba k**a imechezwa hovyo ama ipo hovyo sana ila ni sahihi zaidi kuboresha baadhi ya maeneo ambayo ni moja tu ENEO LA UFUNGAJI (Striker).

Simba ama timu nyingine karibia 90% hapa Afrika haziwezi kuwa na Wachezaji wenye QUALITY k**a ya Ahly unachokifanya unakuwa na copy zao zinazokaribiana tu, hakuna namna Simba akamiliki quality k**a ile kwakuwa FEDHA ni changamoto, mechi wakati mwingine ni kujituma na utulivu tu ambao jana ulikosekana, timu iwe mbovu icheze vile mbele ya Ahly?

Kuna sehemu nyingine yoyote ambayo Simba imekupa hofu zaidi ya eneo la mwisho? Kwangu sioni k**a ni sahihi kuikataa timu kiasi hiki, binafsi bado siamini k**a ni sahihi kuona k**a timu haijafanya kitu, dirisha kubwa wapate Washambuliaji wa maana and off we go.

Ni mpira unacheza vizuri ila unafungwa, unacheza vibaya ila unashinda!

[ ]

.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Zanzibar Rashid Msaraka ametoa ufafanuzi kuhusu 'Clip' inayotembea mitandaoni juu ya kijana ana...
30/03/2024

Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Zanzibar Rashid Msaraka ametoa ufafanuzi kuhusu 'Clip' inayotembea mitandaoni juu ya kijana anayeonekana akichapwa kwa kulewa mchana mwezi wa Ramadhan.

DC Msaraka amebainisha kuwa clip hiyo ni ya zamani tangu 2017 huku akitoa maelezo kuwa:- “Kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar hakuna Sheria yoyote ya kumzuia mtu yoyote ndani ya Zanzibar kula mchana ila kuna Sheria kwa mujibu wa sheria za mwenendo wa makosa ya jinai ya kuchukuliwa hatua k**a utafanya kitendo chochote kitakachoikerahisha jamii.”

“Kwa mfano unapovua nguo hadharani ukakaa kwenye bodaboda uchi hutashtakiwa kwa kukaa uchi bali kwa kufanya kitendo kinachoikerahisha jamii.”— amesema DC Msaraka.

“Kula mchana wa Ramadhani ndani ya Zanzibar ni kitendo kinachochukuliwa k**a kuikerahisha jamii, kulewa hadharani hata siku za kula mchana pia kitendo hicho kinajukuishwa humo humo ndio maana Zanzibar kulewa kwa mujibu wa sheria unatakiwa uanze kulewa saa 10 jioni hadi saa sita usiku mwisho, na hata 'bar' kwa mujibu wa sheria za vileo Zanzibar zinaanza kufunguliwa muda wa saa 10 jioni na kufungwa saa sita usiku.”

“Na vitendo hivyo vya kuikerahisha jamii ni lazima yaani lazima watokee wanajamii watakaonyesha kukerahishwa na tendo hilo.”

“Serikali haikubaliani na mtu kujichukulia hatua mikononi lakini pia haitavumilia vitendo vyovyote vya kuikerahisha jamii vifanyike hadharani miongoni mwa wanajamii.”

Huu unyama cyo wa kawaida wamejitafuta wamejipata visit ulanga,,,,,Bance film production
03/01/2024

Huu unyama cyo wa kawaida wamejitafuta wamejipata visit ulanga,,,,,
Bance film production

Watazamaji wa bance tv msikose kuburudika na miendelezo yote ya Movie zetu. Huko youtube
03/01/2024

Watazamaji wa bance tv msikose kuburudika na miendelezo yote ya Movie zetu. Huko youtube

Address

Mahenge Ulanga
Morogoro
2350

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BANCE TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to BANCE TV:

Videos

Share

Category