09/10/2023
HABARI:
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Tanzania haiwezi kufikia Dira ya Maendeleo ya 2030 huku ikiona wasichana wanaendelea kukeketwa kutokana na mila potofu zenye madhara.
Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa kutokomeza Ukeketaji leo Oktoba 9, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa haiwezekani kujenga uwezo kamili wa rasilimali watu k**a wasichana waliowengi hawatapewa fursa ya elimu na kufikia malengo yao kutokana na madhara ya kukeketwa.
Amebainisha kwamba, kwa mujibu wa takwimu, wanawake na wasichana zaidi ya milioni 200 duniani wamefanyiwa ukeketaji, kati ya hao zaidi ya milioni 20 wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji kupitia wataalamu wa afya.
"Ukeketaji unaondoa utu wa wanawake na watoto wa k**e ikiwa ni pamoja na kuhatarisha afya zao, na maisha yao ya baadaye. Ni imani yangu kuwa, leo katika ukumbi huu uliojaa watetezi wenye shauku, wataalam, na watunga sera, nayaona matumaini na dhamira ya kuwa na ulimwengu ambapo kila msichana anaweza kukua bila kivuli cha ukeketaji." Ameongeza Dkt. Gwajima.