Moja ya matukio ya kuvutia katika ufunguzi wa Ofisi ya Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma ni wimbo wa โNani Kama Mamaโ ambapo Mama zetu wakiongozwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wameucheza na kukumbatiana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango wakipiga Ngoma kuashiria Mtawala ameingia katika nyumba ya Chifu
Picha na @wasafitv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ameongoza Shughuli ya Kukata Utepe katika uzinduzi wa Ikulu Mpya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Picha na @wasafitv
Bendera ya Taifa, Bendera ya Afrika Mashariki na Bendera ya Rais zikipandishwa kwa mara ya kwanza katika Ofisi Mpya ya Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema asilimia 7 ya Watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo huku akitoa rai kwa Wananchi kupima ugonjwa huo mara kwa mara ili kuepuka madhara yake makubwa ikiwemo gharama kubwa ya matibabu yake.
Dkt. Mollel amesema hayo leo May 19, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge Asia Abdukarimu Halamga @asia_halamga katika Mkutano wa 11 kikao cha 29, Bungeni Jijini Dodoma.
Amesema, ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa unahusishwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa kisukari na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Mollel amesema katika kujali afya za Watanzania wakiwemo wenye ugonjwa wa figo, Serikali ya Rais Samia imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 290.9 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali za Mikoa ambapo katika vifaa hivyo vipo vifaa vya matibabu ya kusafisha damu (dialysis) kwa Wagonjwa wa figo.
Aidha, Dkt. Mollel amesema, Serikali ipo katika mpango wa kuona namna ya kupunguza gharama ya matibabu ya figo kupitia huduma ya kusafisha damu ili Wananchi wenye uhitaji waweze kunufaika na huduma hizo, huku akiweka wazi kuendelea kuwatazama wasio na uwezo kabisa kupitia njia ya misamaha.
@asia_halamga
๐ง๐๐๐ฆ ๐๐ฆ ๐ฌ๐ข๐จ๐ก๐ ๐๐๐ฅ๐๐๐๐ก๐ฆ ๐ฆ๐ฃ๐ข๐ฅ๐ง๐ฆ ๐๐๐จ๐ #theclubaboveall๐ฐ๐๐จ๐๐ ๐ง๐๐ ๐โฑ๏ธ| #CAFCC
Marumo Gallants 1-2 Young Africans SC
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko
Mwalimu aliyefundisha shule kadhaa pamoja na Chuo kikuu, kisha akaingia kwenye siasa akawa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na baadaye akawa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mwanza na Kagera. Sasa Albert Chalamila ameteuliwa tena kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
@albertchalamila_ @albert_chalamila
Mwili wa Hayati Benard Membe umefikishwa hapa Karimjee kwa ajili ya heshima za mwisho.
.
Membe atazikwa kijijini kwake Rondo mkoani Lindi.
.
#RIPMembe
Polisi waanza uchunguzi utata wa kifo cha mwanafunzi UDOM
-
Jeshi la Polisi nchini limesema limeona mjadala katika mitandao ya kijamii ikuhusiana na kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Nusura Hassan Abdallah kilichotokea huko Mkoani Kilimanjaro.
Akitoa taarifa hiyo leo Mei 06, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime amesema taarifa hizo zimekuwa zikihusisha kifo hicho na ajali iliyotokea jijini Dodoma Aprili 26, 2023 ikimhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi (Afya), Dk. Festo Dugange ambapo zinadaiwa zimetokana na kipigo kutoka kwa mpenzi wake.
SHEREHE ZA MEI MOSI MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiingia katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro yanapofanyika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye mgeni rasmi katika Maadhimisho haya.
#Meimosi #SSH
#Credit @mamakajatz
@salimasas @ahmed.s.asas @hassan_kashoba
Mbunge Viti Maalum ( Vijana Taifa) Mhe @asia_halamga leo April 28 2023 amechangua kwenye Bajeti ya Wizara ya Madini.
Ambapo kwenye mchango wake Mhe @asia_halamga amesisitiza huduma za afya, usaidizi wa tafiti kwa wachimbaji wadogo, soko la madini kwa wachimbaji wadogo.
#Tanzaniayetu
#Madini yetu #manyara
CDE. SANGU JOSEPH MALAWA AWASIHI VIJANA, KUULINDA NA KUTETEA MUUNGANO
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam, Cde. Sangu Joseph Malawa amewasisitiza vijana wote nchini kuendelea kuenzi Muungano ulioasisiwa na Waasisi wa Mataifa Yetu ya Tanganyika na Zanzibar Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.
Cde. Sangu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kilakala wilayani Temeke jijini Dar es salaam, yaliyolenga pia kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
"Vijana wengi tuliopo kwenye Umoja wa Vijana sasa hivi tumezaliwa baada ya Muungano, lakini pia msisahau sisi Jumuiya ya Vijana ni Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kimetokana na Muungano wa Vyama Viwili vya TANU na ASP, hivyo sisi UVCCM tuna sababu nyingi za kuhakikisha tunaulinda Muungano huu" Amesema Cde. Sangu Joseph Malawa, Mjumbe wa Mkutano UVCCM Mkoa wa Dar es salaam.
@sangujoseph
#VivaVijanaViva #KaziIendelee
Motivational speaker wakiona hii tumekwisha.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. @smchembe amelipongeza jeshi la polisi wilayani humo kwa kufanikiwa kuwatawanya mamia ya wananchi kata ya Segera ambao walivamia gari la mafuta lililoanguka na kuanza kuchota petroli."Wananchi, vitendo hatarishi kama hivyo visijirudie tena".
Happy Independence Day ๐น๐ฟ
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza matokeo ya uchaguzi wa Washindi waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kwenye viti 20 Tanzania Bara.
Kwa upande wa Wanaume Mshindi wa kwanza ni Mahenda Leonard aliyepata kura 845, nafasi ya pili ameishikilia Waziri Innocent Bashungwa mwenye kura 720 akifuatiwa na Steven Wasira mwenye kura 680 na Msome Jackson William kura 591.
Wengine ni Kasheku Msukuma (587), Kasesela Richard ( 574), Wambura Chacha Mwita kura 545, Waziri Bashe Hussein (510), Waziri Nape Nnauye (508), Askofu Josephat Gwajima (497), Waziri January Makamba (452), Waziri Mwigulu Nchemba (450), Macha (435) na Msengi Ibrahimu (428).
Upande wa Wanawake Dkt Angelin Mabula ana kura 770, Dkt Ashatu Kijaji (764), Christina Solomon Mndeme (761) , Hellen Makungu Kura 755, Fenela Mukangara ( 747) na Angellah J. Kairuki (730).
Hongera Mheshimiwa Dkt. @samia_suluhu_hassan Mwenyekiti wa @ccmtanzania Taifa๐๐ ๐โค๐