
11/03/2025
Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa
linawashikilia vijana 13, akiwemo mwanamke mmoja, kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli wa kimtandao.
Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija, amesema watuhumiwa hao walik**atwa wakiwa na laini 36 za mitandao mbalimbali pamoja na zaidi ya simu kumi, ambazo inadaiwa walizitumia katika kutekeleza uhalifu huo.
Kamanda Masija amepongeza juhudi za Jeshi la Polisi katika kuendelea kudhibiti uhalifu wa mtandao na ametoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kujihusisha na vitendo vya utapeli wa kimtandao, Pia amewataka wananchi kuwa makini na taarifa zao za kifedha na binafsi ili kuepuka kuingia katika mtego wa matapeli.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mtandao mpana wa uhalifu huo na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.