The Green Voice TV

The Green Voice  TV Karibu The Green Voice TV, usisahau ku "Subscribe" You tube channel yetu. "Yes we are Green".

  Mashetani wekundu wamekung'utwa wakiwa sebuleni kwao "Old Trafford" dhidi ya Brighton.⏰FT: Man UTD 1-2 Brighton     #
11/01/2026

Mashetani wekundu wamekung'utwa wakiwa sebuleni kwao "Old Trafford" dhidi ya Brighton.

⏰FT: Man UTD 1-2 Brighton

#

SIMBA SC: AHADI KUBWA, UKIMYA MKUBWA, MAUMIVU YA WANASIMBAAhadi ya kishujaa ya CPA Joseph Rwegasira ya kumsajili kila mw...
11/01/2026

SIMBA SC: AHADI KUBWA, UKIMYA MKUBWA, MAUMIVU YA WANASIMBA

Ahadi ya kishujaa ya CPA Joseph Rwegasira ya kumsajili kila mwaka “mchezaji wa Wanasimba” imeendelea kuishi vichwani mwa mashabiki, lakini hadi sasa imebaki kuwa ndoto isiyotimia. Kila dirisha la usajili linapita huku matarajio yakigeuka maumivu, Simba SC ikionekana kukosa mwelekeo wakati wapinzani wakifanya maamuzi mazito na ya kimkakati.

Kinachouma zaidi ni ukimya wa wadhamini na sintofahamu ndani ya uongozi, hali inayowafanya mashabiki wajihisi k**a timu yao inaachwa ichezwe mezani badala ya kuimarishwa. Simba inaonekana kupoteza nguvu ya ushindani si kwa kukosa historia, bali kwa kukosa msimamo na utekelezaji wa ahadi kubwa.

Badala ya kusikilizwa, mashabiki wamejikuta wakilaumiwa—wakiambiwa wanavaa jezi feki. Hili ni pigo kwa uaminifu wao, kwani wao ndio uti wa mgongo wa klabu, wanaojitoa kwa hali na mali bila kuchoka, jua liwake au mvua inyeshe.

Simba SC si jezi wala kauli tamu; ni hisia na matumaini ya mamilioni. Mashabiki hawahitaji lawama, wanahitaji heshima, uwazi na vitendo. Kauli zikigeuke kuwa matendo, ili Msimbazi irudi kuwa ngome ya heshima na ushindani, si simulizi ya ahadi zisizotekelezwa.

🚨🚨 BREAKING: Yanga wamepiga chini ofa mbili kutoka Uarabuni,kwenye vilabu vya Zamalek na CR Belouizdad.Timu hizo mbili z...
11/01/2026

🚨🚨 BREAKING: Yanga wamepiga chini ofa mbili kutoka Uarabuni,kwenye vilabu vya Zamalek na CR Belouizdad.

Timu hizo mbili zinahitaji huduma ya golikipa Djigui Diarra (30) baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Afcon,ila jibu la Yanga limekuwa moja “Diarra is not for sale” (Diarra hauzwi).

Yanga hawataki kusikia chochote zaidi ya kubaki na Diarra.

Kwa habari za uhakika za usajili follow green voice tv

Ndio kusema kisasi ni haki 😂😂😂😂😂Sibonike NM
10/01/2026

Ndio kusema kisasi ni haki 😂😂😂😂😂
Sibonike NM

Hapa mpira ulivuka ama la???Refa wa hii mechi Issa Sy ana kazi sanaa mechi ni ya moto sanaa! 🙌🔥🔥🔥Algeria 0-0 Nigeria dak...
10/01/2026

Hapa mpira ulivuka ama la???
Refa wa hii mechi Issa Sy ana kazi sanaa mechi ni ya moto sanaa! 🙌🔥🔥🔥
Algeria 0-0 Nigeria dakika ya 35

“SIMBA SC 2025/2026: WAKATI TIMU NYINGINE WANAVUNA, WAO WANATAFUTA MASHAMBA YALIYOSHASAFULIWA!” 😂🦁⚽Simba SC wa msimu wa ...
10/01/2026

“SIMBA SC 2025/2026: WAKATI TIMU NYINGINE WANAVUNA, WAO WANATAFUTA MASHAMBA YALIYOSHASAFULIWA!” 😂🦁⚽

Simba SC wa msimu wa 2025/2026 sio Simba wa zamani.
Huyu Simba wa sasa ni k**a amepandishwa daraja ghafla, bado anajifunza kusoma ramani ya soko la usajili.
Zamani Simba alikuwa k**a mkulima hodari — anapanda mapema, anavuna mapema, na anaondoka shambani na gunia limejaa.
Lakini Simba wa sasa? 😅
Ni k**a anakuja shambani baada ya mavuno, anaangalia chini, anasema:
“Bado kuna punje zimeanguka?”
Kwenye usajili, Simba SC ana falsafa mpya kabisa:
Hakimbizani na Yanga, Al Ahly wala Kaizer Chiefs ❌
Hakai mezani panapogombaniwa saini 🔕
Anatafuta mchezaji ambaye Google nayo inashangaa jina lake 🤣
Ni k**a kauli mbiu yao ni:
“Usajili bora ni ule ambao hakuna anayemjua.”
Mashabiki wanapomuona mchezaji mpya wanajiuliza:
“Huyu ametoka ligi ipi? Au scout alimwona TikTok?” 😂
Wakati timu zingine zinavuna mazao mabichi, Simba SC:
👉 Anaokota yaliyosalia
👉 Anaomba ‘bonus’ ya mazoezi
👉 Anaweka matumaini kwenye potential badala ya ubora wa sasa
Kwa kifupi:
🦁 Simba anataka ushindi wa kesho kwa usajili wa jana
🦁 Anaepuka presha k**a kadi nyekundu
🦁 Anaamini “kimya kimya ndiyo siri ya mafanikio”
Mpira hauna hakika, huenda kesho tukapigwa na butwaa.
Lakini kwa sasa…
Simba SC anaonekana k**a timu ya Ligi Kuu inayofanya usajili wa daraja la majaribio. 😄⚽

Bondia namba 1 kwa sasa Tanzania Salmin Kassim Kaberege ana umri wa miaka 22, amepigana mapambano 12, 10 ameshinda mawil...
10/01/2026

Bondia namba 1 kwa sasa Tanzania Salmin Kassim Kaberege ana umri wa miaka 22, amepigana mapambano 12, 10 ameshinda mawili ameenda sare, hajui harufu ya kupigwa, ni bingwa wa WBO regional, na mwaka huu atapigana pambano la kuutetea mkanda wake. Ana nyota 3.5 ni highly ranked boxer nchini 🇹🇿

🚨🚨 JUST IN: Mzamiru Yassin (30) yuko kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na vilabu vya Singida,Mbeya City na TRA.Mzamiru ...
10/01/2026

🚨🚨 JUST IN: Mzamiru Yassin (30) yuko kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na vilabu vya Singida,Mbeya City na TRA.

Mzamiru Yassin Anahitaji changamoto mpya,na mpango wake ni kuondoka Simba January hii.

Mzamiru amebakiza mkata wa miezi sita na Simba,pia Simba wako tayari kumuachia January hii.

🚨 HABARI ZA USAJILI!!Simba SC wameanza mazungumzo na winga wa klabu ya Nyasa Big Bullets, Chikumbutso Salima (22), kwa l...
10/01/2026

🚨 HABARI ZA USAJILI!!

Simba SC wameanza mazungumzo na winga wa klabu ya Nyasa Big Bullets, Chikumbutso Salima (22), kwa lengo la kumsajili katika dirisha dogo la usajili la Januari 2026.

Salima amepewa ofa ya mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba SC. Hata hivyo, kabla ya kusaini mkataba huo, anatarajiwa kufanyiwa majaribio (trials) na timu hiyo ili uongozi ufanye maamuzi ya mwisho kuhusu usajili wake.

🦁⚽

UNAWEZA KUWATAJA KWA MAJINA?
10/01/2026

UNAWEZA KUWATAJA KWA MAJINA?

PESA INATAKA KUSHINDA...... HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA🤔
10/01/2026

PESA INATAKA KUSHINDA...... HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA🤔

UKISTAAJABU YA M***A.......   Mwamuzi wa Algeria Mustapha Ghorbal atachezesha mechi kati ya Misri na mabingwa watetezi I...
10/01/2026

UKISTAAJABU YA M***A.......


Mwamuzi wa Algeria Mustapha Ghorbal atachezesha mechi kati ya Misri na mabingwa watetezi Ivory Coast, hii imekuja baada ya Misri kumkataa mwamuzi kutoka Morocco Jalal Jayed ambaye alipangwa awali, ikiwa ni kulipiza kile walichofanya Morocco kumkataa mwamuzi Mohamed Amin Omar wa Misri kuchezesha mchezo wao wa jana dhidi ya Cameroon ambao wameshinda 2-0. CAF ni ya Waarabu na wanacheza midundo yao.

Address

Rungwe
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Green Voice TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to The Green Voice TV:

Share