Greencity Tv Online

Greencity Tv Online Karibu
Kituo chako bora cha matangazo Online
Kawa Habari za MICHEZO, BURUDANI, MATUKIO na HISTORIA ungana nasi

TUNAKUA KIDIGITALI

15/02/2025

Ibaada ni muhimu ๐Ÿ˜†๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚

BINTI TANZANIA NG'ARA CAMPAIGN SEASON FOUR_____________________________________    Ni msimu mwingine wa kuwaonesha upend...
02/02/2025

BINTI TANZANIA NG'ARA CAMPAIGN SEASON FOUR
_____________________________________

Ni msimu mwingine wa kuwaonesha upendo Mabinti wanafunzi wanaotoka kwenye Familia Duni, karibu tushiriki pamoja kuwanunulia Taulo za K**e (PADS).

Unaweza kuchangia PADS moja kwa moja au Pesa kwa thamani ya Pads kiasi ulichoguswa, Mungu akubariki sana.

โ˜Ž๏ธPADS____ Piga 0693073237 Utukabidhi mchango wako
๐Ÿ’ตPESA____ Lipa kwa M-Pesa mitandao Yote
Namba __ 35246112
Jina: WAMZI H. MWANGOMO


01/11/2024

YOU HEARD...!!!!

Tuambie Msimu Mwingine Wa *Tulia Trust Village* Ndani ya Kata ya Mwasenkwa Jijini Mbeya.

Unatamani Kuona Kitu Gani Kikifanyika Kwenye Kijiji Chenye Asili Yake.

Tumefika Tulia Trust Village Kuona Maendeleo na hivi Karibuni Tunakwenda Kufunga Tulia Trust Village.


Dr. Tulia AcksonDr. Tulia Ackson Tulia Ackson

DIAMOND PLATNUMZ AMEGAWA AJIRA KWA WASHINDI WA TULIA STREET TALENT COMPETITION 2024, AMETANGAZA KUWEKA TAWI LA LEBO YA W...
27/10/2024

DIAMOND PLATNUMZ AMEGAWA AJIRA KWA WASHINDI WA TULIA STREET TALENT COMPETITION 2024, AMETANGAZA KUWEKA TAWI LA LEBO YA WASAFI JIJINI MBEYA.

Leo Oktoba 27. 2024 umetamatika msimu wa 5 wa TULIA STREET TALENT COMPETITION 2024, ambapo mgeni rasmi wa mashindano hayo allikuwa Msanii nyota wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz mbaye ni Mkurugenzi wa WASAFI MEDIA na Lebo ya WASAFI CLASSIC BAND (WCB).

Akiongea na washiriki pamoja na Wanambeya wote waliohudhulia kwenye uwanja wa T.IA Mbeya mjini, ambapo mashindano hayo yamefanyikia. Ametoa pongezi kwa waandaaji wa mashindano hayo ambo ni Taasisi ya TULIA TRUST , kwa namna inavyofanya kazi kubwa na nzuri kwa kuibua vipaji mbalimbali wakiwemo Wachekeshaji (Comedians), Waimbaji (Musicians), Wachezaji (Dancers), Wanamitindo (Model & Fashion) na MaDJ.

Pia ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa TULIA TRUST ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Spika wa Bunge la JMT na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (I.P.U) Mh. Dkt Tulia Ackson Dr. Tulia Ackson , kwa kazi kubwa ya kuwafanya Kipaumbele Wananchi wote hususani wa jimbo lake kwani anafanya mengi mazuri na yenye tija. Amewataka Wananchi kuendelea kumuamini na kutokumpoteza, kwani Mh. Dkt Tulia ni Kiongozi hodari na Shujaz na Mwenye Koneksheni (connections) hivyo mambo mengi yapo safi na Mbeya imetulia.

Diamond Platnumz ameongeza kuwa kwa sasa ana mpango wa kufungua tawi la Studio za Wasafi Record jijini Mbeya, lengo likiwa ni kuendeleza vipaji vilivyopo. Ametangaza kuwa Washindi kila kategori iliyokuwa inashindaniwa, atatoa fulsa huku Mshindi wa kategori ya DJ ametangazwa kuajiriwa WASAFI FM, Mshindi wa kategori ya Comedy kuajiriwa na CHEKA TU, Washindi wa kategori ya Dancers nafasi ya kwanza na ya Pili kushiriki kwenye Video yake atakayotoa hivi karibuni na Washindi wa kategori ya Fashion wa kwanza na wa Pili kulipwa ili kumbunia Mavazi kwaajili ya Show zilizo mbele yake mwezi Novemba.

  Bunge la Kitaifa limeafiki uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais mteule wa Kenya baada ya jina lake kuwasi...
19/10/2024


Bunge la Kitaifa limeafiki uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais mteule wa Kenya baada ya jina lake kuwasilishwa na Rais William Ruto. Wabunge 236 walipiga kura ya 'Ndiyo' kuafiki uteuzi wa Kindiki
Jina lake sasa litawekwa katika gazeti rasmi la serikali na kisha kuapishwa kuanza kuhudumu k**a Naibu Rais .

Katiba inasema pindi rais anapowasilisha uteuzi kwenye Bunge, wabunge watapiga kura ya kulikataa au kuliidhinisha jina hilo. Pia hakuna sharti la kura ya thuluthi mbili.
โ€œProf. Kindiki, ambaye kwa sasa anahudumu k**a Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini kutoka kwa Bunge la Kitaifa kabla ya kushika nafasi ya Naibu Rais. Bunge lazima lipigie kura uteuzi ndani ya siku 60 baada ya kupokea jina hilo.

Baada ya kuidhinishwa, mteule atateuliwa rasmi na Rais kuwa naibu wake. Ingawa Katiba haijaweka bayana muda wa uteuzi huu, unatarajiwa kutokea mara baada ya kuidhinishwa na Bunge.
Katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2022, Kindiki alikuwa miongoni mwa waliopendekezwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto lakini hatimaye akaamua kumchagua Gachagua.

Baadaye alielezea kwamba alimchagua Gachagua kwa sababu ya umri wake na alifikiri wangeelewana zaidi. Mwanzoni mwa kuondolewa kwa Gachagua, kulikuwa na mazungumzo ya Kindiki kuwa ndiye anayefuata kuchukua nafasi yake.

Bunge la Seneti lilipiga kura ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua kufuatia mchakato wa siku mbili uliohusisha ushahidi wa kina . Gachagua aliondolewa baada ya Maseneta kuunga mkono sababu tano kati ya kumi na moja zilizowasilishwa na Mbunge wa kibwezi kaskazini Mwinge Mutuse.

       Bunge la seneti nchini Kenya Alhamisi lilipiga kura na kuidhinisha kuondolewa ofisini kwa Naibu Rais Rigathi Gach...
18/10/2024


Bunge la seneti nchini Kenya Alhamisi lilipiga kura na kuidhinisha kuondolewa ofisini kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kutokana na mashtaka 5 kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake, katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Maseneta 54 kati ya 67 walipiga kura ya kumfukuza Gachagua kwa shtaka la kwanza la "ukiukaji mkubwa wa katiba", zaidi ya theluthi mbili ya idadi inayohitajika kisheria, na kumfanya kuwa naibu rais wa kwanza kulazimishwa kuondoka madarakani kwa mashtaka k**a hayo. Ni hatua ambayo baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanasema huenda ikaitumbukiza nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika mzozo wa kisiasa.

Bunge la Kitaifa lilipiga kura wiki jana kumshtaki Gachagua, ambaye alimsaidia Rais William Ruto kushinda uchaguzi miaka miwili iliyopita lakini ameshambuliwa na washirika wa rais kwa madai ya kukosa uaminifu na msururu wa maoni ya uchochezi ya umma.
โ€œKulingana na hilo, Mheshimiwa Rigathi Gachagua... anakoma kushikilia wadhifa huo,โ€ alisema Spika wa Seneti Amason Kingi.

Mchakato huo hata hivyo, hautakomea hapo. Gachagua amewasilisha maombi kadhaa kupinga shinikizo la kumtimua mamlakani, na jaji mkuu ameteua jopo la majaji watatu kusikiliza hoja zilizowasilishwa.

Gachagua, ambaye amekanusha madai hayo, alipaswa kujitetea dhidi ya mashtaka katika Seneti Alhamisi alasiri kabla ya upigaji kura. Alipokosa kufika, wakili wake Paul Muite alisema naibu huyo wa rais alikuwa amelazwa hospitalini akiwa na maumivu makali ya kifua, na kuitaka Seneti kusitisha shughuli kwa siku kadhaa. Lakini seneti ilikataa kufanya hivyo, na kupelekea timu ya wanasheria wa Gachagua kupinga hatua hiyo na kuondoka bungeni.

Dan Gikonyo, daktari anayemtibu Gachagua, aliwaambia wanahabari kuwa mwanasiasa huyo alilazwa katika hospitali ya Nairobi akiwa na tatizo la moyo Alhamisi mchana, lakini sasa yuko sawa na kuna uwezekano atalazimika kusalia hospitalini kwa saa 24-72. Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, rais ana uhuru wa kumteua naibu mwingine baada ya seneti kuchukua hatua k**a hiyo.

โ˜† Wamzi Hassan

       Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Acks...
14/10/2024


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 14 Oktoba, 2024 amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (CICG) mjini Geneva, Uswisi.

Mkutano huu unalenga kujadili mada kuu inayohusu โ€œMatumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa ajili ya mustakabali wa Amani na Uendelevu.โ€ Mkutano huu umehudhuriwa na takribani washiriki 1,500 wakiwemo Maspika, Naibu Maspika, Wakuu wa Misafara pamoja na Wabunge. Mkutano unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 17 Oktoba, 2024 kwa kutoa maazimio muhimu yatakayolenga kutatua changamoto za kimataifa zinazoikabili dunia kwa sasa.

     Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa...
13/10/2024


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, aliongoza kikao cha K**ati ya Uongozi ya IPU kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani, kilichofanyika tarehe 11 Oktoba 2024, mjini Geneva, Uswisi. Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi Leo tarehe 13 hadi 17 Oktoba 2024, katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Geneva (GICC), Uswisi.

Pamoja na Dkt. Tulia, Wabunge sita wanaowakilisha Bunge la Tanzania katika Umoja huo, wakiongozwa na Mheshimiwa Dkt. Joseph Mhagama, anatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.

TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MIFUKO 50 YA SARUJI KWAAJILI YA UKARABATI SHULE YA MSINGI IKULE RUNGWE.    Rais wa Umoja wa...
12/10/2024

TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MIFUKO 50 YA SARUJI KWAAJILI YA UKARABATI SHULE YA MSINGI IKULE RUNGWE.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust imetoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji kwa shule ya Msingi Ikule Kata ya Masebe Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kwa ajili ya kukarabati ofisi ya walimu ambapo kwa sasa wanatumia moja ya darasa k**a ofisi.

Msaada huo umekabidhiwa na Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tulia Trust Dkt Tulia Ackson.

Mwakanolo amesema Taasisi ilipokea maombi kutoka uongozi wa shule hiyo hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu Taasisi imewiwa kutoa msaada huo Ili kuchochea ubora wa elimu sanjari na kuungana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu.

Innocent Atilyo ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema sehemu kubwa ya shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi ikiwa na madarasa saba na jumla ya watoto zaidi ya mia mbili thelathini ambapo Serikali imetoa milioni thelathini na tano nukta tisa kwa mwaka 2021/2022 kuungana na wananchi.

Bedon Mwasubila ni Diwani wa Kata ya Masebe mbali ya kumshukuru Dkt Tulia Ackson kwa kutoa msaada huo pia amewashukuru wadau mbalimbali wanaochangia ujenzi wa shule hiyo.

Japheth Jema Mwenyekiti wa CCM Kata ya Masebe ameipongeza na kuishukuru Taasisi ya Tulia Trust kupitia Mkurugenzi wake Dkt Tulia Ackson.

Afisa elimu Kata ya Masebe Otino Mwampamba ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa kutoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji kwani itachochea ufanisi kwa walimu ambao hawana ofisi kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Masebe Emmanuel Mwakyambiki amesema msaada umekuja kwa wakati kwani utawapunguzia michango

Shule hiyo yenye walimu watano ,wanne wa kiume na wa k**e mmoja imeanzishwa miaka ya 1960 imekuwa ikikua kitaaluma siku hadi siku.

11/10/2024

๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ
Mchepuko kalipuliwa huku

10/10/2024


MA'DJ KUNUFAIKA NA TULIA STREET TALENT MSIMU WA TANO

Taasisi ya Tulia Trust iliyochini ya Dr. Tulia AcksonDr. Tulia Ackson Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Wa IPU na Mbunge wa Jimbo La Mbeya Mjini Dkt; Tulia Ackson imeandaa tukio kubwa la kifursa upande wa sanaa za burudani zinazowalenga vijana wenye vipaji mbalimbali na kutengenezewa fursa kupitia tamasha la Tulia Street Talent Competition 2024.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani Mbeya Afisa Habari wa Tulia Trust Joshua Mwakanolo leo Oktoba 10,2024 amesema kuwa Tamasha hili linavipengele vikubwa vitano ambavyo ni Kuimba(Singing), kucheza (Dance), Mitindo(Fashion/Model), kuchekesha (Comedy) na DJ Mixing.

โ€œTamasha hili litafanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 27, 2024 kwenye Uwanja wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Mbeya mjini, kuanzia muda wa mchana. Msimu huu utakuwa tofauti na misimu mingine kwa kuhusisha wasanii kutoka tanzania nzima, kwa wasanii wanoamini kuwa tamasha hili ni fursa kwao wanakaribishwa kujisajili kikamilifuโ€ amesema Joshua.

Aidha amesema kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu za kushiriki limeanza Leo Oktoba 10 mpaka Oktoba 20 , 2024 katika vituo vifuatavyo
Mbeya mjini katika ofisi za Tulia Trust Uyole,
Rungwe Ofisi za Tulia Trust na
Kyela Ofisi za Tulia Trust
Kwa waliopo katika Mikoa mingine wawasiliane na Taasisi kwa namba 0657389521 na 0769060738.

Tamasha hili la TULIA street talent competition linaandaliwa kwa msimu wa tano tangu kuanza kwake mwaka 2020.

WAAMBIE BADO TUNAKAZI NAO NA HATUJAMALIZANA NAO

09/10/2024

2019 ๐Ÿ˜ƒ
Mtaje mtu anaekukera sana

Naanza mimi
Tumeachana kwa vurugu, halafu namuona X wangu anatakata. K**a sio kukerana ni nin sasa๐Ÿคจ๐Ÿคจ๐Ÿคจ

KUNA WATU WANAKERA SANA HAPA DUNIANI๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Turudi nyuma   Umemtambua nani na umejifunza nini kuhusu Maisha?๐Ÿ’ช๐Ÿพ๐Ÿ˜Š
08/10/2024

Turudi nyuma

Umemtambua nani na umejifunza nini kuhusu Maisha?

๐Ÿ’ช๐Ÿพ๐Ÿ˜Š

 Yanga sc safari yao ya Makundi inaanzia hapa
08/10/2024


Yanga sc safari yao ya Makundi inaanzia hapa

    Simba SC hawa hapaWatawezana? ๐Ÿ˜€
07/10/2024



Simba SC hawa hapa
Watawezana? ๐Ÿ˜€

     Makundi yote Club Bingwa haya hapa
07/10/2024



Makundi yote Club Bingwa haya hapa

07/10/2024

NEWS

Ajali imetokea Asubuhi ya Leo Oktoba 7. 2024 eneo la SAE Jijini Mbeya, ikihusisha Mabasi mawili ya abilia yaliyogongana uso kwa uso.

Mabasi hayo ni PRIMIER LINE na KAPRICON, ambapo tunaendelea kufatilia idadi ya majeruhi.

Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii.

Address

Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Greencity Tv Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Greencity Tv Online:

Videos

Share