Kaa Tayari, Busokelo TV tutakujuza kila kitu kutoka Dodoma Kwenye Uchaguzi wa Rais wa Tanzania Law Society (TLS)
Subscribe na Tu-Follow kwenye Mitandao ya Kijamii kwa Taarifa zaidi
#busokelotv
Taarifa zaidi Tembelea Busokelo TV
Wafanyabiashara wa soko la Sido Jijini Mbeya na Malalamiko ya Kodi
Urembo wa Kucha Kwa Vijana: Kutoka Picha za Instagram hadi kuwa biashara
Urembo wa kucha umekuwa biashara inayokua haraka sana, na vijana wengi wanavutiwa kujifunza na kufanya kazi katika sekta hii. Kuanzia na picha za Instagram hadi kuanzisha biashara ya urembo wa kucha inahitaji jitihada, ujuzi, na kujitolea
Utunzaji wa Vyanzo vya Maji kwa Njia ya Kisasa
Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Maji wa kisasa nimchakato ambao unaendeleza uratibu wa matumizi ya maji, ardhi na rasilimili zinazo husiana na hizo.
Usimamizi huu Unalenga kuleta manufaa ya hali ya juu zaidi ya kiuchumi na maendeleo ya kijamii kwa kuzingatia usawa bila kuleta athari katika uendelevu wamifumo ikolojia ya maji
Kilimo Cha Mpunga Kilivyo Geuka Fursa kwa Wakazi wa Mbarali
Mbarali ni moja kati ya wilaya zilizopo katika Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania. Wilaya hii ina mazingira mazuri ya kilimo kutokana na ardhi yenye rutuba na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo. Hivyo, kilimo cha mpunga kimekuwa shughuli muhimu na kilichotoa fursa nyingi kwa wakazi wa Mbarali. Hapa kuna maelezo zaidi
Ujenzi wa Shule Shikizi Ulivyo Ongeza Ufaulu kwa Wanafunzi Chunya
Ujenzi wa shule shikizi katika Chunya umesaidia kubadilisha mazingira ya elimu na kutoa fursa bora zaidi kwa wanafunzi kufanya vizuri na kufikia ufaulu mzuri.
Kuwa na wanafunzi wenzao karibu na kujifunza pamoja huzalisha mazingira ya ushindani wa kielimu na kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri zaidi
Tanzama kijana wa ajabu Obasanjo Luchiano akila Panzi akiwa hai😱😱
Anakwambia anaweza kulala chochote kibichi, kuanzia nyama mbichi, minyoo ardhi (worms), Kaa, Nyoka nk nk
Kaa jirani nasi tutakuletea maajabu yake hapa kila tukipata fursa hio
Video 🎥 by Director Iamray More 👌
#busokelotv ##kijanawaajabu #iringa #iamraymore #director
Mradi wa BBT Ulivyo Geuka Fursa kwa Vijana
Ujenzi wa Vituo vya Afya Ulivyo Punguza vifo vya Mama Wajawazito Chunya
Ujenzi wa vituo vya afya katika Chunya umesaidia kuboresha huduma za afya kwa mama wajawazito na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito katika eneo hilo Vituo vya afya vina uwezo wa kutoa huduma za dharura kwa mama wajawazito wakati wa matatizo ya kujifungua, na hivyo kuokoa maisha yao
Kifahamu Kilimo cha zao la Ngano
Ngano inaweza kutoa mapato mazuri kwa wakulima. Bei za ngano zinaweza kuwa nzuri sokoni, na hii inaweza kusaidia wakulima kuongeza kipato chao.
Ngano ni zao la chakula na inaweza kutumiwa kutengeneza mikate, unga, na vyakula vingine vya nafaka. Hii inaifanya kuwa chanzo cha chakula cha msingi kwa idadi kubwa ya watu nchini Tanzania.
Utupaji Taka Ovyo,Unavyo Hatarisha Vyanzo Vya Maji
Kumekuwa na Ongezeko la wananchi wa jiji la Mbeya kuwa utupaji taka ovyo,kutokana na hali hiyo imepelekea wananchi kuanza kutupa taka taka kwenye vyanzo vya maji kama Nzovwe
Kilimo cha Michikich Kilivyo Geuka Fursa Kwa Wanannchi Wilayani Kyela
Kilimo cha michikichi (palm oil) katika Wilaya ya Kyela, Tanzania, kimegeuka kuwa fursa muhimu kwa wakazi wa eneo hilo kwa njia kadhaa
Kilimo cha michikichi kinaweza kutoa mapato mazuri kwa wakulima wa Kyela. Michikichi inatoa mafuta ambayo ni bidhaa muhimu katika tasnia ya chakula na viwanda vingine.
Kupanua Uchumi: Kilimo cha michikichi kina uwezo wa kupanua uchumi wa eneo la Kyela kwa kutoa fursa za biashara na ajira katika sekta ya kilimo na usindikaji wa mazao ya michikichi.
Uboreshaji wa Lishe: Mafuta ya michikichi yanaweza kutumiwa katika vyakula vya kila siku, kusaidia kuongeza lishe ya wakazi wa Kyela.
Michikichi inaweza kutumika katika kutengeneza bidhaa za viwandani kama sabuni, mafuta ya kulainisha ngozi, na mengineyo. Hii inaweza kuwa na faida kwa viwanda vya ndani.
Ulanzi Ulivyogeuka Fursa Kwa Wananchi wa Wilaya ya Makete
Ulanzi ni kinywaji kinachotokana na mmea wa muanzi unaotoa majimaji kama utomvu wa mpira lakini hiki ni kimiminika laini kama maji ya kunywa chenye ladha ya utamu.
Maji haya yanakusanywa kutoka katika mti wa muanzi kwa kutumia kifaa maaalum kama chupa kinachoitwa mbeta. Ugemaji wake ni mara tatu kwa siku, asubuhi ambapo ulanzi unaondolewa kutoka kwenye mbeta na kuwekwa kwenye maplastiki ya ujazo wa lita 20 au ndoo ndogo ndogo.
Mchana ni kugema au kupyatila kama inavyojulikana ambapo mmea huu unakatwa kidogo kwenye ncha ya juu pasipo kutoa ulanzi kutoka katika mbeta na hatimaye jioni mgemaji anatoa ulanzi kama zoezi la asubuhi.
Kuongezeka Ajali za Pikipiki: Je, Ni Wakati wa Kuchukua Hatua?
Licha ya kutoa ajira kwa maelfu ya vijana wa Kitanzania na pia kupunguza tatizo la usafiri mijini litokanalo na foleni, usafiri wa pikipiki maarufu kama 'bodaboda' umeendelea kuua watu kimyakimya na kuwasababishia ulemavu wa kudumu maelfu ya manusura wa ajali za vyombo hivyo kila uchao.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mbali na vifo na ulemavu, bodaboda zimeathiri pia utoaji wa huduma katika hospitali zinazopokea majeruhi wa vyombo hivyo, na wahanaga wakubwa wa ajali hizo ni vijana wa kiume wenye umri wa miaka kati ya 20 na 40
Jiji la Mbeya Kuzongwa na Makanisa
Wakati Mbeya inatajwa kuongoza kwa uwingi wa madhehebu ya dini, mkoa huo pia umekuwa na matukio mengi ya kikatili na kutisha ambayo yameacha kumbukumbu mbaya mbele ya jamii ya Watanzania.
Jiji la Mbeya pekee linatajwa kuwa na madhehebu 450 ya dini za aina mbalimbali, lakini mkoa huo umegubikwa na imani za kishirikina, ukatili, uporaji na mauaji huku baadhi ya madhehebu yakitajwa kupandikiza imani kali zisizozingatia mwelekeo wa Kikristo au Kiislamu
Fahamu Faida ya Kilimo cha Pareto
TANZANIA ni Moja ya Nchi ambayo imekua iking’ara katika soko la dunia kupitia zao la Pareto, zao ambalo baadhi ya wakulima wameligeuzia kisogo, licha ya zao hilo kuwa na mauzo mazuri kwa kilo, ukilinganisha na mazao mengine ambayo yamezoeleka
mahitaji ya Pareto kwa sasa yameongezeka mara dufu, baada ya nchi za Kenya na Tasmani ambazo zilikuwa kikiongoza kwa uzalishaji wa zao hilo duniani kuanza kudolola, kutokana na soko la zao hilo kuyumba miaka ya 2004 na 2005
Sambamba na kuwepo kwa nchi kama, Kenya, Rwanda, Uganda, Tasmania na Papua New Guinea ambazo zinazalisha pareto duniani, bado mahitaji ya soko la Pareto duniani yanafikia tani 20,000 kwa mwaka, huku nchi zote hizo zikishindwa kufikisha hata tani 10,000 kwa mwaka
Mfumo wa Stakabadhi Gharani Ulivyo Wanufaisha Wakulima wa Kokoa
Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na matumizi ya chokoleti duniani, wakulima wa kokoa katika wilaya za Kyela na Rungwe wameanza kufaidika na soko la zao hilo baada ya kuanzishwa kwa Mfumo stakabadhi gharani.ambao unatajwa kuleta neema kwa wakulima
Serikali Ilianzisha Mfumo wa wakulima wa zao hilo kuuza kwa stakabadhi gharama ili kuweza kukomboa mkulima ambaye kwa muda mrefu alikuwa ananyonywa na walanguzi kwa kupangiwa bei ambazo zilikuwa hazimnufaishi mkulima.
Wanawake Wanavyo Zibeba Familia Kupitia Biashara ya Ndizi
Tumezoea kuona familia nyingi za kitanzania,baba wa familia ndiyo nguzo ya utafutaji wa fedha kwa ajili ya kulea familia,kwa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya hii ni tofauti ambapo wanawake ndiyo wamekuwa nguzo ya katika malezi ya familia zao kwa kufanya biashara ya kuuza ndizi.
Wanawake wengi katika wilaya ya Rungwe shughuli yao kubwa ya kujingizia kipato ni biashara ya kuuza ndizi kwenye vituo vya mabasi pamoja na masoko ya Tandale,Kiwila,Lufingo,Ikuti,Kyimo na Ushirika