Hadithi Zetu

Hadithi Zetu ᴋᴀʀɪʙᴜ sᴀɴᴀ ᴋᴀᴛɪᴋᴀ ᴍᴀᴋᴛᴀʙᴀ ʏᴀ ʜᴀᴅɪᴛʜɪ. ᴜᴋᴜʀᴀsᴀ ʜᴜᴜ ɴɪ ᴍᴀᴀʟᴜᴍᴜ ᴋᴡᴀ ᴋᴀᴢɪ ᴢᴀ ғᴀsɪʜɪ & ᴍᴀᴋᴀʟᴀ ᴍʙᴀʟɪᴍʙᴀʟɪ. Pia, tunatoa makala mbalimbali kwenye ukurasa wetu.

Hadithi Zetu ni ukurasa wa Facebook ambao una lengo la kuchapisha kazi za fasihi andishi, simulizi, na makala mbalimbali. Ukurasa huu umeundwa ili kuhuisha na kueneza urithi wa hadithi na tamaduni za Kiafrika kupitia njia ya maandishi. Tunajitahidi kuwa jukwaa la kuelimisha, kuburudisha, na kuhamasisha wengine kwa njia ya hadithi. Kwenye ukurasa wetu, utapata aina mbalimbali za kazi za fasihi andi

shi, ikiwa ni pamoja na hadithi za kusisimua, mashairi, riwaya fupi, na tamthilia. Tunajitahidi kuchapisha kazi zenye ubora na zinazogusa masuala mbalimbali yanayohusiana na jamii, utamaduni, upendo, mazingira, na masuala mengine ya kijamii. Mbali na kazi za fasihi andishi, tunatoa pia simulizi mbalimbali za kuvutia. Hizi ni hadithi za kusisimua, za kuburudisha, na zenye kuelimisha. Simulizi zetu zinaweza kuwa za kisasa au za jadi, zinazohusisha wahusika wenye maisha ya kuvutia na matukio ya kusisimua. Lengo letu ni kutoa burudani na kuwafanya wasomaji wetu kujisikia kushiriki katika ulimwengu wa hadithi. Makala hizi zinajadili mada mbalimbali za kijamii, utamaduni, sanaa, na masuala mengine yanayohusiana na fasihi na simulizi. Tunazingatia kutoa taarifa sahihi na za kuvutia ili kuhamasisha majadiliano na kuelimisha wasomaji wetu. Tunakaribisha wanachama wote wa jamii kuungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook, Hadithi Zetu. Tunahimiza ushiriki wa wadau wa fasihi, waandishi, wasomaji, na wapenda hadithi katika kuchangia kazi zao, kutoa maoni, na kushiriki maarifa na uzoefu wao. Tunatumai kuwa Hadithi Zetu itakuwa sehemu ambayo itawawezesha watu kugundua, kuelimika, na kufurahia upekee wa hadithi za Kiafrika na tamaduni zetu. Karibu sana kujiunga na jumuiya yetu na kushiriki katika uumbaji wa hadithi za kuvutia na za kuelimisha.

📌𝐈𝐌𝐄𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝑴𝑨𝑳𝑰𝑺𝑨 𝑮𝑱 wa 𝗚𝗛𝗙 𝐍𝐀𝐈𝐒𝐎𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐊𝐖𝐀𝐊𝐎 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎.⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇Naitwa Veronica Alphonce (27) mkazi wa K...
03/11/2024

📌𝐈𝐌𝐄𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝑴𝑨𝑳𝑰𝑺𝑨 𝑮𝑱 wa 𝗚𝗛𝗙 𝐍𝐀𝐈𝐒𝐎𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐊𝐖𝐀𝐊𝐎 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎.

⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇

Naitwa Veronica Alphonce (27) mkazi wa Kipawa, DSM. Mwaka 2022 nilifunga ndoa bwana Lawrence John na tukaishi k**a mume na mke. Aprili Mwaka 2023 nikiwa na mimba ya miezi 8, mume wangu alianguka bafuni na kujigonga sehemu ya nyuma ya kichwa kwenye sakafu. Tulimkimbiza hospitali lakini akawa amepoteza maisha.

Mwezi mmoja baadae nilijifungua mtoto wa k**e na kumpa jina Clarence ambalo baba yake alikua amelipendekeza kabla ya kifo chake. Bahati mbaya mwanangu alizaliwa na tatizo la kichwa kikubwa (Hydrocephalus). Madaktari walisema maji yanayojulikana kitaalamu k**a (cerebral spinal fluid) yamezidi kwenye ventrikali (ventricles) au nafasi zilizo wazi (cavities) kwenye ubongo.

Matibabu yake ni kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa mpira maalumu utakaohamisha maji kichwani ili yaende kwenye mzunguko wa damu, external ventricular drain (EVD). Gharama za upasuaji huo ni 2M lakini nilishindwa kuzimudu kutokana na hali ngumu ya maisha baada ya kifo cha mume wangu.

Mimi Najishughulisha na kilimo cha tembele ambacho kinatosheleza mahitaji ya kula tu mimi na mwanangu. Kutokana na kukosa huduma kichwa chake kimekua kikiongezeka ukubwa kila siku. Pia amekua mtu wa kulia mara kwa mara, kushindwa kunyonya vizuri, utosi kuvimba na kupata degedege. Naomba watanzania wanisaidie mwanangu aweze kufanyiwa upasuaji ili nisimpoteze k**a nilivyompoteza baba yake.

:
Kwanza nawashauri akina mama tumieni Folic Acid mkiwa wajawazito. Tatizo la kichwa kikubwa (Hydrocephalus) na lile la mgongo wazi (Spina bifida) kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na ukosefu wa folic acid wakati wa ujauzito.

Pili tujipe masaa 12 tu ya kuokoa maisha ya mtoto Clarence. Ifanye sadaka yako ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya mwezi Novemba iwe maalumu kuokoa maisha ya Clarence. M-PESA #0752581983, Tigopesa #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation.

✅FBI ni moja ya series zangu pendwa kabisa.❓Wewe Je?
18/10/2024

✅FBI ni moja ya series zangu pendwa kabisa.

❓Wewe Je?

📌Picha hizi zinatoka pale kaunti ya Antu, kaskazini mwa China katika jimbo la Jilin, Xueshanfeihs ni eneo la kitalii kut...
08/10/2024

📌Picha hizi zinatoka pale kaunti ya Antu, kaskazini mwa China katika jimbo la Jilin, Xueshanfeihs ni eneo la kitalii kutokana na mazingira yake hewa nzuri inayopatikana katika eneo hilo.

Sisi huku Tanzania tunakata miti hadi iitike "Rabeca" tukiambiwa ukikata mti panda mti, masikio hayasikii hata kidogo.

Wasimamizi wa hifadhi nao baadhi yao hawana uadilifu, wanakula rushwa na kuwarudisha nyuma wenzao wanaosimamia sheria kuonekana ni wanoko sana.

Tunajitetea kuwa "tukale wapi?" "Tusipochoma mkaa tutapata wapi pesa ya kuendesha familu?" Jiulize, hiyo familia (Watoto) wakikua wao watafaidika na nini k**a unakata na kumaliza miti yote kwa kuchoma mkaa?

Serikali mnapowak**ata hawa wachoma mkaa na wauza mkaa, mnawapeleka mahak**ani wanahukumiwa au mnawapiga faini mnawaacha waende mkaa mnautaifisha, mnadhani hawa wataenda wapi?

Kwanini serikali msiweke mpango nzuri kila Halmashauri, kuwakusanya hawa wakata miti, wachoma mikaa na wauza mikaa mkawapa project nyingine ya kuwaingizia kipato kupitia misitu hiyo hiyo na project zingine?
Mfano: Unawaweka kwenye vikundi mnawaanzishia mradi wa kufuga nyuki, wakilinda asali wanawauzia kikundi kingine wanaiongezea thamani asali ile hapo mnakuwa mmewaunganisha na SIDO.
Wengine wanashughulika na mazao mengine yanayozalishwa na nyuki kutengeneza nta nk.

Ifike wakati tufikirie tofauti, tusione ni fahari kujaza magereza tu, matatizo/changamoto na tabia za watu zibadilishwe na kutengenezwa fursa. Fursa hizo ziwasaidie kujiingizia kipato na kutunza mazingira yetu kwa vizazi vya sasa na vya baadae.

🖊Geofrey D.

🔴BOND BY LOVE: The Tale Of Frank And AminataThe cheerful and hardworking young man Frank had big dreams of becoming a su...
07/10/2024

🔴BOND BY LOVE: The Tale Of Frank And Aminata

The cheerful and hardworking young man Frank had big dreams of becoming a successful entrepreneur in Tanzania. However, everything changed when he met a beautiful and kind-hearted girl from Cameroon named Aminata.

Aminata was a university student at the University of Dar es Salaam studying medicine. They met at a social event and Frank was instantly drawn to Aminata’s smile and intelligence.

In a short period of time, Frank and Aminata got to know each other well and eventually started a relationship. Frank was fascinated by the Cameroonian culture that Aminata introduced him to, teaching him about their customs and traditions. He began learning the French language and enjoying Cameroonian cuisine.

However, their love story faced many challenges. At times, Frank would feel heartbroken because of the cultural differences that caused them to argue. Nevertheless, their love was strong and they decided to work hard to maintain their relationship.

After several months of their relationship, Frank decided to propose to Aminata and she gladly accepted. They had a beautiful wedding that left many envious, and their love grew even stronger.

Together, Frank and Aminata collaborated in business and other development projects, becoming a powerhouse in the economies of Tanzania and Cameroon. They showed that love knows no boundaries or cultural limits and that everything is possible in love.

Frank and Aminata were blessed with two children and continued to live a happy and loving life until their old age. They were a great example for young people who wanted to build strong relationships based on love and respect. Their lives were a true story of enduring and conquering all challenges through true love.

📌UJANA⭕Maisha ya ujana ni kipindi cha furaha, changamoto, na uzoefu wa kipekee. Ni wakati ambapo tunajifunza mengi kuhus...
03/10/2024

📌UJANA

⭕Maisha ya ujana ni kipindi cha furaha, changamoto, na uzoefu wa kipekee. Ni wakati ambapo tunajifunza mengi kuhusu dunia na waishio juu ya uso wa Dunia. Tufurahie kila hatua ya safari yetu ya ujana na tujifunze kutokana na kila changamoto tunayopitia. Maisha ya ujana ni zawadi, tunapaswa kuitumia kikamilifu na kufurahia kila wakati.

K**a uliwahi kusikia Maskini anaitwa Freemason nyoosha mkono juu.....K**a uliwahi kusikia Tajiri anaitwa mchwawi, nyoosh...
29/09/2024

K**a uliwahi kusikia Maskini anaitwa Freemason nyoosha mkono juu.....

K**a uliwahi kusikia Tajiri anaitwa mchwawi, nyoosha mkono juu......

🔴Kwenye maisha huwa tunakutana na changamoto nyingi sana. Majaribu ya kila aina huwa yanakuja mbele yetu, kila jaribu li...
17/09/2024

🔴Kwenye maisha huwa tunakutana na changamoto nyingi sana. Majaribu ya kila aina huwa yanakuja mbele yetu, kila jaribu linalokuja mbele yako linakutaka upambane na ushinde.

Karibu upate nakala yako y simulizi hii ya kusisimua iitwayo JARIBU LA USHINDI. Gusa Link hapo chini kujipatia nakala yako.

Mungu alipotuumba wanadamu alituwekea na vipimo vya kutupima ili kutujua k**a kweli tunaweza kufuata au kuishi kwa kufuata maelekezo yake. Hata mzazi anapotaka kumpa kitu mwanaye, jambo la kwanza atampa mtihani mwanaye kumpima kujua jambo fulani na atakapojiridhisha basi atampatia kitu hicho. Ndani....

📌Wewe ni mpenda hadithi?Jipatie Nakala yako ya hadithi ya CHUKIZO kwa  gharama nafuu sana.
16/09/2024

📌Wewe ni mpenda hadithi?
Jipatie Nakala yako ya hadithi ya CHUKIZO kwa gharama nafuu sana.

Katika maisha huwa tunafanya makisa na mara nyingi tunapofanya akosa hayo huwa tunasahau kabisa k**a tumewahi kufanya makosa katika maisha yetu. Tunawewza kufanya makosa hayo kwa kujua au kwa kutokujua na mara nyingi huwa tunajua k**a tunafanya makosa lakini tunapuuzia na kuona hakuna chochote kinac...

🌹SIMULIZI FUPI - BADO NAMKUMBUKA✴Miaka saba iliyopita, alikuwa mrembo haswa, alikuwa kila kitu kwangu, rafiki, ndugu, ji...
02/09/2024

🌹SIMULIZI FUPI - BADO NAMKUMBUKA

✴Miaka saba iliyopita, alikuwa mrembo haswa, alikuwa kila kitu kwangu, rafiki, ndugu, jirani pia mpenzi.Halikuwa jambo la ajabu nilipotafutwa aliulizwa naye alipokuwa akitafutwa nilitafutwa mie walijua tupo pamoja.Darasani tulikuwa pamoja ingawa alikuwa kidato kimoja nyuma yangu ,uwanjani wote tulicheza mpira wa wavu hata UMISETA haikututenga bali tulikuwa pamoja, mitaani ,kanisani hata siku ya disco tulicheza pamoja.Kwa kifupi tulijiona 'mwili mmoja'.....

Si mwingine bali Alice mwanamke aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa kikubwa k**a mchezo na nikajikuta nikiufurahia ulimwengu huo, niliowakera walikuwa wengi ingawa kulikuwa na wachache waliofurahia mahusiano yetu na wengine ambao hawakujua wawe upande upi...nakumbuka wimbo wa AT na Marlow "wanimaliza" ulivuma kipindi penzi letu lipo juu.... Maskini Alice wangu, mrembo aliyekuja kujutia kitendo chake cha kunikabidhi pendo lake kwa kitendo kibaya nilichomfanyia bila kunikosea.

Kweli Alice aliyajutia maamuzi yake ya kunipenda,kuniona mwanaume sahihi wa maisha yake kuniona mtu mwenye makosa ambayo alikuwa tayari kuyavumilia.Lakini nilipoondoka na kwenda kidato cha tano kwenye shule moja jijini Mwanza nikajikuta namsahau taratibu, na nikajiona mjinga kuuona uzuri usoni na mwilini mwake.Nikaanza kuzikumbuka kasoro zake, hakuwa mweupe ,hakuwa 'modo' k**a wengi niliowaona wazuri shuleni na mitaani, hakungea kiswahili kilichonivutia k**a wasichana wengi darasani kwetu.

Ghafla nikamchukia kwa kunifanya nimpende na kunipotezea muda, sikumhurumia kwanza nilizichana picha zake ambazo daima nilikuwa nikizitizama kila nilipotaka kulala nikizibusu, nikachana na kuzichoma kadi zake alizokuwa akinipa tukiwa shuleni ,hata shati zuri la kisasa alilonipa siku ya mahafali yangu wala sikukumbuka, kilio chake siku tulipoagana, nikayaita yale mapenzi 'ya kitoto' nikijiambia "atakuwa kapata mwanaume mwingine bhana, mfupi ka kopo la blueband'' Kwa kifupi nilimwona si kitu lakini....! Baada ya kujifanya nimetambua kasoro za Alice mwanamke aliyejitoa kwangu kwa kila kitu, nikaanza kumtafuta wa kuziba 'mwanya' aliouacha nafsini kwani niliona hukufikia hatua ya kuacha 'pengo'.
Lakini kabla sijaamua kumuacha niliwaza visababu ambavyo ningedai vilikuwa chazo cha kumuacha lakini sikuvipata, nilijaribu kumkera 'aropoke' kwenye simu lakini wapi,nikabuni mchezo wa kumtongoza kwa namba mpya ila wapi mtoto alikuwa kaganda kwangu.Ikafika siku ambayo nilijua iwe isiwe atanaswa na nikamnasa kwa kisa ambacho leo naweza kiita cha kipumbavu eti "aliandika sms kwa herufi kubwa na hakuweka mkato na nukta", nikamuacha.Akili ikatulia kuchagua mrembo shuleni kwetu nilimfikiria Helen binti wa kihabeshi aliyechanganya damu ya Rwanda na Ethiopia lakini kukaa kwake bwenini hakunifurahisha nikamfikiria Violet Mushi dada mkuu lakini tetesi za kuwa alikuwa zaidi ya waumbuaji wa pendapenda nikaachana na fikra hizo hadi nilipomfikiria Harriet jirani yangu mtaani na darasani hapo nikaona poa lakini....!

Harriety msichana mrembo kutokea mkoani Iringa aliyekuwa akiishi na shangazi yake jirani kabisa na nilipokuwa nikiishi na familia ya baba yangu mdogo alikuwa chaguo langu kuziba nafasi ndogo aliyokuwa ameiacha Alice.Kwa kuwa nilikuwa nikisoma naye darasa moja akiwa dawati la pembeni yangu haikuwa kazi ngumu kujenga mazoea 'puuzi' yaliyopelekea ujirani nyumbani na shuleni kabla ya kufanikiwa kuuteka moyo wake 'kimiujiza' kwani tulijikuta tumekula tunda bila hata kuombana ama kuambiana kuwa tulikuwa tukipendana.Kisha tukawa wapenzi.Kipindi hicho Alice hakuacha kunipigia akiomba nimsamehe k**a palikuwa ambapo alikosea ,sikutaka kujibu jumbe zake wala kupokea simu yake.Moyoni mwangu nilimweka Harriety hivyo sikutaka kuharibu penzi langu jipya kwa mwanamke ambaye nilijihisi kuwa nimepotea njia kwa kuendelea kushughulika naye, nikabadili namba ya simu kuukwepa 'usumbufu' wake lakini masikini Alice hakukata tamaa alitumia njia zote kupata namba yangu mpya na kunipigia jambo lilimfanya ujute..

Ndiyo alijuta kwani siku ile nilipojua kuwa ameipata namba yangu ya simu kupitia mdogo wangu ambaye alikuwa akisoma kidato cha kwanza na katika shule aliyokuwa akisoma Alice, nikaamua kumwachia simu Harriety ambaye hadi leo hii ninapoandika sijui alimwambia kitu gani kwani niliukuta ujumbe mmoja wa neno "Asante" kutoka kwa Alice.Sijui ni jambo gani ambalo mwanamke yule alimwambia Alice maana hata ninapoandika ujumbe huu nakumbuka sehemu ya barua hii ambayo baada ya miaka miwili ya kukaa nayo bila kuisoma nimeamua kuisoma na kugundua kuwa nilimtenda vibaya sana Alice mwanamke ambaye alinipenda sana na nahisi ananipenda hadi leo huko aliko.

Mpenzi najua unajua jinsi gani nakupenda licha ya maumivu makali uliyoniachia moyoni mwangu lakini naomba ukumbuke kuwa nakupenda na nitakupenda milele japo nina hakika siwezi kuwa wako tena.Si kwa sababu unaye ambaye anakupa kiburi na kukufanya uhisi kuwa hunihitaji tena , hapana ila ni kwa kuwa siwezi kuwa na wewe tena.Ndiyo siwezi na unaweza ukajiona huhitaji kuwa na mimi na hata ikakuchukua muda mrefu hadi kuamua kuisoma hii barua ila tambua sitoweza kuwa na wewe tena ingawa nakupenda na UNANIPENDA kwa dhati mpenzi.

Unanipenda nalijua hilo na ndiyo maana umeamua kuisoma barua hii.Umedanganywa na uzuri wa Harriety, sawa ni mzuri ila Hakupendi na wala si saizi yako huyo si wa kuolewa bali wa kufanyia mauzo , naam kila mtu anampigania afanyie mauzo mtaani na ndicho akifanyacho we hujui.

Utajuaje wakati anakulevya na penzi lake na uzuri wake autumiao k**a silaha kwako? Sitaki kukulaumu sana kwa kuwa najua ni wanaume wengi sana ambao wangemtamani Herriety hata mie ningemtani ningekuwa wanaume k**a wewe.Siku nilipomwona mara ya kwanza nikajiona kabisa sistahili kushindana naye kukupenda ingawa baadaye nikatambua si mwanamke mwenye mapenzi kwako. Najua hujui ni lini na vipi nilikutana naye lakini naomba nikuambie ukweli huu mchungu kuwa Harriety hakuwa mwanamke mwaminifu, zaidi ya mara ya tatu nimemshuhudia akigombanisha wanaume kwa sababu ya usaliti wake.

Matilaba ya barua yangu si kukuambia kasoro za mpenzi wako Harriety bali ni kukuambia kuwa nakupenda na nakukumbuka pia ingawa siwezi kuwa na wewe , unajua kwanini? Nadhani hujui ingawa utakuwa unabashiri, ngoja tuu nikwambie ukweli Herriety namfahamu na nimekua naye na kucheza naye.Likizo zote tumekuwa tukishinda pamoja na alikuwa akijua wewe ni mpenzi wangu na nilikuwa nikimjua mwanaume aliyekuwa akimpenda sana ingawa tangu zamani uzuri wake umemfanya ashindwe kuikwepa mitego aliyokuwa akitegewa na wanaume "mifisi" yenye tamaa k**a wewe na kujikuta akijihusisha na wanaume wengi kimapenzi bila kupenda hatimaye akaamua kuendelea na tabia hiyo.

Katika kuumia kwangu baada ta kukukosa nikaamua kumuumiza kwa kutembea na mwanaume ambaye alimpenda kwa dhati,kitendo kilichoharibu maisha yangu kwani licha ya kupata kisonono na Virusi vya UKIMWI nilikutana na kipigo kitakatifu baada ya kufumwa na mwanamke ambaye naye alikuwa akimpenda zaidi ya Herriety leo hii ninapoandika nipo Hospitalini nikijaribu kupambana na maumivu ya majeraha ya moto na visu kwani baada ya kufumwa gesti nilichomwachomwa visu vya haja na kutolewa nje nikiitiwa mwizi ambapo nikaonja kidogo maumivu ya mawe na kuchomwa kwa petroli kabla ya polisi waliokuwa doria kuniokoa. Najua utashtuka lakini kushtuka kwako hakutokiokoa na kifo kwani nisipokufa kwa mateso haya basi nikitoka hapa nitajiua maana nimetia aibu kubwa familia yangu nawe unawajua wazazi wangu.

Nikupendaye Alice, naomba usisahau kituko hiki cha mapenzi yetu ya kitoto; pale nilipokusindikiza hadi kwenu kisha nikalala chumbani kwako huku kaka yako na mdogo wako uliyekuwa ukilala naye chumba kimoja kujua. Kituko hiki hunipa tabathamu na nguvu mara chache na nikaamini unanipenda kweli.

Nilimaliza kuisoma barua hiyo kwa tabathamu, si kwa sababu ya kufurahia mateso yake bali ni kituko ambacho hata yeye kuwa katika mateso aliweza kutabathamu.Najua hata wewe unaweza kutabathamu ngoja nikuambie. Siku moja kabla ya kwenda Mwanza kujiunga na kidato cha tano nilienda hadi shuleni ambako Alice alikuwa akisoma. Ulikuwa ni mwendo wa saa k**a mbili hadi mbili na nusu, lakini kwa kuwa nilikuwa nikienda kumuaga niliyekuwa nikimpenda niliona ni k**a safari fupi tuu ya kwenda chooni. Baada ya kuongea hili na lile na mpenzi wangu Alice nikataka kuondoka lakini hakukubali kuniacha niende peke yangu akadai angenisindikiza kidogo.

Nami bila hiyana nikamkubalia na tukaianza safari yetu ambayo ilijaa huba kwa kuwa ilipita kwenye njia iliyokuwa msituni hivyo upweke na ukimya wa njia ulinogesha safari. Taratibu tukiwa tumeshikana mikono wakati mwingine tukikimbuzana ama kufanyia vituko mbalimbali ili mradi kukoleza huba tukajisahau na kujihisi tulikuwa tukisafiri wote na si kusindikizana tena.Baada ya saa tatu ambapo ilikuwa saa moja tukajikuta tumekaribia nyumbani kwetu. "He! imekuwaje tumefika huku?" Aliuliza baada ya kuwa hatua k**a ishirini kutoka nyumbani kwetu.

"Sijui'' Nilimjibu nikitafakari cha kufanya. "Na sina ndugu hapa kijijini kwenu ningezuga hata kuumwa"Aliongea huku bado nafikiria lakini mara tukasikia sauti nilizozifahamu.Alikuwa baba yangu akipita njia ile ile tuliyokuwa akielekea nyumbani kwa babu huku akilalamika mie kutoonekana siku ile wakati nilikuwa na safari. Ni sauti aliyoitambua kwani ilifanana sana na yangu , bila kumweleza alikimbilia kwenye kichaka kilichokuwa karibu huku nikijifanya ninakimbia kuelekea nyumbani na mara nikakutana na baba. "Ulikuwa wapi?" Aliuliza akiwa na hasira.

"Nilienda shuleni kuna mtu alikuwa na picha zangu za mahafali" Nilimjibu nikimpa kibahasha ambacho nilikuwa nikiomba Mungu asikipokee na sijui ni Mungu ama shetani hakukipokea kwani kilikuwa na picha za Alice tuu hakukuwa na picha yangu hata moja. " Shika huko siku zote ulikuwa wapi?, tunakuambia mara nyingi uwe unajiandaa lakini hadi dakika ya mwisho unatuhangaisha nakwambia utaachwa hata siku ya kiyama" Alimalizia kwa utani ambao alikuwa akipenda kuutumia na kumfanya hata mama yangu aliyekuwa na hofu kubwa atabathamu kwani kosa langu lilionekana k**a lake alikuwa akifokewa na baba tukikosea k**a vile ndiye aliyekuwa akitutuma tukosee.

Yakaisha tukafikia sebuleni ambako tulikuta wanafamilia wengine wameshakula.Nikalamna kisha kikao cha wanafamilia kilifanyika kikiwahusisha wazazi kaka yangu mdogo wangu na dada zangu ambao walinipa baraka zao na mafunzo mengi ambayo nahisi hayakuniingia kwani nilikuwa namfikiria Alice kule kichakani alikokuwa amejificha. Saa tano usiku tukaingia kulala ambapo nilitakiwa kuwasubiri ndugu zangu niliokuwa nikilala nao chumba kimoja japo vitanda tofauti walale kisha nikatoka kwenda kumchukua Alice pale kichakani alipokuwa amekaa kwa saa tano.

Ingawa alikuwa na njaa hakutamani chakula hivyo tukaingia kwa kunyata chumbani kisha kulala hadi alfajiri sana ambapo nikamtoa hadi stendi akijifanya msafiri ama anamsindikiza mtu kisha kurudi nikisaidiwa na tabia yangu ya kufanya mazoezi kila asubuhi hivyo nilivyorudi natokwa jasho hakuna aliyenishangaa kati ya wote niliokuta wameamka tayari kunisindikiza stendi. Baada ya kuoga tukaondoka na ndugu zangu hadi stendi. Nikaangaza huku na huko bila kumuona hadi pale gari lilipokaribia kuondoka nikamwona akinipungia mkono wa kwa heri kabla ya kutupa busu lake hewani nami nikimjibu kwa tabathamu. Ni k**a jana hivi lakini miaka saba imepita tangu tukio hilo la kufurahisha litokee.

Hapo nikaanza kukumbuka mambo mazuri na ya kuvutia tuliyowahi kutafana na Alice hapo zile chembechembe za huba zikachipua tena na kujiona namhitaji Alice ambaye kwa barua yake amedai alilazwa zaidi ya mwezi mzima lakini ile barua nimeisoma miaka miwili baada ya kuipokea. Nikaaamua kumpigia Harriety ambaye kugombana naye kutokana na kukosea kunitumia meseji ya mwanaume mwingine ndiko kulinifanya nimkumbuke Alice na kuisoma barua yake ambayo niliipuuza kwa miaka miwili ikiwa ndani ya bahasha bila kufunguliwa. Alipokea simu na kuwa mkali k**a kawaida yake akinikosea akiamini kuwa ningepoa na kumwomba msamaha k**a alivyozoea hata akikosea.Nikamuuliza k**a alikuwa na taarifa zozote juu Alice.

"Kumbe unajua tunafahamiana naye? pole sana Alice alifariki mwaka juzi kwa kisa cha kusikitisha sana nasikia aliiba hivyo akachomwa moto pole sana mpenzi" Aliongea kwa sauti ambayo sikuielewa k**a ilikuwa ya uchungu ama kebehi. Sikumbuki k**a nilifanikiwa kukata simu na chozi likanitoka nikijiona mkosefu. Ni miezi miwili baada ya kuisoma ile barua na kupata taarifa juu ta kifo cha Alice na ni siku moja tangu nitoke kuliangalia kaburi la Alice ambaye sikumwambia neno lolote zaidi ya kumweleza kuwa BADO NAMKUMBUKA k**a yeye alivyodai kwenye barua kuwa Ananikumbuka. Siamini Alice kipenzi changu BADO NAKUKUMBUKA NA NITAKUKUMBUKA MILELE....

Mwisho

🌹𝐇𝐚𝐩𝐩𝐲 𝐁𝐢𝐫𝐭𝐡𝐝𝐚𝐲 𝐀𝐮𝐧𝐭 Tedy Mgaya🌹Ishi sana Aunt angu🎂🍾🥂
25/08/2024

🌹𝐇𝐚𝐩𝐩𝐲 𝐁𝐢𝐫𝐭𝐡𝐝𝐚𝐲 𝐀𝐮𝐧𝐭 Tedy Mgaya🌹

Ishi sana Aunt angu🎂🍾🥂

27/07/2024

📌Niliamua kupita kwenye page kadhaa ikiwemo Samson Charles , Malisa GJ, East Africa TV, millard ayo ili kujua undani wak...
22/07/2024

📌Niliamua kupita kwenye page kadhaa ikiwemo Samson Charles , Malisa GJ, East Africa TV, millard ayo ili kujua undani wake na hiki ndicho nilichokutana nacho, Boniface Mwaitege Yuko hai.

NB:
Ukiona taarifa usiwahie kupost ili upate Likes na Comment nyingi, thibitisha kwanza ndipo upost itakuongezea credit kuliko kukurupuka....

📌NIMEKAA NIKAWAZA📌🔴Wafanyabiashara wadogo wengi hasa nyakati hizi wanamalengo ya kufika mbali. Wana ndoto za kuwafikia w...
22/07/2024

📌NIMEKAA NIKAWAZA📌

🔴Wafanyabiashara wadogo wengi hasa nyakati hizi wanamalengo ya kufika mbali. Wana ndoto za kuwafikia wateja wengi, kuwafikishia huduma na bidhaa popote walipo ndani na baadae nje ya maeneo yao, lakini wana struggle kufikia ndoto hizo ukizinfatia pia mitaji yao ni midogo na uwezo wa kutake risk nao ni mdogo. Hivyo wanarudi nyuma.

🔵Nimejaribu kuwaza, mfano akitokea au wakitokea vijana wa kitanzania kutoka katika vyuo vyetu vya teknolojia ya habari na mawasiliano wakashirikiana na wafanyabiashara wadogo hasa kuchukua maoni yao kutoka kwao kisha wakatengeneza kitu fulani k**a hiki hapa chini.
👇🏿
🔴Wataalamu hawa wa IT (Wanafunzi wanaokaribia ku graduate) kupitia maoni watakayokuwa wamepata kutoka kwa wale wafanyabiashara wadogo wakatengeneza ambayo itawaunganisha wafanyabiashara wadogo na wateja wao.
App hii iwasaidie wafanyabiashara kuweka bidhaa/huduma zao kwenye hiyo App, kisha wateja wakaagiza bidhaa kwenye hiyo App.

🔵Halafu wakatokea vijana wengine wakafadhiliwa na serikali wakaanzisha kampuni ya usafirishaji, wakanunua baiskeli, pikipiki na gari kwa baadae kwa ajili ya kubebea bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara kupeleka kwa wateja. Kupitia hii, mfanyabiashara akaweza kutrack mzigo unaposafirishwa na mteja akaona mzigo wake kila hatua hadi unamfikia kwake.

🔴Hapa watu wengi watapata ajira na wengi watajiajiri, haiwezi kumaliza kabisa tatizo la ajira lakini linaweza kupunguza kwa kiasi kidogo na familia nyingi zikanufaika.

⬛Hili ni wazo ambalo mtu yeyote anaweza kuliboresha kisha....Bado naendelea kuwaza zaidi nitarudi.

🖊GD

Happy Birthday to Me! 🌟🎂🎉Another year older, wiser, and ready to take on the world with a heart full of gratitude and a ...
27/06/2024

Happy Birthday to Me! 🌟🎂🎉

Another year older, wiser, and ready to take on the world with a heart full of gratitude and a soul filled with dreams. 🎈

Today, I celebrate the gift of life, the love of family and friends, and the endless possibilities that lie ahead. Here's to embracing new beginnings, cherishing unforgettable memories, and creating moments that last a lifetime. 🥳💖

As I blow out the candles, I make a wish for happiness, success, and continued blessings in the year ahead. Thank you to everyone who has made my life so special and meaningful. Your love and support mean the world to me. 🎁🎉💫

Let's make this year one to remember, filled with laughter, love, and adventures that light up my soul. Cheers to the journey ahead and the magic of another year lived to the fullest! 🌟🎂🥂

🎉🎂✨

SIMULIZI:𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐈𝐍𝐀𝐍𝐈𝐓𝐄𝐒𝐀MTUNZI: 𝐀𝐃𝐈𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐊. 𝐊𝐖𝐀𝐍𝐆𝐖𝐀𝐘𝐀SEHEMU: 06ɪʟɪᴘᴏɪsʜɪᴀ......Hakuishia hapo alivaa sketi fupo, amb...
22/06/2024

SIMULIZI:𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐈𝐍𝐀𝐍𝐈𝐓𝐄𝐒𝐀
MTUNZI: 𝐀𝐃𝐈𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐊. 𝐊𝐖𝐀𝐍𝐆𝐖𝐀𝐘𝐀
SEHEMU: 06

ɪʟɪᴘᴏɪsʜɪᴀ......

Hakuishia hapo alivaa sketi fupo, ambayo wanaita kimini kilichoonyesha mapaja yaliyonona, na kibilauzi kifupi, wengi huita “kitopu” chenye kuonyesha kitovu kilichoumbika sawia, usoni alipaka poda kwa mbali na kujipulizia manukato yenye harufu ya mahaba. Mke mwenye sura m***i, nyororo kwa macho ya kuita japo mke wangu alijitahidi kwa vitu vyote hivyo lakini ilikuwa sawa na kupiga kinyago ukwenzi, nilibaki k**a zoba na mbege.

sᴀsᴀ ᴇɴᴅᴇʟᴇᴀ......

Juhudi zote za kujipara manukato, tabasamum nono! Nilibaki kuwa sikuuwona uzuri ule, kumbe ni kwasababu nilikuwa siyawezi. Uzalendo nae ulimshinda, ndipo alipaanza kuuliza.
“Mume wangu urembo wote nilonao bado hunitamani? niambie unanipenda au hunipendi” “Nakupenda”
“Sasa k**a unanipenda mbona hunifa…” alizidi kulalama kila siku, kila dakika, kila sekunde.
“Nisamehe mke wangu ongea taratibu jirani watasikia”. Niliongea kwa sauti ya chini nikiwa nimempigia magoti mke wangu, sikupenda jirani watambue udhaifu nilionao.
“Nirahisi kupata msamaha wangu, lakini nataka ufanye ninachokuambia, umenielewa mume wangu” mke wangu alipunguza ukali kidogo na kuanza kupitisha mkono wake wa kushoto akipapasa kifuani mwangu.
“Haya twende tukatizame mkanda wa X kwenye video ya chumbani” mke wangu aliongea kwa kunibembeleza, aliamini yeye k**a mwanamke lazima ambembeleze mumewe,amfanyie vile vitu anavyopenda ili penzi likomaa na kufika kileleni.
Tulifika chumbani nilijitupa kitandani kigoigoi, roho ikiniuma “Ugonjwa huo wa kuuwa nguvu za kiume niliupata wapi? Au huyu mke ni jini nini? Mbona nimemuoa na uume wangu kukosa nguvu, kwanini? Mbona jenifer nilimridhisha vya kutosha. Mama mkwe kaniloga nini?. Hataki niwe na mwanae” Alitoa mkanda kwenye droo za kanda kisha akasema “Mkanda huu nimeaununua kwa ajili yako. Najitahidi kila namana kukuvuta jirani nami mpenzi” Getruda aliongea huku akitoa tabasamu nono.
“Halafu baada ya kuangalia nini kiendeleee?” niliongea kwa wasi wasi mkubwa tena kwa kuropoka, nilihisi kuchanganyikiwa.
“Kwani wewe umenioa niwe nani kwako, au nifanye nini. Niambie sio kuropoka maneno yasiona maana” Getruda alizidi kufoka.
“Vitu vingine vinaleta kero, sijui huyu ni mzigo, au nini?” Getruda alijisemea kimoyo moyo.
“Basi yaishe mpenzi, punguza hasira”
“Ooo! Kumbe ulikuwa unataka tujifunze kitu”
“Ndio, ili tujifunze wazungu wanavyoridhishana”. Getruda alipunguza hasira kidogo yote hayo ni kunifanya nisisimke.
“Kaaa! Pamoja nami?” Kwa kweli nilichanganyikiwa kabisa, nilikkuwa nikiropoka maneno yasiona msingi, hata nilivyomjibu aliniona limbukeni.
“Kwani ajabu, ndio nikae nawe!” Getruda alizidi kushikwa na hasira usiku mzima hatuku lala ni kukoromeana, maneno ya lawama na mengine ya kuomba msamaha.
“Nikae na wewe tu?” nilizidi kumyumbisha kwa maneno ya ajabu ilimradi papambazuke niondoke mikononi mwake. Nilitamani pakuche niondoke niende kazini.
“Hukubali eee!, niambie hutaki?”
“Aaaaa! Na kubali kabisa bila hofu” jibu hilo lilimfurahisha Getruda mke wangu aliamini ningefanya mapenzi muda mfupi.
“Basi vizuri, nitashukuru mume wangu, na nitakupa unachotaka, japo sijawahi kufanya ngono lakini nitakuachia ufanye utakavyo taka.” Mara moja alianza kuimba.
“Basi mume wangu Sweedy, wewe ni wewe sina mwingine, k**a ni kundi la ndege msituni basi wewe ndio chaguo langu, wengine sioni, nakupenda peke yako naomba uangaze pendo letu ling’are giza,…” Alitunga wimbo wa muda mfupi.
Getruda, mke wangu alinifuata kitandani baada ya kuweka mkanda wa mapenzi, alinikumbatiam tukaanza kuviringishana huku na kule. Lakini wasi wasi ulinijaa pale nilipo kumbuka mapenzi na mke wangu, niliamini hakuna chochote kingeendelea zaidi ya kumtesa Getruda. Wala sikuwa tayari ajue udhaifu wangu, nilihofu pindi angejua basi angeomba talaka, hata hivyo siri ingekuwa hadharani, kila kona ya dunia.
Baada ya kuchoka mabusu, alilala kwa chali akiwa ananitizama, kwa hofu nilitizama pembeni, sikuweza kumuangalia usoni.
“Niangalie basi nijue unanipenda” nilipomtizama kwa kujikaza, nilisikia akisema (Ooooohhh! Honey you look at me, without uttering any word”) “Ooooohhh! Mpenzi unanitizama bila kunena neno!” Nilituliza macho uso mwa Getruda, uso ulijaa ubembe. Ingawa nilifahamu shauku ya mke wangu lakini nilishindwa nimfanyie nini ili nionekane kidume na mume hodari, sio sifa ya kuoa tu ndoa Kanisani. Lakini lazima nimburudishe mke wangu hata kwa kumshika shika maungo yake, ili kumtuliza asionekane mwenye sikitiko moyoni.
Hata hivyo mke wangu hakuchoka na vitimbi vyangu, aliendelea kunishika shika, ili kuniondoa uchovu. Aliona muhimu na dawa ni kwenda na mimi bafuni kuoga, tulienda bafuni na kuanza kuoga pamoja, lakini hakuona uume wangu ukisisimka hata kidogo. Hofu ilianza kumuingia hakuamini alivyonihisi aliona ni uchovu tu wa kawaida. Hakuwa na roho ya kukata tamaa, kule bafuni alijitahidi kuushika na kupapasa maungo yangu, sikuonyesha dalili yeyote ile.
Getruda akaniogesha nami nikamuogesha.Tulipomaliza akachukua sabuni na bush la kuogea tukaelekea chumbani tukiwa tumefunga taulo. Getruda alionekana kuwa na hasira kali moyoni.
“Mume wangu naona hunipendi kutoka rohoni, Bali ulilazimishwa na wazazi wako sio hivi hivi ni miezi miwili sasa inatimia toka unioe hutaki kufanya tendo la ndoa. Heshima ya ndoa iko wapi? Naomba unieleze k**a hinitaki niondoke au nini kimekusibu?”
Wakati ananielezea machozi yalikuwa yanambubujika, aliamini kulia sio suluhisho, taratibu alifuta machozi kwa lesso, alinisogelea karibu na kunizungushia mikono kiunoni, huku akininong’oneza “Sweedy kuna kitu chochote nisichokuridhisha mume wangu. Naomba unieleze niweze kujirekebisha. “Tafadhali niambie sasa hivi. Nahitaji kujua, nitaishi vipi bila mapenzi yako?”
“Kila kitu unaniridhisha ila ni…ni…nina…ni….” nilikokoteza maneno yaliyochanganyikanana kigugumizi, nilishindwa kutamka vizuri nilihisi homa kali, nilijua ndoa ingeingia dosari.
“Ila una nini?. Sema mbona humaliziii?” alinikaripia kwa sauti.
“Unaumwa?” aliniuliza.
“Aaaa!, hata kidogo,” nilimjibu kwa sauti ya chini,
“Au…..penginenimekuudhi bila mimi kufahamu…., maana mama husema mimi ni mkaidi na sijui namna ya kumtunza mtu, ni kweli?” Getruda alizidi kunidadisi.
“Hapana” niliitikia kwa sauti ya majonzi.
“Oke, hivi ni kusema kwa sababu ya kazi ndio umenisogeza pembeni?”
“Hivyo ni vibaya mke wangu, nakuahidi nitajitahidi kukupa penzi nono!, ambalo litafuta kumbukumbu zote nilizo kukera”
“K**a sivyo, basi naomba unibusu, nijisikie furaha moyoni” mke wangu aliongea huku akinisogelea karibu zaidi.
Nilisita kidogo kisha nikainamisha kichwa na uso kutokeza upande wa midomo yake na kumbus kwa uvivu uvivu (Kigoigoi). Nilipomgusa tu midomo yake, mara alinikumbatia vilivyo, kwa mikono yake na kuning’ang’ania na mabusu ya mfululizo na muda mrefu na hata aliponiachia hilihisi joto lenye uvuguvugu nikilikosa. Mwanzoni nilimbusu kwa wasi wasi na shingo upande, lakini baadae nikaadhiriwa na mabusu motomoto ya Getruda nikajikuta ashiki zikiwa zimesisimua mwili mzima, nilijibu mashambulizi kwa mabusu ya nguvu huku nikihema roho juu juu.
Baada ya mabusu yaliotuweka hali ya mapenzi, kwani ashiki zilimpanda na kutaka penzi wakati huo huo bila kucheleweshwa. Akrabu ya saa ya ukutani ilionyesha saa kumi na moja na nusu, karibu na kupambazuka. Majogoo yalikuwa yakiwika kila kona ya wafugaji wa kuku.
“Mume wangu sikiliza” Getruda aliniambia, usoni macho yalikuwa yamelegea na kurembua rembua.
“Eee! Sema mama watoto” nilikohoa kinafiki na kusema.
“Karibu kunapambazuka. Nataka uondoe mawazo ya biashara, madeni, sijue kazi mawazo yako yote weka kuhusu penzi langu na wewe, naomba uniridhishe kwa penzi motomoto.Kwani siku sitini sasa toka unioe hujafanya tendo la ndoa na mimi. Hivyo leo ni mwisho, usipofanya tendo la ndoa, talaka yangu naomba, siwezi kukaa k**a pambo, katuni ndani ya nyumba yako. Sijaja kukupikia hapa tumbo liende mbele, mimi sio kijakazi wako, uelewe leo, mimi ni mkeo tena wa ndoa” Getruda alibadilika ghafla na hakutaka kucheka na mimi, alikua anahitaji haki yake.
“Hayo yote uliyosema nimeyatia akilini ila naomba unipe mu….” Kabla sijamalizia maneno, nilikatishwana sauti ya ukali ya Getruda.
“Nikupe nini?, mbona sikuelewi?”
“Fahamu kwamba ninahitaji kuwa na mtoto . Nataka nami niitwe mama Fulani, si jina langu Getruda” Getruda alizidi kunifokea, nilishindwa kuelewa ninani aliyekuwa ananitesa kiasi hicho.Niliwafikiria wabaya wangu wote akilini sikupata aliyenitendea ushenzi huo.

ɪᴛᴀᴇɴᴅᴇʟᴇᴀ.......

Address

Magegele
Makambako
59122

Telephone

+255768465103

Website

https://podcasters.spotify.com/pod/show/hadithizetu, https://www.selar.co/m/hadithiz

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hadithi Zetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Hadithi Zetu:

Share

Category