NI SULUHU TENA 2025 .....
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepitisha azimio la kumteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka huu.
Azimio hilo limepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM ambao ndiyo chombo cha mwisho cha maamuzi ya uteuzi wa mgombea wa tiketi ya urais kupitia chama hicho. Aidha Chama hicho pia kimempitisha Dkt. Hussein Mwinyi kugombea na fasi ya Urais kwa upande wa Zanzibar.
#Tulipamwinga
#FahariaYaIringa
Mufindi FM Radio inakutakia mwaka mpya 2025 wenye mafanikio kwako na uwapendao.
Katika Msimu huu wa Sikuuku Uwongozi wa Mufindi FM Radio Umeamuwa Kufanya mabadiliko Kadhaa kwa Baadhi ya Watangazaji Kutangaza Vipindi Tofauti .
Sasa Tupige Mastory Tumpe Asilimia Ngapi @dj_bikei Kwa kufanya kipindi cha KIBARAZANI...??? 😂😂😅
Ikumbukwe Dj BK anafanya Vipindi Cha Salamu na Burudani.
Vote Hapa Chini👇
Wekundu wa Msimbazi wamepoteza Mchezo Wa kwanza wa makundi kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kichapo cha bao 2:1 Kutoka Kwa CS Constantine
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza kuchunguzwa kwa taarifa ya wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga, iliyopo Nkasi Kusini, Rukwa kufukuzwa shule kwa madai ya wazazi wao kuiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Agizo hilo limekuja baada ya taarifa hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Waziri Mkenda ameielekeza timu ya Wataalamu Udhibiti Ubora kwenda kuchunguza ukweli wa taarifa hiyo.
Aidha, Profesa Mkenda amesema watoto wote wa Kitanzania wana haki ya kusoma, hivyo hakuna mwenye mamlaka ya kumtoa mtoto shuleni kwa sababu za vyama.
#Tulipamwinga
#FahariaYaIringa
Washikirika wetu wa kibiashara ayas
Disemba Zimepita Nyingii Sana ila hiii Mufindi Fm Radio Tunasema ni Disemba Pamwinga...!!!!!
Msimu wa Ofa Maalum kutoka Mufindi FM Tangaza Biashara au Taasisi yako kwa Punguzo Kubwa la Bei.
#DisembaPamwimga
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa tayari amefika Kariakoo, na kuzungumza na wafanyabiashara ambapo ametoa salam za pole kwa niaba ya Rais na kuwataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati zoezi la Uokoaji linaendelea.
Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Mitungi ya Hewa ya Oxygen ipelekwe kwenye eneo hilo ili kuwasaidia manusura waliopo chini ambao bado hawajaokolewa wakati zoezi la uokozi likiendelea.
Hadi sasa watu 28, wameokolewa huku mmoja akiwa amefariki kufuatia kufukiwa na kifusi cha jengo hilo lenye ghorofa 4.
#Tulipamwinga
#FahariaYaIringa
JENGO LA BIASHARA LAANGUKA KARIAKOO...
Moja kati ya Maghorofa yanayotumiwa kwa Biashara katika eneo la Kariakoo limeripotiwa kuporomoka ambapo bado haijafahamika kiwango cha athari kwa Watu na Mali Zilizokuwa Katika jengo Hilo.
Hata hivyo Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamedai kulikuwa na Watu kadhaa ndani ya jengo hilo.
Taarifa zinasema Mpaka sasa Kikosi cha uokoaji kimefika eneo la tukio na kueleza kuwa kitatoa taarifa kamili baadaye.
#Tulipamwinga
#FahariaYaIringa
Msanii Feruzi amefunguka kuwa yuko katika Muendelezo wa Kuandaa EP yake ambayo atamshirikisha Msanii Jose Chameleon kutoka Nchini Uganda ambapo Ep hiyo iko mbioni kukamilika.
Msanii Huyo ameiambia Full Package ya Mufindi Fm kuwa lengo la Ep hiyo ni kupush zaidi Muziki kwa kushirikiana na Wasanii wa Nje kwani Kidole kimoja hakivunji Chawa, hivyo amewataka Mashabiki kuendelea kusapoti nyimbo zake ikiwemo Video mpya ya BOSS sambamba na ngoma ya Teamo ambayo amefanya Na Jose Chameleon.
Cc @ciphalee @edwinkb25 @feroozgram
“Nawashauri Walezi/Wazazi wawe na sehemu ambayo wanaweza kupanda mbogamboga pamoja na ufugaji ili kuondoa na kukomesha udumavu kwa watoto” Bw Watson Mwambusi
Kwako Mzazi/ mlezi hakikisha mlo wa mtoto una virutubishi vyote muhimu ili umlinde na utapiamlo au udumavu , kwa maelezo zaidi piga namba 199 bure.
#KulaKiafya
#LisheBoraMpangoMzima
@cefa_tanzania @elimu_ya_afya