Mashujaa FM

Mashujaa FM Mashujaa Fm tunapatikana mkoa wa lindi, makao makuu yapo manispaa ya Lindi ... tupigie simu kutangaz
(15)

Mafundi wa Michano na Mitindo huru kwenye beat kutoka kwa Magoma,Salute Junior,R one Bmp.Burudani zote hizi ni hapa   kw...
17/08/2024

Mafundi wa Michano na Mitindo huru kwenye beat kutoka kwa Magoma,Salute Junior,R one Bmp.

Burudani zote hizi ni hapa kwenye Uzinduzi wa Mashindano ya kucheza muziki .

Follow Us
Istagram
Facebook
Twitter
Youtube

Baadhi ya Makundi yatakayo shiriki Mashindano ya kucheza  .Ni katika Uzinduzi rasmi wa Mashindano hayo yatakayofanyika w...
16/08/2024

Baadhi ya Makundi yatakayo shiriki Mashindano ya kucheza .

Ni katika Uzinduzi rasmi wa Mashindano hayo yatakayofanyika wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi

Follow Us
Istagram
Facebook
Twitter
Youtube

Kinachoendelea Mashujaa business Center Nangurukuru Kwenye uzinduzi wa Mashindano ya Kudance   ni Michano na dozi ya bur...
16/08/2024

Kinachoendelea Mashujaa business Center Nangurukuru Kwenye uzinduzi wa Mashindano ya Kudance ni Michano na dozi ya burudani kutoka kwa wasanii wa Kilwa

Follow Us
Istagram
Facebook
Twitter
Youtube

Wikiendi Sehemu ya kupoa na Familia ni Mashujaa Business Centre Kilwa.Njoo Upigwe na upepo mwanana, ule chakula kitamu U...
16/08/2024

Wikiendi Sehemu ya kupoa na Familia ni Mashujaa Business Centre Kilwa.

Njoo Upigwe na upepo mwanana, ule chakula kitamu Ushushie na Maji matamu ya Swahili water .

Updates: Jezi mpya za Namungo FC zitakazotumika kwenye msimu wa 2024/25.Follow UsIstagram Facebook  Twitter  Youtube
16/08/2024

Updates: Jezi mpya za Namungo FC zitakazotumika kwenye msimu wa 2024/25.

Follow Us
Istagram
Facebook
Twitter
Youtube

HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea MOHAMED MOYO amechangia fedha kiasi cha shilingi 3,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa s...
16/08/2024

HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea MOHAMED MOYO amechangia fedha kiasi cha shilingi 3,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa shule shikizi ya msingi ya MOHAMEDI MOYO yenye vyumba viwili vya madarasa iliyopo kata ya Chiola wilayani humo. 

MOYO amekabidhi fedha hiyo Agosti 14 kwa wananchi wa kata hiyo huku akiwataka kuitumia vizuri k**a ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Chiola MOHAMED HASSAN CHIWALO amemshukuru mkuu wa wilaya kwa mchango wake na amemhakikishia kuwa, pesa hiyo itakwenda kusimamiwa ipasavyo na tayari wameshaandaa mipango mikakati ya kuchangishana pesa iliyobaki ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

Follow Us
Istagram 
Facebook 
Youtube 

HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan amewarejesha katika Baraza la Mawaziri, Profesa Palamagamba Kabudi na William Lukuvi ku...
15/08/2024

HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan amewarejesha katika Baraza la Mawaziri, Profesa Palamagamba Kabudi na William Lukuvi kupitia Uteuzi wa Agosti 14, 2024

Prof. Kabudi anakuwa Waziri wa Katiba na Sheria huku Lukuvi akiteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amemwondoa Ummy Mwalimu katika Wizara ya Afya na kumteua Jenista Mhagama kuongoza Wizara hiyo

Kabla ya Uteuzi, Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

Songea Boy  anayo   kwenye The vibe show hapa Follow UsIstagram Facebook  Youtube
14/08/2024

Songea Boy anayo kwenye The vibe show hapa

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

MICHEZO: Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea klabu ya Tabora United adhabu ya kufungiwa kusaji...
14/08/2024

MICHEZO: Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea klabu ya Tabora United adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya klabu hiyo kukamilisha malipo ya wachezaji waliokuwa wakiidai.

Taarifa ya kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TFF imebainisha kuwa wachezaji hao wa kigeni ni Jean Didie Touya, Nyongani Junior Mutuale, Daniel Chitambai Chal na Makuntima Kisombe Guylain.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa awali wachezaji hao walifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC wakidai malimbikizo ya mishahara na kuvunjiwa mikataba kinyume na taratibu.

“Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Tabora United kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.” imesema taarifa ya TFF.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Wananchi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wamehimizwa kuhifadhi misitu ili kujiimarisha kiuchumi.Haya yam...
14/08/2024

HABARI: Wananchi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wamehimizwa kuhifadhi misitu ili kujiimarisha kiuchumi.

Haya yameelezwa leo na mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga na Yahaya Mtonda kutoka TFCG wakala wanaotekeleza mradi wa uhifadhi wa misitu mkoani Lindi.

Pamoja na hilo, mradi wa uhifadhi misitu unaenda sambamba na uwezeshwaji wa jamii inayoishi karibu na misitu hiyo ikiwemo kupewa mbinu za ufugaji wa kuku, nyuki na uvunwaji wa hewa ukaa.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Wawekezaji wa ndani Mkoani Lindi wametakiwa kujisajili na kusajili miradi yao kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzan...
13/08/2024

HABARI: Wawekezaji wa ndani Mkoani Lindi wametakiwa kujisajili na kusajili miradi yao kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kutambuliwa na kunufaika na faida mbalimbali k**a vivutio vya kikodi na kupata misamaha ya ushuru wa forodha na kodi ya ongezeko la thamani.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, SHAIBU
NDEMANGA wakati akifungua semina kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Lindi kwa wawekezaji, wafanyabiashara na wajasiriamali Mkoani humo iliyoandaliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).

Semina hiyo ni sehemu ya kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha
uwekezaji wa ndani inayoendelea nchini.

NDEMANGA amesema pindi wawekezaji wanapojisajili na
kutambulika inasaidia Serikali kuwafahamu na kuwasaidia katika utekelezaji wa miradi yao pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumzia faida za wawekezaji kujisajili TIC, Meneja wa
uhamasishaji kutoka katika kituo hicho FELIX JOHN amesema ni pamoja na kuvutia mitaji, kuleta tecknologia mpya hapa nchini,kutengeneza ajira kwa vijana wanaohitimu kutoka kwenye shule na vyuo mbalimbali nchini.

Aidha, FELIX ameeleza kuwa, kwa kipindi cha kuanzia mwezi
Januari hadi Julai 2024 jumla ya miradi 500 imesajiliwa na TIC na matumaini yao ni kwamba, miradi hiyo ikitekelezwa kwa ufanisi itaenda kuzalisha ajira takribani 121,000.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

Michezo inachambuliwa muda huu hapa  na mafundi wa Takwimu Unasikiliza   kuanzia saa 1:15 hadi saa 3:00 jumatatu mpaka j...
12/08/2024

Michezo inachambuliwa muda huu hapa na mafundi wa Takwimu

Unasikiliza kuanzia saa 1:15 hadi saa 3:00 jumatatu mpaka jumamosi

Tuambie unatamani Timu gani msimu huu itwae Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania?



Ni Muda wa kukaa Kibarazani na kupata Stori Mbalimbali kupitia .Sikiliza kipindi cha   Kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzi...
12/08/2024

Ni Muda wa kukaa Kibarazani na kupata Stori Mbalimbali kupitia .

Sikiliza kipindi cha Kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia Saa 10 mpaka saa 12 Jioni.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: “Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika mwaka wa Fedha 2024/2025 imetenga fedha ya TZS bilioni 7.3 kwa ajili ya ununuz...
12/08/2024

HABARI: “Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika mwaka wa Fedha 2024/2025 imetenga fedha ya TZS bilioni 7.3 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na kuwakopesha vijana [wa programu ya BBT] wanaofanya kazi katika maeneo hayo punde wanapohitimu mafunzo ili kuwawezesha kujiajiri.”

“Mwaka 2023/2024, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana umetoa mikopo yenye thamani ya bilioni 1.2 kwa miradi 57 ya vijana.”

“Matokeo ya utafiti wa nguvu kazi iliyofanyika mwaka 2021, inaonesha kuwa kati ya vijana milioni 14.6 wenye uwezo wa kufanya kazi, vijana milioni 1.8 sawa na asilimia 12 hawana ajira. Tatizo la ajira kwa vijana hasa wa k**e lipo asilimia 16.7 ukilinganisha na asilimia 8.3 kwa upande wa vijana wa kiume hapa nchini.” - Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADE...
12/08/2024

HABARI: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA ( BAVICHA), John Pambalu wamek**atwa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema viongozi hao walikuwa wakielekea mkoani Mbeya ili kufuatilia hatma ya Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu, Katibu Mkuu, John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda, Joseph Mbilinyi (SUGU) waliok**atwa jana Agosti 11.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Jeshi la Polisi nchini limesema halijapiga marufuku kufanyika mikutano ya nje ya hadhara na ile ya ndani  ilimra...
12/08/2024

HABARI: Jeshi la Polisi nchini limesema halijapiga marufuku kufanyika mikutano ya nje ya hadhara na ile ya ndani ilimradi inafuata matakwa ya sheria.

Msemaji wa Jeshi la polisi DCP David Misime amesema kilichopigwa marufuku ni mkusanyiko uliokuwa umeitishwa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 12, 2024 jijini Mbeya kwa kivuli cha kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Lindi, Natalis Linuma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo amewapokea maafisa kutoka ...
12/08/2024

HABARI: Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Lindi, Natalis Linuma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo amewapokea maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kujionea uwekezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na wawekezaji wa ndani.

Akizungumza meneja wa uhamasishaji kutoka TIC Felix John amesema kwa Mkoa wa Lindi wamepata fursa ya kutembelea miradi ya uwekezaji miwili wa ndani iliyosajiliwa na kituo hicho,miradi ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa huku akitoa rai kwa wakazi wa Lindi kuchangamkia fursa na kusajili miradi yao ili waweze kunufaika na kwa kupata vivutio vya kikodi na visivyovya kikodi .

Kampeni hii inakwenda sambamba na utoaji wa elimu ya uwekezaji kwa makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji wa ndani pamoja na waandishi wa habari .

Huo ni mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani inayoendelea nchini ambapo baada ya kutoka Mkoa wa Lindi, TIC wataelekea katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

Muda huu kwenye kipindi cha Mwenye Mji kinachorushwa na Tunaangazia suala la "Baadhi ya Mabinti wa kazi kufanya ukatili ...
12/08/2024

Muda huu kwenye kipindi cha Mwenye Mji kinachorushwa na

Tunaangazia suala la "Baadhi ya Mabinti wa kazi kufanya ukatili kwa watoto".

Endelea kusikiliza mpaka saa 7 k**aili mchana hapa kung'amua mambo muhimu ya kijamii.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Wakala wa barabara Tanzania Tanroads Mkoa wa Lindi imeendelea kuchukua hatua ya kuziba mashimo yaliyojitokeza ka...
12/08/2024

HABARI: Wakala wa barabara Tanzania Tanroads Mkoa wa Lindi imeendelea kuchukua hatua ya kuziba mashimo yaliyojitokeza katika barabara ya Masasi -Mnazi mmoja hususan katika eneo la Mtua longa halmashauri ya Mtama.

Barabara hiyo imekuwa na mashimo mengi na hivi karibuni katika eneo hilo la Mtualonga kulitokea ajali iliyokatisha uhai wa mapadri wawili na bruda mmoja kufuatia gari waliokuwa wakisafiria kupiga shimo na kupoteza muelekeo jambo lililosababisha gari hiyo kutumbukia kwenye shimo la kalvati .

Mashujaa Fm imepita katika maeneo hayo na kuona kazi hiyo ya kuziba shimo katika eneo hilo ikiendelea.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

MICHEZO: Tanzania imehitimisha ushiriki wake kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu bila kushinda Medali yoyote baada y...
11/08/2024

MICHEZO: Tanzania imehitimisha ushiriki wake kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu bila kushinda Medali yoyote baada ya Wanariadha wake, Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri kufanya vibaya kwenye Marathoni ya Wanawake katika kilele cha Michezo hiyo iliyoanza Julai 26.

Magdalena Crispin Shauri amemaliza nafasi ya 40 Kati ya wakimbiaji 80 waliomaliza, akitumia muda wa Saa 2 dakika 31 na sekunde 58, wakati Jackline Juma Sakilu ni kati ya wanariadha 11 ambao hawakumaliza mbio hizo.

Mholanzi mwenye asili ya Ethiopia, Sifan Hassan ameshinda Medali ya Dhahabu kwenye Marathoni hiyo akiweka rekodi kwa kutumia muda wa Saa 2 dakika 22 na sekunde 55, akifuatiwa na Tigst Assefa wa Ethiopia na Hellen Obiri wa Kenya katika nafasi ya tatu leo Jijini Paris.

Ikumbukwe jana wakimbiaji wengine wawili wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu na Gabriel Gerald Geay walikimbia Marathoni ya wanaume, ambayo Tamirat Tola wa Ethiopia alishinda Medali ya Dhahabu, Simbu alimaliza nafasi ya 17 akitumia muda wa 2:10:03, lakini Geay alikuwa nje ya kinyang'anyiro kabisa akimaliza nafasi ya 74 kati ya wakimbiaji 81.

Wanamichezo wengine watatu wa Tanzania, waogeleaji Collins Phillip Saliboko na Sophia Anisa Latiff pamoja na Mcheza Judo, Andrew Thomas Mlugu wote walitolewa mapema.

MICHEZO: NGAO YA JAMII | FULLTIME 🏆YANGA 4- 1 AZAM⚽️ 18’ Dube⚽️ Yoro [ OG]⚽️ Aziz Ki⚽️ Mzize⚽️ 13’ Feisal Salum
11/08/2024

MICHEZO: NGAO YA JAMII | FULLTIME 🏆
YANGA 4- 1 AZAM
⚽️ 18’ Dube
⚽️ Yoro [ OG]
⚽️ Aziz Ki
⚽️ Mzize

⚽️ 13’ Feisal Salum

MICHEZO: Goli la Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 11 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo...
11/08/2024

MICHEZO: Goli la Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 11 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu kwenye michuano ya Ngao ya Jamii leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

MICHEZO: MICHEZO: Emmanuel Wanyonyi (20) ameshinda Medali ya Dhahabu katika mbio za mita 800 kwenye Olimpiki za Paris Ag...
11/08/2024

MICHEZO: MICHEZO: Emmanuel Wanyonyi (20) ameshinda Medali ya Dhahabu katika mbio za mita 800 kwenye Olimpiki za Paris Agosti 10, 2024. Inadaiwa ndio Mshindi mwenye umri mdogo zaidi kushinda katika mbio za mita 800 akiwa Mwanariadha wa Tatu mwenye Kasi zaidi Duniani

Wanyonyi alikimbia kwa muda wa 1:41.19 na kufanikiwa kumshinda bingwa wa Dunia, Marco Arop kutoka Canada.

Ushindi huu umeifanya Kenya kushinda mashindano ya mita 800 mara tano mfululizo katika Michezo ya Olimpiki.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

SIMANZI: Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Mandojo amefariki Dunia jijini Dodoma leo.Taarifa ya kifo cha Msanii huyo imet...
11/08/2024

SIMANZI: Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Mandojo amefariki Dunia jijini Dodoma leo.

Taarifa ya kifo cha Msanii huyo imethibitishwa na rafiki yake wa karibu Msafiri L pamoja na msanii mkongwe Soggy Doggy

Kwa mujibu wa Msafiri L anasema marehemu Mandojo amefariki baada ya kupigwa na watu akidhaniwa kuwa ni mwizi usiku wa kuamkia Leo.

Tunaendelea kufuatilia Taarifa hii kwa undani Endelea kufuatilia kurasa zetu.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Serikali Mkaoni Lindi itaendelea kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili yaend...
10/08/2024

HABARI: Serikali Mkaoni Lindi itaendelea kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili yaendelee kufanya kazi zao za maendeleo na kuibua changamoto mbali mbali za wananchi kwa kwa mujibu sheria hususani kwenye kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo vya serikali k**a Takwimu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi SHAIBU NDEMANGA akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi ZAINAB TELACK kwenye mkutano wa mashirika yasiyo ya kiserikali uliofanyika katika ukumbi wa DDC Manispaa ya Lindi.

Ametaka mashirika yote yajisajiri ili yatambulike maana kumekuwa na idadi kubwa ya mashirika Mkoani humo ambapo mengine hayajasajiliwa huku akimtaka msajili wa Mkoa alisimamie hilo.

Wawakilishi kutoka kwenye baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, JONAFREY PEMBE na MWANAIDI BILALI wamepongeza jitihada za mwenyekiti kuwakutanisha pamoja washirika wote ikiwa ni mara yao ya kwanza pia wametaja changamoto ni kupata wafadhili ambao wanaweza kuwapatia fedha za uendeshaji na kutoa elimu kwa jamii hivyo wameiomba serikali kuwatengea bajeti ikiwa muda mwingine wanashindwa hata pesa ya kulipa pango ya majengo.

08/08/2024

Yanga kucheza na Azam FC fainali

FT | Yanga 1-0 Simba

HABARI: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, Tundu Lissu amesema endapo CHADEMA itaacha misingi yake iliyomfanya ajiunge...
08/08/2024

HABARI: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, Tundu Lissu amesema endapo CHADEMA itaacha misingi yake iliyomfanya ajiunge nacho basi ataondoka katika chama hicho kwakuwa si dhambi na CHADEMA si Dini na si mama yake
-
Akizungumza kupitia Mtandao wa Clubhouse amemnukuu Mwalimu Nyerere aliyewahi kusema CCM siyo mama yake na ikiacha misingi yake ataiacha, na kuongeza kuwa “Unataka niseme kwa mazingira yoyote yale vyovyote itakavyokuwa sitahama CHADEMA? ni mama yangu?”
-
Ameongeza “Nitakuwa sina sababu ya kubaki na hiyo siyo dhambi. Ni Chama cha Siasa, Vyama vya Siasa huja na kuondoka, sisi binadamu tunakuja na kuondoka, kwa hiyo usiniombe nijifunge minyoro ya aina hiyo”.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: ACT WAZALENDO WATU 45 WAMEFARIKI KWA TEMBO.Chama cha ACT WAZALENDO mkoa wa lindi kimesema kuna zaidi ya watu 45 ...
08/08/2024

HABARI: ACT WAZALENDO WATU 45 WAMEFARIKI KWA TEMBO.

Chama cha ACT WAZALENDO mkoa wa lindi kimesema kuna zaidi ya watu 45 wameuliwa na mnyama aina ya tembo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi mnazi Mmoja manispaa ya lindi makamu mwenyekiti ACT BARA isihaka mchinjita amesema wanaitaka serikali kushughulikia changamoto hiyo ili kunusuru wananchi wanaopata madhara makubwa.

Sambamba na hilo mchinjita amesema serikali ya CCM Kwa kipindi chote ambacho kimekua madarakani kimeshindwa kutoa huduma muhimu za wananchi ikiwemo,afya, elimu na nyinginezo.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

HABARI: Mashujaa Fm imekua mshindi wa kwanza Kwa Vyombo vya Kanda ya Kusini kwenye Maonesho ya Nane Nane kwa mwaka 2024....
08/08/2024

HABARI: Mashujaa Fm imekua mshindi wa kwanza Kwa Vyombo vya Kanda ya Kusini kwenye Maonesho ya Nane Nane kwa mwaka 2024.

Follow Us
Istagram
Facebook
Youtube

Asante za Kutosha kwa Team ya Bank ya CRDB Kanda ya Kusini kwa kututembelea katika studio zetu za   viwanja vya Nane Nan...
08/08/2024

Asante za Kutosha kwa Team ya Bank ya CRDB Kanda ya Kusini kwa kututembelea katika studio zetu za viwanja vya Nane Nane Ngongo Lindi.

Follow Us
Instagram
Facebook Fm
Youtube Tv

Address

Wailes
Lindi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mashujaa FM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mashujaa FM:

Videos

Share

Category


Other Radio Stations in Lindi

Show All