SHUHUDIA!! UFUNGUZI WA ZIWA TANGANYIKA, BAADA YA KUFUNGWA MIEZI MITATU/ WAZIRI ULEGA ATOA MAAGIZO.
UVUVI ZIWA TANGANYIKA SASA RUKSA.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Hamisi Ulega amefungua rasmi shughuli za Uvuvi katika ziwa Tanganyika baada ya Kufungwa takribani miezi mitatu.
Waziri Ulega amefanya zoezi hilo la ufunguzi katika Mwalo wa Katonga manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma Agosti 15 , 2024 na kubainisha kuwa shughuli za Uvuvi zilisimamishwa kwa miezi hiyo mitatu kwa lengo la kulinda rasilimali za Uvuvi kwenye ziwa hilo.
Ulega ameongeza kuwa uamuzi huo wa Kufunga ziwa ni utekelezaji wa mkataba wa kikanda wa nchi wanachama wa mamlaka wa Tanganyika (LTA) unaoweka hatua za Usimamizi wa Uvuvi Endelevu katika Ziwa Tanganyika.
Aidha , Waziri Ulega ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wavuvi kuwa Kufunguliwa kwa shughuli za Uvuvi kuendane na matumizi sahihi ya zana halali zinazokubalika kwa mujibu wa kanuni na sheria za Uvuvi.
#uvuvi
#mifugo
#Tanganyika
#Maendeleo
#tanzania
Katika kongamano lililoandaliwa na chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) mkoa wa Kigoma, vijana wamekumbushwa umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kujiajiri.
Somo la vijana kutumia fursa kujiajiri liliongozwa na Bwana Nassor Salim.
🎥@pius_video_production
#youthday2024 #internationalyouthday #tanzania #umatitanzania
Katika kuadhikidha siku ya vijana duniani, chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) mkoa wa Kigoma wamefanya kongamano lililohusisha wadau mbalimbali na vijana lengo likiwa ni kuhamasishana mambo mbalimbali.
Katika kongamano hili vijana wamekumbushwa umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kujiajiri somo lililofundishwa na Bwana Nassor Salim.
#youthday2024 #internationalyouthday #tanzania #umatitanzania
FAIDA KUU 10 ZA TANGAWIZI..
Wengi wetu tumekuwa tukitumia tangawizi kama kiungo kwenye vyakula mbali mbali hasa chai pasipo kuzifahamu faida zake upande wa afya.
Hizi hapa ndizo faida kuu kumi za tangawizi ..
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana
2. Huondoa uvimbe mwilini
3. Kuna viua vijisumu ( antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
4. Ni dawa nzuri Kwa kansa ya kwenye damu ( leukaemia)
5. Huua virusi vya homa
6. Huongeza msukumo wa damu mwilini
7. Huzuia damu kuganda
8. Husafisha utumbo mpana
9. Huzuia tatizo la miguu kuwaka moto
10.Husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula Kwa haraka zaidi.
✍🏾@fadhilinyika
KIGOMA UJIJI YATIKISA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MAGHARIBI, MASHIRIKA, TAASISI NA MAJESHI YABWAGWA
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeibuka mshindi pekee wa tuzo mbalimbali katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane Nane ) yaliyokuwa yakiendelea kanda ya Magharibi viwanja vya Nanenane eneo la Ipuli Manispaa ya Tabora kwa Mwaka 2024.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipokea tuzo ya ushindi wa kwanza (01) katika kundi la Halmashauri za Mkoa wa Kigoma na Tabora, na kuwa mshindi wa kwanza (01)wa jumla inayojumuisha makundi ya Mashirika, Taasisiza Fedha, Taasisi za Utafiti, Mawakala na makampuni ya mbegu, Kampuni za Mawasiliano na Majeshi kanda ya magharibi.
Tuzo hizo alizikabidhi Mgeni Rasmi ambaye alifunga maonesho hayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiko Chacha Jana Augusti 8, Mkoa wa Tabora unajumla ya Halmashauri nane (08) na Mkoa wa Kigoma ukiwa na Jumla ya Halmashauri nane (08).
Kauli mbiu ya Mwaka huu “Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi”
#kigoma #nanenane
Kunashoot Moja la mkwala hadaki yani magori mawili hayadaki hayo ni mabishano ya Mashabiki simba na yaga waoneshana ubabe WAO juu ya wachezaji wao
#kicorafmtz #simba #yanga #michezo #tanzania
Full story YouTube channel @kicorafmtz
Wananichi hii ni jezi ya mahaba wakijitapa mbele ya mashabiki wa simba sports club
Full story kicorafmtz
Shabiki wa yanga nakusanya makombe yote yaani siachi hta moja usajilinwetu nimzuri full story YouTube # kicorafmtz
Uzinduzi wa daftari la kudumu la mpiga kura kigomauwanja wa kawawa maadam magreth magoso akireport kutoka kicora media
Full story YouTube #kicora media
Msanii peter msechu azungumza kuhusu daftari la kudumu la mpiga kura baada ya kushuhudia uzinduzi wa daftari la kudumu la mpiga kura Mkoani Kigoma
Full story YouTube #kicora media
Mhe. Kassim majaliwa afanya Uzinduzi wa daftari la kudumu la mpiga kura katika mkoa wa kigoma tarehe 20/7/2024 na kuhimiza watu wote washiliki kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
Full story YouTube #kicora media
Mapya ewura cc yajitosa kuzungumzia hili ,kudai fidia ni haki ya mtumia huduma
#ewuraabena #nishati #uchumi #siasa #maendeleo
#newpost #afrika #kicora #kigoma #kuwasa #news
Tatizo la maji kalalangabo lapatiwa ufumbuzi
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ccm wilaya ya kigoma imekagua mradi wa ujenzi wa tenki jipya na pampu ya kuvuta maji katika kijiji cha kalalangabo kilichopo halmashauri ya wilaya ya kigoma .
Timu ya mashujaa yaunguruma kishujaa kuelekea msimu ujao wa ligi kuu yaweka bayana kushika nafasi ya nne za juu. Msimu wa ligi NBC 2025/2026
Full story YouTube (kicora radio media)
Camera man @stephano_pius_
Written @bitaliholazaro
Timu ya mashujaa FC ya ahidi kupanda nafasi kutoka nafasi ya nane hadi kufikia nafasi ya nne na kushiriki kucheza mashindano ya kitaifa 2025/2026
Full story on YouTube (kicora radio media)
Graphic designer @stephano_pius_
Written @bitaliholazaro
Timu ya Dodoma Jiji ikiwasili uwanjani like Tanganyika ili kupambana na wageni wao mashujaa FC kutafuta Alama tatu ili kuendelea kushiriki ligi kuu
Tazama kikosi cha Timu ya mashujaa FC kikiingia uwanjani ili kukabiliana na Timu ya Dodoma Jiji kuelekea mwisho Wa ligi kuu na kila mmoja kutafuta Ushindi Wa Alama tatu ili kuendelea kushiriki ligi kuu