Nguruka Tv

Nguruka Tv Home of Entertainment & Sports news

Rais Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyer...
10/04/2022

Rais Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyepokea kwa niaba ya Familia yake katika Kumbukizi ya miaka 100 iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani.

HABARI KUBWA MAGAZETI LEO JUMAPILI APRIL 10.2022
10/04/2022

HABARI KUBWA MAGAZETI LEO JUMAPILI APRIL 10.2022

Anaandika BIG 3 POINTS ...LAMPS ✍Frank Lampard alii set timu yake isipoteze mchezo angalau wapate sare , lakini amekusan...
09/04/2022

Anaandika

BIG 3 POINTS ...LAMPS

✍Frank Lampard alii set timu yake isipoteze mchezo angalau wapate sare , lakini amekusanya alama 3 dhidi ya Man United ambayo imekosa mawazo sahihi uwanjani

✍Everton walitoka kwenye 4-4-2 na kucheza 4-2-3-1 huku Gordon na Richarlison jukumu lao la kwanza ni kuwasaidia mabeki wao wawili wa pembeni pale United wakiwa na mpira huku Iwobi ambaye alikuwa namba 10 ni kushuka chini zaidi kuwasaidia Allan na Delph ....kiufupi walikuwa wanazuia kwa 4-5-1

✍Ajabu ni kwamba kwa muundo huo bado United walifanikiwa kuifikia safu yao ya ulinzi kwa kupasia mpira haraka na mbele huku wakifanya mikimbio ya mbele kilichokosekana na umaliziaji mzuri na umahiri wa Pickford golini .

✍Pongezi kwa Everton kwa kutumia uzembe wa United katikati ya uwanja ...pasi mbaya ya Fred kwa Matic , wakaanzisha shambulizi hapo hapo

1: Kosa la kwanza la Fred
2: Kosa la pili kwa Wan Bissaka , pasi mbaya kwa Richarlison badala ya Wan Bissaka ku sprint akaanza kujogg mpaka mbrazil anachukua mpira anageuka na kupiga pasi ndani ambayo " deflection " kwa Maguire ikazaa goli pekee la ushindi

✍United wamevuna walichopanda , hakuna namna ambayo unaona walivyocheza wanastahili kupata chochote kitu ...kadri siku zinavyoenda ndio wanazidi kuwa vibaya .....Everton walicheza k**a vile maisha yao yanategemea mechi ya leo , walikimbia zaidi, kwenye 50/50 walikuwa imara , walicheza wakiwa wanajali jezi walizovaa ....licha ya kwamba uzuiaji wao Everton bado ni hafifu sana .

NOTE

1: Ukitoa Alex Telles na Lindelof napata tabu kupata mchezaji mwingine wa United ambaye anastahili kutoka uwanjani kichwa juu .

2: Anthony Gordon akiongezewa coaching zaidi inawezekana Everton baadae wakavuna hela nzuri ...maana atauzwa tu .😀

3: Hizi ni ALAMA 3 kubwa sana kwa Frank Lampard kwenye vita ya kushuka daraja kule chini k**a angepoteza leo basi ingekuwa BYE BYE BYE

4: Kwa Man United nafikiri ni RASMI sasa mbio zao za TOP 4 zimefia leo .

Full Time : Everton 1-0 United

06/04/2022

Hapa ni katika kijiji cha msomera wialayani Handeni Mkoani,ambapo serikali imepatenga k**a makazi ya kudumu kwa wamasai Waishio ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. Zoezi hili la uhamisho wa hiari limehusisha vijiji vya Olorieni,Enduren,kakesio,Olbalbal,Misigyo,engaresero,Aleirai,Alaitole,Nainokanoka Pamoja na Ngorongoro wanatarajiwa kuhamia katika Ardhi mpya ya kijiji cha msomera Huko Handeni Tanga.

Makumbusho ya FIFA imepata jezi ya mlinzi wa Comoro 🇰🇲 Chaker Alhadhur ambaye alicheza nafasi ya Golikipa katika mchezo ...
06/04/2022

Makumbusho ya FIFA imepata jezi ya mlinzi wa Comoro 🇰🇲 Chaker Alhadhur ambaye alicheza nafasi ya Golikipa katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Cameroon 🇨🇲 katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwezi Januari

Alhadhur anaingia kwenye kumbukumbu ya dunia kwenye mchezo wa soka.

Kocha wa Simba Pablo Franco amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Machi, 2022.
06/04/2022

Kocha wa Simba Pablo Franco amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Machi, 2022.

Baraza la Uongozi la Soka Duniani, FIFA, limechagua waamuzi 8 kutoka bara la Afrika kuchezesha michuano ya Kombe la Duni...
05/04/2022

Baraza la Uongozi la Soka Duniani, FIFA, limechagua waamuzi 8 kutoka bara la Afrika kuchezesha michuano ya Kombe la Dunia la Qatar 2022 inayotarajiwa Novemba/Desemba baadaye mwaka huu.

Waamuzi saba kati ya wanane waliochaguliwa ni miongoni mwa waamuzi 10 waliochezesha Mchujo wa Kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 mwezi Machi 2022.

Wanaoongoza orodha ya wasimamizi bora wa mechi barani Afrika kushughulikia michezo kwenye hafla ya soka duniani ni mwamuzi wa Gambia, Papa Gassama, wengine ni Victor Gomez wa Afrika Kusini, Tesssema Balmak wa Ethiopia.

Mustapha Ghorba wa Algeria, Redouane Jiyed wa Morocco, Mzambia Janny Sikwaze na Msenegali Ndiaye wanakamilisha orodha ya waamuzi wa Afrika watakaochezea Qatar 2022.

Toleo la 22 la Kombe la Dunia litaanza Qatar, Doha tarehe 21 Novemba 2022.

Orodha Kamili ya Waamuzi wa Kiafrika Waliochaguliwa kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2022.

• Mustapha Ghorbal (Algeria) 🇩🇿
• Redouane Jiyed (Morocco)🇲🇦
• Papa Bakary Gassama (Gambia)🇬🇲
• Tesssema Balmak (Ethiopia) 🇪🇹
• Victor Gomez (Afrika Kusini)🇿🇦
• Janny Sikazwe (Zambia)🇿🇲
• Maguette N’diaye (Senegal)🇸🇳

31/03/2022

WASANII BONGOMUVIE WAACHA HISTORIA ARUSHA,WAWAFUATA MASHABIKI HOSPITALI.

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya  kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za ...
31/03/2022

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Mzee Philip Mangula. Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.

"Bohari ya Dawa (MSD) inatakiwa kufanyiwa overhaul (maboresho) k**a tulivyofanya kwa TANESCO, MSD walifikia hatua ya kup...
30/03/2022

"Bohari ya Dawa (MSD) inatakiwa kufanyiwa overhaul (maboresho) k**a tulivyofanya kwa TANESCO, MSD walifikia hatua ya kupata zabuni SADC, lakini sasa haiko vizuri japo SADC bado ina imani nayo," - Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

“Taasisi zilizopata hati zenye shaka,hati mbaya na hati nilizoshindwa kutolea maoni ni k**a ifuatavyo; Jiji la zamani la...
30/03/2022

“Taasisi zilizopata hati zenye shaka,hati mbaya na hati nilizoshindwa kutolea maoni ni k**a ifuatavyo; Jiji la zamani la Dar es Salaam imepata hati yenye mashaka,Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,Longido,Mlele,Musoma, Sengerema" CAG, DK Kichere.

"MSD ililipwa kiasi cha Sh14.1 bilioni kununua dawa na vifaa tiba vya hospitali za rufaa 27. Hata hivyo, MSD haikupeleka...
30/03/2022

"MSD ililipwa kiasi cha Sh14.1 bilioni kununua dawa na vifaa tiba vya hospitali za rufaa 27. Hata hivyo, MSD haikupeleka dawa na vifaa tiba kwa zaidi ya mwaka mmoja ,"- Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere.

Mashirika ya umma 26 yanajiendesha kwa miaka 12 sasa bila kuwa na bodi za wakurugenzi.
30/03/2022

Mashirika ya umma 26 yanajiendesha kwa miaka 12 sasa bila kuwa na bodi za wakurugenzi.



Wateja 1,207 wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) walitozwa bili za maji katika mwaka wa ...
30/03/2022

Wateja 1,207 wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) walitozwa bili za maji katika mwaka wa fedha 2020/21 bila mamlaka kusoma mita zao za maji.
CAG Kichere

29/03/2022

STEVE NYERERE AIKWAA NAFASI YA MSEMAJI MSAIDIZI YANGA/MANARA AFUNGUKA HAYA.

Siku chache baada ya kujiuzulu nafasi ya msemaji wa shirikisho la muziki Tanzania,Muigizaji mwenye ushawishi nchiji Steve Nyerere amepata shavu katika Anga za michezo baada ya Msemaji wa Yanga Haji Manara kumteua kwa nafasi ya msemaji msaidizi katika Klabu hiyo.

Manara ameyasema hayo wakati akizungum a katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Mkutano uliofanyika jijini Arusha.

Mahak**a ya Rufani Tanzania (Iringa) imefuta kesi iliyokuwa ikimkabili Abdul Nondo, baada ya ofisi ya DPP kueleza kuwa h...
23/03/2022

Mahak**a ya Rufani Tanzania (Iringa) imefuta kesi iliyokuwa ikimkabili Abdul Nondo, baada ya ofisi ya DPP kueleza kuwa haina nia ya kuendelea na kesi hiyo.

DPP alikata rufaa baada ya Mahak**a Kuu kumpa ushindi Nondo ambaye alituhumwa kwa kuchapisha na kutoa taarifa za uongo.

"Miradi hii ilipoanzishwa, ilianzishwa awamu ya tano mimi nikiwa makamu wa Rais... Sasa kwa kunitazama sura na kusema 'a...
23/03/2022

"Miradi hii ilipoanzishwa, ilianzishwa awamu ya tano mimi nikiwa makamu wa Rais... Sasa kwa kunitazama sura na kusema 'asingeweza kuendesha hii miradi,' nadhani hekima haikutumika."- Rais Samia Suluhu Hassan akizundua nyumba za Magomeni Kota.

Rais Samia Suluhu amezindua nyumba 644 za Magomeni Kota, Dar es Salaam.Ujenzi ulianza Oktoba 2016 na umegharimu TZS bili...
23/03/2022

Rais Samia Suluhu amezindua nyumba 644 za Magomeni Kota, Dar es Salaam.

Ujenzi ulianza Oktoba 2016 na umegharimu TZS bilioni 52.2.

Eneo hilo lina ukubwa wa ekari 32, na zilizotumika sasa ni ekari 9.

Eneo hilo lina majengo ya kibiashara, michezo na mapumziko.

📸

Manchester United wamefanya mahojiano na Erik ten Hag, Mkutano ulifanyika wiki hii.  🔴  Man Utd wamefurahishwa na kiwang...
23/03/2022

Manchester United wamefanya mahojiano na Erik ten Hag, Mkutano ulifanyika wiki hii. 🔴

Man Utd wamefurahishwa na kiwango chake cha Ligha lakini uamuzi wa mwisho utahusisha mambo mengi.

Bodi itawahoji Makocha wengine pia.

Source

Habari kubwa Magazeti ya Tanzania Leo March 23,2022
23/03/2022

Habari kubwa Magazeti ya Tanzania Leo March 23,2022

21/03/2022

Hii inaitwa Mkaushoo

Baadhi ya Wasanii wametoa saa 48 kwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), Steve Nyerere kujiuzulu kwa maelezo...
21/03/2022

Baadhi ya Wasanii wametoa saa 48 kwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), Steve Nyerere kujiuzulu kwa maelezo kwamba hawamtaki.

Wasanii wametoa msimamo huo katika kikao kilichoandaliwa na shirikisho kujadili uteuzi huo ulioibua mjadala mkubwa tangu kutangazwa.

Legacy ⚽🔥😉
20/03/2022

Legacy ⚽🔥😉

Jiwe la Simba ugenini leo dhidi ga Asec Mimosas
20/03/2022

Jiwe la Simba ugenini leo dhidi ga Asec Mimosas

Address

Kibondo
Kigoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nguruka Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Nguruka Tv:

Videos

Share

Category

Nearby media companies


Other TV Channels in Kigoma

Show All

You may also like