07/06/2020
➡️VIMONDO 👉SEHEMU II...
K**a kimondo ni kikubwa zaidi, ni sehemu zake za nje tu zinazochomwa, na kiini kinaanguka kwenye uso wa Dunia. Mara nyingi kimondo kinapasuka hewani na kumwaga vipande vyake.
Kati ya vimondo kumi vikubwa kabisa duniani ambavyo mabaki yake yanaonekana, kimojawapo ni Kimondo cha Mbozi nchini Tanzania. Cha kwanza kabisa kinapatikana Namibia kikiwa na urefu wa mita 2.7.
JE! UNAIJUA MVUA YAKE
Vipande vya vimondo-anga mara nyingi hupatikana kwenye anga-nje na kuonekana k**a wingu lililotawanyika sana. Wakati Dunia linapopita eneo la wingu la aina hiyo vipande vidogo vya vimondo-anga huingia katika angahewa kwa kasi kubwa na kuungua. Mvua ya vimondo huonekana k**a kuongezeka kwa mianga ya vimondo angani kwa kipindi cha siku kadhaa, ilhali idadi kubwa ya vimondo huwaka kwa siku chache tu.
Mvua ya vimondo kwa kawaida unasababishwa na mabaki ya nyotamkia. Wingu la vipande hivyo linazunguka Jua kwenye obiti inayokutana na obiti ya Dunia, kwa hiyo kuna mawingu ya namna hiyo yanayorudi kila mwaka. Vipande vya wingu husogea angani kwa pamoja; vikigusana na angahewa la Dunia mianga yake inaonekana kutokea katika sehemu fulani ya anga. Hivyo mvua ya vimondo hupewa jina kutokana na eneo la kundinyota ambako inaonekana, k**a vile Perseidi na Leonidi Perseidi huwa na jina la Perseus (Farisi) ikionekana kila mwaka mnamo 12 Agosti na Leonidi huitwa hivyo kutokana na Leo (Simba ikionekana mnamo 17 Novemba.
👉 HATARI ZA VIMONDO
Kimondo ni hatari kwa vyombo vya angani kwa sababu ya kasi yake kubwa. Hata punje ndogo yaweza kusababisha uharibifu mwingi.
Duniani kuna hatari fulani lakini hali halisi si kubwa ingawa vimondo vinaingia kila saa katika angahewa. Lakini theluthi mbili za uso wa Dunia ni bahari na sehemu kubwa ya nchi kavu haina watu. Katika miaka yote ya karne ya 20 kuna taarifa 21 pekee za nyumba kugongwa na kimondo.
..Inaendelea sehemu ya Tatu k**a umeikosa sehemu ya kwanza Nenda Kiswahili Lifestyle Hacs Vlogger - Cyprian S.